DIANA
(Kisa cha kusisimua)
Ilikuwa Ni Saa 10 Na Nusu Jioni Kwenye Kiwanda Cha Usambazaji Nyama
.
Diana Siku Hiyo Alikuwa Wa Mwisho Kuondoka Kazini Alikuwa Akimalizia Kufungasha Nyama Zilizokuwa Zimechinjwa......
.
Baada Ya Kumaliza Kazi Ya Kufungasha Diana Alifungua Mlango Wa Chumba Hicho Na Kinyanyua Hatua Kutoka Kwenye chumba Cha Kufungashia Na Kuelekea Kwenye Chumba Cha Kihifadhia (Cold Room) Chumba Chenye Baridi Kali Kuzifanya Nyama Zisioze............
.
Diana Alifungua Mlango Wa Cold Room Na Kuingia Ndani!!!!!!
.
Ile Anamaliza Mguu Wa Mwisho Tu Kuingia Ndani Mlango Ulijibamiza Na Kujifunga, Lakini Diana Hakukali Chochote Kwa Kuwa Alikuwa Ameshikilia Nyama Mkononi.....
.
Baada Ya Kuweka Nyama Diana Alirudi Mlangoni Kufungua Mlango Ili Atoke Nje Lakini Alichokutana Nacho Hakuamini Macho Yake.........
.
Mlango Ulikuwa Umejiloki!!!!!!
.
Mapigo Ya Moyo Wa Diani Yalianza Kwenda Mbio Kama Gari Bovu Huku Huku Akihema Juujuu Kama Utu Alikuwa Anakimbizwa............,.
.
Diana Alijaribu Kufungua Mlango Ule Kwa Kila Namna Lakini Waapi Juhudi Zake Ziligonga Mwamba Alijaribu Kupiga Mateke Ili Angalau Avunje Mlangoni Lakini Bado Aliambulia Patupu..........
.
Diana Alijaribu Kupiga Kelele Kuomba Msaada Lakini Hakukuwa Na Mtu Maeneo Yale Wafanya Kazi Wote Walikuwa Wameshaondoka Na Vile Vile Sauti Ilikuwa Inatoka Kwa Uchache Sana Kiasi Kwamba Mtu Akiwa Mbali Kidogo Tu Hawezi Kusikia....,...
Baada Ya Kama Masaa Matatu Hivi Diana Alikuwa Amezidiwa Na Baridi Ya Chumba Kile Na Kuanguka Chini Huku Akisaga Saga Miguu Chini Mwili Ulikuwa Umeishiwa Nguvu Na Karibu Ya Kuganda Hakukuwa Na Msaada Wowote.............
.
Katika Hali Isio Tarajiwa Mlizi Wa Geti Wa Kiwanda Kile (Mr Juma) Alitokea Na Kuvunja Mlango Wa Chumba Kile Na Kumuokoa Diana Na Kumuwahisha Hispitali Haraka Sana..............
.
Hadi Kufikia Majira Ya Saa 4 Hivi Usiku Diana Alirudisha Fahamu........
.
Baada Ya Diana Kurudisha Fahamu Alimwita Mlinzi Yule Na Kumuuliza "Juma Ulijuaje Nipo Ndani Ya Cold Room Na Kuja Kuniokoa Wakati Wewe Kazi Yako Ni Kulinda Getini Tu Na Wala Sio Kawaida Yako Kuingia Ndani Ya Kiwanda???"
.
Juma Alijibu!!!!!
.
"""""Kiukweli Nimekuwa Nikifanya Kazi Hapa Kiwandani Huu Ni Mwaka Wa 21 Sasa Maelfu Ya Wafanya Kazi Wanakuja Na Kuondoka..................
.
Kila Asubuhi Wafanya Kazi Wanapita Getini Wanaingia Ndani Na Jioni Kutoka Lakini Wewe Ulikuwa Ni Mtu Pekee Ulikuwa Kila Asubuhi Ukipita Getini Ulikuwa Ukinisalimia Kwa Kuniambia Habari Za Asubuhi Juma! Umeakaje!!! Na Pindi Unapoondoka Jioni Ulikuwa Hipiti Bila Kuniaga Kwa Kuniambia Juma Kwaheri Tutaonana Kesho...........
.
Wafanya Kazi Wote Walikuwa Wakinipita Kana Kwamba Mimi Ni Sanamu Nimekaa Getini Au Ni Mtu Nisie Onekana.........
.
Leo Pia Ilikuwa Kama Kawaida Yako Ulipita Asubuhi Na Kunisalimia, Kufika Jioni Baada Ya Saa Za Kazi Nilikuwa Nikiisubili Kwaheri Yako Kwa Hamu Kubwa Lakini Hadi Kufika Saa Moja Usiku Katika Hali Isio Ya Kawaida Sikupata Kusikia Sauti Yako Ikiniaga.............
.
Ile Salamu Yako Kila Asubuhi Na Kwaheri Yako Kila Jioni Ilikuwa Ikinifanya Na Mimi Nijione Ni Mtu Na Nilivyoikosa Jioni Ya Leo Niliona Kama Kumpungukiwa Na Kitu.........
.
Na Kuhisi Labda Kuna Kitu Hakiko Sawa..............
.
Ndio Maana Niliamua Kuingia Ndani Na Kuona Nini Kinaendelea
.
Baada Ya Kuingia Chumba Cha Kufungasha Nyama Nilikutana Na Kibegi Chako Ndio Nikahisi Upo Ndani......
.
Baada Ya Kuita Bila Ya Mafanikio Na Kuingia Kila Chumba Sikukuona
.
Nikaja Kwenye Cold Room Na Kujaribu Kufungua Mlango Lakini Haukuwa Unafunguka Na Baada Ya Kutega Sikio Mlangoni Kwa MAKINI Nikahisi Kama Kuna Mtu Anasaga Saga Miguu Chini.......
.
Na Ndio Kilichomifanya Kuvunja Mlango Kuona Kuna Nini Kinaendelea Ndani Na Kwa Bahati Nikakukuta Wewe........""""
.
Funzo
.
Kuwa Mwenye Huruma Na UPENDO Na Muheshimu Kila Mtu Anaekuzunguka.....
.
Vile Vile Ni Muhimu Kusalimia Watu Unao Kutana Nao Njiani Kwani Huwezi Jua Linaloweza Kukupata Hata Dakika 10 Zijazo Kutoka Sasa.......
.
IMEANDALIWA Na Ali Issa
Tags
Visa vya Kusisimua