I am legend imetoka 2007,ndani ya hii movie tunaonyeshwa Jiji Zima la newyork city liliangamizwa na mavampire na binadamu wote walio salia waligeuka kuwa vampire ,binadamu pekee aliye Baki hai pasi na kuathirika ni will Smith peke yake
Kutokana na taaluma aliyo kuwa nayo ya udoctor alikuwa anafanya majaribio ya kujaribu kuwatibu watu na wanyama wengine walioathirika na kugeuka kuwa vampire Ili kurejea katika hali zao za kawaida
Good news ni kwamba maandalizi ya sehem ya pili tayali yameanza,ndani ya hatua ya pili tutakuwa na Michael b Jordan,wengi wanajiuliza will Smith anarudi vipi Kwenye part two ya I am legend Wakati hatua ya kwanza tuliona akijilipua na bomu ndani ya maabara na kupoteza maisha na wale vampire waliovamia nyumba yake
Lakini Ukweli ni kwamba hii movie ilitoka mala mbili,moja ndio hiyo tunaonyeshwa will Smith anajilipua na bomu na kufa na wale vampire,na nyingie inaonyesha yule mkuu wa mavampire anamchukua yule vampire wa kike aliyekuwa kakamatwa na kufanyiwa majaribio maabara na will Smith Ili kumrejesha katika hali ya ubinadamu
Kwahiyo hatua ya pili itaendelezea hapo baada ya yule kiongozi wa mavampire kumchukua dem wake aliyekamatwa na will Smith na kutokomea nae.✍️
Tags
Movies na Series