TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JUKUMU LA KILA MMOJA KATIKA KUDUMISHA MAHUSIANO

JUKUMU LA KILA MMOJA KATIKA KUDUMISHA MAHUSIANO
Mahusiano ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Haijalishi ni uhusiano wa aina gani lakini hakuna namna mtu anaweza kuishi bila kuhusiana na wenzie kwa namna moja au nyingine. Leo tuzungumzie kuhusu mahusiano ya kimapenzi,uchumba na ndoa. 
Mada yetu ya leo tunaipa jina la JUKUMU LA KILA MMOJA KATIKA KUDUMISHA MAHUSIANO. Tukumbuke kua hakuna mahusiano yanayojengwa na mtu peke yake. Mahusiano ya kimapenzi yanaundwa na watu wawili. Watu wengi hujikuta katika majuto ama katika ndoa au hata katika hatua ya uchumba baada ya kugundua kua mtu aliyenaye sie aliyekua anamtarajia. Watu hujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi baada ya kuona na kukubaliana na sifa kadhaa za mwenza wake haswa sifa za nje akiamini kua atapata matarajio yake yote kwa ukamilifu uleule uliopo akilini mwake lakini anapogundua sio kama alivyokua natarajia huamua kuanza vituko. Leo nataka kukwambia bado haujachelewa unaweza kua na mtu mwenyesifa utakazo unachotakiwa kufanya ni kunifuatilia katika dondoo zifuatazo.

1. Weka matarajio kiasi juu ya mwenza wako.
Wengi wameingia katika uchumba ama ndoa wakitumaini kuona picha waliokuanayo vichwani ndio itakua hivyo. Wengi hutarajia mambo makubwa sana kutoka kwa wenza wao. Kwa mfano maisha ya juu, shopping za kila mara, majumba ya kifahari, na maisha yaliyo bora bila kujali kua vyote hivyo ni matokeo. Jitahidi kuweka maratajio yenye mipaka juu ya mwenza unayemtaka. Hii itakusaidia kupata mtu sahihi na atakaye jail uwepo wako katika maisha yake. Fikili ukipata mtu mwenye kila kitu thamani yako itakua wapi. Jitahidi kua sehemu ya kujenga matarajio makubwa.

2. Kuwa wa kwanza kua mjenzi wa penzi lenu.
Hapa ndipo watu wengi wanafeli, wanahitaji kufanyiwa mambo mema kama vile kuletewa zawadi, kutolewa out, surprises, na mambo mengi mazuri lakini inapotokea hayo mambo hayapo wanahisi mtu aliyenaye si sahihi. Kwanini usiwe wakwanza kumfanyia hayo ili kumjenga? Jitahidi kuonyema utofauti wako na wapenzi wengine aliokwisha kua nao.

3. Elewa udhaifu wa mwenza wako 
Jitahidi sana kumjua mpenzi wako hasa katika madhaifu na uwezo wake katika mambo mbalimbali. Kwa yale madhaifu aliyonayo ambayo unahisi unaweza kuyaweka sawa fanya hivyo ila kama hauwezi basi tafuta namna ya kuyazungumza au kuendana nao. Kwa mfano mwenza wako hajui kuvaa, mnunulie mavazi, hapendi kukutext, mfanye aone umuhimu huo, mfano hapendi mambo ya zawadi, mpatie kwanza wewe na umueleze kua hua unapenda zawadi. Kumbuka usione vyaelea vimeundwa.

4. Usipende kulaumu kila kitu
Kuna wenza wengine wanamdomo balaa, jambo dogo tu ataongea hadi kukuche. Inapotokea madhaifu jitahidi kuwa wa kwanza kumtia moyo ndipo umueleze kua inawezekana kufanya vizuri zaidi. Sio mboga imeongezwa chumvi kidogo unazila chakula, unatukana hii inaperekea mtu kujisikia vibaya na hata kupunguza mapenzi. Kunawatu ikifika mida ya kwenda nyumbani wanatamani masaa yarudi nyuma.

5. Jenga ufalme wako
Fanye mwenza wako akuelewe, nini unapenda na nini haupendi mapema kabla hata hamjafika mbali. Usimzoeshe mambo usiopenda maana yatakupa shida badae kubadilisha.

6. Weka maslahi yako pembeni na ubebe maslahi ya pamoja
Angalio ni nini kimewafanya kua pamoja kuliko sababu za wewe kua katika mahusiano. Wenza wengi huweka mbele maslahi yao binafsi. Hii husababisha mahusino mengi kuvunjika haswa pale kila mmoja anapovutia kwake. Ni vyema kila mmoja ajue kua uhusiano wao ni matokeo ya upendo kati yao na wanawajibe wa kujaliana kila mmoja akimuona mwenzake kua bora. Lakini mmoja akijiona yeye ni bora hapo mahusiano yanakua dhaifu kwani mmoja wao atajiona ni kama mtumwa.

7. Jifunze dondoo mbalimbali za kudumisha mapenzi kila wakati
Education is the power. Unapopata elimu juu ya mapenzi itakufanya kudumisha mapenzi yenu na kuwa na mvuto kwa mwenza wako.pia itakusaidia kuwa tofauti kila siku.
Kumbuka Mungu anachukia kuachana

8. Kuvunjika kwa uhusiano wenu wewe ni sehemu ya sababu
Kumbuka hata kama utakua na sababu nyingi kiasi gani. Mwisho wa siku utakua ni sehemu ya kushindwa huko. Jitahidi kujenga kuliko kubomoa. Siku zote beba majukumu ya uhusiano wenu bila kujali mwenza wako anatimiza wajibu wake kiasi gani. Kwa kufanya hivyo unaweza kumfanya mwenza wako kujifunza kutoka kwako.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post