TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

UMUTWALI 01

MWANDISHI: SADARI KISESA
WHATSAPP: 0785276697
SIMULIZI: UMUTWALI

                   SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI...
Umutwali kibantu baba wa kambo. Umutwali anasadikika amejaa tamaa anahisi dhuruma njia rahisi ya mafanikio lahasha! anajidanganya hajui kama dhuruma inaleta majuto, kwanini utamani mali ya mwingine thubutu kupambana upate mali yako. Tambua cha mtu hakiliwi na kitakapoliwa lazima uishi tumbo joto, roho haikusuti unapoweka kibindoni mali ya mwingine? ama kweli mhaini sio rafiki. Bora umfadhili Mbuzi utamnywa mchuzi kuliko kumfadhili mhaini ukaambulia mauzi, Umutwali kama Kinyonga anaficha asili hasiweze kutambulika anaweza kuwa mwafrika hata mtu kutoka ughaibuni. Tahadhari mwogope mtu huyo bila hivyo atadondosha mafanikio tena jihami kama sanamu lililopo Posta, Dar es salaam.

SONGA NAYO...
Utambulisho anaitwa Donald Mtalanze, amezaliwa katika familia yenye ukwasi yenye mtoto mmoja. Mzazi wake wa kiume anaitwa Msondo Mtalanze daktari katika hospitali ya Muhimbili na mzazi wake wa kike anaitwa Zonda Zwambanga mwalimu katika shule ya Anazak. Yeye mtoto wa pekee katika familia na mwanafunzi bora katika shule ya sekondari ya Loyola, familia yake iliishi kwa upendo na furaha pia ilijiwekea misingi ya kuwajibika ipasavyo. Wazazi wake waliwajibika kwa ufanisi kazini na yeye aliwajibika vema shuleni, ilikuwa kawaida kuwahi shule akaweka bidii katika masomo ili baadae awe msomi kama wazazi wake. Kanuni za familia zilifuatwa anayewahi kuamka kabla ya wenzake kuamka anawaamsha wenzake, wazazi siku hiyo hawakufuata kanuni waliwahi kuamka lakini hawakuamsha wengine. Walijiandaa wakawahi kazini wakamwacha dada wa nyumbani na Donald wakiendekeza usingizi wakaja kuamka baadae, Donald kabla hajanyanyuka kitandani akajinyoosha mwili mara viungo vyake vikalia kokoko!. Alikwenda kukoga baada kujinyoosha mwili na kunyanyuka kitandani alipomaliza akarudi kujiandaa kisha akaongoza kwenda kula chakula, alikutana ana kwa ana na dada wa nyumbani sebuleni akiwa anamaliza kusafisha sebule akamwita.

“Angel...” aliita Donald mara baada kufika sehemu husika na kukaa.

“Abeeh!...” Angel kama aitwavyo aliitika akaongoza alipoitwa mara baada kumaliza kusafisha sebule.

“Upo poa?....”

“Nipo poa....”

“Wazazi wamekwenda kazini?,” Donald aliuliza huku akiendelea na kifungua kinywa mara baada kujitengea kifungua kinywa.

“Wamekwenda kazini tena mapema sana. Hawajakuaga?.”

“Hawajaniaga kwakuwa nililala,” Donald alijibu huku akijitwika begi mara baada kumaliza kifungua kinywa.

Hakuhitaji kuchelewa akaaga hatimaye akaondoka kwa kukamata barabara ya vumbi iendayo Kimara suca, alifika katika kituo cha daladala akasubiri kwa wasaa alhamdulillah! daladala ya Mbezi Temeke ikawasili kwakuwa kondakta hakutaka wanafunzi akapanda kwa kasumba. Aliongoza kwenda kukaa katika kiti cha katikati cha mwisho daladala ilipowasili Kimara Baruti, alimwona mama mmoja mjamzito ukikadiria ulikuwa ujauzito wa miezi nane alipanda daladala kwa tabu.

“Mama, njoo ukae,” Donald aliita kwa sauti akimwita mama yule mjamzito.

“Nakuja mwanangu” mama mjamzito alisema huku akisogea akipishana na abiria wengine waliosimama.

“Mwanangu, unaonekana una heshima sana. Endelea kuwa na heshima” mama mjamzito alisema huku akitabasamu mara baada kukaa.

Donald hakuendeleza maongezi alishika bomba za daladala akizuia asipepesuke kama mlevi daladala ilipowasili Chicago, alishuka akaachana na barabara kuu akaingia katika njia za mkato akiwa njiani akamwona mwanafunzi mwenzake nadhifu mlimbwende anayesoma nae darasa moja.

“Fetty...” Donald aliita kwa mkato huku akikimbia mbio akimkimbilia mhusika.

“Abeeh...” Fatuma kama aitwavyo aliitika huku akigeuka kumtazama anayemwita.

“Kumbe wewe” Fatuma alistaajabu huku akimngoja mlengwa wake mara baada kumjua.

“Kumbe na wewe unachelewaga?” Fatuma alihoji mara baada mlengwa kukaribia aliposimama.

“Siku mojamoja nachelewa,” Donald alijitetea huku wakiongoza pamoja.

“Basi fanya tuwahi tusije kuchelewa zaidi,” Fatuma alisema huku akionyesha tabasamu mwanana lililochanua kama Uaridi.

Waliongeza mwendo wawahi shule, kwakuwa walichelewa wakakuta wanafunzi washaingia darasani wakaingia kwa kunyata mithili ya Kobe, waliongoza kwenda kukaa ilhali wasijue kama mwalimu amekaa darasani kwa kujichanganya na wanafunzi. Walishangaa kuona wanafunzi wakiangua vicheko mara ikasikika sauti ya kike ya mwalimu ikiuliza kwa kufoka. 

“Huu ndiyo muda wa kuja shule?” mwalimu alifoka huku akitoa macho kwa jazba.

“Hapanaaa!...” baadhi wanafunzi wakajibu kwa kupayuka.

“Ona hawa mweu wanakuja shule muda huu kama shule ya baba yao” mwalimu alisema kisha akahamuru walengwa wasonge mbele kupiga magoti, alifura akabadilika kawa Mbogo.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post