FAHAMU JINSI MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YALIVYOATHIRI NAMNA WATU WENGI WAVYOJIONA...
__________________________
Hivi unafahamu kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta athari nyingi zaidi kuliko faida miongoni mwa watu wengi hasa linapokuja suala la namna wanavyojiona?
Unachopaswa kujua ni kwamba kila kilicho na faida hakikosi hasara!
Kutokana na ukweli huo huna budi kukubaliana na mimi kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja kuathiri sana watu kimtizamo pamoja na hata namna wanavyojiona!
kwanini nasema maendeleo haya yamebadilisha watu kimtizamo?
Sababu kubwa inayonisukuma niseme hili ni kwa sababu watu wengi wamejikuta wakitumia sayansi na teknolojia kama kioo cha kujitizamia!
Ambapo mwisho wa siku wanaishia kujiona wao ni wabaya kimuonekano, (hasa wakihusisha na rangi zao pamoja na muonekano wa maumbile yao)
Kutokana na hilo wanaanza kujishushia thamani na kujiona wao kama siyo kitu, pasipo kujua kwamba kioo walichotumia kujitizamia siyo kioo halisi!
Kwa mfano maendeleo ya sayansi na teknolojia yamekuja na ugunduzi wa baadhi ya viungo bandia (vinavyopandikizwa mwilini mwa binadamu), utengenezwaji wa baadhi ya vidonge ambavyo ni mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile, kutengeneza shepu pamoja na kuchubua rangi (yaani kutoka rangi nyeusi kwenda rangi nyeupe).
Hii inamaanisha kwamba kutokana na upumbavu ulioletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia mwanamke mweusi, mwenye umbo la kawaida, ambaye ana rangi nyeusi anajiona yeye kama si kitu mbele ya mwanamke mwenye rangi nyeupe, (inayotokana na kujichubua), mwenye maumbile ya kutengenezwa na mwenye mwonekano mzuri kutokana na matumizi ya vidonge asijue kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya hao wanawake walivyo na vile yeye alivyo!
Wanawake hawa hujiona wao si kitu na hawawezi hata wakaolewa eti kwa sababu ya rangi zao, maumbile yao pamoja na muonekano wao kitu ambacho hakina ukweli wowote!
Ambapo mwisho wa siku hujikuta nao wakipambana waweze kubadili muonekano wao ili wawe na mvuto Kwa wanaume! Swali linakuja mara baada ya kuvutia tutarajie nini?...
Ukichimba kwa undani zaidi katika kulichunguza suala hili, utagundua kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yamewafanya watu wengi wajione kwamba wao waliumbwa waje watumikie ngono tu hapa duniani.
Hali hii imewafanya wajikute wakiwa na mitizamo ya kujali zaidi mvuto unaolenga zaidi eneo la sex, wakasahau kabisa kuhusu hata kusudi la kuumbwa kwao hapa duniani pamoja na mchango walionao katika kubadili jamii yetu!
My friend, hauhitaji kutumia nguvu kubwa sana kubaini hili, hebu jaribu kuangalia jinsi wanawake wa leo wanavyohangaika kila leo kuchubua rangi zao kisa wapendeze mbele ya wanaume. Wanawake hawa wanakumbwa na sex mentality. Kwamba hicho ndicho anachokiona nafsini mwake!
Kuna wengine wanahangaika kumeza vidonge ili waongeze nyonga zao pamoja na makalio yao kisa tu wapendeze na wavutie machoni pa wanaume hii nayo ni sex mentality na si kitu kingine.
Wapo wengine wanahangaika kuvaa nusu uchi huku wakiacha maungo yao wazi kisa tu wawavutie wanaume hawa nao wana sex mentality.
Na, ubaya ni kwamba hawajui sisi kama wanaume siku hizi tunaenda kwa imani na siyo kwa kuona tena hahahaha!
Hata hivyo ni juzi tu hapo Elon Musk kagundua midoli ya kike kwa ajili ya kufanya nayo sex, ugunduzi huo umeleta athari kwa wanaume wengi wengi na kuwafanya wazidi kujiona kwamba sex ni kila kitu kwao, kiasi kwamba wanajiona kama waliumbwa hapa duniani kwa ajili ya kufanya sex tu kitu ambacho siyo kweli kabisa!
Moja ya hoja anayotumia kuuza midoli hiyo ni pale anaposema midoli hiyo itapunguza gharama ukilinganisha na ukiwa unaishi na mwanamke, sasa na wewe mwanaume unayedanganywa kirahisi kama eva alivyodanganywa pale bustanini na nyoka, unataka kumaanisha kwamba huo mdoli utakuzalia watoto?
Na, kama unakwepa gharama kuna kitu hakipo sawa kwenye mfumo wa ubongo wako, kwani wewe mwenyewe hautumii gharama?
Je, unatumia shingapi kama bajeti ya kula kwa siku?
Je, huo mdoli utaulisha? Actually ni hapana, lakini mwanamke atakula...
Sasa kama wewe mwanaume una gharama za kula, kwa hiyo mwanamke wako unataka nani amlishe?
ACHA kupenda mteremko maisha hayapo hivyo hata siku moja.
Unamuona mwanaume yuko smart sana, anapiga suti Kali, barabarani anatembea kwa madaha kumbe ndani anaishi na mdoli hahaha inasikitisha sana....
My brother mdoli utakufanyia nini kingine zaidi ya sex?
Kwa hiyo unataka kumaanisha Muumba wetu kutuumbia wanawake wa nyama alikuwa ni mpumbavu na alikuwa hajielewi ama?
Unahitaji kufikiri juu ya hili my brother, na kama ulikuwa una mpango wa kuja kununua hiyo midoli hebu acha upumbavu wewe hukuumbwa uje uwe mtumwa wa ngono!
Kadhalika maendeleo ya sayansi na teknolojia yamewatengenezea watu wengi sana wajione kuwa wao sex ni kila kwao na hakuna kingine wanaweza kufanya zaidi ya sex hapa duniani!
Ingia kwenye website mbalimbali, kila mahali yametapakaa maponi pamoja na video za ngono, nowadays wanatumia hata intanet pamoja na vyombo mbalimbali vya habari ili kueneza ushoga lengo likiwa tu kupandikiza mtizamo wa sex mentality akilini mwa watu, ambapo mwishowe wataanza ili kuona sex ni kila kitu kwao!
Mpenzi, unatakiwa kujua kwamba kile kinachoingia ndicho kitapima kile kitakachotoka, kwamba kama kila siku utakuwa unaingiza taarifa kuhusu sex, mawazo utakayotoa hayatakuwa nje na eneo la sex, hii inamaanisha kwamba utakuwa mtumwa wa ngono na utakuwa mtumwa kweli kwa maana umejiona hivyo.
Usiruhusu maendeleo ya sayansi na teknolojia yakufanye uwe mtumwa wa ngono my friend.
Unapowaza jana nilikuwa na nani, leo nitakuwa na nani au nitafute laki tatu nikanunue dawa ya kujichubua, ndivyo unavyozidi kujifirisi na kumtajirisha mwenye kampuni inayotengeneza madawa hayo!
Leo nakusanua tu, kuna watu waliishi kabla ya sayansi na teknolojia kuja na walifurahia maisha!
Pia, ni vema ukafahamu kwamba hakuna jipya chini ya jua!
Hata haya yanayofanyika, yalishafanyika na yatafanyika, hii inamaanisha kwamba wewe siyo kwanza kuyafanya.
Kwa mantiki hiyo usiruhusu ujinga ulioletwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia ukuendeshe!
Usihangaikie sana mwili kisa ngono, kumbuka huo mwili utakuja kuzikwa hapa chini maana u mavumbi wewe na mavumbini utarudi usijifanye hulijui hili, mimi nakusanua tu.
Kasome yakobo 4:4 pamoja na 1 petro 3:3 kuna ujumbe wako.
Achana na sex mentality, jione ukileta mchango mzuri kwenye jamii yako!
Je, kupitia sex unaleta, mchango gani zaidi ya kupata maradhi, kufirisika na kupata laana na mikosi?
Mungu hakukuumba kwa ajili ya hilo! Tafuta kusudi la kuumbwa kwako my friend!
Usiruhusu sayansi na teknolojia ikuendeshe bali itumie kwa manufaa uweze kubadili jamii yako na taifa lako!
Je nini nifanye ili nibadili mtizamo wangu juu ya namna ninavyojiona?
Usijalii utajifunza kwenye mwendelezo wa somo hili kwenye makala zijazo!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika eskingunge.blogspot.com
Tags
Elimu