TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SIRA YA NABII HUD ALAIH SALAAM 03

*SIRA YA NABII HUD ALAIH SALAAM NO 3*


*NO:3️⃣*



 Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake

Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.s), hakutetereka katika msimamo wake wa kutangaza Ufalme wa Allah(s.w) na kufikisha ujumbe wake. Hakutetereka kwa sababu alitegemea ulinzi wa yule aliyemtuma, mwenye uwezo juu ya kila kitu kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



“..........Akasema (Hud) mimi namshuhudia Mwenyezi Mungu, nanyi shuhudieni ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowashirikisha (na Mwenyezi Mungu) mkaacha (kumuabudu)



yeye (pekee). Basi nyote nifanyieni hila (za kunidhuru) kisha msinipe muhula wowote”.(11:54-55).



Mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa (Mwenyezi Mungu) anamsanifu atakavyo. Bila shaka Mola wangu yuko juu ya njia iliyonyooka.(11:56)





Na kama mkirudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya Makhalifa (wakazi wa mahala hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni mwenye kuhifadhi kila kitu.”. (11:57)



Ushindi wa Nabii Hud(a.s) Juu ya Makafiri

Makafiri walivyozidi kutakabari na kuzidisha fisadi katika ardhi ikiwa ni pamoja na kutaka kumdhuru Nabii Hud(a.s) na wale walioamini pamoja naye, Allah(s.w) alipitisha hukumu yake ya kuwahilikisha makafiri na kuwanusuru waumini kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



Ilipofika amri yetu ya (kuangamizwa) tulimuokoa Hud pamoja na wale walioamini pamoja naye kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa katika adhabu ngumu.(11:58)




Na hao ndio ‘Ad. Walikanusha aya za Mola wao, na wakawaasi
Mitume yake na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.(11:59)



Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na siku ya kiyama. Sikilizeni hakika ‘Ad walimkufuru Mola wao. Wakaangamizwa hao
‘Ad kaumu ya Hud.” (11:60)

Jeshi la Allah(s.w) lililotumika dhidi ya makafiri katika jamii ya akina ‘Ad ni upepo mkali uliovuma mfululizo kwa siku nane (mausiku Sabaa na michana minane) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



Basi walipoliona wingu likiyaelekea mabonde yao, walisema: “Wingu hili la kutunyeshea mvua.” (Wakaambiwa) “Bali haya ni ile mliyokuwa mkitaka ije kwa upesi, (adhabu ya Mwenyezi Mungu). Ni upepo ambao ndani yake iko adhabu iumizayo.” “Unaoangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake.” Basi wakawa si wenye kuonekana tena ila nyumba zao tu (ndizo zilizosalia). Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu waovu. (46:24-25)




Na bila shaka tuliwastawisha katika yale tusiyokustawisheni nyinyi, na tuliwapa masikio na macho na nyoyo; lakini masikio yao na macho yao na nyoyo zao hazikuwafaa chochote walipokuwa wakikanusha Aya za Mwenyezi Mungu, na yakawazunguka yale waliyoyafanyia mzaha. (46:26)




Na katika (habari za), Adi (ziko alama kadhalika). (Kumbusha) Tulipowapelekea upepo wa papazi uangamizao. Haukuacha chochote ulichokijia ila ulikifanya kama kamba mbovu. (51:41-42)




Walikadhibisha kina Adi (nao); basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! Hakika tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhsi iendeleayo (kwao mpaka leo). Ukiwang’oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kana kwamba ni magogo ya mitende iliyong’olewa. Basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! (54:18-21).



Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)

*JE TUNAJIFUNZA NINI KUTOKANA NA HISTORIA HII??*



📗 Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s.w) na lengo la binaadamu hapa ulimwenguni.



(ii) Kutomchelea yeyote katika kufanyakazi ya kulingania
Uislamu na kuusimamisha katika jamii.



(iii) Katika kufanyakazi ya kuhuisha Uislamu katika jamii tutarajie malipo kutoka kwa Allah(s.w) peke yake.



(iv) Katika kufanya kazi ya kulingania na kusimamisha Uislamu katika jamii tumtegemee Allah(s.w) peke yake.



(v) Waislamu wakijizatiti ipasavyo, watawashinda makafiri.
Pamoja na nguvu kubwa walizonazo.



*MWISHO*

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post