NIKUMBUKENI WANANGU
Ilikuwa ni siku kubwa sana kwa watoto watatu wa familia moja.Ilikuwa ni siku ya kufungua kampuni kubwa ya pamoja.Siku ambayo ilikuwa imeudhuliwa na watu wengi wenye wazfa mkubwa.Viongozi wa serikali,wafanya biashara wakubwa na watu wengine ambao walihudhuria hafla hiyo.Lakini wakati sherehe ile ilipokuwa ikiendelea ulifika muda wa kutoa pongezi kwa vijana hao watatu.
Watu walitoa pongezi zao na mwisho wa siku mc alisimama na kuwaambia kwamba kuna ujumbe amepewa kama zawadi alikuwa anataka kuusoma.Kutokana na sifa waliyokuwa nayo wale watoto wakamwambia mc ausome ili kila mmoja aweze kusikia nini ambacho kimeandikwa katika ujumbe ule wa pongezi.Mc akliufungua ujumbe ule na kuanza kuusoma huku watu wote kwenye ukumbi wakiwa kimya.
“Kwanza naomba mnisamehe kwa hiki nilichokiandika.Naomba mnisamehe kwasababu nahisi nitakuwa nawatia aibu kwa marafiki zenu pamoja na watu wengine wa karibu.Naomba mnisamehee Mama yenu naweza nikawa nimekurupuka kuyaandika haya.Naomba mnisamehee mama yenu labda kutokana na umri wangu kuwa mkubwa nahisi ninaweza kuwa nimerudia akili zangu za utotoni.Ila wanangu nitajaribu kutuliza akili yangu ili niandike machache ambayo yananitia uchunguMc aliongea kisha akawaangalia watu ambao walikuwa pale ukumbini na kuendelea
Nawakumbuka sana wanangu kipindi kile mpo wadogo.Nakumbuka sana vile mlivyokuwa mnaniita mama bila ya kukoma.Nilikuwa nahisi furaha sana kila mlipokuwa mnaniita.Siyo kwenye wakati wa furaha tu ila hata wakati ambao mliokuwa mnahitaji msaada wangu.Nilikuwa napata amani ya moyo nikiona watoto wangu mkitambua kwamba mimi ni mama yenu na mnahitaji msaada wangu.
Lengo langu siyo kuzungumza habari za miaka ya nyuma kipindi mpo watoto.Lengo langu ni kuzungumzia haya ya kipindi hiki ambacho kila mmoja wenu anaakili ya kiutu uzima.Najua wapo mnaoitwa Mama na wapo mnaoitwa Baba,Hongereni sana katika ilo ni hatua kubwa sana kuanzisha familia.
Mama yenu kwa upande mwingine ni mzima ila utu uzima kidogo unanifanya niugue mara kwa mara.Nadhani mtakuwa mnalikumbuka lile shamba la bondeni ambalo tulikuwa tunalima mpunga,Kwasasa nashindwa kulima kwasababu nguvu ya kushuka kule imeniishia na sina uwezo wa kuwalipa vibarua.Siyo nia yangu kuzungumzia hili,ila imeninibidi kuzungumza ili niwaonyeshe kiasi gani nguvu imepungua mwilini mwangu.Kuna muda inanilazimu kuinuka na kulima kwenye lile shamba la karibu na nyumbani ili nijipatie chakula ambacho kimekuwa adimu sana kwangu kwa kipindi hiki.Nadhani mnamkumbuka vizuri Hamida mtoto wa mzee Salehe,Huyu nitamzungumzia mbele kidogo.
Mnaikumbuka ile nyumba ambayo aliniacha nayo marehemu Baba yenu,ile nyumba ambayo kipindi kile mpo wadogo milikuwa mnasema ni mbaya inatakiwa niivunje ili nitengeneze nyingine,najua mlikuwa mnaongea kama watoto ila kiukweli hata mimi nilitamani kufanya hivyo ila uwezo sikuwa nao.Hela ambayo ningeitumia kutengenezea walau kibanda kingine ndiyo hiyo nilikuwa naibana ili mpate kwenda shule na kutafuta chakula kwaajili yetu.Nilitamani sana siku moja watoto wangu mpate elimu ambayo ingeweza kufungua maisha yenu.Nilitumai Elimu ambayo mngeipata mngeweza kuitumia kwenye kutafuta mbinu ya kutengeneza nyumba hii.
Nadhani kila mmoja anaikumbuka ile siku ambayo aliondoka hapa nyumbani.Kila mmoja nilimpatia baraka ili afanikiwe katika maisha yake.Kufanikiwa siyo kuwa na hela nyingi sana ila hata kama una afya ya kutosha ni moja ya mafakinio yako.Baraka nilizowapa wanangu zilikuwa ni za kheri na kuamini kuwa uko muendapo mtapata afya njema pamoja na mafanikio mengine.
Nashukuru Mungu kwa habari ambazo nazipata mnaendelea vizuri.Nashindwa kuzungumza na ninyi moja kwa moja kwasababu mara nyingi nikiomba simu na kuwapigia mnasema kwamba mpo busy na kazi.Ni kweli maandiko yanasema kwamba asiyefanya kazi na asile na ndiyo maana mkiniambia kwamba kazi zinawabana uwa naelewa mapema.
Ni kweli wanangu kazi ni muhimu kwa mustakabali wa maisha yetu ila mimi Mama yenu napenda walau kusikia sauti ambazo nilishazizoea tangu mpo watoto.Natamani sana kusikia lile jina la Mama ambalo mlikuwa mnaniita.Sijajua kwanini nakuwa na hamu sana na ninyi wanangu,naweza nikasema labda ni upendo wangu kwenu.Hivi kuna hata mmoja wenu ananikumbuka kama ninavyowakumbuka?.Msiuzunike wanangu maana yangu haikuwa mbaya kuwauliza swali ili.Lakini nimependa kuwauliza kwasababu miaka sasa imekatika pasipokuwa na mawasiliano nanyi au mtu yoyote kuja hapa nyumbani.
Poleni sana na majukumu pia hongereni kwasababu nimesikia kwamba mmefungua kampuni kubwa ya pamoja.Hiyo ni hatua kubwa sana wanangu ila mmesahau hiyo hatua ilianzia huku nilipo.Najua kwasasa mnaweza mkaona hakuna umuhimu ila ile mihogo ya kuchemsha ambayo mlikuwa mnakula asubuhi kabla ya kwenda shule ndiyo ilikuwa inawapa nguvu mpaka sasa mnakula vyakula vya kileo.
Wanangu mimi Mama yenu wala sihitaji Tunu ya dhahabu kwa malezi mazuri niliyowapatia,Bali nahitaji kumbukumbu yenu kwangu,ni miaka mingi sana imepita pasipo kuwaona ninyi wote.Sijajua nini tatizo?.Kwa umri niliofikia sihitaji kupewa mali wala fedha,nahitaji kuwaona wanangu ambao ndiyo furaha yangu.Nahitaji tu kuwaona wanangu ili kabla sijafa nitimize yale maneno ambayo nilimuahidi Baba yenu kwamba nitawatunza mpaka pale nitakapokamilisha safari yangu hapa Duniani.
Kwako mwanangu wa kike.sitopenda nikuambie mengi ila tambua kwamba kuna siku utaitwa Mama.Naomba umpe mwanano malezi bora atakapokosea mkumbushe kama mimi nilivyowakumbusha leo.Narudia tena kusema Hongereni sana kwa kufungua kampuni,hongereni sana kwa mafanikio mliyoyapata.Ila wanangu napenda kuwakumbusha kwamba mafabnikio ya kwanza ni Upendo.
Sina mengi ya kuzungumza Barua hii nimempatia Hamida mtoto wa mzee Salehe najua mtakuwa mnamfahamu.Kipindi mnaondoka yeye alikuwa ni mdogo.Hamida amekuwa msaada wangu mkubwa sana hapa kijijini.Yeye mara nyingi ndiyo uniangalia na hata chakula yeye ndiyo ananipatia.Namshukuru sana Hamida kwa mambo mengi anayonifanyia.Nimempa ujumbe huu aulete kwenu kwenye siku muhimu kama ya leo,Siku ambayo mna furaha ya kufungua kampuni yenu laakini furaha yenu inaweza kuingia dosari baada ya kusoma ujumbe huu.Naomba mnisamehee wanangu siyo lengo langu kuwakatisha furaha yenu ila lengo langu ni kuwakumbusha kwamba Mama yenu nipo.Niwatakie sherehe njema na Mungu awasimamie kweny kila jambo.NIKUMBUKENI WANANGU
Ni mimi mama yenu
Baada ya ujumbe ule kusomwa hali ya pale ndani ilibadilika na kila mtoto alikuwa analia.Sherehe ilikuwa chungu,KIla mmoja alianza kumkumbuka mama yake,Hakika ulikuwa ni ujumbe ambao uliwarudisha miaka mingi mno kipindi amabacho mama yao alipokuwa na nguvu ya kuwahudumia.Ni miaka sasa imekatika tangu watoke kijijini na kuishi mjini pasipo kumkumbuka mama yao.Watoto wale walilia sana kiasi kwamba ukumbi mzima ulibadilika ikawa sehemu kuwabembeleza.
Ikawabidi watoto wale watatu wafunge safari ya kuelekea nyumbani kwao ambapo walikuta hali ya sitofahamu.Walikuta nyumbani kwao kuna msiba na aliyekuwa amefariki ni mama yao.Uzuni ilizidi kutawala katika nyuso zao lakini waliletewa karatasi ndogoi amabyo ilikuwa na ujumbe mfupi tu
"Poleni wanangu kwa kutokuwaambia hili,Mwanzoni nilisema naumwa kwasababu ya uzee ila kiukweli mama yenu nilikuwa na magonjwa ambayo nililazimika kuja huko mlipo ila kutokana na ubusy wenu,nilishindwa kuwaambia.Nafurahi kwenda kumuona Baba yenu na kumwambia nimetimiza kile nilichomuaidi.Naomba mnipumzishe pembeni ya mume wangu”
Ujumbe ndiyo ulisomeka hivyo.Watoto wale walilia na kusaga meno huku kila mmoja akitamani walau mama yao aamke ili aweze kuomba msamaa.Kila mmoja alikuwa akijilaumu kwa nafasi yake.Hakika yalikuwa ni majuto makubwa mno.
MWISHOO
Tags
Visa vya Kusisimua