﷽
*Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh*
*HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD*
*NO:1️⃣*
Baada ya Nuhu(a.s) Mtume aliyemfuatia ni Nabii Hud(a.s). Hud(a.s) alitumwa na Mola wake kuwalingania kabila (taifa) la ‘Ad. Kabila la ‘Ad lilikuwa likijulikana kama ‘Ad-al-ram au ‘Ad-Ula. ‘Ad walikuwa wakiishi kusini ya Bara Arab, eneo la kati ya Oman hadi Hadharamut na Yemen. Akina ‘Ad waliongoza katika teknologia ya kujenga majumba marefu katika makazi yao:
“Je, hukuona jinsi Mola wako alivyowafanya ‘Ad? Iram (waliokuwa)wanamajumba mar efu mar efu. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika miji. (89:6-8)
Baada ya muda kupita, ‘Ad waliacha mafundisho sahihi ya Nabii Nuhu(a.s) ya kumpwekesha Allah(s.w) na wakarejea tena kwenye kuabudia masanamu wakiongozwa na wakuu wa jamii. Ndipo, Hud(a.s) akatumwa na Mola wake kuhuisha tena Uislamu.
“Na kwa ‘Ad (tulimpeleka) ndugu yao Hud akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Allah, nyinyi hamna Mungu ila yeye. Basi hamuogopi?” (7:65)
Mbinu za Hud(a.s) Katika Kufikisha Ujumbe
Katika kulingania Uislamu kwa watu wake, Hud(a.s) alitumia mbinu zifuatazo:
Kwanza alijieleza kwa uwazi na kuwanasihi watu wake:
“Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sio mpumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu. Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu. Na mimi kwenu ni (mtu) nasihi muaminifu.(7:67-68)
Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu kwa (ulimi wa) mtu aliye mmoja katika nyinyi ili akuonyeni? (Muabuduni Mwenyezi Mungu) na mkumbuke alivyokufanyeni Khalifa baada ya watu wa Nuhu.Na akakuzidisheni sana katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.” (7:69)
Pili aliwapa hoja kwanini wanalazimika kumuamini Allah na kumuabudu ipasavyo.
Mcheni yule ambaye amekupeni haya mnayoyajua.” “Amekupeni (chungu ya) wanyama na watoto wanaume.” “Na mabustani na chemchem, (mito).” (26:132-134)
Tatu, aliwabashiria kupata malipo mema hapa hapa ulimwe nguni endapo watamcha Allah(s.w) ipasavyo:
“Enyi watu wangu! Ombeni msamaha kwa Mola wenu (kwa mabaya yenu yaliyopita) kisha mtubie kwake, atakuleteeni mawingu yateremshayo mvua tele, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu (mlizonazo). Wala msikengeuke kuwa waovu.” (11:52)
Nne, aliwahofisha watu wake na adhabu kali ya Allah(s.w)
iwapo watamuasi.
“Na kama mtarudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya makhalifa (wakazi wa mahali hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi; wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.” (11:57)
“(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao Hud.‘Je, hamtamu ogopa (Mwenyezi Mungu hata nikikutajieni adhabu yot itakayokufikieni kwa mabaya yenu mnayoyafanya)? Bila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.” (26:124-125).
Tano,aliwafahamisha kwa uwazi watu wake kuwa hakutarajia kupata malipo ya Utume wake kutoa kwao.
“Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira juu ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa yule aliyeniumba. Basi hamyatii akilini (haya ninayokuambieni)?” (11:51).
“Wala sikutakieni juu yake ujira, ujira wangu haupo ila kwa
Mola wa walimwengu wote.” (26:127)
*ITAENDELEA...................*
Tags
visa Vya kale