📌 *JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE NYUMBANI*
*MAHITAJI:*
🔗Maji 1/2 kikombe
🔗Maziwa ya unga kikombe 1
🔗Siagi 1/2 (unsalted butter)
🔗Sukari kikombe 1
🔗Unga wa cocoa kikombe 1
🔗Vanila kijiko 1
*JINSI YA KUPIKA.*
*1.* paka mafuta sinia au tray.
*2.* Weka maji na sukari ktk sufuria acha ichemke mpaka ukigusa kati ya vidole iwe inanata,kisha weka vanila na siagi ikiyeyuka tia cocoa.
*2.* Koroga ichanganyike vizuri kisha weka maziwa ya unga kisha anza kusonga kama ugali mwanzoni itakua donge laini songa hadi liwe gumu kiasi kisha mwaga kwenye ile sinia au tray ulioipaka mafuta,itandaze vizuri kisha kata vipande acha ipoe ikisha poa toa vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa. Enjoy
Tags
Jikoni Leo