ALINIKATAA AKIJUA NI MASIKINI LAKINI RAFIKI YAKE AKANIKUBALI BILA KUJUA MIMI NI BILIONEAðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜
EP 01 & 02
"Aaaaah malkia Scola yani kila nikikuona nahisi moyo wangu unasuuzika kabisa! Kwanza nikuamkie Vipi mambo mrembo!"Beatus alimsalimia Scola kwa uchangamfu sana asubuhi hiyo wakati Scola akiwa ameongozana na rafiki yake aliyeitwa Femi.
"Sikia Beatus usiniaharibie siku tafadhali unanisikia!" Alisema Scola huku akiwa amebadilika sura ghafla.
"Mh! sasa Scola na wewe kipi cha kukasirisha, mbona Beatus amekusalimia tu vizuri kwa uchangamfu" Femi alimuuliza Scola.
"Sasa ananiita mrembo mimi ni mrembo wake mimi? au akiniangalia nina hadhi naye msiiiiiiiiw Shobo tu" Alisema Scola huku akitoa msonyo mkali Beatus akabaki anacheka tu.
"Acha kucheka cheka kama malaya aliyeona bia, ndio nishakukanya mazoea na mimi sitaki" Scola alimwambia Beatus. "Mmh lakini Scola mbona sioni kosa la Beatus" Femi alizidi kuhoji.
"Yani Femi hakuna mkaka aliyenitoka rohoni kama huyu" Alisema Scola huku akimtizama Beatus kwa dharau. "Kwanini" Femi alizidi kuhoji. "Basi tu yani simpendi simpendi" alisema Scola kumfanya Femi ashangae"Mh makubwa haya yani unamchukia mtu bila sababu, haya Mwaya Beatus we endelea zako kupalilia maua sisi acha tuingie ofisini"'Femi alimuaga Beatus ambaye alikuwa kaduwaa tu akimtizama Scola. Basi Wakaingia ofisini, Beatus akawa anaendelea kupalilia maua nje ya ofisi hiyo.
Tangu Scola amshushue Beatus, kijana huyo alikata mazoea na Scola kisha akamishia upendo wake kwa Femi, mapenzi kati yake na Femi yakawa moto moto, wakabadilishana mpaka namba za simu.
Asubuhi Beatus alishtuka usingizini baada ya kusikia miito wa simu yake, alinyoosha mkono mpaka simu ilipo na kuna anayempigia ni Femi. "Umeamkaje Beatu Bae wangu!" Femi alimsalimia Beatus. "Salama tu dear vipi wewe" Beatus aliuliza.
"Mie nimeamka sala mbona umechelewa kazini mpaka saizi, yani bosi huku pamoja na wafanyakazi wengine wanakusakama hasa Scola kwamba eti ushalewa kazi, na Scola anachochea eti ufukuzwe kazi awekwe kijakazi mwingine ili ushike adabu" Femi alimwambia Beatus. "Acha nioge nije mama!" Beatus alijibu kisha akakata simu.
Aliingia bafuni kwake na kuoga vizuri kwenye bomba la Shawa, alipotoka bafuni akapigilia suti yake safi ambayo hata bosi wake hana, hakutaka kuvaa yale masembere yake aliyozoea kwenda nayo ofisini siku zote,
JE ITAKUWA FEMI NA SCOLA WAKIMUONA BEATUS KATIKA MUONEKANO HUO MPYA! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 HAKIKA SEHEMU IJAYO SIO YA KUKOSA!!
Tags
simulizi