MASKINI JEURI.
Mwandishi:Idd J. Rashid.
Sehemu ya 01.
Ilikuwa ni majira ya asubuhi ambapo kijana Idd halimaarufu kwa jina la jitu jina alikuwa akijiandaa ili kwenda katika kazi yake ya kuuza matunda aliyokuwa akiifanya kila na kumuingizia kipato kilichokidhi mahitaji yake ya kila siku.Idd ama jitu kwa jina lake la utani alipigwa mswaki harakaharaka akaoga pamoja na kuvaa nguo zilizomkaa vizuri na kumpendeza sana japo nguo zile zilionyesha kuanza kupoteza rangi yake ya asili lakini zilimpendeza kutokana na udobi mahiri aliozifanyia nguo zile.mara baada ya kuvaa vile akachukua kipisi cha kioo pamoja na kitana kisha akachana vizuri nywele zake huku akijitazama kwenye kioo na mara baada ya kuchana akaendelea kujitizama kwa muda kisha akatabasamu na kujiambia mwenyewe.
"Japo maskini ila napendeza na kuonekana kijana wa sasa hata nikiingia mtaani hakuna yeyote atakayejua kama huwa nina maisha magumu!"
Jitu alizungumza maneno yale kisha akacheka peke yake huku akijitazama kwenye kioo kisha akakiweka pembeni na kupiga magoti chini kwenye simenti iliyochimbika akakitanisha mikono yake kwa pamoja na kuanza kuanza kuzungumza tena.
"Eee mwenyezi mungu nakuomba unisaidie siku ya leo iweze kuwa ni siku njema kwangu na yenye bahati kubwa maishani mwangu.mguu nitakoutoa hapa uujalie neema kibao na mafanikio makubwa.Eee mwenyezi nakuomba uniepushe na shari zote za waja wako na unijaalie kipato kikubwa katika biashara yangu amen!"
Jitu alitamka dua ile kwa hisia sana kisha mara baada ya kumaliza akasimama na kutoka ndani ya chumba chake kilichokuwa ni miongoni mwa vyumba viwili na sebule vya nyumba yao ya mgongo wa tembo.nyumba ambayo alikuwa akiishi yeye na mama yake pamoja na mjomba wake mdogo aliyekuwa akiitwa Juma.
"Shikamoo mama!"
Jitu alimsalimia mama yake aliyekuwa akipika vitumbua vya biashara aliyokuwa akiifanya kwa kipindi kirefu sana.
"Marhaba mwanangu umeamka salama!"
"Mi namshukuru mungu nipo buheri wa afya hofu kwako wewe na anko?"
"Anko wako hajambo tu ila bado kalala si unajua tena ni boss mtarajiwa aliyekosa kitambi tu!"
"Hahaha! Sawa mama mi ngoja niende kwenye mihangaiko!"
"Sawa mwanangu mungu akusimamie kila utakachoshika kigeuke dhahabu na kukuletea tija!"
"Sawa mama yangu nakupenda sana!"
"Nakupenda pia mwanangu!"
Jitu alizungumza maneno yale huku akitoa kiasi kadhaa cha pesa na kumkabidhi mama yake aliyekuwa akipika vitumbua na kuondoka zake.
Mara baada ya jitu kuondoka alielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa mama saida kwani alikuwa akimdai kiasi kadha cha fedha kutokana na kumfanyia kazi za usafi nyumbani kwake siku moja iliyopita lakini akaahidiwa kulipwa asubuhi ya siku iliyofuata.
Alifika getini kwa mama saida na kubonyeza kengele iliyompelekea mlinzi afungue geti.
"Mambo vipi kaka!"
"Freshi tu jitu mbona asubuhi sana!"
"Nimekuja kumcheki huyu mama hapa nina miadi naye kidogo!"
"Ah sawa basi pita ndani!"
Jitu akapita ndani na kwa bahati nzuri akafanikiwa kumkuta mama saida mwenyewe akiwa nje japo alikuwa ndani ya tenge moja tu.
"Mama shikamoo!"
Jitu alimsalimia yule mwanamama kwa heshima
"Safi tu mambo!"
Mwanamama yule ambaye alionekana kuwa na rika la mama yake jitu aliitikia salamu ile jinsi alivyojua mwenyewe lakini wala haikumshamgaza wala kumshtua jitu kwani alizoea mambo hayo kutoka kwa mwanamama yule.
"Safi tu mama sasa nimeijia mzigo wangu!"
"Ooh! Mzigo wako nakumbuka vema sana na nimeshauandaa kwa ajili yako pita ndani tafadhali ili nikukabidhi!"
Jitu aliposikia maneno hayo akahisi kama kuna kitu hakipo sawa.
"Usijali mama wewe niletee tu hapa wala hamna shida nitasubiri!"
"Usijali bwana jitu au unaogopa? hebu njoo ndani bhana kwanza hapo nje kuna kibaridi sana wewe njoo ndani!"
Mwanamama alijaribu kumshawishi jitu kuingia hadi akaamua tu kuingia kwani alikuwa na shida ya pesa yake.
Mara baada ya kuingia ndani mwanamama akaelekea moja kwa moja hadi chumbani kwake huku akimuacha jitu akishangaashangaa kwenye sebule ya kisasa iliyopendeza sana.dakika chache baadae mwanamama akarudi sebuleni huku mkononi akiwa kashikilia kiasi cha pesa kilichobanwa vema na rubber band.
"Jitu jisikie upo huru hapa ni sawa na nyumbani kwako maana wewe ndiye ulipaswa kuwa mume wangusi unajua vile ninavyokupenda!"
Yalikuwa ni maneno ya mama saida yaliyoambatana na mitego kibao iliyolenga kumnasa jitu lakini jitu wala hakuonyesha kutegeka kwa aina yoyote.
"Mama nipatie pesa yangu ninawahi huko mjini nikafungue kabanda changu!"
Jitu alizungumza kwa sauti ya kawaida kabisa.
"Usijali jitu kuhusu hii siku ya leo wewe hata ukiipoteza ni sawa tu kwani nimejipanga kukupatia kiasi cha pesa ambacho sidhani hata kama umewahi kukishika wewe ishi na mimi tu walau kwa hii siku moja ambayo mume wangu kasafiri nipe kile kitu moyo unapenda tafadhali jitu nakupenda mnoo!"
Mama saida alizungumza huku akimsogelea jitu kwa ukaribu kabisa na kutaka kumkalia mapajani lakini jitu akawahi kumkwepa na kusimama kwa haraka kisha akachukua moja ya kati ya vile vibunda vitano vya hela na kuhesabu noti tatu za shilingi elfu kumi kisha akatoka mule ndani kwa kasi ya ajabu na kwenda zake huku nyuma akimuacha mwanamama kaduwaa asiamini kilichokuwa kikitokea.
"Vijana wengine wa ajabu sana yani hakana pesa kamaskini lakini kanakataa vibunda vya pesa pamoja na utamu mh! Sawa bhana lakini sitakoma kumfuatilia nitamuwinda kila pande hadi nimpate maana siyo kwa uzuri ulena siyo kwa mvuto ule alionao japo maskini ila anang'aa!"
*** ***
Majira ya saa tano asubuhi mwanadada mrembo aliyejulikana kwa jina la morin alikuwa ndani ya gari yake ya kifahari akikatiza maeneo ya uswahilini.
Aliendesha gari yake kwa mwendo mdogomdogo katika barabara ya vumbi huku akiwa makini sana kukwepa mashimo ya hapa na pale.kila aliyekuwa akiiona gari yake aliitolea macho hadi ilipoishia lakini morin mwenyewe wala hakujali kuhusiana na hilo yeye aliendelea na safari yake ambayo hakufanikiwa kuimaliza kwa gari kutokana na sehemu aliyokuwa akienda ilikuwa ndanindani sana hivyo ilimlazimu kupaki gari yake pembeni ya barabara kisha akaingia vichochoroni na kuanza kukatiza pasipo kujali chochote.
"Sijui huyu mama nitamkuta au atakuwa ameshahama ngoja tu nifike ili ikiwezekana nijue hali yake ya kimaisha ikiwezekana nimtoe huku maana msaada alionipatia wakati ule ni lazima niulipie fadhira!"
Morin alizungumza mwenyewe huku akizidi kukatiza chocho kwa chocho.
***** ******
Wakati huohuo jitu alikuwa katika kibanda chake cha kuuzia matunda na alikuwa akifikiria kufuata mzigo mwingine wa matunda kwani ule aliokuwa nao ulikuwa ukielekea kuisha.
"Mungu amenionyesha ukuu wake mapema tu sasa hapa itabidi nifukuzie tu mzigo mpya!"
Jitu alizungumza mwenyewe huku akifunga kibanda chake na kuanza kuondoka kwa mguu kuelekea sokoni lakini kabla hajafika mbali akasikia mlio wa simu yake ukilia.
"Mama shikamoo...! eeh amekuja tena huyo mama...! si anatudai shilingi elfu tano tu lakini?..basi nakuja hapo nyumbani sasa hivi mama yangu mwambie atulie tu pesa yake ipo njiani"
Simu ikakatwa kisha jitu akageuza njia na kuanza kurudi nyumbani kwani hapakuwa mbali sana.
*** ****
Upande wa morin yeye aliendelea kukatiza vichochoro vya uswahili kwa kujiamini akiwa hana hili wala lile ghafla akazungukwa na kundi la vijana takribani sita waliokuwa na visu vilivyokuwa na kutu huku mwingine mmoja akiwa na kopo lililojaa kinyesi vijana wale walimuogofya sana morin kiasi cha kumfanya awe na wasiwasi mkubwa.
"Sasa dada mzuri kama wewe unatafuta nini kitaani hapa au umekosea njia?sasa kama umekosea njia basi furaha kwetu sasa leo lazima tukufanye nyama yetu na hivi upo mzuri!"
Ilikuwa ni sauti nzito ya moja ya vijana wale alioleonekana kama kiongozi wa kundi.
"Unasubiri nini mkuu hebu msaule chap tu si tujilie vitamu!"
Kijana mwingine alizungumza na kumfanya yule kiongozi wao ashike gauni aliyoivaa morin na kutaka kuivuta kwa nguvu lakini kabla hajafanya hivyo akapigwa jiwe la kichwa na mtu ambaye hawakuelewa alifika muda gani eneo lile.
Jiwe lile lilimpelekea yule jamaa aanze kuvuja damu huku wale wenzie wakimgeukia yule aliyerusha jiwe ambaye hakuwa mwingine ila ni jitu.
"Mbwa nyie kama mmeshindwa kutafuta hela msiwafanye raia wakakosa amani!"
Jitu alizungumza kwa kujiamini sana kiasi cha kumpelekea morin ahisi kama amepata mkombozi wa kumuepush na kubakwa.
"Mpuuzi huyo mpelekeni ICU au kama vipi mumyeyusheni kabisa!"
Ilikuwa ni amri iliyotolewa na yule jamaa aliyepigwa jiwe amri ambayo iliwapelekea wale vijana wote waandae silaha zao vema kisha wakaanza kumfuata jitu kwa kasi kwa lengo la kumshambulia kwa silaha zao.
ITAENDELEA.
Je, unafikiri ni kipi kinafuata..jitu ataweza kukabilina na hao vijana au ndiyo anajichimbia kaburi lake mwenyewe? Vipi kumuhusu morin yeye ni nani haswa na alifuata nini kule uswahilini ikiwa maisha yake ni safi???Nakusihi tu usikose sehemu inayofuata ya simulizi hii kali na ya kipekee sana.
Tags
simulizi