TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SAFARI YA TANGA ILIOGEUKA SAFARI YA KUZIMU 01

*SAFARI YA TANGA ILIVYOGEUKA KUWA SAFARI YA KUZIMU*
*SEHEMU YA KWANZA.*
_____________________________________

Maji yenye baridi kali yaliyotua mwilini mwangu, yalinifanya nistuke kutoka katika usingizi mzito ambao sikumbuki hata niliuanza saa ngapi. 
haraka nilifumbua macho yangu lakini yule aliyenimwagia maji yale kamwe sikumuona badala yake sauti za wanyama hasa fisi paka na bundi ndizo zilizonikaribisha eneo lile ambalo lilikuwa limetawaliwa na kiza kizito kilichoenda sambamba na upepo mkali.
haraka nilianza kuizungusha shingo yangu fupi nene , huku na huko lakini nilichokiona kamwe sikuyaamini macho yangu , makaburi yasiyopungua elfu moja yalikuwa yamenizunguka na mimi nilikuwa katikati.
nilistuka sana ule ujasiri ambao watu wengi walikuwa wakinisifu kuwa ninao wote ulikuwa umenikimbia, mapigo yangu ya moyo yalidunda kwa kasi , jasho jingi halikuacha kunitoka. 
haraka nilijaribu kujizoa pale chini ili nisimame lakini napo nilikutana na kizuizi, miguu yangu yote miwili ilikuwa imefungwa nyororo pia nyororo zile hazikuishia kupita miguuni tu bali hata kwenye mikono napo nilikuwa nimefungwa , hapo sasa nilianza kujitazama, na ndipo nilipojikuta nawehuka kabisaa.
kitambaa chepesi chenye weupe wa kung'aa , ambacho mara nyingi hutumika katika kufunikia maiti za kiislamu ( Sanda) ndicho kilichokuwa mwilini mwangu , tena nikiwa nimevalishwa katika mtindo ule ule kama wanavyovyalishwa maiti za kiislamu  pia puani na masikioni napo niliwekwa pamba.
hapo nilizidi kuogopa machozi nayo yalikuwa yakinitiririka kama maji lakini hata hivyo sikuwa na la kufanya kwani miguuni na mikononi nilikuwa nimefungwa minyororo imara ambayo ilinishinda nguvu pale nilipojaribu kuivuta kwa lengo la kutaka kujinasua, hivyo nilibaki nimesimama pale pale  nikiwa sina la kufanya.
"hutakiwi kulia wala kuogopa Razack, bali unatakiwa kuyaanza maisha yako mapya ya huku Kuzimu....kwa sababu hiki ndio kituo cha safari yako.."
sauti moja nzito iliyojirudia rudia ilipenya katika masikio yangu , nilistuka niliangaza huku na kule lakini sikumuona hata huyo aliyesema, lakini nilipotega vyema masikio yangu niligundua sauti ile ilikuwa inatoka pale pale nilipokaa kwa chini.
niliruka kiasi na nilipotazama ndipo nilipogundua kuwa muda wote ule nilikuwa nimekaa juu ya kaburi na ile sauti ilikuwa inatoka chini ya kaburi lile lile, mapigo yangu ya moyo yalizidi kudunda kwa kasi na kwa nguvu kuna muda nilikuwa nikihisi kama moyo unataka kuchana kifua na kuruka mbali.
"we..we ni nan..."
nilisema lakini kilichonishangaza ni kwamba hata sauti yangu yenyewe haikuwa tena ile ambayo nilikuwa nikiijua , ilikuwa tayari ishabadilika.
lilikuwa besi na pia ilikuwa ikitoa kitu kama mwangwi, ( inajirudiarudia)
"Hahahhaa Razack... mimi ni Mfalme wa kuzimu, pia ni mwenyeji wako, karibu katika ufalme wetu huu wa kuzimu..umekukuja katika wakati sahihi kama ulivyoelekezwa"
"kuzimu...,! mbona.."
nilistuka, macho yalinitoka mdomo ulikuwa mzito.
maelezo ya yule mtu ambaye alikuwa chini ya lile kaburi ambalo nilikuwa nimelikalia kwa juu , yalinitisha mno.
nilijaribu kuzirejelea kumbukumbu zangu nyuma lakini hata hivyo sikukumbuka kitu chochote.
"ndio kuzimu..!,wewe ni mfu tayari, ushakufa...."
"mimi..!, nimekufa..?"
"ndio wew ushakufa..si unaona upo katika makazi yako mapya"
"hapana mimi sijafa.."
"hahahah huamini..embu jitazame"
Yule mtu alisema. 
na kweli nilianza kujitazama kwanzia chini mpaka juu, nilikuwa sina tofauti na maiti , mwilini  nilikuwa nimevalishwa sanda pia masikioni na puani nilikuwa nimewekwa pamba.
lakini hata hivyo yule mtu hakuniacha nipate utulivu wa mwili wala akili, aliendelea kunipa maneno ambayo ndani yake yalikuwa yamebeba ujumbe ambao ulinifanya nizidi kujihangaisha, kiakili , kimwili na kihisia pia.
"tazama katika hilo jiwe hapo"
haraka niligeuka na kutembeza macho yangu mpaka katika lile jiwe ambalo hukaaga upande wa kichwani na kutoa maelezo mafupi juu ya marehemu, hapo sikuamini kwa kile nilichokiona, 
"RAZACK ADNAN DONSO 
KUZALIWA 3-5-1989
KUFA 24-07-2017" 
niliyasoma maelezo yale.
jina lilikuwa ni langu pia tarehe ya kuzaliwa na mwaka pia vilikuwa vyangu lakini hii tarehe ya kufa ndiyo ilinichanganya.
"ina maana mimi nimekufa...! kweli..nimekufaje sasa"
"hahaha karibu sana..."
ile sauti ilisema kisha ikatoweka kwa zaidi ya dakika tano sikuisikia , kimya kizito kikatawala upepo mkali ukafatia, nilibaki nimepigwa na butwaa lakini hata hivyo taratibu nilijikuta napoteza nguvu viungo vya mwili wangu vilianza kuwa dhaifu, usingizi mzito ulinikamata mpaka nikajikuta nalaza mgongo wangu pale juu ya kaburi, huku kichwa nikikielezea upande wa lile jiwe ambalo lilikuwa linatoa taarifa chache kuhusu kuzaliwa kwangu na kufa kwangu. 
dakika mbili mbele nilikuwa tayari nishazama katika dimbwi zito la usingizi.

Itaendelea....

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post