TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

KUTOKA KWA MADEBE LIDAI 01

  ................. Simulizi Hii imetolewa/kuchukilwa Toka Katika Ukurasa Wa Facebook Wa MADEBE LIDAI...............
Baba alinisisitizia kuchukua likizo kazini nirudi nyumbani nikamuone. Na alitaka nikae huko mwezi mmoja. Nilikua na mambo mengi sana kazini na nikamwambia sitaweza kupumzika kazi mwezi mzima. Lakini aliniambia mwezi mmoja wa kung'ang'ania kazi naweza kuujutia maisha yangu yote.

Kwa namna alivyokua anaongea niliogopa. Baba yangu hakua mtu wa kudekadeka. Mara nyingi alijifanya 'mgumu' hata alipokua anaumia sana. Nilipomsikia anaongea vile nilijua nahitajika kwenda kumuona. Nikachukua likizo nikaenda.

Nilifika nyumbani nikamkuta yupo hoi kitandani. Kweli alikua anaumwa, alikua kaisha, alikua kakonda, afya imedhoofu na alikua hawezi hata kunyanyuka. Alikua mpole, anaongea taratibu na mnyonge sana. Kwa mtu aliyekua anamfahamu angemuonea huruma na hata kutoa machozi. Nilimuangalia kwa huruma lakini alilazimisha tabasamu, hakutaka kuonekana mnyonge.

Aliniambia "Wewe ndiye mtoto wangu wa kwanza. Una wadogo zako sita. Wa kike wawili na wa kiume wanne. Kuna kitu nataka nikufundishe kabla sijafa ili uje kuwa baba bora kwa wanao na si kuwa kama mimi"

Nilimuitikia nikidhani kuwa kuna kitu ataniambia, lakini mpaka likizo inaisha hakuniambia kitu chochote. Nilishangaa na kumuuliza mbona kaniahidi kuniambia kitu lakini hajaniambia na likizo inaisha natakiwa kurudi kazini?

Alitabasmau na kuniambia kuwa ameshaniambia. Nilifikiria sana nikijaribu kukumbuka kama kuna kitu labda aliniambia nikakisahau lakini sikukumbuka. Nilifikiri sana sikukumbuka chochote. Nikamwambia Baba mbona sikumbuki chochote. Alitabasamu tena, huku akiongea kwa shida, kisha akaniuliza nimekaa pale siku ngapi? Niilimuambia siku 23. Akaniuliza tena wewe una shangazi wangapi? Nikamuambia wawili. Akaniuliza na Baba wadogo? nikamuambia watatu.

Akaniuliza tangu nikae hapo walishakuja mara ngapi? Nilimuambia Shangazi mmoja alikuja mara tatu, kuna mwingine kila baada ya siku mbili anakuja. Baba wadogo aliyekuja ni mmoja tu, naye alikuja mara moja kwani wote wapo mjini na familia zao.

Alitabasamu tena na kuniuliza vipi mama yako tangu uje hapa yeye kaja mara ngapi? Nilishanga ana nikadhani Baba ameanza kuchanganyikiwa.

Inaendelea Part 2..! 

Mama Bosi] Mama Bosi]

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post