MLANGO ULIOJIFUNGA WENYEWE PUNDE BAADA YA MTEMI SERERI KUFARIKI. TANGIA MWAKA 1947 HAUJAFUNGULIWA MPAKA LEO, KILA WALIPOJARIBU ULISHINDINAKANA KUFUNGUKA, JE SABABU NI NINI?.
Ndugu zangu naomba leo tuzungumzie hasa Kujifunga kwa mlango huu wa nyumba ya mtemi wa kondoa Sultani Salim Kimolo jina lingine Mtemi huyu alikuwa akiitwa SERERI.
Alikuwa mtawala wa kijadi Wa kondoa makao yake yalikuwa utemini kolo katika jengo hili ambalo mlango ulijifunga mwaka 1947. Jengo hili lilijengwa mwaka 1898 hadi leo jengo hili lipo, Mbele ya nyumba hii ndipo ulipo mlango huu mkubwa uliojifunga wenyewe.
Mlango huu ulijifunga baada tu ya jeneza la marehem mtemi sultani Salim Kimolo kutolewa kupitia mlango huo kupelekwa katika nyumba yake ya milele. Jeneza lilipo toka tu, Kulitokea kama kaupepo hivi kalikuwa kanavuma, Kutokana na kaupepo kale Ghafla waliona mlango umejifunga wenyewe.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema Mara baada ya jeneza kutolewa tu kulitokea upepo kutokana na upepo huo mlango huo ulijifunga kuanzia hapo mlango huo haujawahi kufunguliwa. Zilifanyika jitihada za dhati kuufungua mlango huo lakin jitihada hizi zilishindikana ndipo mrithi wake Sultani kheri. Kimolo Akapiga marufuku kuwa mlango huo wauache wasiufungue.
Wauache hivyo hivyo kama ulivyo mlango huo. Hadi leo Baada ya mlango kujifunga watu huwa wanazunguka kuingia ndani ya nyumba hii kwa kupitia mlango wa nyuma. Mrithi wake Kheri kimolo alitawala hadi mwalimu nyerere alipopiga marufuku tawala zote za watemi na machifu. Hadi utawala wa mtemi kheri ulipo fika kikomo mlango huu haujawahi kufunguliwa. Bado mlango huu haujafunguliwa hadi leo hii.
Kwa wale Wanaotaka kwenda kuuona mlango huu ni rahisi sana kama unatoka Arusha au DODOMA, Ukifika Sehemu inaitwa kolo shuka. Halafu angalia upande wa Magharibi Utaona nyumba zimejitenga zenyewe. Hapo ndiyo utemini na ndiyo yalipo majengo hayo, ukiona vipi uliza hapo stendi utapelekwa
Tags
Historia