TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

KUTOKA KWA MADEBE LIDAI 02

PART 2
.....Simulizi hii imetolewa/kuchukilwa katika Ukurasa Wa Facebook Wa MADEBE LIDAI........
Nikamwambia “Baba Mama mbona kila siku yuko hapa, ndiyo anakupikia, anakusafisha, anakufanyia kila kitu? Inamaana umesahau?”

Nilidhani Baba akili zimeanza kumpotea lakini alitabasamu na kuniambia “Hapana mwanangu, sijasahau kuwa Mama yako yupo hapa, ila nilimsahau kipindi namuoa. Niliendekeza ndugu na kuwajali sana. Niliwapa kila msaada waliohitaji huku Mama yako akiwa tu ndani. Sikumsikiliza, sikumheshimu, sikumjali, na nilikua nikimpiga kwa maneno tu ya ndugu zangu.

Alivumilia kwakua hakuwa na pa kwenda. Wazazi wake walishafariki na ndugu zake kila mmoja alikua na familia yake. Lakini leo yeye ndiye yupo na mimi katika hali zote na nyakati zote. Ananihudumia kwa kila kitu wakati huu ambao mimi sina pa kwenda.

Alivuta pumzi kisha akaendelea kusema "Ndugu zangu wote niliowasaidia leo wana maisha mazuri lakini wapo busy na familia zao. Hawana muda wa kuja kunisalimia. Mara chache hunipigia simu kujua naendeleaje. Lakini Mama yako ananiogesha na kunilisha kila siku. Nyie wanangu mpo huko mjini mna maisha yenu. Mnakuja kuniona mara moja moja. Siwalaumu maana najua si jukumu lenu. Nawashukuru kwa kuja kunisalimia hata kwa kupangiana zamu.

Lakini Mama yako hana cha zamu, akilala akiamka yuko na mimi. akigeuka ni mimi, akila ni mimi, akipumua ni mimi, nikijisaidia ni yeye, nikitapika ni yeye, nikidondoka ni yeye.

Zamani nilikua namuambia kama umenichoka bado ondoka lakini leo siwezi hata kujisaidia bila yeye. Mwanangu wapende ndugu zako lakini kama hutaki kufa kwa unyonge kama mimi basi Mpende zaidi mke wako. Huyo ndiye Mungu alipanga mzeeke naye.

Ndugu watakuja kukusalimia tu na kukupa pole lakini wakubeba kinyesi chako ni mkeo. Mfanye abebe huku akikumbuka mema uliyomfanyia na si mateso uliyompa. Mwanangu ukimnyanyasa mwanamke lazima utateseka tu. Akitangulia kufa yeye utabaki na watoto wanaokuchukiaa kwakua ulimtesa Mama yao. Na ukitangulia wewe basi yeye ndiye atakua karibu kukuhudumia wakati wa ugonjwa. Mheshimu sana mke wako.”

Baba alimaliza kuongea, akaniambia nimuache apumzike. Siku iliyofuata niliondoka kurudi mjini lakini sikufika, nilipigiwa simu kuwa Baba yangu kafariki dunia.

INAENDELEA PART 3

Mama Bosi] Mama Bosi]

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post