TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SABABU 6 ZA KUJIFUNZA MICROSOFT EXCEL

Microsoft Excel ni Program ya kimahesabu inayotumika kuhifadhi data katika muundo wa nambari, maneno, grafu na chati. Microsoft Excel inatumika katika makampuni biashara na katika taasisi mbalimbali. Pia watu binafsi hutumia program hii kwa matumizi mbambali. Kuna sababu sita (6) za msingi za wewe kujifunza Microsoft Excel.
1. Kuongeza ufanisi katika kazi.
Program ya microsoft excel inakusaidia kuongeza ufanisi katika kazi unazofanya kutokana na uwezo wake wa kurahisisha kazi na kuokoa muda. Mfano kama ulitakiwa kutengeneza ripoti 100 kwa njia ya mkono ungeweza kutumia hata siku nzima kuandaa tu, lakini kupitia Microsoft excel unaweza kukamilisha kazi hiyo ndani ya saa 1 au masaa mawili tu.

2. Kutunza taarifa binafsi
Unaweza kutumia program ya Microsoft Excel kutunza taarifa zako binafsi kama vile orodha ya vitu, bajeti yako binafsi au kufanyia mahesabu muhimu ya manunuzi / matumizi unayoyafanya.

3. Kufanya mahesabu ya kibiashara
Program ya Microsoft excel ina umuhimu mkubwa sana katika biashara. Uwezo wake wa kufanya mahesabu kiutomatiki ndio unaoipa umuhimu huo. Microsoft Excel katika biashara inatumika kutunzia taarifa za mauzo, taarifa za wateja pamoja na kufanya mahesabu na michanganuo ya mauzo pamoja na kuandaa ripoti.

Mahesabu Excel

4. Kujiongezea sifa ya kuajiriwa
Dunia imebadilika sana na teknolojia ndio kila kitu katika maisha yetu ya sasa. Kutokana na umuhimu mkubwa wa program hii ya Microsoft Excel makampuni na taasisi nyingi huwa wanahitaji watu wenye uwezo wa kutumia computer ikiwemo na program hii ya Microsoft Excel. Hivyo kujifunza Microsoft Excel kutakusaidia Kujiongezea sifa muhimu inayohitajika na waajiri wengi katika kipindi hiki.

5. Kutengeneza Kalenda.
Kalenda ni nyenzo muhimu ya kudhibiti muda kwa kupangilia muda na matukio au kazi tunazojipangia kutekeleza katika muda husika. Kupitia program ya Microsoft Excel unaweza kuandaa kalenda binafsi, kalenda ya ofisi au Kalenda ya mwaka ikionyesha miezi yote 12 na matukio muhimu katika mwaka husika.

Kalenda-excel
6. Kujiajiri
Ujuzi wa Microsoft Excel unaweza kukusaidia kujiajiri na kuingiza kipato. Unaweza kujiajiri kupitia ujuzi wa Microsoft Excel kwa Kutengeneza Template za Mauzo na Kuziuza kwawatu wengine. Pia unaweza kutengeneza Kalenda mbalimbali za watu binafsi, familia, shule au kampuni na wakakulipa.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post