TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

KUTANA NA CHUMBA CHA AJABU CHENYE KUTISHA MNOO, AMBACHO HATA SERIKALI YENYEWE YA INDIA INAOGOPA KUKIFUNGUA, HAKIJAWAHI KUFUNGULIWA TOKEA KILIPOFUNGWA.

KUTANA NA CHUMBA CHA AJABU CHENYE KUTISHA MNOO, AMBACHO HATA SERIKALI YENYEWE YA INDIA INAOGOPA KUKIFUNGUA, HAKIJAWAHI KUFUNGULIWA TOKEA KILIPOFUNGWA. 
Kuna jumba la ibada huko India lijulikanalo kama Padmanabhaswamy ambalo kuta zake za nje zimetengenezwa kwa dhahabu. 

Jumba hili liko sehemu ijulikanayo kama Thiruvananthapuram katika Mji wa Kerala. Jumba hili ni kati ya vivutio ya utalii ambapo utembelewa na watalii wengi kila mwaka. Lakini katika jumba hili kuna mali yenye thamani kubwa sana ambayo ilikuwa imefichwa kwa muda mrefu kwa karne na karne.

Jumba la ibada la Padmanabhaswamy ni mojawapo kati ya nyumba za ibada 108 wa Hindu zinazotumika katika kumwabudu mungu wao ajulikanaye kama Vishnu. 

Jumba hili linalindwa na familia yenye damu ya kifalme ijulikanayo kama familia ya Travancore. Uamuzi wa kuweka jumba hili mikononi mwa familia hii ulifanyika mwaka 1729. Jumba hili na kila kilichomo kilikuwa kinamilikiwa na Padmanabhaswamy pamoja na hii familia ya kifalme niliyotaja hapo juu. Lakini kuna mambo yalitokea na familia hiyo ya kifalme ikanyanganywa haki ya kuendelea kutunza jumba hilo, uamuzi huo ulifanya na mahakama kuu ya India. Hili jambo lilipelekea kugundulika kwa siri kubwa iliyokuwa imejificha kwenye jumba hilo ambalo limejengwa miaka mingi hata kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.

Mwaka 2011, jamaa ajulikanaye kama Sunder Rajan alifungua shitaka kwenye mahakama kuu ya india akidai kwamba familia ya Transcore iliyokuwa inalinda jumba hilo ilikuwa inatumia vibaya mali zilizokuwa kwenye jumba hilo. Wakati shauri hilo likiendelea, mahakama iliunda jopo la watu saba ambao walipewa kazi ya kuingia ndani ya jumba hilo na kukagua mali zote zilizomo ikiwemo pia nakala zozote zitakazokuwa zimehifadhiwa humo.
Jopo la watu hao saba, waligundua kuwa ndani ya jumba hilo kulikuwa na vyumba vya siri sita ambavyo, walihisi vitakuwa vina mali. Milango ya kuingia kwenye vyumba hivyo imetengenezwa kwa chuma ila haina na sehemu ya kuweka funguo, wala kufuri, wala bawaba, wala vitasa wala klitu chochote ambacho kingekufanya upate namba ya kuwaza jinsi ya kuufungua hiyo mlango.

Baada ya kufanikiwa kufungua milango hiyo kwa kutumia vifaa vya kisasa na muda mrefu, waligundua kuna mali yenye thamani ya dolla bilioni 22. Msomaji hii ni karibu tilion za Kitanzania 70, Mali hii inajumuisha midori, shanga, mikufu, shilingi za pesa ya zamani sana, mabakuli, vifuu vya nazi vya dhahabu, dhahabu iliyotengenezwa kwa mfano wa mayai, almasi kubwa kubwa n.k
Pia kulikuwa na almas kubwa kubwa ambazo nyingine zilifikia karati 110, nadhani kwa wanaojua vipimo vya madini haya watakuwa wanaelewa.

Wataalamu wa mambo ya kale wanakisia kwamba kimdori kidogo cha Vinshu kutoka katika hazina hiyo kinaweza kuwa na thamani ya dola milioni 30, karibia bilion 65 za Kibongo ndugu msomaji.

Wakati wakifungua vyumba hivyo vya siri walivipatia majina kwa herufi kuanzia Chuma A mpaka F kutokana na vilivyokuwa vimepangana. 

SASA KIMBEMBE NI CHUMBA B. 

#Sasa kimbembe ni kufungua mlango wa "#CHUMBA_B" ilishindikana baada ya milango ya vyumba vyote kuwa imefunguliwa kasoro hiki chumba ambacho mlango wake ni wa tofauti kabisa na vile vingine na nje ya mlango kumewekwa onyo kuwa kuna ulinzi wa mijoka mikubwa.

Katika nakala walizokuta mle ndani zikiwa zinaonyesha mali zilikohifadhiwa, vile vyumba vingine viliandikwa kuwa vina mali lakini hiki chumba B hakijaorodheshwa kama chumba ambacho kimehifadhiwa mali, jambo linaloleta maswali mbona ndicho chumba chenye ulinzi mkali kuliko vyote.

Chumba hiki kina milango mitatu, mlango wa kwanza lilikuwa geti la grill la kawaida nyuma ya hilo geti kulikuwa na mlango mkubwa wa mbao walipofungua mlango wa mbao ndipo wakakutana na lango kubwa la chuma lisilokuwa na sehemu au kitu chochote cha kuashiria jinsi ya kuufungua. Pia juu yake likiwa na urembo mfano wa mijoka miwili aina ya cobra ambapo hii uashiria onyo kwa yeyote atakaye jaribu kufungua na kuingia katika chumba hicho kuwa atakutana na adhabu kali sana.

Tofauti na milango ya vyumba vingine walau ilikuwa na bolts huu wa hiki chumba ni chuma kitupu hauna hata bolt hata moja.
Wahindu wao wanasema wazi kwamba juhudi zozote zitakazofanyika kwa kutumia utaalamu wowote na kufanikiwa kufungua mlango wa chumba hicho, utapelekea janga kubwa ambalo linaweza kuteketeza mji mzima au India nzima pamoja na dunia kwa ujumla.

Pia hawa Wahindu wanaendelea kusema kuwa Kuna watu saba waliojaribu kufungua huo mlango, makubwa yaliwakuta........ 

ITAENDELEA.

*************

PIA,

UNAWEZA KUJIUNGA NA GROUP LETU LA SIMULIZI HUKO WHATSAPP KWA AJILI YA KUSOMA MAKALA NYINGI ZAIDI ZA KUSISIMUA KILA SIKU. 

UNALIPIA KIASI CHA SHILINGI 1500 TU KWA MWEZI MZIMA. 

HIVYO KAMA UKIPENDEZWA KUJUMUIKA NA MEMBERS WENGINE KULE KATIKA GROUP, MTUMIE MESEJI ADMIN KWA KUBOFYA LINK HAPO CHINI AMBAYO ITAKULETA KWA URAHISI MOJA KWA MOJA WHATSAPP KWA ADMIN KWA MAELEKEZO ZAIDI YA UTARATIBU WA KUJIUNGA.


KAMA BADO HAUJAJIUNGA NASI KATIKA GROUP MPAKA LEO HII, JUA KUWA UNAPITWA NA MENGI.

*******************

#PIA USISAHAU KUFOLLOW UKURASA HUU WA STORIES ZA KUSTAAJABISHA, PAMOJA NA KUSHEA ILI NA WENGINE NAO WAPATE KUELIMIKA🙏

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post