JINSI YA KUTENGENEZA PEANUT BUTTER - SIAGI YA KARANGA
Mahitaji Ya Kutengeneza Peanut Butter
1. Karanga vikombe 2
2. Asali au sukari kijiko 1 na nusu cha chakula
3. Mafuta ya kupikia kijiko 1 na nusu cha chakula
4. Chumvi ½ kijiko cha chai
Jinsi Ya Kutayarisha Peanut Butter
1. Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe
2. Ziache zipoe kisha toa maganda
3. Mimina karanga,chumvi na mafuta katika blender ama food processor...saga hadi iwe laini
4. Ongeza asali, chumvi, sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini...
5. Hifadhi katika chupa yako kisha weka kwenye FriJi
NB ; UKILA NA MKATE USISHANGAE KUSIKIA KITU KINAKUAMBIA UKANUNUE MKATE MWINGINE MZIMA
Tags
Jikoni