Mwili wa mwanamke ni tofauti na wa mwanaume linapokuja swala la kufanya mapenzi. Mwanaume ni rahisi sana kupata ashki hasa akiona mwili wa mwanamke ukiwa uchi.
Mwanaume anachohitaji ili apate ashki ni kuwaza ngono, pamoja na kuona mwili wa mwanamke, hiyo inatosha kumuweka tayari kufanya . Kwa kawaida mwanaume huwa anapata ashki kwenye maeneo yake ya siri peke yake na siyo mwili mzima kama ilivyo kwa mwanamke.
Mwanamke yeye ili aweze kupata ashki na awe tayari kufanya tendo, inatakiwa aandaliwe vya kutosha, kwani mwili wake wote unatakiwa upate ashki na siyo sehemu zake za siri peke yake kama ilivyo kwa mwanaume.
Kuamsha sehemu za siri za mwanaume ni rahisi sana, ni eneo dogo, na huchukua muda mfupi sana, chini ya dakika moja. Lakini kuamsha mwili wa mwanamke ili uwe tayari kufanya ngono siyo rahisi kufanya hicho, inahitaji muda mrefu, zaidi ya dakika tano mpaka saa moja au zaidi kutegemea aina ya maandalizi au aina ya mwanamke.
Kwa hiyo wanaume wanatakiwa wafahamu tofauti hizi, ili kupunguza lawama zipungue kama sio kuzifuta kabisa.
Kwa kawaida baadhi ya wanaume huwa na haraka sana, huwa wana papara sana, na sijui huwa wanataka kuwahi nini na wapi. Mwanaume huwa hana subira wakati wa kufanya ngono, anataka afanye haraka, amalize kisha ageukie ukutani. Sijui huko ukutani huwa kuna nini, huu ni ukatili, haukubaliki. Haitakiwi mwanaume amwingilie mwanamke kama mwanamke hajawa tayari kwa tendo.
Maandalizi kabla ya ngono ni jambo muhimu sana kuliko hata ngono yenyewe. Kama maandalizi yakiwa mazuri utaifurahiya ngono, lakini maandalizi yakiwa hafifu huwezi kuifurahia ngono.
Kuna njia nyingi sana za kumuandaa mwanamke, nitazitaja chache. Mojawapo ni njia ya mazungumzo, mwanaume anatajkiw aaongee na mpenzi wake kwa lugha nzuri, kwa maneno matamu na yenye mahaba. Atumie muda mwingi kuzungumza naye, asiwe na haraka kuanza kufanya ngono.
Mazungumzo yahusu masuala ya uhusiano ukiwemo upendo. Usizungumzie madeni yako unayodaiwam, usizungumzie matatizo yako au ya familia yenu. Baadhi ya wanwake wanaweza kujisikia kujamiiana kutokana na mazungumzo peke yake. Lakini pia kuna baadhi ya wanawake wengine ambao huwa hawapendi kufanya ngono unapokutana nao kwa mara ya kwanza, wanataka tu mzungumze tu na si zaidi ya hapo.
Jambo hili kwa wanaume walio wengi ni gumu sana, wao wanataka ngono siku hiyo hiyo ya kwanza. Sisemi kufanya hivyo ni vibaya au vizuri, inategemea mazingira na makubaliano yenu.
Njia ya pili ni ya kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake. Njia hii inaweza kwenda sambamba na ile ya kwanza. Wakati unamshikashika usitumie nguvu, mshike kama vile unampapasa. Achana na mambo yote uliyoambiwa na rafiki zako kwamba mwanamke ukimshika sehemu fulani ndio anajisikia kufanya ngono, Fanya kile unachokiona kwa wakati huo.
Wanawake wote wanatofautiana. Linapokuja swala la kujamiiana mwili wa mwanamke unaweza kuufananisha na dunia hii tunayoishi. Una milima na mabonde, mito, maziwa na bahari, una mbuga za wanyama kwa kifupi ni kwamba, una kila kitu unachokiona hapa duniani, ni juu ya mwanaume kuwa mvumbuzi wa maeneo mbalimbali atakayoyatumia kumuandaa mwanamke aliye naye ile awe tayari kufanya ngono na kufika kileleni kwa urahisi.
Mwanaume anatakiwa atumie milango yote sita ya fahamu ili kujua ni maeneo gani anapoyagusa yanamfanya mwanamke ajisikie vizuri zaidi, yanamfanya asisimke. Pia ni maeneo gani akiyagusa yanamfanya ajisikie vibaya.
Kwa kawaida, maeneo fulani yanaweza yakamfanya mwanamke fulani ajisikie vizuri, lakini maeneo hayo hayo ukimshika mwanamke mwingine anajisikia vibaya au anakereka.