ALINIKATAA AKIJUA NI MASIKINI LAKINI RAFIKI YAKE AKANIKUBALI BILA KUJUA MIMI NI BILIONEA😭😭😳,🚐
EP 03.
Sikuwa na haraka sana ya kufika ofisini, niliendesha gari langu polepole huku nikiburudika na mziki laini ulioitwa "Why I love you" ulioimbwa na mwanamki wa kimarekani anayejulikana kwa jina la Major. Niliendesha gari huku na mimi nikiimba kwa kufuatisha mziki huo ambao niliupenda sana.
Mara simu yangu ikaita, nilipoangalia nani ananipigia alikuwa ni Femi, nilimsevu "MY sweet heart ❤️" basi nikapokea simu yake huku niliendelea kuendesha gari langu taratibu bila tabu.
"Jamani Beatus mpenzi unajua utakosa kazi wewe! yani mpaka bosi, hivi unampango kweli wa kuja kazini leo dear" Aliniuliza Femi."Honey nakuja ondoa shaka kipenzi" Nilimwambia FEMI.
"Yani bosi amekasirika mno uwanja wa ofisi ni mchafu haujafagiliwa mpaka saa tano hii yani ukimuona bosi alivyovimbisha mashafu hakika Beatus ukifika lazima upewe barua ya kufukuzwa kazi, nitaumia sana kwasababu sipendi nikuone unateseka" Nilimwambia FEMI.
"Kuhusu mimi usijali sana kipenzi tafadhali relax" Nilimwambia.
"Acha ujinga Beatus unajua unafanya masihara wewe na kazi za watu we shauri yako najua utakayempa tabu ni mimi na ndio maana najali kwasababu nakupenda!" alisema Femi kwa sauti ya msisitizo, aliongea kama anataka kulia vile, ni kweli alinipenda sana tena sana licha ya muonekano wangu bandia wa kifukara ambao nilikuwa nikimuonyeshea kwa siku zote, basi nilimuomba anipe dakika tano tu nitakuwa nimefika ofisini.
"Sawa jitahidi maana mwenzio nimekutetea huku mpaka nitaonekana ni Muono"Aliniambia FEMI kisha akakata simu.
"Punde nlifika nje ya geti la ofisini na kupiga honi ya gari, mlinzi ambaye tulikuwa tukishauriana mambo mengi kuhusu maisha alifungua geti, alipotupia jicho ndani ya gari wakati naingiza gari ndani ya geti macho yalimtoka kwa mshangao mkubwa asiamini kabisa anachokiona. Muda wote alikuwa ameduwaa huku akinisindikiza kwa macho mpaka nikaingiza gari ndani na kwenda kuliweka sehemu ya maegesho,nje walikuwa wapo FEMI, bosi na wafanyakazi wengine walikuwa wamesimama wakilitizama tu gari, nadhani walikuwa wanasubiri kuona ni nani atakayeshuka ndani ya gari, kwani nilipoingiza gari ndani nilipandisha viyoo vya gari juu.
Basi nilivuta pumzi ndefu huku nikijiweka sawa namna ya kuwasaprise... Nikafungua mlango wa gari taratibu, ile natoka tu nje mara ghafla...
JE NINI KILITOKEA? HAKIKA YAJAYO YANAFURAHISHA, LIKE NA COMENT YAKO NDIVYO VITAKUFANYA UONE SEHEMU IJAYO
Tags
simulizi