Hivi Uliwahi Kusikia STORI ya Wale Mabinti 30 waliolelewa Pamoja........?
Kwanza kabisa tunaoneshwa wasichana watatu wakiwa Juu ya ghorofa wakionekana kupanga mpango wa kuliteka Gari lenye dhahabu.
Tunaambiwa kuwa mabinti hawa ni sehemu ya uzao wa mabinti 30 ambao walizaliwa miama 23 iliyopita. Swali je, ni kwanini wajitenge? Kwanini wanataka gari la dhahabu?
SIMULIZI HII NAITOA BURE SIKU YA LEO......
Movie inaanza; Walikuwa Mabinti 30 ambao wametoka katika mazingira magumu, kisha mtu anayeitwa Don Milla, alimchukua kila mmoja akamfundisha mambo mbalimbali, elimu ya sanyasi, uchumi na teknolojia ilikuwa katika kila kichwa cha mabinti hawa. Miongoni mwa vitu alivyowafundisha ilikuwa ni pamoja na mapigano kwa sababu alitaka kuwatumia katika kazi zake za uuzaji wa madawa ya kulevya, kuteka watu pamoja na kufanya uharifu katikati ya Jiji.
Miaka 23 mbele, Rose anaona kama anamtumikia mtu ambaye amlipi chochote. Anahitaji kuwa huru na kuyaanza maisha yake, anawaambia wasichana wengine wawili (Farida na Xiomara) kwamba wamefanya kazi kwa muda mrefu chini ya Don Milla bila kulipwa kiasi chochote hivyo ni muda wa wao kuondoka kama ikiwezekana wakaanzishe kundi lao ambalo litafanya kazi kama wanayoifanya kwa Don Milla.
Nani wa kwenda kwa Don Milla kumueleza kwamba wameamua kuachana naye? Walimfahamu Don sio mtu wa masiara linapokuja suala la maslahi ya GENGE lake. Mwisho Rose anajitoa mhanga, anakwenda kumtaarifu Don kwamba wanampango wa kuondoka. Don Milla anafikiria kwa muda kisha anawapa 'Go ahead' lakini anawasihi, isitokee siku wakaingilia biashara zake iwe kwa hiyari yao ama wametumwa na mtu kwa sababu atakachowafanya hakitakuwa na mswalie mtume. Maiti zao zitachomwa moto katika mnara wowote ndani ya Jiji.
Rose, Farida na Xiomara wanaondoka katika ngome iliyowalea kwa miaka 23. Wanachomoka kwa Don Milla huku wakiwaacha wasichana wengine 27 ambao waliamua kubakia katika mikono ya Don kwa sababu walikuwa na hofu kama wakiondoka wote basi Don angewatafuta na kuwaua.
Jioni moja, wakiwa katika Jumba Kubwa, Rose anawaambia wenzake kwamba lazima wawe matajiri kupitia Don Milla na kuna Gari la dhahabu linaaafirishwa na vijana wa Don Milla. Wafanye juu chini wahakikishe kuwa wanateka gari hilo na kupata dhahabu.
Wenzake wanakataa kwa sababu walijua kuwa kuteka gari hilo ni sawa na kumshika makende Don Milla lakini Rose anawashawishi. Hakukuwa na wakupinga, wote wanakubali kwenda kuliteka gari ambalo limebeba dhahabu za Boss wao wa zamani, mmiliki wa genge la Kiharifu.
Wanafanikiwa kuiba gari la dhahabu lakini Rose anawageuka, kwanza anampiga risasi ya kichwani Farida kisha anaondoka na gari la dhahabu huku akidondosha kidani chenye Jina la Xiomara.
Anafanya hivi akiwa na uhakika kuwa atakayeokota Kidani ni lazima atajua kwamba aliyefanya wizi na uharifu ni Xiomara. Wazo lake linatiki, Kidani kinaokotwa na Don Milla. Naye anasema SIOMARA atafutwe popote ulimwenguni.
Xiomara inabifi amtafute Rose kwa hudi na uvumba ili kulipa kisasi cha ndugu yake yaani FARIDA ambaye amepigwa risasi.
Kumbuka Xiomara sio aliyechukua gari la dhahabu bali ni Rose. Je, Siomara atakubali kutupiwa msala sio wake? Atapatikana akiwa hai ama amekufa?
Riwaya inaitwa XIOMARA ANATAFUTWA ina kurasa 487. Niliyeandika ni mimi nafahamika kwa jina la Sam Darfur. Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi Bora wa mwaka 2024 kupitia tuzo za Simulizi Club.
Naomba niitoe bure siku ya leo kwa watu 200 tu wa mwanzo. Njoo WhatsApp kisha andika XIOMARA. Tafadhari, andika hivyo inatosha usiweke neno lingine. Namba ni 0717255498.
Tags
simulizi