TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

HISTORIA YA NENO SHIKAMOO NA MARAHABA

HISTORIA YA NENO SHIKAMOO NA MARAHABA
Ukweli ni kwamba kuna idadi kubwa ya watu wanatumia neno shikamoo kama sehemu ya kuonyesha heshima au salamu kwa mtu aliyekuzidi umri(yaani maamkizi). Lakini jambo la msingi hapa ni kuelewa maana na historia ya na maneno “Shikamioo” na “Marahaba”.

 Na wengi tunafahamu kuwa kila jambo lina mwanzo wake na mwanzo wake huwa una sababu zake na sababu zake huwa na historia yake. Ifahamike kuwa kabla ya miaka ya 600 BK au BM, Wabantu walishafika Pwani ya Afrika mashariki. Na wapo wanaomini kuwa wakazi wa kwanza na walioleta maendeleo Pwani ya Afrika mashariki ni Waarabu ambao waliwaita Washirazi. Na ukweli ni kwamba Wabantu walishapata kuishi hapo na hata wageni waliofika walikiri suala hilo. Na kwa kuwa Wabantu walipata kuishi hapo walikuwa na mitindo yao wa maisha na walikuwa wakiheshimiana. Kikubwa zaidi Wabantu walikuwa na salamu zao. 
Kwa mfano Wazaramo (historia yao itaandikwa) walikuwa na salamu yao kama ifuatavyo, aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia  “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni. Lakini mambo yalibadilika pale walipokuja Waarabu na kuanzisha biashara ya utumwa. Na hapo tukapata makundi mawili yaani “mtumwa” na “bwana” na mtumwa alipaswa kumuamkia Bwana  kwa neno la “Nashika Miuu” akiwa na maana ya  “Nashika Miguu”. 

Na kila mtumwa alipaswa kujua na kutambua salamu hii. Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake. kuanzia miaka ya 600-1700, salamu hii ilikuwa ikitumika maeneo ya Pwani tu. Na kuanzia miaka ya 1700 mwishoni na 1800 mwanzoni Waarabu walianza kuingia maeneo ya ndani ya Afrika mashariki. 

Na kila walipofika salamu hii waliitumia na baadhi ya machifu walipenda sana salamu hii. Na kujikuta wakiwa na matamshi tofauti juu ya salamu hiyo. Na kwa wakati wote huo ilikuwa ni salamu ilikuwa ni Nashika Miuu na sio Shikamoo kama ilivyo sasa. Na kutokana na watu tofauti kutumia salamu hii, wapo waliotamka Shikamuu kama neno moja. Na mpaka miaka ya 1930, kipindi ambacho Kiswahili kinafanyiwa usanifishaji ndipo tukapata neno shikamoo. Na kuhusu neno Marahaba, lina maana ya asante. Na neno hili huitikiwa na Yule anaeamkiwa (Bwana) ambaye miguu yake imeshikwa na mtumwa. Na mpaka sasa salamu hii inatumiwa sana na Watanzania wengi licha ya kuwa na salamu zao za kikabila. 
Na ukweli ni kwamba neno hili hata kiingereza chake halina., yaani hatuna msamiati wa neno shikamoo kwenye lugha ya kiingereza. Hii ndio historia fupi ya neno Shikamoo na Marahaba.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post