TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JENNIFER 1-5

*JENNIFER*
*SEHEMU YA KWANZA*
Unaweza kuishi na watu au ndugu ukahisi n watu wako wa Karibu kumbe ndio watu wa kwanza wanaokutia nuksi na mikosi kwenye maisha yako.
Naitwa Jenipher kwetu tulizaliwa wawili tu mm na mdogo wangu wa kike.
Tulikuwa kwa upendo Sana kiasi kana kwamba hata kuumwa tuliumwa pamoja mara nyingi Sana na hata tatizo la mmoja lilituumiza wote kwanza hatukuwa tumepishana Sana maana tulipishana miaka miwili tu.
Miaka ilienda hatimae tukakuwa.
Mimi nilitangulia kumaliza kwa miaka miwili juu yake na nilifanikiwa kwenda chuo maana sikupitia form 6.
Nilisoma nikamaliza diploma nikafanikiwa kujiunga na degree ambapo nilikuwa nasomea labaratory technicians.
Nilipokuwa chuo mdogo wangu alikuwa anaitwa Janeth yeye alikuwa ndio yupo form 6.
Akamaliza ila yeye akaenda kusomea ualimu wa chemistry na biology..
Akiwa chuo siku moja alikuja kunitembelea ambapo mm nilikuwa nasomea UDSM yeye alikuwa SUA
Tulitoka tukaenda sehemu jion maana alikuwa yeye sio mwenyeji wa Dar na hajawah kufika maana nyumban kwetu n Babat.
Tulienda sehemu jion ilikuwa n restaurant tukapata chakula cha jion wakati tunakaribia kitoka alikuja kijana alikuwa smart nyie akaniita Jenipher.
Nilishtuka maana sikuwa ninamfahamu akajitambulisha kuwa anaitwa Michael na tupo wote UD.
Sikutaka Kubisha maana hauwez kumfaham kila mtu chuoni.
Tukapiga piga story mwishon akaomba namba zangu za simu sikutaka kumpa maana niliona Kama ni haraka Sana ila Janeth akampa za kwake akasema hakuna shida Kama ukiwasiliana na mm basi utakuwa umewasiliana na Dada yangu Jenipher.
Kiukweli sikuona shida na niliona kama n kitu cha kawaida na mwisho tukaagana.
Kuanzia siku ile safari za Jane zilikuwa hazikauki Dar.
Nilishangaa maana niliamin hakuna mtu anaemfaham Dar es salam zaidi yangu na akawa hasemi anapoenda maana nilikuwa nakaa offcumpus so unaweza kurudi tu na usimkute hata nyumban.
na ukimuuliza yaan anakuwa hana jibu la moja kwa moja la kukupa n Kama akawa anajing'ata ng'ata tu.
Siku moja alikuja Dar kama kawaida yake aakatoka Ila alivyorud alikuwa na hasira sana akapitiliza kulala.
Kiukwel sikumuuluza na alivyoamka akanifata akanambia unajua unabahat sana.
Nikamwambia kwann.
Akasema kuna vitu hata huvipambanii Ila vinajiweka kwenye mstar venyewe tofaut na sisi tunaopambana kupata.
Sikumuelewa nikamuuliza sababu ya kusema hivyo n ipi .
Kabla hajanijibu ghafla simu yake ikawa inaita ilikuwa imesaviwa Michael na kikopa chekundu.
Janeth akakurupuka akatoka Nje kwenda kuongea na simu.
Sinaga destury ya kufatilia mambo ya watu Ila moyo wangu ulikuwa unaniambia nitoke nikamsikilize.
Nikasikia akisema yaan unahangaika na mtu asiekutaka unatuacha cc tunaokupenda...
Alafu siwez kuruhusu uwe nae akat ushanila yaan mm n wako tu.
Janeth akawa anasema.
Sikuelewa na niliona n mambo ya watu nisiyaingilie.
Kesho yake Janeth aliondoka mapema ajarudi chuon kwao Morogoro.
Kwenye majira ya saa 8 nilikuwa natoka naenda sokon nikaona gari limesimama pemben ya nilipokuwa naishi sikuangaika nalo mara nikaona mtu kashuka kumcheki vzr n Michael.
Akanizalimia akanambia anaomba kuzungumza na mm.
Sikuona shida nikaingia kwenye gari kumsikiliza.
Jenipher unajua mm nimekuwa nikikufuatilia sana akanambia.
Kwa nn nikamuuliza.
Kabla hajanijibu simu yake ikawa inaita iliseviwa Janeth msf sikuelewa maana ya msf baadae ndio nikaja kujua n msumbufu.
Nakuja.................

*SEHEMU YA PILI*

Akakata simu alafu akaizima kabisa.
Akanambia mamaa mm sio mwanafunzi mwenzio Kama nilivyokuambia mwanzo.
Mm naitwa Michael nilikuja siku moja kumtembelea mdogo wangu nadhan utakuwa hata humfaham yaan nikajikuta nimetokea kukupenda mno yaan.
Yaan ulinivutia sana.
Nikaanza kukufatilia kiukweli nikagundua ww n binti mtulivu sana maana nilikuwa naogopa sana wadada wa chuo akasema.
Na ile siku uliyokuja na mdogo wako nilikuwa nataka kuwa karibu yako ila kwa bahat mbaya ilishindikana 
Na katika kuzungumza na mdogo wako akanambia unamahusiano naomba unambie hapa mbele yangu je nikwel unamahusiano maana sijawah kukuona na mtu akasema.
Nilishindwa nimjibu nn maana kiukweli nilishawah kuwa na mahusiano mamoja kabla Ila kwa wakati ule nilikuwa zangu single tu na sikuwa nadate na mtu yoyote yule.
Sikutaka kumdanfanya nikamwambia sina mahusiano akatabasam kisha akanambia naomba kuwa rafiki na mtu wa karibu kwako.
Sikuona shida na hilo manaa anacompany nzuri.
Tukaanza kuwa marafiki wazuri akawa anakuja kunifata tunatoka.
Ingwa ananitania sana kuhusu kunipenda ila sikuona shida maana sikuwa na hisia nae.
Siku moja mdogo wangu alikuja akanikuta niko nyumban kwangu mm pamoja na Michael nikamuona kakosa raha Ila sikuelewa sababu.
Basi baada ya muda Michael akaondoka mdogo wangu Janeth akanifata akanambia dada samahan naomba nkuambie jambo. 
Sawa niambie nikamjibu 
Mm kuanzia namuona Michael nilitokea kumpenda sana akasema.
So unataka nikuunganishr nae nikamuuliza.
Kama ikiwezekana kwan hajawah kukutongoza akaniuliza.
No hajawah kunitongoza nikamjibu.
Kwakuwa sikuwa na hisia na Michael siku moja nikamuita nikamueleza hisia za mdg wangu kwake basi akaniangalia kisha akanambia Jenipher laiti mdogo wako angekuwa na moyo Kama wakomuda huu tungekuwa tunaongelea habar nyingine kab is a akasema Michael.
Hakuoneonekana kukubali mm kumuonganisha na Janeth yaan alionekana kama anataka ukaribu na mm sana.
siku moja Michael alikuja kunichukua na kama kawaida Janeth muda mwingi alikuwa kwangu kuliko ambavyo anaenda chuon kwao.
Michael alikuwa amekuja kunichukua akamkuta na Janeth nyumban kwangu kiukweli hatukuweza kumuacha tukatoka nae na Michael alikuja na kijana mwingine akanambia n binamu yake.
Tulitoka tukaenda sehemu tulivu sana n Kama Michael aliiandaa hii siku lakin hakuna aliejua maana n sehemu ambayo n Kama iliandaliwa kabisa.
Tumefika tukakaa mara yule binamu yake akasimama akataka kuondoka na mm nikasimama kwaakili zangu nikawa nataka kumuachia Janeth uwanja maana alionekana anania ya kweli na anampenda Michael. 
Ni kama Michael alitaka kunizuia ila ndio hivyo nilishadhamiria kuwaachia nafasi.
Tukanyanyuka tukaenda pemben na yule binamu yake na Michael ambae alinambia anaitwa Yesse.
Tulipiga story Sana nikiamin nimewaachia uwanja wamalizane lakin ghafla ikaingia sms kutoka kwa Michael inasema.
Hujafanya sawa Jenipher maana nilitaman tuzungumze leo na uelewe kila kitu sikumjibu nikawa naendelea na story na yule yesse na alionekana ameinjoy sana company yang u akaniomba namba za simu sikubisha nikampa ili wakati Michael atatoka na Janeth na mm niwe na company nikiamin kufanya hivyo nitawapa wakati mzuri Janeth na Michael kujenga bila kyjua Kama wanatibuanaga kila siku.
Janeth alienda chuo kuna siku Michael akaja kwangu nikamkaribisha maana huwa anakawaida ya kuja.
Akawa amepoa sana tofaut na kawaida yake yaan.
Nikamuuliza unashida gan akawa kimya.
Nikamuuliza umemuambia Janeth kuhusu hali yako bado akawa kumya nikachukua simu nikawa nataka kumpugia Janeth simu ikawa inaita nikashangaa kanipokonya simu alafu kaweka loud spekear.
Janeth akapokea alivyoona Janeth kapokea akaanza kutoa ya moyoni sasa.
Jenipher unajua unanikatili kiasi Gani,mm sikumfata Janeth nilikufata ww,naomba unisikilize kwa makin sana ninachokiongea na unielewe.
Nilichukua namba za Janeth ili aniunganishe na ww maana niliamin n mdogo wako anaweza kunisaidia kukupata ila mkanigeuzia mambo hali ya kuwa nakuwaza na kukufikiria ww alafu ww unaniunganisha na mdogo wako.
Najua ananisikia na naomba na ww uelewe kuwa Nakupenda Jenipher na nisiwe muongo siwez kuvumilia tena.
Nakuja............................

.
*SEHEMU YA TATU*

Nikama nilishikwa na butwaa maana akili yangu ilishamchukulia Michael kama shemeji na sikuwah kumuwazia vingine ingawa alionesha dalili nyingi za kitaka ukaribu na mm.
Alipomaliza akanisogelea alafu akakata simu.
Jenipher akili yangu inanituma kuwa ww n mke wangu na inanituma Kama wa ndio mama wa wanangu so nikiwa nina maradhi ya mwili au akili ww ndio kimbilio langu la kwanza kwa maana Nakupenda sana na nataman ww ndio uwe wa mwisho kwenye kutatua maradhi yangu akasema.
Siku zote nilikuwa namchukulia kawaida Ila siku ile maneno yake yaliniingia sana yaan mpaka nikaanza kuhisi moyo unaenda mbio.
Akanisogelea alafu akaninong'one za akasema Nakupenda Jenipher.
Moyo ukawa unanituma kuwa nampenda Ila akili ikawa inanituma kuwa huyu sio haki yangu maana mdogo wangu ameshatamka Kuwa anampenda so sikuona haja ya mm kuwa nae.
Lakin Janeth amenambia anakupenda nikamwambia.
Na mm Nakupenda ww akasema.
Sikutaka kuendelea kumsukiliza maana niliona Kama ananivuruga tu.
Nikamwambia kuwa naomba aondoke akanishika akanivuta miili yetu ikawa imegusana kisha akanitazama kwa sekunde kadhaa saa ngapi asisogeze lipsi zake kwangu.
Nyie hisia hizi zilivyozinasaliti nikajikuta nampa ushirikiano tukaanza kukiss akawa anapumua kwa nguvu akaanza kunishika shika aseee kujizuia sikuwa naweza hata kumzuia nikamuacha afanye anachotaka nyie tukajikuta tumezama kuleee.
Nimekurupuka baadae nikaona nimefanya kosa kubwa Sana maana nikawa najihisi Kama nimelala na mwanaume wa mdogo wangu maana alishanambia mapema sana kuwa anampenda sana Michael alafu leo hii mm nimelala nae.
Michael yeye kaamka anafuraha akanibeba tukaenda kuoga akanambia Nakupenda sana jenipher.
Na Janeth nikamuuliza.
Naomba ukitaka kutaja jina la mtu bora utaje jina langu.
Tumemaliza sikuwa na raha hata yaan nikawa najiona msaliti mkubwa sana.
Michael aliondoka asubuh akanambia anaenda kazin maana alinidanganya tu siku ile kuwa yeye n mwanachuo kumbe n daktar muhimbili.
Basi kila dakika  ananitumia vi sms vya namna ananipenda na anavyonimiss.
Sikuwa na raha kabisa maana niliona kama namkosea sana mdg wangu.
Nikamtafuta yule binam yake Michael maana tulikuwa tunazungumza sana na n kama tulikuwa marafiki wa karibu.
Nikamueleza situation ilivyo na waswas wangu juu ya mdogo wangu akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaniuliza unataka nn.
Nikamwambia nahis kuchanganyikiwa maans bado naona sijafanya sawa.
Tulikiwa tumekaa akasogeza kiti chake mpaka karibu yangu akachukua kichwa changu akakilaza kwenye mabega yake kisha akanambia kila ukitaka kulia mm nipo kwaajili ya kufuta machozi,my shoulders are always there for u to lean akasema.
Nakuja ......................

*SEHEMU YA NNE*

Nikatulia kwa dakika kadhaa nikamuomba niondoke.
Upo sawa lakin Mamy akauliza Yesse.
Usijali nipo sawa.
Akanisinikiza mpaka kwangu kusha akaondoka zake naingia ndani namkuta Michael.
Nilishtuka maana niliamin nina ufunguo mmoja tu so inakuwaje aingie ndan na mm nilifunga mlango.
Akanionesha ufunguo mwingine yaan sijajua hata aliuchonga lini.
Akaniuliza umetoka wapi.
Nilikywa na Yesse nikamjibu.
Akaniangalia kisha akasema ndio ulienda kumlilia kwakuwa umeanzisha mahusuano na mm maana ww nakujua.
Nikamwambia hapana mm nilienda kwaajili ya mambo yangu tu na sio unachowaza.
Mara Janeth akampigia simu Michael akaikata nikamuomba aipokee na aweke loud speaker akanambia ila usipanic my wife mm Nakupenda ww.
Nikamwambia asiwe na mashaka cha msingi apokee na aweke loud speaker kwwli akapokea.
Michael kwann unanitesa kiasi hichi,unajua kabusa dada yangu hana mpango na ww na unajua mm kuanzia siku yakwanza nilipokuona nilikupenda kwann unanitesa kiasi hichi akasema.
Lakin unajua kabisa nampenda nani akasema Michael.
Najua unampwnda jenipher lakin hana muda na ww kwann usiniangalie mm ambae napambana kuwa na ww.
Siwez kuacha kumpenda mtu ninaempenda so naomba unisahau na uendelee na maisha yako maana mm sina time na ww akasema.
Lakin mm Nakupenda akasema Janeth.
Na mm nampenda Jenipher,akajibu Michael na naomba uniache niendelee kupigania ninachokipenda akaendelea kusema Michael.
Kisha akakata simu alafu akanigeukia.
Naomba tuachane nikamwambia.
Kama sitaki akajibu Michael.
Nikajikuta na an za kulia.
Nililia kwa dakika kadhaa Michael akanisogelea akanambia naomba usiwe na huzun mm nitakulinda dhidi ya kila kitu.
Na naomba usijilaum kwa lolote lile akanambia  .
Naogopa kutengeneza vita na mdogo wangu nadhan either umchague yeye au utuache sote maana n vurugu tunajutengenezea.
Jenipher hivi unahis naweza kukuacha akasema Michael.
Namaliza chuo mwaka huu nadhan nikimaliza utakuwa n mwisho wetu maana mm sitaki kumgomban mwanaume tena na Ndg yangu wa damu so naomba tusionane tena na mm sihitaji kuwa na ukaribu tena na ww nikamwambia.
Nataman uwe na ujauzito akasema hapo ndipo nikashtyka maana sikuwaza Kama ile siku tulifanya mapenzi tena bila Kinga.
Ndio kama alama ya hatar ikacheza kidogo.
Nilishtuka nikamwambia naomba uondoke akanisogelea akanikiss kisha akaondoka.
Nyie nilianza kulia.
Nililia mno mara ikaingia sms kutoka kwa Michael.
Usilie sana mpenzi wangu unaniumiza na mm sikutegemea mambo Kama yangekuwa hivi niliamin unaweza ukawa wangu kiurahisi mno ila mambo yamekuwa magumu ila naomba nikuahidi kuwa chochote kitakachokupa furaha nipo tayar kukifanya ila hakikisha kinakupa furaha akaendelea kusema.
Nakuja ..............

 
*SEHEMU YA TANO*

Nikazidi kulia maana moyo wangu ulikuwa unanituma kama nampenda Sana Michael Ila niliona kabisa sistahili kuwa nae.
Muda ulienda nikawa simuon tena Michael kdg nikaanza kumsahau ila bado nilikuwa na ukaribu na binamu yake maana alikuwa ananipa company nzuri na alikuwa ananiondoa upweke kwa kiasi kikubwa sana.
Muda ulienda na hatimae mwaka ukapita nikamaliza  chuo nikaanza kutafuta kazi ambapo nilirudi babat kwa wazaz wangu na mawasiliano kati yangu na Yesse yakawa yanaendelea kupamba moto lakin wakti wote ambao nipo nyumban Janeth hakuwah kurudi likizo ila sikujal kumbe bana alikuwa na ujauzito.
Yesse akanitafutia kazi ila sasa n muhimbili sikutaka kwenda maana sikutaka kukutana na  Michael manaa niliamin bado atakuwa anafanya kazi hapo.
Nikapata kama part time job nikawa nalipwa lipwa.
Yesse akawa akipata muda tunatoka tinapata dinner na vitu kama hivyo.
Alinisaidia kulipa kodi ya miezi mitatu ilikuwa n single self.
Hakuwah kunitongoza na siku zote alikuwa Kama rafiki tu kwangu.
Muda ulienda akaja kunitongoza sikuona shida maana sikuwa na mahusiano.
Mambo yalikuwa n bulbul kati yetu na sijui nilipitiwa na nn mpaka nikasahau kabisa kama anaundugu na Michael maana n muda mrefu sijamuona karibu yake.
Akataka kunioa sikuona shida kwanza akanifanyia katafrija kadogo cha suprise ya kunivisha pete sasa baada ya Yesse kunivalisha pete ndio mambo yakaharibika.
Siku moja ikaingia sms kwa namba ngeni inasema.
Najua hukuona thaman ya upendo wako ukaukataa kwa sababu ya mtu ambae hana hata mbele wala nyuma na kuniacha niteseke ila Jenipher hata kama sio leo basi mbingun naomba kuwa mumeo.
Nilijisikia vubaya na moja kwa moja nilijua n Michael.
Baada ya Yesse kunivisha pete ya uchumba alikuja Janeth ninapoishi alikuwa na mtoto mdogo wa kike alimuita Melinda.
Kalikuwa karrmbo kweli na kana kama miaka miwili.
Nilishangaa ilikuwaje aww na katoto ka miaka miwili kasoro na hali ya kuwa sijamuona kwa Kama mwaka na nusu.
Mshale wa hatar ukanicheza kuwa inawezekana hata alivyokuwa anakuja kwangu kipindi yuko chuo alikuwa na mimba.
Sasa n mimba ya nani nikaendelea kujiuliza maana kiykweli sikupata majibu kuhusu hayo maswali yote niliyojiuliza.
Akaniomba nisiwaambie wazaz wetu kuwa amezaa na anaomba amuache mtoto kwangu kwakuwa anaenda kumalizia mwaka wa mwisho chuon.
Sikuona shida maana mtoto wa Janeth n mwanangu na kwwli alikuwa anasoma so nikaamin akimaliza masomo atakuja kumchukua mwanae.
Sikutaka hata kutafuta house girl nikawa nampeleka Melinda daycare asubuh na nikitoka kazin namfata narudi nae nyumban Kama mwanangu.
Sasa kuanzia Janeth aliponiachia mtoto akawa hapatikan kwenye simu wala hajawah Kunitafuta kuulizia habar za mwanae.
Sikuona shida maana niliamin bado n mwanafunzi so huenda hataki kuchanganya malezi na shule ila nilikuwa nataman sana kumjua baba wa yule mtoto manaa niliamin hata kama yeye anasoma basi mwanaume anatakiwa kumhudumia mwanae.
Siku moja nikiwa kazin Michael alikuja akataka kuonana na mm.
Sikuona shida hata kdg nnikatoka nikaenda kuzungumza nae.
Alikuwa kawaida kama alivyo ila alikuwa n kama mtu mwenye majonzi sana.
Jenipher kwann hukunichagua mm ukamchagua yesse akasema.
Nahisi hii n personal issue yangu nikamjibu.
Akanambia Jeni mamaa wanaume tunataka utulivu na kuheshimiwa tu na niwanawake wachache Sana wanaoweza kutupa hivyo vitu na niliviona kwako kati ya maelfu ya wanawake ambao nimwshawaona na kuishi nao nikataka mm ndio nipate tulizo kwako Ila bahat mbaya hukuwah kunielewa.
Jenipher naomba unusamehe kwa ninachokuambia ila naomba usiolewe na Yesse utaniua mm akasema.
Mtoto wa Janeth ni wakwangu nnilishtuka yaan n Kama sikutegemea.
Kwann unaniambia nikamuuliza.
Kwasababu nahisi unatakiwa kujua akaendelea kusema.
Tukiwa tunaendelea na mzungumzo ghalfa akanipigia Yesse.
Upo wapi akaniiliza.
Nikamwambia nilipo.
Upo na nani akaendelea kuuliza.
Nipo na Michael nikaswma maana sikutaka kumdanya.
Basi akakata simu Michael aliondoka zake jion nikarudi nyumban nikamkuta yesse mlangon kavimba mno akanambia Kama ulikuwa unampenda sana Michael ungenambia kuliko kukubali kuwa karibu na mm alafu urudiane na ex wako na ukasahau kama n ndugu yangu akaendelea kusema kkisha akaondoka.
Nakuja ............

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post