TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

HAKIKA HUYU NDIYE HAYATI RAIS SADDAM HUSSEIN ALIYEISHIA KUNYONGWA, INAHUZUNISHA.

HAKIKA HUYU NDIYE HAYATI  RAIS SADDAM HUSSEIN ALIYEISHIA KUNYONGWA, INAHUZUNISHA. 
Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti alinyongwa katika makao makuu ya idara ya upelelezi katika jeshi katika wilaya ya Kadhimiyah kaskazini mwa Baghdad. Maafisa ambao walishuhudia kuuwawa kwa Saddam Hussein ambae aliyekuwa na umri wa miaka 69 mapema alfajiri, walisema aliendelea kuwa mkaidi hadi mwisho wake, akipambana na maadui zake wa Iran na Marekani na kuwasifu wapiganaji ambao wameipeleka Iraq katika ukingo wa vita vya wenywe kwa wenyewe.

Saddam Hussein alinyongwa siku ya tarehe 30 12 2006, saa 8 usiku Kwa saa za Iraq. Kwamujibu wa duru za ndani siku ananyongwa hakuchagua chakula chochote ila aliomba maji ya kunywa ya moto. Taarifa zinasema Masaa 24 kabla hajanyongwa hakulala kabisa, mlinzi wa gereza alikuwa anamchungulia mara Kwa mara na kumwona akisoma Quran.

Siku aliyo nyongwa alikataa kuvalishwa kitambaa cheusi usoni wakati wa kunyongwa na badala yake akawaomba wauaji wake wamvalishe kitambaa hicho shingoni ili kamba isimchubue wakati akinyongwa. Na baada ya kuvishwa kitanzi alidhihakiwa Sana akiambiwa "Nenda kuzimu Shetani wewe". Saddam Hussein alinyongwa huku akiwa kavaa suti nyeusi na tai na akiwa kachana vizuri Sana nywele zake.

Saddam Hussein aliaga Dunia ndani ya dakika moja tu. Kitanzi kiliachwa dakika 12 nzima ndo wakakitoa. Baada ya kutolewa kwenye kitanzi maiti yake ilifunikwa na shuka jeupe na kisha kupakiwa katika herikopta ya kijeshi hadi alikozaliwa mji wa Tikrit..

SADDAM HUSSEIN ABD AL-TIKRITI NI NANI?
Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti alizaliwa tarehe 28, Aprili mwaka 1937 katika kijiji cha Tikrit katikati ya Iraq, na aliingia madarakani tarehe 16 Julai 1979 na kulitawala taifa hilo kwa mkono wa chuma hadi tarehe 9 Aprili 2003 alipoondolewa kwa nguvu na majeshi ya Marekani kupitia iliyoitwa operation desert sehemu ya pili.

Kuuawa au kunyongwa kwa Saddam imekuja kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama Maalum iliyomtia hatiani kwa mauaji ya wanakijiji waarabu wa madhehebu ya Shia wapatao 150 baada ya kushindwa kwa jaribio la kumuua mwaka 1982. Pia alikabiliwa na mashitaka mengine ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wakurdi 180,000 wengi wao wakiwa raia wa Iraq mwishoni mwa miaka ya 1980.

Kiongozi huyo aliyeitawala Iraq kama rais wa tano wa nchi hiyo alionekana akiwa amebeba kitabu kitukufu cha Koran huku akisema kwa sauti kuu kuwa 'hakuna Mungu mwingine bali Allah na Muhammad ni Mtume wake' (Laillah haillah Muhammad Rasuli Allah) siku ya kutekelezwa kwa hukumu ya kifo chake, alinyongwa katika kasri ya wizara ya Sheria.

HISTORIA YA SADDAM HUSSEIN KATIKA SIASA MPAKA KIFO CHAKE.
Mwezi Oktoba, 1959 Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti alihusika katika jaribio lililoshindikana la kumuua mtawala wa Iraq kipindi hicho aliyeitwa Jenerali Abdul Karim Qassem, na kukimbilia uhamishoni katika nchi ya Misri alikoishi kwa miaka minne. Saddam alirejea Baghdad Februari, 1963 na kujiunga na chama cha Baath kilichoingia madarakani katika mapinduzi ya kijeshi na kuondolewa madarakani miezi tisa baadaye, na viongozi wa chama hicho kutupwa gerezani.

Hata hivyo alichaguliwa kuwa Makamu Katibu Mkuu wa chama hicho akiwa gerezani huku wenzake wakiendeleza harakati za mapinduzi ambayo yalifanikiwa miaka mitano baadaye. Akiwa mwanachama na kiongozi wa chama cha Baath Arab Social Party kilichofuata sera za ujamaa wa kiarabu na uchumi ulioendelea, Saddam alichukua jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba anastawisha maisha ya wananchi wake huku akikazana kuleta mapinduzi ya kiuchumi miongoni mwa mataifa yaliyoko kwenye jumuiya ya kiarabu.

Saddam ambaye ameacha wajane watatu; Sajida Talfah, Nidal al-Hamdani na Samira Shahbandar alikuwa miongoni mwa viongozi wa mstari wa mbele katika mapinduzi yaliyokiweka chama chake madarakani Julai 1968 baada ya kumuondoa madarakani, Abdul Mohamed Aref, na kukiwezesha kutawala Iraq kwa kipindi kirefu.

Akiwa Makamu wa Rais chini ya uongozi wa mpwa wake, Jenerali Ahmed Hassan al-Bakr, Saddam aliongoza na kuendekeza chokochoko baina ya utawala na viongozi wa kijeshi katika utawala huo na kuimarisha wapambe wake katika safu ya uongozi na usalama kwenye kada ya utawala kwa lengo la kudhoofisha uongozi wa kijeshi.

Wakati rais wa nne wa Iraq, Jenerali Hassan al-Bark akijihusisha na kazi ya kutaifisha kampuni kubwa ya uchimbaji mafuta ya Iraq Petroleum Company na kuyalipa makampuni mengine ya kigeni na kuyaondoa nchini, Saddam alikuwa akijikita katika kufanya kazi ya kuhakikisha kuwa anaendelea kujijenga katika uongozi wa Iraq.

Utawala wa Baath ulikabiliwa na upinzani kutoka kwa Wakurdi ambao waliendeleza chokochoko dhidi ya utawala wa Baghdad na kupelekea kusainiwa kwa kwa mkataba wa mpaka baina ya Iraq na kiongozi wa kidini wa Iran, Shah mwezi Machi 1975; ingawaje Shah huyo aligeuka na kuendelea kuwapa misaada wakurdi hao.

Kiongozi wa Iraq, Jenerali Hassan al-Bark, alilazimika kustaafu kwa kilichoelezwa kuwa na umri mkubwa mwezi Julai 1979 na Saddam ambaye alikuwa muislamu wa madhehebu ya Sunni alichukua uongozi wa taifa hilo ingawaje wadadisi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa Jenerali huyo alilazimika kustaafu kufuatia saddam kujiimarisha na kuchukua uongozi usio rasmi wa taifa.
Ghasia zilizoendelezwa na Wakurdi katika mpaka wa Iran na Iraq ilipelekea kuanza kwa vita vilivyodumu kwa miaka minane kati ya Iran na Iraq, mwezi Septemba 1980. Iraq ambayo imetokea kuwa wahasimu wakubwa wa Marekani, katika vita hivyo ilikuwa ikisaidiwa na taifa hilo kubwa duniani dhidi ya Iran katika vita vilivyogharimu maisha ya watu wapatao milioni moja .

Alipigana vita hivi kwa lengo la kuondoa tishio la kikabila na kidini lililokuwa likiukabili utawala wake kutoka kwa makundi yaliyokuwa yakitaka kujitawala au kupewa uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe ndani ya mipaka ya kikabila na kidini nchini Iraq. Wakati wa vita hivyo, Saddam alijulikana kama shujaa pekee wa Kisunni aliyesimama kidete dhidi ya wahasimu wa Marekani na Israel katika jumuiya ya kiarabu na hii ilimjengea heshima mbele ya mataifa hayo ambayo yalikuja kumgeuka baadaye kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa amani mwezi Agosti, 1988 kati yake na Iran.

Katika vita hivyo, kiongozi huyo wa Iraq alijivunia nguvu za maaskari wake 190,000, vifaru 4,500, magari ya kivita4,000, ndege za kivita 500 na helikopta 400 dhidi ya Iran ambayo ilikuwa na nguvu za wanajeshi 305,000, wanamgambo 500,000, vifaru 1,000, ndege za kivita 65 na helikopta720. Ingawaje chaguzi kadhaa za urais zimeendeshwa kipindi cha utawala wake, Saddam aliwachukulia hatua kali na za mateso watu wote walionyesha kuupinga utawala wake, waliokataa kupiga kura au waliopiga kura za kumpinga.


kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post