Wapenda kula nyama nyekundu kuweni makini
Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA,
Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng'ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k, na kwa hivi sasa watu wengi hupatwa na ugonjwa wa Brucella ambao hupimwa kupitia kipimo cha damu,
DALILI ZA UGONJWA WA BRUCELLA
fahamu kuhusu dalili mbali mbali za ugonjwa wa Brucella, kwa kusoma baadhi ya dalili hizo hapa chini;
1. Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
2. Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
3. Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali
4. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
5. Mgonjwa kutoa jasho kupita kiasi
6. Mwili kuchoka sana pamoja na kuwa dhaifu
7. Mgonjwa Kupata maumivu ya joints,misuli pamoja na maumivu ya mgongo
8. Mgonjwa Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara
9. Pia mgonjwa huweza kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za ndani ya chemba za moyo yaani endocarditis
10. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuvimba kwa joints pamoja na mifupa ya uti wa mgongo yaani spinal bones, tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama Spondylitis.
Endelea Na makala hii kwa kina na ufafanuzi mkubwa toka kwa Mtaalam na Mshauri wa Maswala ya Afya HAPA
Tags
AFYA