KANUNI UNAZOTAKIWA KUZINGATIA KUHUSU FEDHA.
*KANUNI NO. 1*
Kamwe usikope fedha na hasa ya riba kwa ajili ya kuanzishia biashara (isipokuwa kwa mkopo ambao marejesho yake yanatokana na mshahara. Hii ni kwa sababu biashara huchukuwa muda mrefu kusimama yenyewe na kuanza kupata faida wakati marejesho ya mikopo mingi huanza mwezi baadaye ama hata kabla. Hivyo kamwe usikope mkopo ili
kuanzishia biashara ukitegemea hiyo hiyo biashara iweze kukulipia mkopo pamoja na riba yake.
*KANUNI NO 2*
Kamwe usitumie fedha ambayo bado hujaipata / hujaimiliki. Wala usimuahidi mtu fedha kwa kutegemea fedha uliyoahidiwa na mtu mwingine. Usije ukamsikia mtu akikuambia "fulani njoo kesho ofisini kwangu saa 3 asubuhi uchukuwe shs. Milioni 2 halafu wewe akaenda dukani kukopa vitu ukitegemea kulipa utakapokuwa umechukua ile fedha uliyoahidiwa.
*KANUNI NO. 3*
Kama una nia ya kuweka akiba, kila upatapo fedha hakikisha huanzi kununua mahitaji yako kwanza kabla hujatenga fedha unayotaka kuweka akiba ukitegemea kwamba utaweka akiba kile kitakachobaki. Kwa kawaida huwa hakuna fedha inayobaki kwa sababu ilimradi fedha ya kutumia ipo, matumizi huwa hayakosekani na vitu ya kununua huwa vinaalikana lakini kama fedha ya kutumia haipo unaweza kutafuta njia nyingine ya kukabili changamoto zako. Ndiyo maana ni vema utaweka fedha ya akiba mbali kabisa na wewe na hiyo itakufanya ujione huna fedha kabisa.
*KANUNI NO 4*
Iwapo utapata fursa ya kukutana na watu mwenye mafanikio kiuchumi kamwe usiwaombe fedha. Waombe ushauri /waeleze mawazo yako jinsi unavyofikiri namna utakavyofanya ili kupata fedha. Wanaweza wakaamua wao mwenyewe hata kukupa fedha watakapoona kuwa mawazo yako ni mazuri na ya msingi. Lakini kamwe lengo lako lisiwe kupata fedha toka kwao.
*KANUNI NO 5*
Kamwe usitunze mbegu yako bila kuipanda. Watu wengi wanaishia kwenye kuweka akiba tu. Ni vigumu sana, kwa mfano kwa mfanyakazi, kuweka akiba tu na kupata mahitaji yote yatakayomfanya awe na kiwango kile kile cha maisha hasa hasa baada ya kustaafu. Unapoweka akiba hiyo ni mbegu; ipande. Unapoziweka tu mbegu nyingine huanza kuoza (thamani yake huweza kupungua kwa sababu ya mfumuko wa bei na vitu kama hivyo.) Ndiyo maana ni vizuri kujifunza aina mbalimbali za uwekezaji unazoweza kutumia kukuza akiba yako. Hapa simaanishi kwamba lazima uwekeze kwenye biashara, kwa sababu unaweza kupoteza kirahisi fedha zako za akiba, hapa nazungumzia kuifanyia uwekezaji kama kununua hisa.
*KANUNI NO 6*
Kamwe usimkopee fedha mtu ambaye hutaki kumpoteza ama kukosana naye. Pale ambapo utamkopea hakikisha ndani ya moyo wako uwe umeamua kwamba ikitokea huyo mtu hajakulipa, hutakufa ukimnung'unikia huyo mtu. Wala hutampoteza huyo mtu kama rafiki. Kama utaona mtu utakaye mkopea anaweza akashindwa kurejesha mkopo na mkabaki marafiki basi mkopee. Lakini ukiona itakufanya hata umchukie pamoja na hata ukoo wake tafadhali mshauri huyo rafiki aende benki.
*KANUNI NO 7*
Kamwe usije akaweka sahihi yako kumdhamini mtu kwenye mambo ya fedha kama hutaki na hauko tayari kuja kumlipia huyo mtu hapo baadaye. Je unahitaji nieleze zaidi ya hapo kwa hili? Hapana, linajieleza lenyewe.
*KANUNI NO 8*
Epuka kuweka fedha ambayo hujapanga kuitumia ndani ya kipindi kifupi sehemu ambayo inafikika kirahisi. Kwa mfano, usitembee na shs. Laki moja wakati ambapo ulichopanga kununua ama kufanya kinagharimu shs. Elfu ishirini tu. Utavikuta na kuvitamani vitu ambavyo hukupanga kuvinunua ama kuvifanya.
* KANUNI NO 9*
Kamwe usitumie fedha kwa kitu ambacho hakina ulazima kwako kwa wakati huo. Kabla hujatoa fedha yako kulipia kitu fulani hakikisha kwanza unajiuliza swali hili "kitatokea kitu gani kama sitanunua kitu hiki?" Kama utaona unaweza kuishi vizuri na bila kuathirika na kukosekana kwa kitu hicho tabasamu tu na ondoka zako,
* KANUNI NO 10*
Kamwe usifanye kitu ili kujionesha kuwa wewe ni tajiri. Kwa mfano kutumia shs elfu sabini kununua kitu kwa kuwa tu kinauzwa supermarket wakati kitu hicho hicho ungekipata Kariakoo kwa elfu thelathini. Kufanya hivyo ni kosa kubwa kikanuni isipokuwa kwa wale waliovuka kiwango cha hadhi ya kifedha kimaisha.
* KANUNI NO 11
Kamwe usiwe na tabia ya kutumia kipato chako chote ama zaidi ya kipato chako. Kufanya hivyo ni sawa na kuwa na tanki la maji lenye bomba dogo la kuingizia maji wakati hilo tanki lina bomba kubwa la kutolea. Hata siku moja haliwezi kujaa. Na ikawa bomba la kuingizia maji litaendelea kupungua ukubwa wake ndivyo ambavyo tanki litaisha maji haraka. Lakini ukifanya kinyume chake yaani bomba kubwa liwe la kuingizia maji na lile dogo liwe la kutolea, hapo maji yatajaa na kufurika. Hivyo hakikisha kila wakati na muda wote unaongeza ukubwa wa bomba linaloingiza na kupunguza bomba linalotoa.
*KANUNI NO 12*
Kamwe usiwe na mipango ya muda mfupi tu na kusahau kuwa na mipango ya muda mrefu pia na wala usikazanie kuwa mipango ya muda mrefu tu ukasahau kuwa pia na mipango ya muda mfupi. Dada mmoja aliambiwa ardhi ni mali. Basi akakusanya fedha kwa muda mrefu akanunua heka 30 za ardhi. Kwa sasa ana ardhi lakini hana hela za matumizi wala za kuendeleza ardhi yake na haoni hata jinsi ambavyo atatumia ardhi yake ili apate fedha hata kwa siku za usoni. Hebu jiulize; kuwa na heka 30 za ardhi huku huna fedha ya chakula kwa familia yako au ya kumpelekea mtoto wako hospitali huo ni utajiri au umaskini? Nadhani huyu dada alijali zaidi mipango ya muda mrefu akasahau mipango ya muda mfupi.
LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na
kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na
kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika
Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya
na Makampuni mbalimbali.
5. ** Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya
electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na
vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. ** Kuuza software; mfano Antivirus, Operating
Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit,
socks,
batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo,
Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na
vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. ** Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza
popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta
na zinazotumia mafuta
16. ** Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na
hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. ** Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. ** Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za
mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement,
vifaa
vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba
na
miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building
contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua
(solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya
solar n.k
34. ** Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. ** Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters,
HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa
vingine.
40. ** Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. ** Kufungua kampuni ya kutoa huduma za
internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. ** Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au
mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. ** · Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi,
Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku,
Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51. ** · Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na
kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. ** Kuchimba/Kuuza Madini
56. ** Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na
fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. ** Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika
sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. ** Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki
na
magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi
ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. ** Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding
machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. ** Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha
wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya
redio na televisheni
79. ** Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni
(TV
Games)
80. ** Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na
winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. ** Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali
zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom,
TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. ** Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe,
mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa
barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha,
kutoboa na kuchana mbao
92. ** Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme
wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. ** Kukodisha matenki ya maji**
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na
kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA,
TIGOPESA, EZY PESA
100. ** Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi
(Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and
fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya
matumizi
ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe,
vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. ** Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya
anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. ** Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa
kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. ** Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. ** Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. ** Kununua nyumba katika Maghorofa
(Apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/
sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. ** Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea
fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya mlm (network marketing)
149. ** Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya
kilimo. 151. kutengeneza sabuni za kunawia mikono na kuziuza 152. kutengeneza dawa za kusafishia vyoo, mabafu na
kuziuza 153. kuanzisha kampuni za usafi na kutafuta tenda ktk
taasisi mbalimbal 154. kuanzisha botanical garden na kufungua duka la
chemikali na kusaka tenda mashuleni na vyuo 154. n.k,...
KAMA YOTE HAYA UMESHINDWA KUPATA LA
KUFANYA, WEWE UTAKUWA USHAPOTEA,
ENDELEA NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU
SERIKALI.
Mtumie na mwenzio aone
Tags
Maarifa