1~~~~5
NDOA YANGU - 01
“Kwanini unanifanyia hivii?” nilimuuliza mume wangu, ingali macho yakiwa kwake, dhahiri hakuonyesha kabisa kujali maneno yangu, ndiyo kwanza aliendelea kufanya kazi yake.
Hakika sikupendezwa na hali ile, nilikuwa nimezoeshwa kila nizungum-zapo kitu lazima aache kile alichokuwa akikifanya na kunitazama, hata kama si kufungua kinywa chake.
“Inamaana hunisikia baba Tinti?” nikasema tena, sasa niliitoa sauti yangu ikiwa na ukali kidogo, huku maneno nayo yakipanda juu kiasi, sikuwa hivyo tu bali kifua nacho kilijaa, ni kama hewa ilinipungua mapafuni.
Bado hakushangazwa na kile nilichokizungumza, wala kushtuka, alisimama na kujivuta hadi mbele ya kabati letu la nguo, kabla ya kufanya chochote, alisimama mbele ya kioo na nusu mwili kujaa mule kwenye kioo. Kabati letu lilikuwa na kubwa na lenye kioo kikubwa, ukisimama basi nusu ya mwili unaonekana, yaani kuanzia magotini kwenda juu.
Nikama kuna kitu alikuwa akikitazama, maana kwa macho yangu yenye wivu ndani yake, niliweza shuhudia tabasamu lake, roho ikaniuma na kuona kwanini mwanaume huyu awe na tabasamu kwenye kioo na si kwangu? Ina maana kioo kilimvutia kuliko mimi mkewe?
Sikutaka tena kuendelea kubaki mule chumbani, kwa hasira na uso wenye kuvimba, nilisimama na kuanza kutoka nje, nikijua labda angeniita, lakini haikuwa hivyo, ndiyo kwanza aliendelea kuuchuna na kuzidisha tabasamu mbele ya kioo. Ananicheka? Nilijiuliza.
Uso wake uliokuwa mzuri kwa macho yangu, hakika niliweza kuuona, mume wangu ni mwanaume mzuri mno na katu siwezi mfananisha na mwanaume mwingine, namuona mfalme ndani ya nyumba yangu, hana kasoro kabisa. Sifa za mwanaume niliyekuwa nikimtaka miaka nenda rudi hatimaye Mungu alinibariki. Raymond mume wangu na barafu wa moyo wangu, alikuwa mnene kiasi, mwili niliokuwa nikiutaka, kifua chake kipana kilichokuwa kikikibeba kichwa changu nyakati za usiku, mrefu na maji ya kunde, kichwa kikubwa kisicho na chogo, macho yake hunichochea, hisia zaidi na kumpenda mara dufu pindi yanitazamapo, hakuwa na roho mbaya, mpole na mtaratibu, msikivu na si mwanaume mpenda anasa, ananijari kwa kila kitu si mimi tu bali na watoto wake, hupenda ushauri wangu, ndiyo maana tunamaendeleo makubwa ndani ya miaka kumi ya ndoa yetu.
Hakika hunivutia kila sekunde, huhisi furaha na amani pindi niwepo naye, ananifanya kujiona malkia ndani ya nyumba yetu, ananifanya kujiona wa thamani mno, ila leo hii naumia na kukosa amani furaha kisa yeye.
Sikuweza kwenda nje, nilibaki nimesimama katikati ya kizingiti cha mlango wetu macho yakiwa kwake, bado niliendelea kumuona wa maana, hakika nampenda sana mume wangu.
“Raymond,”nilimuita tena, ingali bado, nikiwa pale pale mlangoni, midomo sasa ilinicheza, sikufahamu ni kwanini hali ile ilinitokea, nakumbuka nina kama miaka 12 sijapatwa na hali ile, Raymond ndiye aliyenifanya kuondokwa na hali ile.
Lakini leo hii huyu huyu ananifanya kurejewa na hali ile, nilikuwa ni mwanamke mzuri kwake naweza sema hivyo, maana aliiona thamani yangu na kunihifadhi ndani kwake, kunifanya niwe msaidizi, na mama wa watoto wake, mwanamke wa ndoto yake na mshauri pindi akwazwapo na lolote, je dakika hii yote haya yameondoka?
Nilishindwa kuizuia ile hali, masikini mimi Teddy chozi lilianza kunichuruzika, sikujua kama linatoka, niligundua hilo mara baada ya tone moja kutua juu ya mkono wangu wa kulia, mkono uliokuwa umekishikilia kichwa changu.
Halikuwa tone tu, bali hata kamasi nyepesi, nazo hazikuwa nyuma kunijulizika, aaah nilishtuka mara baada ya kugundua nimepatwa na mafua ya ghafla.
Mume wangu Raymond hakubabaika na neno lolote, ndiyo kwana alinyosha mkono na kuifungua kabati, akavuta tai moja, ni tai niliwahi mnunulia, enzo zile za uchumba wetu, ilikuwa ni tai nzuri sana, tai niliyoichukuwa kwa gharama kubwa, pale Mlimani city.
Aliishika kwanza, na kuitupia macho, ni kama alikuwa akiifikiria , dakika moja nilimuona akiirudisha sehemu yake na kuvuta nyingine, nayo niliinunua mimi, Raymond hakuwa na kawaida ya kununua tai, soksi, boksa na hata vest, nguo za jioni vyote hivi nilivifanya mimi, pia nami sikuwa na utaratibu wa kununua sindiria, nguo za ndani, hata nguo za kulalia, mume wangu alinijari wa hilo, ilikuwa ni kawaida yake kila mwanzo wa mwezi na mwisho wa mwezi kuniletea vitu hivyo, hakika alinifanya kuwa malkia mwema kwake.
Nilitamani kumsogelea, ila miguu haikuwa na nguvu kabisa, nguo yangu ya kulalia ambayo bado iliendelea kuganda mwilini mwangu, niliiona nzito. Hakunitazama, alichokifanya ni kuanza kuifunga ile tai shingoni mwake, bado aliendelea kutabasamu.
“Se..se..se..seee…aaaah!”
Sikuweza sema, sasa kilio kilikuwa wazi, hapo ndipo alipoizungusha shingo yake na kunitazama kwa mara ya kwanza. Tazama ile haikuwa na kitendo chochote chema zaidi ya kuvutiwa mdomo na kukujwa pembeni.
“Aaaah…mume wangu amekuwa hiviii?”
Nilijiuliza nafsini, sasa chozi likikata, macho kwake, sina kilio tena, katu sikuwahi muona Raymond katika hali ile, alikuwa mwanaume mcheshi na mwerevu sana kwangu, iweje awe hivi?
Aah sikuweza kuendelea kusimama tena pale mlango, kwa hasira za wazi wazi niliondoka na kuishia jikoni, huko sikuwa na kazi ya kufanya, dada wa kazi alikuwa tayari kashakamilisha kazi zake.
“Leo umewahi kuamka…shikamoo dada?”
Marietha binti toka mkoani Ruvuma alinisalimia, nilimsikia lakini kinywa kilikuwa kizito, sikuweza kuijibu ile salamu zaidi ya kumtazama tu. Marietha hakujali, ilionyesha naye alitingwa na kazi ndiyo maana alikaa kimya na kuendelea kuzungusha chapati ndani ya kikaango. Nahisi alishaga nigundua.
Jiko likuwa kubwa, kila kitu nilikiona hovyo asubuhi hiyo, niliona kama jipya, sikukaa na humo niliondoka na kuishia sebuleni, hiyo ni baada ya kunasa mazungumzo toka chumbani kwangu.
“Samahani.. haikuwa kusudio langu…naomba unisamehe, naahidi nitarishughulikia leo…..sitaki ukose amani mama….sipendezwi na hali hiyo!”
Hayo ndiyo ngoma zangu za masikio zilinisa, moyo ulibadili mapigo, macho nayo yakaipoteza ile nuru ya kawaida, nikashindwa kupumua vizuri na kujilaza kwenye kochi dogo la mtu mmoja, kochi ambalo halikuweza kuumudu mwili wangu uliokuwa mkubwa kiasi.
Sikujua kwanini nilikuwa na mwili mkubwa kiasi kile, Teddy mie nilijaliwa na kijimwili kidogo toka utotoni mwangu, iweje leo niwe na jimwili kubwa kama hili? Huwa nasitajabu mno.
Nikiwa pale, ubongo ukaanza kupiga rivasi, kauli za mume wangu Raymond na mtu wa pili simuni zikajongea, samahani, ….naomba unisamehe….naahidi sitorudia…..sitaki ukose amani mama, ooh ziliniumiza, sijui ni lini mume wangu amesema maneno haya mbele yangu, sina kumbukumbu kabisa.
NDOA YANGU.
Nikiwa pale kochini nimetulia, mlango wa chumba chetu ulifunguliwa, Raymnod kipenzi ya roho yangu akatokeza akiwa amependenza, kiwivu cha wazi kilinikamata, ile hasira iliyokuwa imejisokota mwanzo iliyeyuka., mithili ya barafu ndani ya maji moto.
Tabasamu nilimtolea, na mwili kupatwa nguvu, sijui ni muda gani niliweza simama, ila cha kushangaza , nilijikuta nikiwa nimesimama mbele yake, nikiendelea kutabasamu.
“Nimekumisi my love!”
Nilimweleza huku nikiitandaza mikono yangu, sikulia tena, kimya chake sikukitilia manani, nilichokifanya ni kumsogelea na kukilaza kichwa changu kifuani kwake upande wa kushoto, macho nikiwa nimeyafumba.
Joto lake lililokuwa adimu enzi hizi, lilianza kuniigia, sekunde tatu zilikuwa nyingi Raymond alinitoa kifuani kwake na kusimama pembeni, usoni hana furaha nami hata kidogo.
Ile furaha iliyokuwa imeanza kujitokeza iliyoyoma, rafiki yangu huzuni, niliyekuwa nimemuweka kando alijogea tena na kusimama nami, chozi lilinitoka Teddy mie.
Hakulijali chozi hili, chozi lililokuwa la thamani mno, chozi ambalo halikusitahili kutoka bila sababu, chozi ambalo alilifanya mfalme wangu litoke, nilijikunyata mfano wa mtoto yatima.
Raymond hakusema, alichokifanya ni kuzamisha mkono wake, mfukoni na kutoka na wallet, kwa haraka kama alikuwa anakimbizwa alichomoa noti mbili zenye thamani ya elfu kumi kumi na kuzitupia juu ya meza kisha akatoka nje, mlangoni akisalimiana na Marietha, tena salamu nzuri na yenye upendo ndani yake. Ila kwangu sikuipata.
Sikutamani kuona tena hayo, nilijizoa zoa na kurudi chumbani kwetu, bado machozi yakiendelea kuchora ramani mashavuni kwangu, miguu yangu ilikoma mara baada ya kulifikia kabati, mboni za macho nikazitupia mbele ya kioo.
Oooh! sura yangu ilitisha, haikuwa yenye mvuto kama zamani, kumbe imekuwa hivi? Ilikuwa ni sura yenye huzuni, kila sekunde, sura iliyojawa na makunyanzi, nilikuwa mwanamke wa miaka 35 ila sikuwa na utofauti na mwanamke mwenye umri wa miaka 70!
Mboni za macho hazikuishi hapo tu, nilizipa kazi ya kushuka chini zaidi, nilipofika kifuani kwangu, ndipo uchungu ulipoongezeka mara dufu, matiti yangu yalikuwa yamelala, kwanini yamelala? Nani aliyefanya kulala? Raymond, ndiyo hakuna mwingine bali ni yeye tu!
Alinioa nikiwa kigori mtoto mbichi, maziwa yakiwa yamesimama wima, yakilichungulia jua angani, akanipenda na kuyasifia, akanichukua na kuniweka ndani, akanipa mimba za watoto wake, kwa heshima na mapenzi ya dhati nikambebea watoto wake tumboni kwangu, nilijifungua na kuwanyonyesha watoto wake, leo hii hao hao watoto wake wamefanya maziwa yangu kulala! Ina maana bila yeye maziwa yangu yangekuwa wima?
Fikra zilikwenda mbali sana, ni miaka kadhaa iliyokuwa imepita, ni kama nilijiona namna nilivyokuwa msichana mzuri enzi hizo, sikutaka kuishia hapo, sasa nilitaka kuuchunguza mwili wangu, nguo yangu ya kulalia nikawa imeiondoa, nilibaki na nguo ya ndani tu.
Pumzi yenye huzuni ndani yake ilinitoka, na ni mara baada ya kutua juu ya tumbo langu, tumbo lililokuwa na makovu mawili makubwa, nilifumba macho, maumivu makali moyoni, hiyo ni mara baada ya kukumbuka kile kilichosababisha tumbo langu kuwa vile.
Nikiwa bado nimefumba macho, nilihisi mikono ikikishika kiuno changu, sikushtuka, taratibu niliyafumbua na kutazama mbele ya kioo, uso wa Raymond ukaonekana mbele ya uso wa kioo.
Mwanamke mimi sikujaliwa ukali, sikujaliwa kutunza hasira, hasira zangu huyeyuka pindi tu nimuonapo mfalme wangu Raymond. Kulia kote kuliondoka, nikawa nimempatia tabasamu kwa mara ya pili asubuhi hiyo ya saa moja kamili.
“I love you ( nakupenda)”
Hicho ndicho alichokisema mfalme wa boma, sikumjibu kwa maneno, nilichokifanya ni kumgeukia, mikono niliipitisha mabegani mwake, huku naye yake ikipita kiunoni mwangu, polepole akawa anaizungusha mikono yake, mgongoni mwangu, nilijihisi furaha, raha na hata burudani, ni muda mrefu Raymond hajauchezea mwili wangu.
Sikumuogopa, alikuwa mume wangu halali wa ndoa, nami bila hiyana, nilianza kuiondoa tai, kisha shati, nikaondoa na vesti, kisha nilishuka kiunoni na kuanza kucheza na mkanda, mkanda niliokuwa nimeununua mimi. Miezi sita nyuma. Kabla ya kuachishwa kazi.
Niliufungua taratibu, na kuuodoa kabisa, kisha nilizivuta nguo zote za chini, mwili wake ukawa wazi, kabisa, hamasa ya kufanya tendo la ndoa lililokuwa halali, iliujaa moyo wangu, sikupoteza wakati, limvuta Raymond na kumsukumia kitandani, kisha nilianza kumchezea michezo ya maandalizi kabla ya kuingia hubani.
Raymond hakutaka michezo, sijui kwanini amekuwa hivi, amekuwa mchoyo na mbinafisi, hanipi haki yangu kama zamani, aliiondoa mikono yangu iliyokuwa kwenye nyumba yake ya kifalme na kunilaza namna alivyokuwa akitaka, mara moja akaanza kuniingilia bila hata maandalizi.
Sikufichi sikuwa namfurahia hata kidogo, ni kama alikuwa akinibaka, maana nilihisi maumivu badala ya kuburudika, dakika sita zilikuwa nyingi akawa amefika mwisho wa safari yake na kuniacha njiani, nililia na kujilaumu kwanini nilikubali kulazwa pale kitandani.
Hakujali sonononeko langu, liko wapi lile neno alilonieleza ananipenda kabla ya kuniangusha kitandani? Raymond alizama bafuni bila hata kunishirikisha uogaji huo, dakika tu mlango ukawa umefunguliwa nay eye kutoka, akajifuta haraka haraka bila hata kunitazama, kisha akavaa nguo na kutoka, akiwa amenijuza kile kilichopelekea yeye kurudi mule ndani.
***
“Ndoa hii ya nini sasa?...kwanini imekuwa shubili kiasi hiki? Mfalme wangu ananitesa,”niliyasema maneno yake, ingali bado kitandani, shuka jeupe likiwa juu ya kifua changu, chozi likizidi kunitoka.
Dakika sita za mume wangu kuondoka, mlango ulisukumwa na binti yangu mdogo, na ni labda wa mwisho kwa kipndi hiki, aliingia chumbani kwangu. Ilikuwa ni kawaida yake kuja chumbani kwetu kila siku asubuhi. Tulimzoesha.
Huyu alikuwa Terry, ana ndugu zake watatu, Tinti, James na John, Terry alishangazwa na hali ile, nililijua hilo mara baada ya kumuona amesimama hasemi kitu macho kwangu.
“Good morning mamy!”
Nilianza kwa salamu hiyo, ila cha kushangaza binti yangu, hakuonyesha furaha hata kidogo, hakunijibu salamu yangu.
“Baby what the matter? Niliendelea kumuuliza kwa lugha ya kuzungu, nilipenda kusema na wanangu kwa lugha hiyo.
“Come here my love,” nisema huku nikijivuta pale kitandani, isivyo bahati shuka nililokuwa nimelisokota kifuani kwangu lilianguka chini, utupu ukawa umeonekana kwa binti huyu aliyekuwa na miaka minne.
“I am really sorry,” nilimweleza huku nikiinama kuliokota, ile nasimama, Terry binti yangu hakuwepo, unyayo wake uliishilia machoni mwangu.
Sikupenda kabisa kumuona akiwa katika hali ile, nilivuta moja ya kanga na kuisokota kifuani kisha nilimfuta chumbani kwao.
“Mamy we need to talk,”nilimweleza huku nikipachika tabasamu mara baada ya kuingia mule chumbani na kumkuta akilia, roho iliniuma, sikupenda kabisa wanangu kuwa katika hali ile, nilimsogelea na kupiga magoti mbele yake, mikono yangu ikiwa usoni mwake, kumfuta chozi, ghafla ndugu zake walinizunguka.
“Mamy we want to know what happen between you and our dady?”
Sikuwajibu, nilibaki nawatazama mmoja baada ya mwingine na kujiuliza maswali rukuki mtimani mwangu. Dakika moja mlango ulisukumwa mfalme wangu alisimama na kutuzama, sikuweza sema kitu nilitulia.
NDOA YANGU 2
Sikuwa na cha kujieleza, nilibaki kimya, mboni zangu zikiwa chini, ni kama vile niliwaonea aibu, mapigo ya moyo wangu nayo hayakuwa sawa, yalibadilika. Kifua kilikuwa kikipanda juu na kurudi ndani, kwa kasi, kana kwamba nilifumaniwa.
Hakuna aliyesema nami, hata binti yangu aliyekuwa mkubwa zaidi ya wenzake naye alikuwa kimya, huyu ni Tinti binti wa miaka 11 sasa, alinitazama.
“Dada una nini leo?” Marietha aliniuliza,
Aah! Kumbe hakuwa mume wangu Raymond, Marietha ndiye aliyeusukuma mlango na kuingia, iweje mimi nimuone mume wangu Raymond? Aah! Kwanini akili yangu imetawaliwa na mwanaume huyu? Ina maana hakuwa yeye? Hapana sikutaka kuamini hilo, kwa macho yangu mawili nilimuona yeye! Sasa mbona siye!
Sikusema chochote kwa Marietha, nilimuonea aibu! Hakuwa na hofu nami, msichana huyu alishanizoe, alinitazama kwa dakika mbili, kisha akaanza kumtazama mmoja baada ya mwingine, jicho lake lilikwamia kwa Terry, binti yangu aliyekuwa bado analia.
Sikupendezwa na uliaji wake, watoto wangu nawapenda sana, huwa sifurahii hata kidogo waliapo, Je nini sababu ya kilio cha Terry asubuhi hii? Ni mimi? Ndiyo. Mimi chanzo! Je nimempiga? Hapana, ila nini sasa?
Sikumpokea kama nilivyomzoesha kila siku, mara moja niligundua mie ndiye mkandarasi wa kilio kile, Terry alikuwa na madeko mno, ndiyo, tulimdekeza, siyo mimi tu hata baba yake. Mfalme wangu. Raymond alimzoesha vibaya. Alimdekeza, naweza sema katika watoto wote huyu alikuwa kiboko.
“Dada kuna nini jamani?” Marietha, aliuliza tena, sasa sauti yake ilitoka kwa juu kiasi, alinikalipia, sikumjibu nilimtazama tu, jicho langu kali lilimfanya kunyong’onyea, akaelewa.
“Nisamehe dada,”alisema kwa upole na unyenyekevu, miguu akiishusha chini na kunipigia magoti, sikupenda kuabudiwa, kwanini afanye hivyo? Sikuwa Mungu wake, haraka sana nilimzuia na neno langu la kwanza toka kupambazuke likanasika masioni mwake.
“Hakuna tatizo, leo sijamuimbia Terry, ndiyo maana analia,” nilimfafanulia kwa sauti ya upole, mikono yangu yote ikizunguka mabegani mwake, nikimvuta juu na sote tulisimama, sasa sikuwa na Terry. Marietha aliula muda wake.
Nilimshika mabegani, macho yakimtazama, sasa nilimbandikia na tabasamu, halikutoka moyoni, lilikuwa la plastiki, ndiyo ilikuwa lazima nimuonyeshe jino langu, matatizo yangu yalikuwa yangu, sikupenda yafike kwao. Msingi wa nyumba ni mimi. Nikiteleza tu nyumba yote chali.
Akili ilipiga rivasi, nikaiona siku ya ‘sendoff’ yangu, siku ambayo imekuwa ikiishi akilini mwangu kwa miaka mingi sasa, kungwi wangu aliifanya kazi yake, alinifunza mengi, namna ya kuishi na mume na hata nje ya mume!
Alikuwa mwanamke wa makamo, ni maarufu sana hapa jiijini Dar es Salaam, anatoka Zanzibar visiwa vya Unguja, neno lake moja kati ya mengi aliyonieleza ndilo lililokuwa likifanya kazi muda huo. Sikupaswa kuyaonyesha matatizo ya chumbani kwangu, mbele ya watoto.
“Chai tayari?”
“Ndiyo. Niliwafuata hawa kwenda kunywa wamenikimbia sebuleni,”alijieleza kwa mapana, hanitazami tena machoni. Nililijua hilo, huwa namkosesha raha msichana huyu ninapomtazama kwa jicho kali, nilijua chanzo ni mimi pia!
Sikusema samahani, eti niliona sina uwezo wa kumweleza hivyo! Sasa sikuwa na Marietha, nilitaka kwanza kumalizana na Terry, niligeuka kwake, huku nikiwa naisokota vyema kanga yangu kifuani, nilimsogelea na kupiga magoti, mikono yangu ikawa mabegani mwake na kumweleza.
“Msamehe mama, anakupenda, je nikuimbie?”
Tabasamu mashavuni mwangu. Hakunijibu kwa mdomo zaidi ya kutingisha kichwa kwenda nyuma na kurudi mbele, bado machozi yakimtoka. Nilimpatia tabasamu, kisha nilimvuta kifuani na kumkumbatia kwa dakika chake, joto lake lilinipeleka mbali.
Mume wangu, jamani, kwanini lakini! Niliuuma mdomo wa chini kwa hisia, kisha nikaufuta uso kwa kiganja cha mkono wangu wa kushoto, mkono niliokuwa nikipenda sana kuutumia, yaani mashoto.
“Terry, your mother in the way, cooking chapatti how may do you want?”
Huo ndio wimbo niliomuimbia, nikiivuta sauti yangu na kuipandisha juu taratibu kwa ustadi wa hali ya juu, mikono nayo ikipiga makofi, sambamba na unesaji wa mwili wangu,kulia na kushoto bila kuchoka, kwa mabali mtoto alianza kutabasamu, nilizidisha madoido na kuwafanya wote mule ndani kucheka. Sina kipaji cha uimbaji, sauti yangu haikuwa na mpagilio wa vina na ulali, nilimba imba tu.
Aah nilifurahi na kujiona Malkia mwema ndani ya nyumba yake, mimi ndiye chanzo cha furaha, lazima niwapatie furaha hata kama nimekwazwa.
Niliwavuta wote na kukumbatia kwa pamoja, kisha tulipiga magoti na kusali sala ya asubuhi, moyoni kila mtu akiwa na furaha, kiasi hata mimi hali yangu ilitulia.
“I want three chapati?”
“Really?”
“Yes mamy, and you?”
“Only one!”
Tulisema huku sote tukijongea mezani, mkono yangu ikiwa imekamata vinganja vya wanangu, sikuweza kunywa chai, asubuhi ile, haikuwa kawaida yangu, niliwandalia watoto, nilipohakikisha kila kitu kipo sawa, nilirudi chumbani kwangu kukiweka sawa.
***
Pua zangu zilipokelewa na manukato ya Raymond, mwili ulisisimka, nikasimama mlangoni na kufumba macho, mkono mmoja ukiwa usoni, mgongo nikiuegemeza ukutani, kila kitu kilichokuwa kimejitokeza asubuhi ile kilirejea tena ubongoni, nilimuona mume wangu, sura yake nilisimama mbele ya uso wangu.
Hata kuingia sikuingia, dakika nne zilizimika mlangoni pale, nilishusha pumzi nzito, kisha nilijikaza na kuzama ndani, nyuma nikiacha nimefunga mlango tena kwa kuubamiza na sauti ya juu ilisikika..
Sikuwa sawa kichwani, akili ilivurugwa, matendo ya mume wangu yalisimama tena, roho ikaniuma mara dufu. Yale maombi tuliyofanya na wanangu sikuyakumbuka tena, hiyo ni baada ya kukumbuka kile kilichotokea kitandani muda mfupi.
Nilikisonya kitanda na kukichukia, kilio cha kwikwi kilianza tena, sikujua hata ni muda gani nilijiinamia kwenye mkono wa kochi moja lililokuwemo chumbani mule, nikilia!
Nilihisi maumivu makali, kila baada ya kuyakumbuka matendo ya mume wangu, amebadilika, je nini chanzo ya mabadiliko yake? Simpi haki yake ya ndoa? Hapana nafanya hivyo kila anaponihitaji, sina mamlaka juu ya mwili wangu, naye hana pia. Yeye hafanyi hivyo, ninapomhitaji. Simpikii kila siku, ‘no,’ napika mwenyewe chakula cha jioni, nilifundwa kabla ya ndoa, chakula cha baba, mama ndiye hupika, labda siku ambazo ni mgonjwa, simtuzi, nakataa namtunza na kumuweka sawa, hata huko nje wale ‘slay queen’ hum-mezea mate. Nishamsariti? Sina kumbukumbu kabisa na uchafu huo. Dhambi hii iniepuke.
Sikupata jawabu la mzingo wa maswali yangu hayo, nilijikaza na kusimama, nilikisogelea kitanda chetu na kukiweka sawa, mara baada ya kubadili mashuka, kwa huzuni niliweka kila kitu pahali pake, kisha nilikisafisha chumba chote, kwa kudeki na kufuta vumbi, kabla ya kuingia bafuni kufanya usafi kisha kuoga.
***
Chumba chetu kilikuwa kikubwa mno, vitanda viwili vya sita kwa sita vinaweza ingia, kulikuwa na kabati la nguo, kochi la mtu mmoja, meza ndogo, ‘dressing table’ pamoja na runinga ndogo ambayo ilikuwa ya kwangu kabla ya kuolewa.
Hatukujaza vitu vingi, kujaa kwa vitu vingi tulihofia mafua, maana vumbi lingegeuza makazi yake, hewa safi itoke wapi? Sikuwa mwanamke mvivu, niliyajua vyema majukumu yangu, chumba changu hakikufanyiwa usafi na mtu mwingine zaidi yangu ama mume wangu Raymond siku ambazo alipenda yeye kunisaidia ama zile za ugonjwa, nguo zetu nilifua mwenyewe. Marietha ambaye kwa sasa ameishi nasi kwa miaka mitano alifua za watoto tu nazo ni baadhi.
Usafi ulipokuwa tayari, nilizama bafuni, bafu lililokuwa chumbani kule kule, ile naingia tu nilipokelewa na uso wa kioo, uso wangu ulijaa mule, niliganda na kujitazama, kama dakika moja na kitu, kisha niliyapuuzia mawazo yaliyokuwa yakija kwa ‘speed’, haraka kama nakimbizwa niliondoka eneo lile,nikilivuta taulo na kuliweka pahala pake, kisha nilijivuta na kusimama chini ya bomba mvua, niliyafungua maji, yakawa yananimwagikia taratibu, mikono nikizungusha kila kona ya mwili wangu, macho niliyafumba.
Niliichukua sabuni na kuipakaa mwilini mwangu, nikianzia shingoni, nikashuka kifuani, mkono uliganda baada ya kugusa ziwa langu la kulia. Mbele.
Hisia zilisafiri, hii ndiyo sehemu yangu ya wadudu, nilishindwa kuoga,akili ilikwenda mbali, uso wa mume wangu ulisimama tena, nilihisi ndiye aliyekuwa akinipakaza sabuni, nikawa nafumba macho na kuyafumbua kwa hisia kali.
Hamu ya kufanya tendo la ndoa ilinivamia. Ndiyo. Nilihitaji, nina muda sijafurahia tendo hili, nanyimwa na hata ninapopatiwa napatiwa kwa ubakaji, sifurahii kabisa.
Sikujali, nilihitaji, sikujua ni saa ngapi nilianza kujihudumia mwenyewe, ile nashtuka ni mara baaada ya kufika mwisho, mule mule bafuni, soni ilinikamata na chuki moyoni, nijifyonza na kuchukia kile nilichokifanya, sijawahi fanya mchezo huo mchafu maishani mwangu kwanini iwe leo. Teddy mimi napotea! Mmh.
Namna nilivyokuwa na hasira na kile nilichokifanya, sikutaka tena kubaki bafuni, nilijimwangia mwangia maji na kusafisha kisha, nilitoka na kuvaa mara baada ya kujifuta na kujipaka mafuta, kisha niliwafuata wanangu sebuleni.
***
Sikufichi siku yangu haikwenda poa hata kidogo, kila mara nilimuwaza ‘king’ wangu, siku hiyo masaa niliyaona hayaendi, hadi inatimia saa kumi na mbili jioni muda wa mume wangu kurejea nyumbani, nishachungulia nje mpaka basi.
“Shikamoo baba…shikamoo baba…shikamooo baba!”
Wanangu walitoa salamu kwa baba yao, naye aliipokea kama kawaida yake, usoni akiwa na furaha kama siku zote, furaha yake ilinifanya nami kufurahi.
Sikutaka kumsumbua pale alipokuwa akisema na familia yake, nilimuacha amalize ndipo nimsalimie, kama kawaida yetu, tuliishi kizungu, kumbusu mume wangu mbele ya wananetu lilikuwa jambo la kawaida, ja ajabu hiyo aliikwepa na kuzama chumbani.
Nilinyong’onyea kwa muda, nikawa nawatazama wanangu nao wananitazama mimi, sikusema kitu, nilinyanyuka na kumfuata kule chumbani.
Hakushtuka na wala kujihangaisha nami, hata baada ya kuingia chumbani, aliendelea kuvua nguo zake, kitu ambacho hakuwa akikifanya, mkewe nilimvua, nilitamani kumfuata, ila hofu ikawa inausakama mtima wangu, sasa nikawa mwoga mithili ya binti mpya kwa mwanaume, eti nikawa nang’ata kidole cha shahada. Eehee!
“Teddy huna sababu ya kumuogopa, huyo ni mumeo,”sauti ilisikika nafsini ikinieleza, ghafla nilipatwa na ujasiri, nilijivuta na kusimama mgongoni kwake, mikono yangu nikiipitisha kifuani kwake. Raymond akatulia, hakutaka kunigusa, utulivu huo ulizalisha nguvu mpya, nilikisogeza kichwa changu sikioni kwake na kumweleza.
“Pole na kazi my king,” nilisema huku nikimbusu, kisha naye akanishika na kunivutia kwa mbele, akinitazama kwa jicho la huba na kunieleza.
“Ahsante….ila kwa sasa nimechoka nahitaji kupumzika!”
Alimaliza kunieleza na kunisukuma, kisha akavuta taulo na kuzama bafuni, akiniacha sina la kufanya. Furaha yote ilikimbia.
Itaendelea …………….
NDOA YANGU - 03
Niliuuma mdomo wa chini sambamba na kitendo cha kufumba macho, kisha nilishusha pumzi nzito na kuketi kitandani, mkono wangu wa kushoto ukiwa umeshika shavu la mkono huo. Sikumuelewa mume wangu, alinichanganya mno kwa vitendo vyake hivyo. Nilijiuliza maswali mengi, yasiyo na majibu, lakini sikupata jawabu la aina yeyote.
“Honey!”
Nilimuita mara baada ya yeye kutoka bafuni, Raymond hakuniitikia, alinitzama mara moja na kunipatia mgongo. Nilifumba tena macho na kushusha pumzi, kisha nilisimama pale kitandani na kumsogelea alipokuw amesimama.
“Kuna tatizo? Nilimuuliza.
“Mmh!” alinijibu hivyo sambamba na kitendo cha kutingisha kichwa, kisha aliinama na kuchukua kopo la ‘lotion’ kabla ya kulifikia nilimuwahi na kulishika, mkononi mwangu na kumweleza.
“Nisamehe!”
“Umenikosea?” alinitupia swali na kisha aliongeza.
“Nipatie hiyo ‘lotion’
Sikutaka kumuudhi, nilimjua, Raymond wangu hakupenda maneno, hakuwa mpenda ugomvi, alikuwa mwaname mmoja mkomya na mtaratibu, nilimpatia na kuketi tena kitandani nikiendelea kumtazama.
“Nakwenda kutazama mpira!”
“Baby! Mpira? Eeh!|
“Yes mpira? Kuna tatizo,”aliniuliza huku akiweka mikono mifukoni, roho iliingiwa na ubaridi mkali, nilihisi kitu chenye ncha kali kikiusakama mtima wangu, hata siku moja hakuwahi sema name namna ile, wale mimi sema naye namna ile, iweje leo hii aseme nami hivyo? Jamni nini tatizo.
Nilinyamaza kidogo, akili ilikimbilia sebuleni, nikaiona Runinga yetu sambamba na decoda ya dst tv, decoda aliyoinunua mwenyewe sababu ya kutazama mpira, utazamaji wake huo uliniambukiza nami, naweza sema nyumba nzima ni wapenzi wa mpira,
“Baby lakini decoda inaonyesha hawajakata,”anilisema kwa utaratibu, nikimtazama kwa jicho la upole, lenye kusema kitu.
“Sijisikii kutazama nyumbani, sina mood nawe!”
“Yesuu…..ooh okay…okay….haaku..,”niliyasema hayo huku nikikipiga piga kichwa upande wa mbele, nikiufumba mdomo na macho pia, neno la mwisho toka kinywani mwake lilinifanya niseme hivyo.
Raymond my husband, king of my family baba Terry hana mood nami? Nilitamani kufungua mdomo na kusema kitu, tayari nilishachelewa Raymond hakuwa chumbani mule, sauti ya ubamizwaji wa mlango ndiyo iliyonishtua toka mawazoni na kunijuza kuwa mule chumbani nilibaki mwenyewe.
“Raymond nimekukosea nini? Tatizo liko wapi? Kwanini hunielezi Hasemi nami? Nimemfanyia nini? Unanijibu hivyo leo? Kauli gani hizo?”
Nilibaki nasema mwenyewe, tena si ndani ya nafsi bali niliyatamka maneno yale kwa sauti ya juu, akili yangu ilinieleza huwenda Raymond wangu angeweza sikia na kurudi chumbani mule, lakini haikuwa hivyo, sikuiona sura yake, wala harufu ya mafuta ya mwili wake, hakuja. Machozi kama bomba mvua yalianza kunimwagika, sikuweza kujizuia sikuweza kabisa, roho iliniuma vilivyo, mapenzi yaliniliza mimi.
***
Hakuna kilichobadilika, Raymond aliondoka mule ndani, muda mfupi tu wa yeye kurejea, hakuwa na tabia hizo hata kidogo, nilizoea kumuoana nyumbani dakika ile, kama siyo chumbani kwetu basi sebuleni akicheza na watoto wake, akiwaelekeza kwa kina kile walichokuwa wamefundishwa shuleni, hakika Raymond alikuwa zaidi ya mume kwangu, zaidi ya baba kwa watoto wake, alikuwa rafiki mzuri kwao. Hiyo ndiyo raha ya kuolewa na mwanaume msomi, watoto hawana sababu ya ‘tutioni’, ya nini? Ingali mwalimu yupo!
Sikutumia dakika chake kulia, nilikata zaidi ya dakika 45, mule chumbani, nilipoona nimetosheka nilisimama na kutembea hadi mbele ya kioo kikubwa cha kabati la nguo, nilisimama hapo na kuanza kujitazama tena mara ya tatu ndani ya masaa 12 tu!.
Niliyaona mabadiliko makubwa, ndani ya sura yangu haikuwa na mvuto hata kidogo, siyo ile ya miaka kadhaa nyuma, sura iliyokuwa na ushawishi wa hali ya juu, sura iliyokuwa ikichengua akili za vidume, ikiwalaza hoi, ikiwafanya wachafuke, ikiwagombanisha wao kwa wao, leo hii haipoo! Khaa! Sura iliyonifanya nichukuliwe na kuwekwa ndani.
Nilikuwa na sura nyingine tofauti kabisa, uso ulianza kukunjamana, uso ulikuwa wenye simanzi nyingi, ulikunjamana kila kona, hakukuwa na mvuto hata kidogo, nilishusha pumzi tena mara baada ya kugundua hilo. Kwa moyo wa unyonge na wenye masikitiko makubwa nilirejea taratibu sehemu niliyotoka na kuketi, dakika hiyo hiyo mlango uligongwa na mgongaji alikuwa na fujo ya hali ya juu.
Nilijikaza na kujiweka sawa, daima sikuwa mtu wa kuonyesha nini kilitokea kwangu, hata mume wangu hakuwa akifahamu vingine vilivyokuwa vikinipata, sikutaka kabisa kuyaonyesha machozi kila sehemu, haraka nilijifuta na kusimama kisha nilipiga hatua kuuendea mlango.
“Mamy siri za familia zimeanza,” Tinti alinieleza huku akinitazama machoni, binti yangu huyu mkuwa alikuwa mdadisi mno, alipenda kunitazama usoni kila alipozungumza nami, hakuwa na soni hata chembe, kuna kipindi miye ndiye niliyemuonea haya! Na kutazama chini!
“Nakuja,”nilimjibu huku nikigeuka na kuanza kurudi chumbani, sikutaka kumtazama usoni, kuna dalili ya kilio ndani nilianza kuiona, kuendelea kusimama pale kungesababisha machozi kunitoka, hicho ndicho kilichonikimbiza mbele ya uso wa binti yangu!
“Subili,”alisema huku akiushika mkono wangu na kunifanya nisimame, bado sikumtazama, jamani eti mwanangu namkimbia?
“Unamwa?” aliniuliza ingali bado akinitazama namna ile ile.
“Mh…siumwi!”
“Mbona unalia?”
“Tintiii, silii, hata silii!”
Hakusema chochote zaidi ya kunyosha mkono wake na kuupangusa uso wangu, hapo ndipo niliposhtuka na kugundua kumbe nilikuwa nalia, natoa na machozi, niliona soni, aibu ilijaa moyoni, sikuweza kuendelea kusimama pale mlangoni nilijitoa mkononi mwake na kuingia chumbani.
Chumba kilikuwa kikubwa, kila kitu jioni kilibadilika, ile furaha changa na hafifu moyoni mwangu iliondoka, mapenzi yaliniumiza vilivyo.
“Nani?”
“Mimi!”
Sauti ya binti yangu ilinasika ngomani, Tinti hakuwa ameondoka, pale mlangoni, bado aliendelea kusimama, nahisi hakupendezwa na hali ile, ndiyo maana aliendelea kuwa pale.
“Unasemaje?” nilimjibu kwa sauti pia, sikutaka kutoka, nilihisi kumuonea aibu, kingine huwa nina hasira za haraka mno, uwezekano wa kumuadhibu pasina kuwa na sababu ulikuwepo, maumivu yangu yangeishia kwake, ndiyo maana niliamua kubaki mule ndani.
“Ngoo! Ngoo! Ngoo!”
Sauti ya ugongwaji mlango iliniingia tena, sikupenda kabisa usumbufu muda ule, bado sikuwa sawa, Raymond alinisumbua, aliniliza na kunisononesha, nilisimama kwa haraka na kutembea hadi mlangoni, moyoni nikiwa na hasira za hali ya juu na Tinti! Nilipanga kumtandika makofi ya maana, kwanini anisumbue namna ile!
“Mamy siri za familiaaa,”sauti ya Terry ilisikika, huku akinitazama machoni, sikuweza kusema, kuondoka na wala kumkalipia, nilibaki nimeganda pale mlangoni, sina la kufanya, zile hasira zilizokuwa zimekandikana mtima sikujua ziliyeyukia wapi.
“Twendeeee!”
Terry alinieleza huku akiuvuta mkono wangu na kuanza kuondoa, sikutaka kumbishia niliambatana naye hadi Sebuleni na kuketi, naweza sema watoto wangu nimewazoesha hivyo, kila mchezo uliokuwa na umaana ndani yake sikuona sababu ya kuketi nao, tulicheka kwa pamoja na hata kupachikana majina ya wagizaji mule ndani, Tinti tulipenda kumuita dada jambazi, yaani yule muigizaji Breda.
***
Akili haikuwa kwenye mchezo ule, macho tu yalikuwa mbele, ila miye sikuwepo kabisa, Raymond aliichengua akili yangu, alinichanganya vya kutosha, aliniumiza. Hadi mchezo unakatika sikuwa nimeambulia chochote, nilinyanyuka pale sebuleni na kuelekea jikoni, muda wa kuandaa chakula cha jioni uliwadia.
Siku hiyo nilipanga kuandaa chakula kizuri na pendwa kwa mume wangu, sikupenda kuiona tofauti kati yetu, niliamua kujishusha na kunyenyekea, yeye ndiye baba mwenye nyumba, niko chini yake yanipasa kuwa hivyo!
Daima sikuumbiwa ugomvi mtoto wa mwanamke mwenzenu, upole, ucheshi, uchangamfu , uvumilivu na hata kile kijimoyo kidogo cha utoaji jamani nimejaliwa ndiyo maana niliamua kufanya hivyo.
Jikoni sikutaka kuyaingiza yale mawazo, sikutaka tena kumuweka Raymond ndani ya ubongo wa mbele, niliamini kama ningendelea kumuweka uwezekano wa kuharibu chakula ulikuwepo tena wa kiasi kikubwa, nilichokifanya ni kujitilishia furaha mtoto wa mwenzenu nikaanza kuimba nyimba hasahasa nilijiimbia Tenzi za rohoni, nyimbo nilizokuwa nikizipenda vilivyo.
Moyo ulijawa na furaha, makunyazi lukuki yaliyokuwa yamekandikana usoni yaliyoyoma, cheko likaanza kuonekana na kusahahu kika kitu, hata pale aliporejea Raymond wangu bado nilikuwa vile vile.
Yeye hakunisemesha zaidi ya kuketi sebuleni na watoto wake hadi pale chakula kilipokuwa mezani ndipo alipoungana nami, sote kwa pamoja tulikula kwa furaha, namna nilivyokuwa amimi naye vilevile, hakutaka kabisa kuionyesha tofauti yetu mbele ya watoto, kuna muda alinitania, hapo mwenzenu nilicheka kwa furaha na kuona yote yamekwisha, mara baada ya chakula tuliungana sote kusali sala ya jioni na kisha tuliagana kwa upendo, kila mtu akaingia chumbani kwake kulala.
“Pole na kazi laazizi!”
Nilianza kumsemesha mara baada ya kuingia chumbani, sikuwa nimezungumza naye vyema siku hiyo.
“Asante,”aliitikia pasina kuonyesha furaha ya neno lenyewe, usoni hakuwa na furaha nami hata kidogo, sikutaka kujitwika mzingo wa mawazo, sikutaka kujiumiza kwa nisichikijua.
“Siku yako ilikwendaje?”
“Vyema!”
“Mh!”
Niliguna huku nikishusha pumzi na kumtazama, hakuonyesha dalili yeyote juu yangu, nilianza kujisikia vibaya, bado hakujari ndo kwanza alikuwa bize na simu yake, na kuna wakati aliweza tabasamu na hata kucheka kwa chini chini.
“Baby!”
Nilimuita. Raymond hakuitika na wala kujisumbua nami, akili na kila kitu kwake vilitawaliwa na simu, nilimtazama kama dakika moja na ya pili nilisimama na kuingia bafuni, humo sikwenda kufanya chochote zaidi ya kulia weeee nilipotosheka nilijimwagia maji na kutoka.
Mboni zangu zilipokelewa na mume wangu aliyekuwa amelala na kujifunika gubigubi, nilimtazama pale kitandani kama dakika moja na nukta, kisha nami nilijongea na kulala kando yake, dakika mbili za miye kuingia kwenye shuka, aliamka na kulala miguuni kitu kilichonishangaza mno.
Yaani leo mzungu wa nne? Eeeh!
Itaendelea ……………………….
NDOA YANGU - 04
Sikuamini kile kilichotekea, sikumbuki ni lini mume wangu ama mimi mwenyewe nilifanya tendo lile, hayo yote yalikuwa mageni, yenye mshangao ndani yake, ndoa yetu imekuwa yenye amani tele, ndoa yenye funzo hata kuko nje, ndoa ambayo nilijivunia nayo vilivyo, ndoa iliyonifanya kuwa tukunyenye namna ile, siwezi ficha hakika mwenzenu nilibalikiwa kuwa na ndoa yenye amani.
Nyumba yetu ilitawaliwa na amani kila siku, amani iliyoishi nasi na hata kujenga majengo ya kudumu yenye matofari imara na sementi imara pia, sikuwahi gombana na mfalme wa nyumba yangu, sikuwahi lizwa ama mwaga chozi na mume wangu, Raymond alikuwa mwanamume mwema kati ya wanaume wote. Nilijivunia kuolewa naye, leo hii nashangazwa mno na kitendo chake cha kulala mzungu wa nne. Inamnaa hataki kulala nami? Makubwa!
Sikuweza vumilia kitendo kile, toka kumekucha siku hiyo moyo wangu hauna amani hata kidogo, simanzi, huzuni, masikitiko na kila kitu kilichoambatana na hayo ndivyo nilivyokumbana navyo.
Akili ilikuwa usingizini, ililala, tena usingizi wa pono, wenye mkoromo wa hali ya juu ndani yake na wenye ndoto za kila aina, sikuelewa sababu ya yeye kuwa vile, nilijaribu kupiga rivasi akili na kurudi nyuma, nilianza kuchunguza kipi kilichopelekea baba mwenye nyumba yangu kuwa vile.
“ Je ni lipi ovu nililofanya kwake? Nimemkalipia? Maana mwanaume huyu hapendi kukalipiwa hata kidogo, hata kama ni yeye kanikosea, sasa wapi nimemkwanza jamani?”
Ni baadhi ya wingi wa maswali yaliyokuwa yakigonga ubongoni mwangu na kuondoka, nilizinyanyua mbavu zangu na kuketi kitandani, kifuani nikiwa na kanga nyepesi,mboni zangu nilielekea kwake, alikuwa kimya ndani ya shuka, hana habari nami.
Sijazoea maisha yale, sijazoeshwa kuwa vile, huwa siwezi kuvumilia hilo, nilikohoa kikohozi kikavu na kufungua kinywa changu, nilizungumza.
“Raymond!”
Nilimuita kwa jina lake halisi, tukiwa namna ile huwa siwezi tumia jina jingine zaidi ya lake halisi, jina alilopatiwa na wazazi wake. Hakuniitikia, alikuwa kimya shukani, nilimtazama mara ya pili, tazama yangu ikiambatana na kitendo cha kujivuta hadi eneo alilokuwa amelala.
“Baby…Raymond!”
“Nini? Tatizo nini wee mwanamkee?,”alisema maneno yale kwa ukali, akiusukuma mkono wangu uliokuwa mwilini mwake, akanyanyuka na kuketi sura akiwa ameivuta, akaongeza neno.
“Una shida gani nami?”
Kimya. Sikuweza sema lolote, uso wake ulinitisha, haukuwa uso wa kawaida, amani yote iliyeyuka mithili ya barafu jotoni. Ulikuwa uso wenye shari shari, sikumuelewa kabisa mwanaume huyu.
“Nakuuliza una nini?”
Bado sikumjibu kwa maneno, nilitingisha kichwa kuashiria hakuna kitu, alinikata jicho kali na kunifyonza kisha akalala, tena akijiviringisha kwenye shuka milithili ya marehemu ndani ya jeneza, hiyo yote ilimanisha hataki gusana nami wala lolote toka kwangu.
***
Moyo ulisononoke, uliumia maumivu makali mno, maumivu yasiyosimulika, kitu kama ngumi kilisimama kooni, kilinisukuma na kuaanza kulia, sasa hiyo ilikuwa mara ya tatu kulia kwa siku moja! Mwanzo nilijikaza na kulia kimya kimya, vijana wa kileo wanadai kilio cha samaki baharini, lakini kadiri dakika zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele ndivyo uzalendo ulinishia na kuangua kilio cha juu.
“Una nini wewee?”
Raymond aliniuliza, ingali akiwa shukani, sikumjibu niliendelea kulia na sasa kilio kilizidi kuongezeka, kwikwi na kamasi nyepesi havikuwa nyuma kunitoka, mwanamke mimi.
“Teddy,”aliniita huku akinigusa begani, sikutaka kumtazama maana kila nilivyokuwa nafanya hivyo ndivyo nilipokuwa nazidisha kilio.
“Wee Teddy, una tatizo gani?”
“Mmh!”
“Sasa kama hakuna nini kinakuliza?”
“Si..si..liiii,”nilisema kwa sauti yenye kilio ndani yake, bado sikutaka kuutazama uso wake.
“Okay. Kama hulii usiku mwema,lia ukichoka utalala!”
Alisema na kisha kuzilaza mbavu zake juu ya godoro na kuniacha nalia hadi pale kilio kiliponikauka na kulala vivyo hivyo pasina kuufunika mwili na chochote hadi siku ya pili niliposhtuka mara baada ya kuhisi naguswa kichwani.
“Mamy! Mamy!”
Kijisauti cha kitoto kilizitekenya ngoma zangu, kwa mbali nilihisi mtu akiniita, taratibu nilifumbua macho yangu yaliyokuwa mazito kiasi, mwanga mkali kiasi ulinipokea, nilitulia kwa dakika moja na nukta kadhaa, ndipo nilipoweza baini kuwa kulikuwa kumepambazuka.
“Mamy,” Terry aliniita tena, safari hii akipanda kitandani kwangu na kuketi kando yangu, vidole vyake laini viliendelea kuzichezea nywele zangu.
“Mwaah, nakupenda mama,”alisema huku akinibusu shavuni, niliachia tabasamu na kumtazama, sura yake ilishabiana na ya baba yake, utofauti tu Terry alichukua rangi yangu.
“Shikamo Terry!”
“Marahabaa mama, shikamoooo!”
“Hahaha..aya bhana marahaba, hujambo wewe na nduguzo?”
“Eeh. Mama baba yuko wapi?”
Nilinyamaza kwa dakika kadhaa, kichwani nikifikiri jambo, toka usiku wa jana tulipolala sijamtia machoni mwangu, ina maana ameondoka pasina kuniaga? Je tabia hii imeanza lini? Na kipi kimefanya aondoke pasina kuniamsha? Si kawaida yetu!
“Hayuko sebeuleni?” nilimtupia swali, juu ya swali, hiyo ndiyo tabia yangu, mara nyingi hufanya hivyo.
“Sijamuonaa!”
“Eeeh?”
Nilinyanyuka na kuketi, macho yakitazama mule chumbani, kana kwamba kilikuwa chumba kipya kwangu, kauli za binti yangu mdogo zilinichanganya kiasi, nilikuwa na maswali mengi mno.
“Tangulia!”
Terry alishuka pale kitandani na kuanza kutembea kuelekea sebuleni, miye nyuma.
“Marietha, hujamuona Baba Terry?”
“Hata dada. Shikamoo!”
“Marahaba. Basi sawa!”
Nilimjibu na kurudi chumani, wazo la kumtafuta simuni ndilo lililokaa kichwani mwangu, hicho ndicho nilichokifanya mara baada ya kuingia chumbani, ndani ya dakika mbili nilikuwa mazungumzoni na mume wangu.
“Kwani kuna tatizo?” aliniuliza kwa sauti ya kishari shari.
“Hakuna tatizo lakini si vyema wewe kuondoka nyumbani pasina kuagana.
“Nikuage wewe kama nani? Mama yangu? Mzee Masanja ama Mungu wangu?”
“Usifike huko, nimesema kwa nia njema tu na hii tabia hukuwa nayo!”
“Ndo imeanza sasa!”
Hapo hapo akakata simu na kuniacha hoi kwa maneno yake. Nikiwa kimya natafakari kila neno, sina historia ya kujibiwa naye namna ile, hata sekunde moja, mwanaume huyu hajawahi nisemea namna ile, kwali hii ndiyo imeanza.
Ndoa hizi loh!
Sikutaka kuyaweka mawazoni hayo, nilijikaza kisabuni na kuona ya kawaida, niliweka kila kitu vyema chumbani kwetu na kisha niliingia bafuni kuoga, huko sikukawia sana, ilinichukua dakika kadhaa nikawa nimekamilisha kila kitu na kuugana na familia yangu.
“Leo mama umependeza unakwenda wapi?” Tinti alinidaka mara baada ya kutokeza chumbani, nilitabasamu na kumueleza.
“Leo ni siku yangu ya kuzaliwa!”
“Hee! “alishangaa, huku akinitazama kanakwamba hakuwahi niona kokote, wote mule ndani walinitazama pia.
“Jamani hata kunipongeza hamtaki? Naondoka!
“Hapana mama, happy born our beloved mamy!”
Walisema huku wakinisogelea, nami sikuwa na budi kuwakaribisha kifuani kwangu na kuwakumbatia, nilikuwa na furaha mno kuona kizazi changu kikinifurahia, nilijiona bonge la malkia mkubwa kwao, muhimili wa maisha yao, cheko langu ni cheko lao pia, kulia kwangu pia kilio kwao, hilo nililigundua mara baada ya kuwaonyesha hilo.
Mama ni muhimili mkubwa mno kwa wanawe! Nililigundua.
“Baba anajua?” Marietha aliniuliza.
“Sitaki kumueleza nataka akirudi ndo ajue!”
“Hutapata zawadi ooh,” Tinti alidakia, huyu alikuwa mpenda ‘birth day’ kama nini, alinishinda kwa tabia, akiona ndani hakuna vinono, basi hujilazimishia birthday yake hahahaha! Kwa mwaka mmoja anaweza zaliwa hata mara nne!
Niliwaachia na sote kuketi kitini, dakika chache Marietha dada wa kazi alitukaribisha mezani kupata kifungua kinywa hatukumuangusha, tulijongea na kukishambulia dakika chake meza ilikuwa nyeupe, siye kwa ulaji mwisho wa reli!
Siku hiyo nilishinda vizuri mno, kichwani nikipanga kuandaa chakula bora na pendwa kwa watoto wangu sambamba na mume wangu, kiliiva mapema, huwa sipendi kuhangaika na majiko ifikapo saa mbili za usiku.
Mida hiyo huwa ya kuketi sebuleni na kufuatilia matukio ya siku runingani, ndiyo wakati huo sote tulikuwa sebuleni tukitazama taarifa ya habari kupita Teddy Television. Kituo kilichokuwa kikirusha matangazo yake kwa hali ya juu, wengi walikipenda.
Hatukuwa tumekula, Raymond hakuwa amerejea, haikuwa kawaida yake kuchelewa, mwanaume huyu alifika nyumbani kwake mapema mno, kabla ya jua kuzama. Hadi taarifa ya habari inakatika Raymond hakuwa amerejea na muda huo watoto walianza kusinzia.
Niliumia kuona wakipata chakula pasina kuwa na baba yao, lakini sikuwa na la kufanya, niliwachukua na kuwapeleka mezani, wakapata chakula cha jioni na kisha tuliungana sote kusali sala ya jioni kisha niliwapeleka chumbani kwao kulala, kisha nilirudi sebuleni kumsubilia mfalme wangu, mwanaume ninayempenda kwa dhati.
***
Ilikuwa saa tatu, kamili ikaingia na nusu, nusu na dakika 45 na kisha saa nne kamili usiku Raymond hakuwa amerejea nyumbani. Hapo ndipo nilipoingiwa na hofu, nilinyanyuka na kuanza kutembea kuelekea chumbani kabla ya kuufikia mlango wa chumba chetu, nilinasa sauti ya mtu akigonga mlango wa sebuleni.
Nilisimama na kusikiliza, sekunde moja mlango ulikagongwa tena na safari hii, mgongaji alizunguma. Mmh. Raymond wangu ndo anarejea muda huu? Looh!
Niliuendea na kuufugua, akaingia pasina kunisalimia hadi pale mimi nilipomuanza, napo aliitikia kwa sauti ya mkato akinyosha chumbani kwetu!
Nilitingisha kichwa, huku nikifunga mlango, mara baada ya kumueleza Mario kufunga geti vizuri, huyu alikuwa mlinzi wetu, kijana mchapakazi vilivyo.
“Habari za kutwa?”
“Njema!”
“Okay. My king, mbona leo umechelewa?”nilimuuliza kwa sauti ya chini, nikimtazama suoni.
“Na pangiwa kurudi kwangu?”
“Hupangiwi, lakini vyema ungenitaarifu, mie ni mkeo nahaki ya kujua pia sababu ya wewe kuchelewa,unaweza patwa na tatizo!”
“Eeeh. Aya!”
“Okay. Unakula kwanza ama unaoga?”
“Sina njaa,” alisema huku akivua shati na kurusha kulia kwake, sehemu tuliyokuwa tukiweka nguo zetu chafu, akanitazama kama dakika moja kisha akaanza kuvua suruali yake, hapo ndipo nilipongua kitu kingine, Raymond alikuwa na nguo mpya ya ndani, nguo ambayo sikuwahi iona kabisa, nilishtuka na kumkazia macho, dakika hiyo hiyo niliona bite ya busu kwenye kora la shati lake, nilihisi kutetemeka kwa baridi, kifua kilijaa upepo, nilitembea na kulishika lile shati, nilichokuna nacho kwenye shati, kilinifanya kumwaga chozi, nikimtazama kwa jicho la huzuni.
Itaendelea …………
NDOA YANGU - 05
Sikuweza kufanya chochote, ubongo ulipigwa shoti, nilihisi kitu chenye asili ya ubaridi kikitembea taratibu kutoka kichwani kushuka kwenye uti wa mgongo, sikuelewa nini kile. Mwili haukuwa na nguvu, nilihisi dalili za ugonjwa wa kiharusi.
“Ni..ni..nii hiiii,”nilijikaza ingali, mwili wangu ukiwa na mabadiliko ya hali ya juu, nilitetemeka sikujua ni tetemeko la baridi ama hasira, bado nilikuwa ndani ya usingizi mzito na ubongo ukiwa na tongotongo la hali ya juu. Mume wangu na mwanaume niliyekuwa nampenda kwa dhati ndiye aliyenifanya kuwa vile, kupigwa shoti la ubongo na kuhisi dalili za kiharusi!
“Nini?” aliniuliza kwa sauti ya kawaida kabisa, sauti isiyohisi chochote, hakuwa na muda nami, Raymond alikuwa bize akihangaika kuchukua taulo ndani ya kabati ili aingie bafuni.
“Naulizaa nini hiiiii?”nilisema kwa sauti ya juu, sauti yenye ukali ndani, sauti yenye kumkalipia kana kwamba yule alikuwa mwanangu,mdogo wangu ama yeyote kati ya hao niliowataja,sikujua kwanini niliingiwa na hali ile, ukali ulijaa mwili mzima, pua nazo hazikuwa nyuma kutingishika, nilitetemkea zaidi ya pale. Tetemeko la hasira lenye kuchanganyikana na maumivu makali ndani yake.
“Unaniuliza hivyo wewe kama nani?” aliniuliza akiwa amesimama mbele yangu, mkono mmoja kiunoni, akinitazama kuanzia juu na kunishusha chini. Macho yamemtoka pima, hana kicheko, uso wa mbuzi.
“Nakuuliza wewe nani mpaka uniulize hivyo?” akasema tena, safari hii hakutamka kwa sauti ya mwanzo, sasa ilipanda juu, na ikikolezwa ukali ndani, ilionekana aliudhishwa na maneno yangu, bado sikuweza kusema chochote, sikuwa na nguvu za kufungua kinywa na kuzungumza.
“Nini hiki?” nilimuuliza huku nikiambatanisha na kitendo cha kumuonyesha lile eneo lenye bite ya busu, alilichukua shati mkononi mwangu kwa nguvu na kunisukuma, bahati ilikuwa kwangu, sikuweza kuanguka, japo alinisukuma kwa nguvu kiasi. Niliishia kuyumba kidogo.
“Lakini kwanini unakuwa hivyo?”
“Nakuaje? Nini tatizo? Unakuwa huna akili? Sijui kwanini ninyi wanawake mko hivyo, unawaza ujinga ujinga tua, akili zako kweli zinachaji? Unakili wewe?” aliniuliza huku akinisogelea, mwili wake ukiwa umetuna kwa hasira, sikuwa na nguvu za kufanya chochote, nilinywea na kuwa mdogo kama kidoge cha piritoni. Muonekanao wake ulinitisha, alikuwa mtu mwingine kabisa, hata siku moja sikuwa muona akiwa katika hali ile.
Sijui kwa sababu huwa hatugombani! Mara kwa mara, ndiyo maana sikulijua hilo. Alizidi kunifuata eneo nililokuwa nimesimama na kuushika mkono wangu akauweka kiganjani mwamke akasema.
“Unahisi nafanya nini? Unahisi nina mwanamke mwingine eeh?”
“Sijasema hivyo?”
“Ila? Nini dhamira yako? Na kwanini unanikalipia kama mwanao, mimi ni Tinti, Terry?”
Sikumjibu niliishia kutingisha kichwa kuashiria kuwa yeye si kama hao mabinti zangu, huyu ni mume wangu na upande mwingine ni mfalme wangu, malkia nilikuwa na sababu ya kuwa chini kwa namna yeyote ile, hata kama yeye anakosa, nilitakiwa nitumie akili ya ziada!
“Sasa kama ni hivyo kwanini unaniijia juu, okay, nambie umeona nini,”alisema huku akinivuta na sote tuliketi kitandani.
“Baby kwenye shati lako kuna bite ya busu, kuna harufu ya manukato mengine tena ya mwanamke, hapo ulipo una nguo mpya ya ndani, kwanini nisihoji? Kwanini nisiulize?” niljikakamua na kusema, kiasi sura yake ilipungua yale makunyazi ya mwanzo, upole wake ulianza kuonekana.
“Unahisi labda nini?’ alitupa swali juu ya swali.
“Lazima nihisi vibaya, ninahaki ya kufikiria ‘negative’ juu yako, mimi ni mkeo lazima niwe makini ninapohisi naibiwa!”
“Una uhakika na hayo?”
Nilikosa cha kuzungumza, Raymond hakuwa na hata ile chembe ya hofu, kwake ilikuwa kawaida mno, hakutishwa na maneno yangu.
“Sina mwanamke na kama unahisi hivyo endelea kuhisi hivyo hivyo,”alisema na kunyanyuka pale kitandani akaingia bafuni akiniacha njia panda sijui nini cha kufanya.
“Shittt!” nililitamka neno lile, huku nikiulaza mgongo wangu juu ya godoro chali, viganja vya mikono yangu vikiufunika uso, moyoni nina maumivu yasiyopimika, machozi machoni yakinilenga lenga.
***
Usiku wetu haukuwa mzuri hata kidogo, kila mtu aliwaza lake, kwangu ulikuwa usiku mzito haswa, haukuwa na usingizi hata chembe, nilikesha nahesabu mapambo ya dali letu hadi kunapambazuka sikuwa nimepitiwa na chembe ya usingizi.
“Baby,”nilimuita ‘king’ wangu kwa sauti ya chini, yenye kunong’ona ndani yake, ilikuwa sauti ya mahaba, sauti yenye kitu ndani yake. Hiyo ilikuwa saa kumi na moja alfajiri,muda ambao alitakiwa kuamka na kujiandaa kuelelekea kazini.
“Mmh,”alinitikia ndani ya sauti yenye usingizi, usiku ule hatukuwa tumelala sehemu moja kama kawaida mzungu wanne alichukua nafasi yake, lakini asubuhi ile ilinilazimu kuiweka hasira yangu kando, kukubali yaishe, kusimama katika nafasi yangu ya uwanamke, kuwa mtiifu na msitarabu kwa mume, ndiyo maana nilikuwa sehemu ile nimelala kando yake, kichwa changu kikiwa juu ya kifua chake.
“Kumekuchaaaa unatakiwa kuamkaaa,” nilimweleza huku nikiutembeza mkono wangu kila kona ya mwili wake, nilikuwa na sababu ya kufanya vile, joto la mwili halikuwa la kawaida,lilipanda juu, kulikuwa na dalili za uhitaji wa chakula cha alfajiri ndiyo maana niliamua kuyaweka kando yote yaliyokuwa yamejitokeza na akili yangu kuilekezea kule.
Nilikuwa na siku kadhaa sijapewa chakula kile, mume wangu alianza kuwa mchoyo sikujua ni wapi alikuwa akila, ndiyo maana asubuhi ile niliamua kutumia nafasi ile angalau niweza pata hata mlo mmoja tu!
“Kumechuchaa?”
“Eeeh! Pole nimekusumbua?”
“Hapana, acha niamke,”akasema huku akianza kunyanyuka, nilimzuia kwa mkono wangu wa kulia, kwa kumrudisha kitandani kisha niliupeleka mkono uleule kwa Raymond mdogo, aliyekuwa amesimama wima, akitaka kunisalimia, kwa kasi ya mwewe angani nililala juu yake, nikiendelea kumsumbua kila kona ya mwili, sasa sikutaka kuzungumza maneno, nilizungumza kwa matendo ni kipi nilikihitaji kutoka kwake.
Hakuwa mbishi, namna Raymond mdogo alivyokuwa machachari, ilimuwia vingumu mno kukataa, kushiriki nami kwa asilimia mia moja, sikuwa hiyo nilifurahia mno, kana kwamba ilikuwa mara yetu ya kwanza kulala, alicheza nafasi yake kwa usahihi, hakika alikuwa ‘forward’ wa aina yake, alijua kucheza na nyavu, na kutupia magori yenye ujazo wa hali ya juu.
“Asante sana,”nilimshukuru huku nikimbusu juu ya lipis, kisha nilishuka kitandani na kuliendelea kabati la nguo zetu, nilivuta taulo mbili moja nilijifunga na moja nilimfunga mume wangu kipenzi na kisha tuliingia bafuni kuoga kwa pamoja, cheko, matani na kila aina ya furaha ilichukua nafasi yake,
Akili yangu haikukumbuka tena yale ya nyuma, penzi jipya lilizaliwa upya, asubuhi hiyo nilikuwa na furaha mno, hadi anaondoka aliniacha nikiwa mwenye furaha, furaha iliyowashangaza hata wanagu, maana siku mbili nyuma sikuwa sawa.
Masaa yalikimbia mithili ya saa mbovu, jioni iliingia pasina kujua, familia yangu ilikuwa mbele ya runinga tukifuatilia siri za familia, mchezo wa kuingiza niliokuwa naupenda kuzidi maelezo, kuna baadhi ya wachezaji walinivutia vilivyo ndiyo maana sikupenda unipite hata kidogo. Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, niliingia jikoni kutayarisha chakula cha jioni, mabacho kila siku nilikuwa nakiandaa mwenye. Kilipokuwa tayari niliuweka mwili wangu katika hali ya usafi kwa kujisafisha na kisha kuvaa nguo nyepesi ya kulalia, nikiisindikiza na kipande cha kanga juu, kisha niliketi sebuleni na wanangu tukitazama taarifa ya habari huku nikiendelea kumgojea mume wangu ambaye hadi muda huo hakuwa merejea tabia aliyoianzisha siku mbili zilizokuwa zimepita.
Moyoni sikuwa na hofu naye, hata kidogo maana nilihisi ni tabia yake mpya aliyoianzisha toka siku moja nyuma, kuchelewa kurejea nyumbani, hivyo niliendelea kutazama runinga hadi majira ya saa mbili na dakika 45 nilipohisi watoto wamechoka niliamua kuwapatia chakula wakala na kisha niliwapeleka chumbani kwao, kabla ya kuketi sebuleni kumsubili mume wangu.
Nilimgojea mno, ilinichukua masaa zaidi ya mawili nikiwa pale, dalili za yeye kurejea hazikuonekana, mishale ya saa tano na dakika kadhaa za usiku niliingiwa na wazo la kupigia simu, nilijizoa zoa pale kochini na kuingia chumbani, huko ndiko kulikokuwa na simu yangu ambayo ilikuwa kwenye chaji.
Niliichomoa na himahima nilikimbilia upande wa majini, “Mfalume!” ndilo jina nililokuwa nalitafuta, mara baada ya kulipata niliiruhusu simu kutoka, nikiiweke sikio langu la kushoto.
‘Namba unayopiga haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baaye!”
Sauti ya kike ilinipokea na kisha kuzungumza nami namna ile, sikuamini kile nilichokisikia nilipiga tena majibu yalikuwa ni yale yale, sikukubali nilipiga tena, bado mrembo wa upande wa pili aliendelea kunieleza namna ile, nilihisi kuchoka.
Sikutaka kukubali, nilimtafua kwa laini yingine ya Tigo nako hakupatika, nilihisi kuchoka zaidi, furaha yote iliyoyoma, mawazo mabaya moyoni yakashika nafasi sikuweza kutoka chumabi nilibaki mule nikiwa nimejilaza chali kitandani,miguu ikining’nia aridhini hadi nilipokuja kushtulia na sauti ya Raymnod ambaye sikujua aliingia saa ngapi chumbani mule na ni nani aliyemfungulia mlango wa sebuleni.
“Ndo kulala gani huko?” alinitupia swali akiketi kando yangu, nilijinyanyua na kuketi, mwili wote ukihisi maumivu makali mno, hasa hasa shingo na miguu, ambayo ilikuwa mizito, na yenye kukamatwa na gazi.
“Hujambo?”
Sikumjibu, nilikuwa kimya nikiizungusha akili yangu kichwani, nilikuwa na mengi ya kujua, mosi kwanini nilihisi maumivu, pili nani alimfungulia mlango na tatu kwanini simu zake hazikupatikana.
“Ulikuwa wapi na simu ulizima kwa nini?” nilimtupia swali mboni za macho zikiwa kwake. Uso mkavu kama wa mbuzi.
“Chaji!” alijibu kwa uwepesi, na kisha alitoka pale kitandani na kaunza kuvua, dakika moja za yeye kulianza zoezi hilo, mlango ulingongwa huku ukisukumwa, bahati haukufunguka maana ulifungwa kwa ndani, nilisimama kivivu na kuanza kuuendelea, miguu na mwili wote vikiniiuma.
Nilifika na kuufungau, kisha nilitoa kichwa, suo wa Terry ulinipokea kwa tabasamu bashasha.
“Shikamoo mama, muuza maziwa anakuita!”
“Eeh!,”nilishtushwa vilivyo na kauli yake, dalili ya kuhisi huwenda naota ndiyo iliyokamata hatamu, nilijitazama harakaharaka kwa dakika kadhaa, kisha nilimtazama Terry bado hakushtushwa na mshangao wangu.
“Mama muuza maziwa anakuitaaaa,”kilisema huku kikinishika mkono na kuanza kunivuta kutoka nje, akili ikiwa mbali, haijui moja na mbili.
“Terry unanipeleka wapi?”
“Njee, twendee unaitwa!”
Nilishusha pumzi nzito mara baada ya kuipandisha hewa kupitia tundu zangu za pua, macho yakizunguka kulia na kushoto mule ndani, kana kwamba nilikuwa mgeni eneo lile.
“Shikamoo mama,”Tinti naye alinisalimu pamoja na Richard mtoto wangu wa kiume na wa pekee ndani ya familia yetu.
“Inamaana kumekucha?”
“Eeeh! Hahahaha kumekuchaaa mamaa, na kesho ni sikukuuu ya Krismasi hujatununulia nguo, “ Richard alinidaka na kuzidi kunishangaza, sikuwa nikijua kama saa ile ilikuwa asubuhi, na kama ni asubuhi Raymond mume wangu alilala wapi?
Itaendelea ……
Full 1000 tu
Whtsp 0678173301
Tags:
simulizi