TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

𝗧𝗛𝗘 𝗦𝗛𝗔𝗧𝗧𝗘𝗥𝗘𝗗 𝗗𝗥𝗘𝗔𝗠𝗦 𝗔𝗡𝗗 𝗦𝗜𝗟𝗘𝗡𝗧 𝗟𝗘𝗦𝗦𝗢𝗡𝗦

𝗛𝗔𝗗𝗜𝗧𝗛𝗜 𝗙𝗨𝗣𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗦𝗜𝗦𝗜𝗠𝗨𝗔

𝗧𝗛𝗘 𝗦𝗛𝗔𝗧𝗧𝗘𝗥𝗘𝗗 𝗗𝗥𝗘𝗔𝗠𝗦 𝗔𝗡𝗗 𝗦𝗜𝗟𝗘𝗡𝗧 𝗟𝗘𝗦𝗦𝗢𝗡𝗦

𝗕𝗬 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜
Hapo zamani za kale alikuwepo binti mmoja wa miaka 19 jina lake aliitwa Anna, alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja wa miaka 29 jina lake aliitwa Ali

Ali alimpenda sana Anna kwa dhati ya moyo wake kiasi kwamba hawezi tafuta mtu mwingine, alimpenda na kumpa kila anachohitaji ili kudumisha upendo wao

Upendo wao ukazidi kuimarika, Anna akaanza kuona ndoto ya kuolewa na Ali, alimuona ndio mtu wa pekee katika maisha yake, Ali alimuamini Anna halikadhalika

Muda unavyozidi kusogea, Anna akaanza kugundua kitu ambacho amefichwa na Ali baada ya kuona mipango ya ndoa haipo na haizungumziwi tena, kitu hiki kilimpa sana wasiwasi Anna

Anna akagundua ni mjamzito, hakuwa na furaha baada  kuona mpenzi wake amebadilika, ukweli aliokuja kugundua hapo baadae ni kwamba Ali tayari amefunga ndoa na mwanamke mwingine jina lake anaitwa Wivina ambaye amezaa nae mtoto mmoja

Anna akasalitiwa, alivunjika moyo sana na kujiona hana thamani yoyote na kupoteza matumaini baada ya kujua ukweli uliokuwa umejificha katika maisha ya Ali, akaanza kujihisi ni mkosefu, alijilaumu sana

Anna akajisikia vibaya lakini yote alimuachia Mungu, akabaki kuwa single mother. Akafanya maamuzi yenye busara na hekima kukubali changamoto hiyo na kumlea mtoto wake kwa maadili ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo, familia yake ilimuunga mkono pia lakini safari ilikuwa ngumu sana

Licha ya changamoto alizopitia alisimama imara, alijiendeleza zaidi kielimu katika kutimiza na kupambania vipaumbele vyake ili mtoto apate haki zake za msingi. Kujituma kwake kulihamasisha wengine zaidi katika jamii

Anna akakutana na mtu mwingine aliyemuheshimu, kujali na kutii na kuunga mkono ndoto zake. Uhusiano wao ulilenga zaidi kuelewana na kuheshimiana tofauti na uhusiano wa zamani na Ali

Anna akapigania haki za mabinti wengine katika jamii, kutoa ushuhuda wake kuwaelimisha wengine kuhusu umuhimu wa kujiheshimu, mawasiliano imara na kuweka mipaka katika mahusiano

Anna anaakisi safari yake na somo alilolipata. Ametambua umuhimu wa kujiheshimu, mawasiliano imara na kuweka mipaka katika mahusiano. Hadithi yake imekuwa taa na mwangaza wa matumaini na elimu kwa wengine waliopitia changamoto kama yake...!

𝗛𝗔𝗗𝗜𝗧𝗛𝗜 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗨 𝗜𝗠𝗘𝗜𝗦𝗛𝗜𝗔 𝗛𝗔𝗣𝗔

𝗨𝗝𝗨𝗠𝗕𝗘

"Heshima, mawasiliano imara na kuweka mipaka katika mahusiano ni muhimu zaidi"

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post