TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JINSI Ya KUJITENGENEZEA Na KUJIONGEZEA THAMANI SOKONI.

JINSI Ya KUJITENGENEZEA Na KUJIONGEZEA THAMANI SOKONI...
________________________
Hivi unafahamu kwamba thamani ya mtu ndiyo hupima hadhi yake pamoja na kipato anachoweza kukitengeneza? 

Unatakiwa kujua kwamba utabadili maisha yako siku utakayoamua kuongeza thamani Yako!

Na kama hutoamua Kujiongezea  thamani hakuna atakayekufanyia hivyo! 

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba, siku ambayo thamani yako itapanda, ndiyo siku ambayo ulimwengu utakutambua wewe ni nani!

Hakuna kipya chini ya jua, maandiko matakatifu yanasema hivyo! 

Hii inamaanisha kwamba kwa chochote kile utakachokifanya, tayari kuna watu walishafanya, lakini pia kuna wengine ambao wanafanya kitu hichohicho na kwa namna moja ambayo hata wewe unafanya! 

Hivyo basi ili kufikia hatua ya kutambuliwa na watu wengine, ni lazima uwe umejiongezea thamani kubwa sana, kiasi kwamba utaweza kutofautishwa na wengine! 

Kwa ujumla thamani ni kipimo rasmi ambacho, humstahilisha, humheshimisha pamoja kumtambulisha mtu!

Je, kwa namna unavyojiona, wewe ni mtu wa thamani?
Je, umeweza kutengeneza thamani gani kazini kwako?
Je, unajivunia kuleta matokeo gani kazini kwako?
Je kwa kile unachokifanya umeweza kutengeneza thamani gani?

Kumbuka kama hutojiongezea thamani utabaki kuwa mtu wa kawaida tu!

Je nifanye nini ili niongeze thamani maishani mwangu? 
Usijali fanya yafuatayo my friend!

1. Tengeneza Utambulisho Wako (Jenga Jina Lako Kwanza)...

Thamani ya mtu imebebwa kupitia jina lake! Sizungumzii jina la kubatizwa! 
Nazungumzia jina lako juu ya kile unachokifanya pamoja na namna kinavyokutambulisha kwa watu! 

Unachopaswa kujua ni kwamba, dunia ya sasa inakabiliwa na uhaba wa watu waliokosa majina pamoja na utambulisho fasaha juu ya kile  wanachoweza kukifanya!

Ukichimba kwa undani zaidi utagundua kwamba, kuanzia ofisini, kwenye ulimwengu wa dini, kwenye ulimwengu wa siasa, kwenye ulimwengu wa taaluma, kwenye ulimwengu wa biashara na kwingineko kwingi kuna uhaba wa watu kama hawa! 

Hii inamaanisha kwamba, endapo utaamua kutengeneza jina na thamani Yako, utakuwa kama dhahabu!

Utaanza kung'ang'aniwa pamoja na kuhitajika kila mahali!

Ndugu jiongezee thamani, kwani katika ulimwengu huu tulionao leo, kama wasomi wapo wa kutosha, kama wafanyakazi wapo wengi wa kutosha, kama wafanyabiashara wapo wengi wa kutosha! 

Hii inamaanisha kwamba kama hutojiongezea thamani, uhitaji wako utakuwa mdogo sana, kwani hakuna yeyote yule atakayekuhitaji!

Unatakiwa kujua kwamba wakati wa kutengeneza utambulisho wako yule unayemuona kabla ya mwingine yeyote yule hajakuona huyo ndiye wewe halisi!

Jione katika viwango vya juu! Kwani yule unayemuona ndiye utakayekuwa!

2. Jitengeneze Kuwa Mahiri! 

Ukiweza kutengeneza utambulisho pamoja na kujenga jina lako, unatakiwa uoneshe umahiri wako juu ya kile unachoweza kukifanya!
Unatakiwa kujua kwamba, utambulisho pasipo kuwa mahiri si kitu! 

Dunia tuliyonayo leo hii inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na watu ambao hawana uwezo wa kufanya kazi kwa umahiri!

Kwa mfano tuna wahitimu kutoka ngazi za chuo, ambao hawawezi wakazungumza kiingereza vizuri!
Hawawezi kuandika barua pasipo kukosea!
Hawawezi hata kutatua changamoto ndogondogo tu wanazokumbana nazo maishani mwao!
Wanataka waelekezwe kufanya jambo fulani ilihali ni wajibu wao!
Wanataka wasimamiwe katika kila jambo!
Wanataka mishahara mikubwa huku wakiwa hawana juhudi yoyote ile kazini!
Wana ndoto kubwa sana ila akili zao ni finyu!
Wanataka matokeo makubwa kwenye mambo madogo, na kupata matokeo madogo kwenye mambo makubwa!
Ndugu unatakiwa ujenge uwezo wako wa kuwa na umahiri kwenye taaluma Yako! 

Onesha umahiri kwa kile unachokifanya, ama hakika utaongeza thamani yako!

Unatakiwa kujua kwamba hakuna mwajiri yeyote yule ambaye huwa yupo tayari kumpoteza mafanyakazi Mahiri kazini!
Atatumia kila mbinu ya kumfanya abaki kwenye taasisi yake hata kwa kumpa masilahi mapana zaidi!

3. Onesha uwezo wako!
Thamani yako inategemea sana na ule uwezo unaouonesha kwa watu!
Unatakiwa kujua kwamba, uwezo wako utapima umbali utakaoenda kimaisha pamoja na thamani utakayoitengeneza!  
Huenda tayari ushajitengenezea jina lako, umeshakuwa mahiri katika eneo fulani, basi utakachopaswa kufanya hapa ni kudhihirisha huo uwezo wako ulionao! 

Yaani unatakiwa uwashawishi watu wajue kwamba hata wewe unaweza!
Unatakiwa kujua kwamba, hakuna atajayejua kwamba wewe unaweza kufanya jambo fulani ikiwa wewe mwenyewe hutoamua kumuonesha kwamba unaweza!

Mpenzi msomaji unatakiwa uwe na uwezo wa maeneo mbalimbali!
Kwa mfano mimi hapa kama mwandishi nina uwezo wa kufundisha (teacher by professional), nina uwezo wa kuandika, nina uwezo wa kushauri, nina uwezo wa copywriting, nina uwezo wa kuhariri, nina uwezo wa kusimamia na kuongoza watu (Mentaship)
Hii inamaanisha karibu kila eneo Nina uwezo nalo!
Kutokana na ukweli huo, ni kwamba nina uwezo wa kuishi popote pale na kuwa yeyote yule!

4. Kuwa na ujasiri! 
Ili upate kujitengenezea thamani kubwa, unahitaji kuwa na ujasiri mkubwa sana!
Inahitaji ujasiri mkubwa sana wa kudhihirisha uwezo wako mbele za watu!
Kuna watu wako na uwezo mkubwa tu, ni mahiri na shupavu kabisa, lakini hawana ujasiri wa kufanya hayo yote ili yafahamike kwa watu!
Unahitaji ujasiri wa kutimiza majukumu mbalimbali
Unahitaji ujasiri ili uweze kukabili changamoto mbalimbali ( usipende kuonewa onewa huruma)

Na Emmanuel Samuel King'ung'e
 
Unahitaji ujasiri ili uweze kuvuka kipindi kigumu!
My friend unatakiwa kujua kwamba, hakuna kitu kizuri kinachopatikana kirahisi, na ndiyo maana Dunia ya sasa hivi inahitaji watu ambao ni majasiri sana!
Hakuna mwajiri ambaye atakuwa tayari kumpoteza mafanyakazi ambaye ni jasiri!
Ndugu unahitaji kuwa jasiri ili kuongeza thamani Yako!
Kumbuka huwezi kutembea kwenye maji kama hutoamua kutoka kwenye boti!
Hii inamaanisha kwamba, huwezi ukatoka hapo ulipo na kwenda hatua nyingine kama hutokuwa jasiri! 
Unahitaji kuwa jasiri ili kuongeza thamani Yako!
Kuwa jasiri!

5. Endana Na Utamaduni Unaotawala Eneo Husika! 
Ili kuongeza thamani, unatakiwa uendane na Utamaduni Unaotawala Eneo Husika! 
Kwa mfano tufanye unafanya kazi kwenye taasisi Fulani. Na taasisi hiyo inamtaka kila mtu avae sare! 
Ubaya unakuja pale ambapo unajikuta huvai sare pamoja na kutokufuata taratibu zilizowekwa!  
Je unahisi taasisi itakuthamini ikiwa wewe hujaithamini?
Na, kama wewe umeshindwa kuthamini taratibu zinazotawala eneo la taasisi yako, je ni nani atakuthamini wewe?
Ndugu Hebu jiongezee thamani kwa kuendana pamoja na kufuata taratibu za eneo Husika!
Kuanzia leo hii anza kuvaa nguo nzuri, anza kuwa na tabia njema, anza kufanya kila kitu ambacho Unapaswa ukifanye Kwa usahihi!
Hii itakupa point na kukufanya wewe hapo uonekane bora zaidi kuliko wengine kwenye taasisi yenu, hali itakayokuongezea thamani kwenye eneo la Kazi!
Mpenzi msomaji endapo utajiongezea thamani, utashangaa hata kazi ambayo wenzako watafanya kwa masaa matatu, wewe ukija utafanya kazi hiyohiyo kwa saa moja tu na kwa kiwango bora zaidi kuliko wao!
Unaona inavyofurahisha ee! Hebu na wewe jiongezee thamani!

Huenda ukawa unajiuliza naongezaje thamani! 

Utajiongezea thamani endapo utajitambua wewe ni nani pamoja na kuanza kutafuta maarifa kwa kusoma Neno la Mungu pamoja na vitabu mbalimbali!
Soma vitabu ujiongezee thamani!
Kwa leo unatosha!

Nakutakia tafakari njema!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e;. Mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post