Wakati mtume Muhammad (swallah
allahu alayhi wasallam) anakwenda
katika safari yake ya Miiraji wakati
yuko njiani akapita sehemu akasikia
harufu nzuri kabisa. Mtume
(swallah allahu alayhi wasallam)
akamuuliza mwalim wake Jibril hii
ni harufu ya nini? Jibril
akamwambia hiyo ni harufu ya
kaburi la msusi wa mtoto wa firaun. Mtume
(swalla allahu alayhi wasallam)
akamwambia Jibril naomba unipe
"Siku moja wakati msusi wa nywele
akimsuka mtoto wa Firauni ( Firauni )
katika nchi ya misri ni cheo cha
ufalme kwa maana hiyo kila mfarume aliyetawala
katika nchi ya misiri aliitwa ( Firauni ); chanuo
lake lilimdondoka.
Wakati lilipomdondoka akaliokota
huku akisema: "BISMILLAH". Mtoto
wa Firaun akamuuliza ina maana
unamuabudu Mungu mwengine
asiekuwa baba yangu? Msusi
akamjibu ndio namuabudu Mungu
mwengine ambae ni ALLAH. Mtoto
wa Firaun akachukua khabari zile
na kumfikishia baba yake. Msusi
akaitwa mbele ya Firaun ili
akajieleze. Akaulizwa na Firaun je
una Mungu mwengine nisiekuwa
mimi? Msusi akajibu ndio Mungu
wangu ni Allah nae ndie Mungu wa
Firaun akakasirika kwa majibu yale
kwani yeye alijipa sifa ya uungu.
Firaun akaagiza litafutwe sufuria
kubwa sana na litiwe ndani yake
maji na yapashwe moto mpaka
yapashike haswa. Watumishi wake
wakatii amri ile na kutafuta sufuria
na kutiwa maji. Maji yalipata moto
mpaka waliokuwepo karibu yake
wakihisi ukali wa mvuke. Yule
msusi akachukuliwa yeye na familia
yake akaambiwa usiposema kuwa
Firaun ndio Mungu basi utaingia
ndani ya sufuria na kuunguzwa
wewe na familia yako. Akaulizwa
nani Mungu wako? Msusi akajibu
Mungu wangu ni Allah na ndio
mungu wa viumbe vyote.
Akachukuliwa mume wake na
akatumbukizwa ndani ya sufuria la
maji ya moto akaungua mpaka
akafariki. Akaulizwa tena ni nani
Mungu wako? Msusi akajibu Mungu
wangu ni Allah na ndie mungu wa
viumbe vyote. Akachukuliwa mtoto
wake wa kwanza akatiwa ndani ya
maji ya moto huku akilia mama
mama mpaka sauti ikamalizika
akafariki. Akaulizwa tena nani
Mungu wako? Msusi akajibu Mungu
wangu ni Allah na ndie mungu wa
viumbe vyote. Akachukuliwa mtoto
wa pili nae akatumbukizwa ndani ya
maji ya moto na akafa.
Msusi
alikuwa na mtoto mchanga
akachukuliwa mtoto yule na
akawekwa karibu na sufuria la ya
maji moto akaulizwa nani Mungu
wako? Msusi akasema na Allah yaa
rabbi nini nifanye? Alifanya hivi
kwa sababu ya kumuonea huruma
mtoto wake mchanga. Naam miujiza
ikajiri kitoto kichanga kikatoa kauli
ewe mama yangu usisite sisi
tunaenda peponi. Mwanamke bila
ya kusita akajibu kuwa mola wangu
ni ALLAH na ni mola wa viumbe
vyote. Wakataka kuwatia katika maji
ya moto yule msusi akasema
naomba kitu kimoja? Naomba sote
mtuzike katika kaburi moja. Baada
ya kupeleka ombi lake mtoto wake
mchanga pamoja na yeye
mwenyewe wakatiwa katika maji ya
moto na wakafariki. Na wakazikwa
katika kaburi moja na hiyo ndio
khabari yao hadi ukawa unasikia
Naaam hawa ndio wale ambao
walimshiba Allah ndani ya nyoyo
zao. Hawakujali chochote zaidi ya
Allah pekee. Wakawa tayari kumtaja
Allah kwa lolote wakawa tayari
kupoteza chochote kwa ajili ya
Allah ila wasije kumshirikisha Allah.
Je vipi mimi na wewe ambao hata
swala zetu zinatupa mtihani? Je
vipi mimi na wewe ambao
tunachukulia dini ya Allah kama
utani? Je vipi mimi na wewe ambao
hatuko tayari kupoteza mali zetu na
vitu vyetu vya thamani kwa ajili ya
Allah? Tuchukue mazingatio
makubwa kutoka katika kisa hiki na
iwe ni sababu ya kuzibadilisha
nyoyo zetu na turudi kwa Allah.
Tutubieni kwa Allah toba ya kweli.
Tunamuomba Allah atupe husnul khaatima njema
na atufishe hali ya kuwa yuko radhi nasi sisi
pamoja na wazazi wetu na
atujaalie miongoni mwa waja wake wema
watakaoingi katika pepo yake ya
Tags
visa Vya kale