TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

UKOMBOZI WA FIKRA

UKOMBOZI WA FIKRA ..
Siku moja Mwanafalsafa SOCRATES aliwasha taa mchana kweupe na akaenda nayo kwenye soko la Athenes, kule Ugiriki. Pale sokoni wananchi wengi walimshangaa sana Socrates wakamuuliza; kwa nini amewasha taa sokoni wakati ni mchana na mwanga wa taa yake wala hauonekani kutokana na mwanga wa jua uliopo.

SOCRATES aliwajibu hivi, ‘’Pamoja na nuru hii ya jua kuwepo lakini akili za watu wengi bado ziko kwenye giza nene’’....

Utafiti uliofanywa mwaka 2010 na asasi ya Marekani inayoitwa PEW Research Centre, ulibaini na kuonesha kwamba asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika ushirikina. Na sio katika matumizi ya akili zao...

Idadi kubwa ya matatizo mengi  uyaonayo siku hizi yanasababishwa na watu kutokuzitumia akili zao...

  MWENYEZI-MUNGU aliliona jambo hili ndomaana Akasema...
   " Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa"
      ( Hosea 4:6 )
Siku hizi Haishangazi sana kila kona unakopita utakutana na vibao barabarani vya waganga wa kienyeji vyenye Matangazo  yanayosomeka hivi,...

.......“Dk. Bingwa kutoka Congo anatoa huduma zifuatazo: Kumrudisha mpenzi wa zamani, kuongeza nguvu za kiume, kuongeza akili za darasani, kumsahaulisha mdai wako, kuongeza mvuto kwa warembo, kupandishwa cheo kazini... Nakuendelea........

Haishangazi siku hizi kuona Matangazo mengi katika Mitandao  ya kijamii ya Kupata utajiri kwa njia nyepesi ambayo ni njia ya ushirikina...

Na idadi kubwa ya vijana kwa jinsi ambavyo hatutaki kufuata kanuni hakali za kutafuta Mafanikio kwa kutumia akili zetu, tumejikuta tukihamasika zaidi katika kujiunga Kupitia Matangazo hayo ili tuupate huo utajiri wa Masharti kama unavyonadiwa...
Mafanikio ya kweli hayawezekani bila mabadiliko ya fikra yako mwenyewe na wale ambao hawawezi kubadili namna wanavyofikiri hawawezi kubadili chochote katika maisha yao...

KIJANA mbele yetu kuna kazi  ngumu ya kulijenga Taifa letu, Hembu itumie akili yako katika kufikiri vizuri...

Baba wa kiroho, SAI BABA, aliwahi kusema maneno haya, tumia Akili yako vizuri kuyatafakari..

Maisha ni wimbo---- UIMBE...
Maisha ni mchezo---UCHEZE.,
Maisha ni changamoto--- IKABILI.
Maisha ni ndoto---- IELEWE...
Maisha ni sadaka---- ITOE...
Maisha ni upendo--- UFAIDI..
Maisha ni lengo---- LIINGIE...
Maisha ni kengele---- IGONGE...
Maisha ni barabara---- IPITE ..
Maisha ni mti---- UPANDE....
Mwanafalsafa Anselm Stolz aliwahi  kufundisha hivi,...
     “Ukimpa mtu samaki atamla mara moja, lakini ukimfundisha kuvua atakula samaki kila siku”....

KIJANA wa leo, samaki waliopewa vijana wenzetu wa jana hawakuwa na msaada kwao ndomaana leo tunazidi kuwasikia vijana wenzetu wakilalamika kuhusu Ajira kwasababu mfumo wa Elimu haukuwa fundisha kuvua samaki wenyewe  ila uliwaletea samaki na kuwaanda kuwa tegemezi kwa ajili ya  kupokea tuu nasio kutafuta...

 Hivyo, ni jukumu letu kama vijana wakitanzania  kuzitumia akili zetu wenyewe,  tukifundishana wenyewe namna ya kuvua samaki ili tujijengee uwezo endelevu utakaokuwa msaada Katika maisha yetu nakwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo......

KIJANA, ishinde tamaa yako. Mafanikio halali hayapatikani kwa njia nyepesi. Mafanikio kwa njia nyepesi  yatagharimu maisha yako, yatagharimu ndugu,jamaa na marafiki zako, yatagharimu familia yako. Na yatakufanya ujutie maamuzi yako hapo baadae ..
 Kama vijana ikiwa tutazitumia akili zetu ipasavyo, na kila mmoja wetu akagundua kusudi la maisha yake kwa kutambua uwezo uliopo ndani yake, Tutafanya makubwa zaidi katika ulimwengu huu......

 " Twayaweza Mambo Yote Katika Yeye Atutiaye nguvu"..
        ( ( Wafilipi 4:13))

     MUNGUTUBARIKI VIJANA..
      TUKUMBUSHE KUITUMIA AKILI YETU..
...

                 ✍️✍️✍️✍️✍️

Kuendelea kupata masomo yenye kukuelimisha, kukujenga na kukuhamasisha katika maisha yako...

Karibu ujiunge katika DARASA KA SAIKOLOJIA WHATSAPP....

Gharama za kujiunga katika DARASA hili ni shilingi elfu 3,000/= Tuuu.

   Kwa maelekezo kuhusu kujiunga, 
   Tuma Neno KUJIUNGA kwenda namba..
       0765900743(WhatsApp

    TUZIDI KUJIFUNZA, NA 
          TUSICHOKE KUJIFUNZA...
                 ✍️✍️✍️✍️

Mwanasaikolojia & Mshauri,
     Mwalimu Sunzu 🗯️
          0765900743..

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post