TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

HUYU NDIYO NYEGERE, MNYAMA MWENYE WIVU NA UBABE KUPITA KIASI.

HUYU NDIYO NYEGERE, MNYAMA MWENYE WIVU NA UBABE KUPITA KIASI.
Nyegere ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi duniani, anayeogofya hata wakali kama nyoka, chui na simba. Hawa wote huufyata kwa nyegere. Haogopi mnyama yoyote, humkabili simba au hata chui zaidi ya mmoja na kuwashinda na wala hategemei msaada wa wenzake kushinda maadui zake.

Ana ngozi ngumu zaidi kuliko mnyama yoyote wa mwituni na hivyo ni ngumu kumuua kwa mshale au hata panga. Upana (thickness) wa ngozi yake unapaelekea hata ile sindano ya nyuki kudunda. Mungu kwa uumbaji amemjaalia nyegere kuwa na kucha ndefu na ngumu zinazomsaidia kushambulia viumbe mbalimbali.

MNYAMA MWENYE WIVU. 

Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani kwa jike lake. Nyegere hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike hilo. Hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa. Wivu wa nyegere humfanya awachukie sana binadamu wanaume. Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, na walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za nyegere.
Nyegere anaweza kuuvamia mzinga na kuujambia, kisha hula kidogo asali na nyingine huipeleka kwa mke wake. Nyegere ana uwezo wa kufuatilia harufu ya mrina asali aliyeupakua mzinga ule mpaka nyumbani. Hufanya hivyo akiamini mrina asali ameiba asali yake. Akifika nyumbani kwa mrina asali, huvunja mlango, huingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara).

Mara kadhaa imewahi kuripotiwa matukio ya watu vijijini kushambuliwa kwa namna hii.

CHAKULA

Mnyama huyu hula vitu vyote ikiwemo nyama na majani na hii imemfanya kustahamili shuruba za mazingira yote iwe nyikani ama mwituni. Chakula kikubwa cha nyegere ni asali. Nyegere hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia. Baada ya kufanya hivyo, nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula.

Pia hula nyoka wa aina yoyote, ana sumu kali ambayo akimng’ata nyoka wa aina yoyote haponi, ingawa wapo nyoka wenye sumu ambao nyegere akiwala anaweza kuzimia kwa masaa kadhaa kutokana na ukali wa sumu ambayo inamuua mwanadamu kwa dakika tu.
MAMBO 8 USIYOYAJUA KUHUSU NYEGERE. 

1. Nyegere ni mnyama mwenye asili ya Afrika, Mashariki ya Kati na Hindi.

2. Nyegere ni mnyama mdogo kiumbo anayeweza kuleta balaa hata kwa wanyama wakubwa mithili ya tembo na kifaru.

3. Nyegere ni mnyama wa aina yake sana. Wataalamu wa elimu ya viumbe wanasema yeye ni mnyama ambaye anapenda sana kujitungia safari zisizokuwa za lazima.
Nyegere akiwa katika safari zake hasa zile zisizokuwa za lazima, popote anapochoka hufanya...............!!!

ITAENDELEA.

*************

PIA,

UNAWEZA KUJIUNGA NA GROUP LETU LA SIMULIZI HUKO WHATSAPP KWA AJILI YA KUSOMA MAKALA NYINGI ZAIDI ZA KUSISIMUA KILA SIKU. 

UNALIPIA KIASI CHA SHILINGI 1500 TU KWA MWEZI MZIMA. 

HIVYO KAMA UKIPENDEZWA KUJUMUIKA NA MEMBERS WENGINE KULE KATIKA GROUP, MTUMIE MESEJI ADMIN KWA KUBOFYA LINK HAPO CHINI AMBAYO ITAKULETA KWA URAHISI MOJA KWA MOJA WHATSAPP KWA ADMIN KWA MAELEKEZO ZAIDI YA UTARATIBU WA KUJIUNGA.


KAMA BADO HAUJAJIUNGA NASI KATIKA GROUP MPAKA LEO HII, JUA KUWA UNAPITWA NA MENGI.

*******************

#PIA USISAHAU KUFOLLOW UKURASA HUU WA STORIES ZA KUSTAAJABISHA, PAMOJA NA KUSHEA ILI NA WENGINE NAO WAPATE KUELIMIKA🙏

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post