Habari za muda huu wapendwa followers wetu
Loe tumeangazia vyakula vya asili vya watu jamii ya wanyawezi wenyeji wa mkoa huu wa tabora.
katika makala hii tumeangazia moja kati ya mboga ya asili pendwa kwa wanyamwezi wa tabora
mboga hiyo sio nyingine bali ni mboga ya asili ijulikanayo kama NSANSA.
NSANSA Hii ni moja kati ya mboga ya asili na mboga pendwa kabisa ya wanyamwezi mboga hii asili yake inatokana na majani ya mmea wa kunde na mmea wa muhogo/kisamvu
asili ya mboga hii inasadikika kuanza kutengenezwa na kuwa maarufu kipindi cha utemi hasa kipindi cha mtemi milambo ikiwa na lengo la njia ya kuhifadhi chakula ili kiweze kudumu kwa muda mmrefu na bado kiwe rafiki kwa matumizi
JINSI INAVYO ANDALIWA NSANSA
Kama tulivyo tangulia kusema katika utangulizi wetu mboga hii inatokana na mmea wa kunde pamoja na mmea wa muhogo/kisamvu
hivyo jinsi ya kuandaa mboga hii nikama ifuatavyo.
.Chuma majani ya laini ya kunde ama majani laini ya mmea wa muhogo
.Chambua kwa kutoa migongo ya majani ili libaki jani pekee
.Anika juani kwa muda wa masaa 24 mpaka 42 kulingana na hali ya hewa
.Kisha yakisha kauka yapekeche taratibu kama unayasanga kwa mkono [fanya taratibu]
.Kisha chukua majani hayo osha kwa maji mengi ili kuondoa mchanga uliopo katika majani hayo
. Chemsha mpaka yalainike kisha weka tena juani kwa muda kidogo kisha unaweza kuyapikicha tena kupunguza ukubwa wa majani kama ukihitaji
. Baada ya yote sasa mboga yako ya nsansa inakua tayari imekamirika kwa asilimia 100.
JINSI YA KUPIKA
MAHITAJI
.Jiko
.Sufuria
.Kitunguu maji [1]
.Nyanya maji [1 ama2]
.Mafuta kiasi ya kupikia
.Karanga ya kusangwa [kama utahitaji]
. Chukua kiasi cha mboga upendacho
. weka kwenye maji safi kwa muda kiasi kuondoa kabisa mchanga
. Chemsha mboga mpaka iive
. Kisha tengeneza mchuzi wa nyanya na kitunguu pepmbeni
. kisha changanya na mboga yako
. iweke karanga yako ya kusagwa katika mboga yako [kama utahitaji]
. Subiri kwa muda wa dk 10
' Mboga itakua tayari kuliwa, inafaa sana kuliwa katika ugari ama wali
Tags
TaboraYetu
Nice one
ReplyDelete