Love doesnt ask why...it comes from the heart..nevre express..dont you know that love..doesnt think twice.." simu ya mkononi ilikua ikiita mfululizo na nyimbo tamu ya mwanamama celine dion iliyokua imesetiwa kama ringtone ilimfanya kijana mtanashati Abel kuuendelea kuuchapa usingizi vilivyo bila kujali simu aliyokua akipigiwa. Muito wa simu uliendelea kwa sauti ya juu iliyochanganyika na vibration na hivyo kutokeza kelele zilizobadilika na kua kero. Abel anajivuta na kupapasa kitandani kwa uchovu anachukua simu na
kuisogeza karibu na uso wake " Namba ngeni washaanza pumbav" anasema kijana abel kwa sauti ya uchovu na kisha kuitupia sim pembeni na kuendelea kuuchapa usingizi. "Love...doesnt ask why...it comes from the heart..never..express" inaita tena simu kwa sauti ya juu, abel anaivuta na kuitazama "emmy" jina linasoma katika screen "nilijua tu ah" anajisemea kijana abel na kuitupia tena simu kitandani na kuendelea kuuchapa usingizi. "love doesnt ask why.... simu inaendelea kuita bila kuchoka licha ya kupuuzwa. safari hii abel anaamua kuachana nayo kabisa na polepole utamu wa nyimbo ya celin dion unamnogea na kumpeleka katika usingizi mnono. lakini ghafra usingizi mtamu ukiwa ndo unaanza kumnogea kijana abel " NGO NGO NGO! mlango unagongwa kwa nguvu. abel anashtuka na usingizini na kusikilizia anapoona kimya anarudi kulala NGO NGO NGO NGO NGO! mlango unagongwa tena kwa nguvu zaidi! abel anajivuta na kuamka taratiibu na kujinyoshanyosha, kisha kinyonge anashuka kitandani na kuanza kutembea kuelekea ulipo mlango. anafika na kushika kitasa....anapofungua.."aah ona sasa" anasema kwa hasira kijana abel "tunasumbuana tu mtu anagonga kwa nguuvu mpaka watu tuajua ni sisi tunaogongewa milango kumbe mtaa wa sita bwana" anasema akiwa anafunga mlango baada ya kugundua mgongaji alikua anagonga kwa jirani yake na sio kwake. anarudi kiuchovu mapaka kitandani na kuinyanyua simu yake "16 missed calls 12sms" screen inasoma. anaamua kufungua missed call na kunza kushuka chini emmy..emmy..emmy..witi..witi...manka...majina ya waliopiga yalisomeka hivyo...vanillah..joy..Ajira mwenge.."MMAMAAA" alishtuka kijana abel baada ya kukutana na jina "ajira mwenge"!
%Love%Love%Love%
"I LOVE YOU DAD" anatamka binti mdogo mrembo akiwa amemkumbatia baba yake kwa nguvu na kummiminia mabusu ya mfululizo mashavuni. "i love you too daughter" anasema mzee mrefu kidogo mwenye rangi ya majikunde na kurudisha mabusu kwenye mashavu ya binti. " hakikisheni mnamfikisha salama na kumrudisha..nafikiri mnafahamu jinsi hari ya kisiasa ilivyo hapa nchini ni hatari mno..mnanipata!? anasema mzee yule kwa msisitizo akiwa amewageukia vijana kadhaa waliovalia suti nyeusi maridadi zikiendana na miwani zao nyeusi zilizofanya waonekane maridadi zaidi. "usijali mheshimiwa rais tutamrudisha salama" anasema mmoja wa wale vijana na kutoa saluti kwa mzee na kufuatiwa na wenzake pia ambao nao waliotoa saluti kwa mzee na kisha kumfunfulia mlango wa gari binti na safari ikaanza toka ikulu. gari inapoondoka mzee ananyanyua simu anabofya namba kadhaa na kuweka sikioni. "halo..eeh njema..binti yangu amependa aje hapohapo kituoni kwako badala kwa hiyo huna haja tena ya kuja huku ila tu hakikisha unamfanyia checkup vizuri mana analalamika macho yanamsumbua sana" anamaliza kutoa maelekezo kwa daktari na kukata simu kisha anaduwaa kidogo akiwa ameshika kidevu kama anayefikilia kitu fulani kisha anagutuka na kuamua kuingia ndani
%Love%Love%Love%
Kijana Abel anakimbia anaitupa simu kitandani na kuvua nguo kwa haraka..anajifunga taulo na kuchukua ndoo ya maji haraka anakimbilia yalipo madumu matano ya maji madumu pekee yaliyopo chumbani kwake..ananyanyua dumu haraka amimine maji "loo patupu" dumu halikua na maji analilusha pembeni na kutingisha la 2 patupu..la tatu patupu...la nne..patupu..kabla hajatingisha la tano anakumbuka kuwa maji yote yaliisha jana usiku na hakuweza kwenda kuchota mengine kwani muda ulikua umeenda. "mama yangu na nimeshachelewa" anajisemea kwa sauti ya kukata tamaa. "aah nitavaa hivyohivyo nani atajua kama sijaoga.." anajisemea abel na haraka analikimbilia lilipo begi lake dogo la nguo na kuanza kupekua "mamaa nguo zote chafu" anasema kwa mshangao "nimekwisha" anasema huku akiendelea kupekuapekua begi na ndipo hatimae anafanikiwa kukoropoa shati jeupe safi na suruarl nyeusi zilizokua zimejikunja vilivyo."afadhali" anajisemea na haraka anakimbilia ilipo pasi anatandika shuka kitandani na kuwasha pasi na haraka anaanza kunyoosha shati kwa spidi. lakini anapomaliza kunyosha mkono mmoja na ubavu mmoja pasi inazimika."nini tenaa" anasema kwa uchungu kijana abel. anajaribu kuwasha na kuzima switch wapi pasi haiwaki. akiwa katika zoezi la kuwasha na kuzima switch ndipo anakumbuka kua umeme ulikua umebakia units 0.11 jana usiku hivyo ni dhahiri kabisa umeisha. "anachoka kijana na kujitupa kitandani kwa nguvu. lakini ghafra anagutuka"nitavaa hivyohivyo potelea mbali kazi ni muhimu zaidi acha nichekwe kwa leo tu lakini nikifanikisha kazi pale haya yote yatabaki historia ila daah ningejua ningeamka kipindi kile simu ilipokua inaita dharau zingine hizi bana" anajisemea abel huku tayari akiwa ameshamaliza kuvaa suluari..anavaa shati na kisha anainama uvunguni mwa kitanda na kuvuta raba nyeupe safi. "anatabasamu kidogo anapoona laba ni safi tena zinan'aa mno. anavaa haraka anajiangalia kwenye kioo na kujiweka sawa kidogoanachukua simu yake kitandani na kutoka hara anafunga mlango wake kwa kufuli dogo na kuondoka kwa spidi."looh sijapiga hata mswaki" anajisemea akiwa anaelekea kituo cha daladala. "aah potelea mbali si leo tu kwanza jana usiku nilipiga kabla ya kulala" anajifariji na kuendelea kwenda spidi kuelekea kituoni safari hii akikimbia.
%Love%Love%Love%
"I love you so much dad" anasema binti mchanga mrembo huku akimkumbatia kwa bashasha mzee wa makamo kidogo! "I love you too daughter" anajibu mzee yule huku wakiwa wamekumbatiana tukio lililofuatiwa na mabusu kemkem kama ishara ya upendo wa dhati baina ya wawili hao! "see you dad and am gonna miss you a lot" anasema bint yule kabla hajafunguliwa mlango wa gari aina ya toyota vx nyeusi! "me too daughter" anajibu mzee na kisha kuwageukia kundi la vijana waliovalia full suti nyeusi. "nafikili mnafahamu huu ni wakati wa uchaguzi na hivyo harinya kisiasa hapa nchini si nzuri...hivyo bas hakikisheni mnakua makini nahitaji binti yangu arudi salama hapa sawa!? anazungumza mzee msisitizo. "sawa muheshimiwa" anajibu mmoja wa vijana wale na kisha wote wanapiga saluti na kuingia kwenye magari tofauti.safari inaanza.
%Love$ Love%Love%
Abel anafika kituoni na kukuta umati mkubwa wa watu wakisubiri usafiri huku wengine wakigombania kwa nguvu kuingia kwenye baadhi ya mabasi yaliyokua yakiingia kituoni hapo." Duh hapa ntachomoka kweli hili nyomi" anajisemea abel kimoyomoyo huku akiwa tayari kashaungana na umati mkubwa kusubiri basi lenye unafuu.mabasi yaliyokua yakija mojamoja ni wenye nguvu pekee ndio waliokua wakifanikiwa kuingia tena kwa mikiki mizito. Abel akiwa amesimama akisubili gari mawazo yake yanampeleka mbali " doh hapa kodi inaisha mwezi huu..maji sina umeme sina ndani sina akiba kabisaa nikiikosa hii kazi sijui hata nitaishije hapa mjini..."PIIIIII" akiwa bado anawaza anashtushwa na honi ya gari aina ya coster ikiingia kituoni ikiwa tupu! haraka anaruka na kupambana kuingia mlangoni anasukumwa huku na kule "hii siiachi hata kwa dawa nisukumeni tu" anawaza kimoyomoyo akiwa bado anashindana kuingia ndani. anapotazama pembeni yake anamuona bibi kizee mmoja nae akipambana vilivyo kuingia ndani na mara njemba moja inamsukuma yule bibi kwa nguvu na kumuangusha chini. Abel anamuwahi mkono haraka kabla bibi yule hajafika chini na kumvuta huku akizidi kupambana na hatimae wote wawili wanafanikiwa kuingia ndani. "dada mpishee huyu bibi akae humuoni ni myu mzima sana"? anasema abel akimtazama dada aliyeketi siti ya mwanzo akiwa na headphone masikioni."unasema..!? anajibi bidada huku akichomoa phone upande mmoja. "nakwambia mpishe huyu bibi akae hawezi kusimama" anarudia kusema abel. bidada anarudisha phone masikoni bila kujibu chochote na kuendelea kukaa. safari inaanza kuelekea ubungo.
%Love%Love$Love%
"Maeneo ya shekilango ving'ola vinasikika na magari yote yanapisha barabarani kuupisha msafara wa mheshimiwa. lakini ghafra gari moja dogo aina ya toyota corola linatoka pembeni ya barabara na kujichomeka mbele ya msafara. Gari inayoongoza msafara inawasha taa za ishara ya onyo la kulitaka gari hilo kupisha lakini wapi linaendelea kwenda tena kwa mwendo mdogo kama lilsioelewa kinachoendelea. gari inayoongoza msafara inaongeza spidi ili kuikuta na kuipa onyo lakini nayo inaongeza mwendo zaidi na mara wanapokatiza mataa ya ubungo gari aina ya kenta inatokea barabara ya mwenge na kuigonga gari inayoongoza msafara!! Ajali mbaya inatokea na gari za nyuma zote zinagongana na zingine kupinduka. toyota corola ambayo ilikua tayari imeshapita kwenye mataa inasimama na mara njemba nne zilizoshiba zinashuka zikiwa na silaha aina ya bunduki na huku zikiwa zimefunika sura zao" PAAAAH" mlio wa risasi unasikika! mshikemshike unatokea na watu watu wanaanza kukimbia huku na kule "PAA PAAH PAAAAH" milio ya risasi inasikika tena mfululizo. haraka njemba moja kati ya zile nne inakimbilia moja kati ya magari ya msafara yaliopinduka na kufungua malango..binti mrembo anaaguka chini tokana na gari kuinama.
%Love&Love$Love%
Coster aliyopanda abel inasimama ubungo tokana na foleni ya mataa na baadhi ya abiria akiwemo kijana abel wanaamua kushuka ili kutembea kwa miguu kuokoa muda kwani kipande kilichobaki ni kidogo. Akiwa anatembea kwa haraka kuelekea ilio stendi ya kwenda mwenge abel anasikia kitu kama kishindo kikubwa kinachofutiwa na kelele nyingi. akiwa bado anashangaa "PAAAAAAH" mlio wa risasi unasikika! anaufahamu vizuri kwani anauzoefu nazo wa kiasi fulani alioupata toka katika kazi za ulizi alizowahi kufanya maeneo mbalimbali. akiwa bado amezubaa "PAAAAH" Mlio wa risasi unasikika tena na mdada fulani mrembo aliyekua mbele yake anaanguka chini huku akitokwa na damu nyingi. Abel anapomtazama anamkubuka ni yule aliyegoma kumpisha bibi kwenye daladala. mara "PAAAA" mlio wa risasi unasikika tena na kumchubua sikio. haraka anaruka na kulala pembeni ya jiwe kubwa linalotumika kwenye ujenzi wa barabara! akiwa hapo anashuhudia njemba fulani iliyofunika sura ikimnyanyua binti toka ndani ya gari aina ya toyota vx iliyokua imepinduka na kumweka begani tayari kwa kuondoka nae..anapomtzama binti vizuri anashtuka na kutoa macho! "HAA" anajikuta akishangaa kwa nguvu kijana abel! ile njemba ikiwa na siraha mkononi inageuka na kumtazama......ITAENDELEA
JE NINI KITAMKUTA KIJANA ABEL!? NI KWA NII AMESHTUKA ALIPOMWONA BINTI!? tafadhali usikose sehemu ya pili ya riwaya hii ya kusisimua iitwayo mtoto wa rais. ili kuipata ingia google muda wowote na andika ZURIA KISMA CHA BURUDANI au mtoto wa rais episode 2 au andika www.zurialetu.blogspot.com! kwa maoni na ushauri mchango n.k wasiliana na mtunzi Josh E Mfara >> 0654243453
Tags
riwaya