YUZO 👌👌
*SEHEMU YA KWANZA*
Mimi ni mama wa Watoto wawili mzazi mwenzangu tulishindwana tabia aliniletea mwanamke ndani akanifukuza nikaondoka kurudi kwetu nikiwa na mtoto mmoja ila wakati huo sijui kuwa nina ujauzito nilipofika nyumbani baada Kama ya wiki nikaumwa Sana kwenda kupima nikakutwa na mimba ya mwezi mmoja nikampigia simu kumueleza alikataa katakata kuwa hajazaa na Mimi na Wala nisimtambue kuwa baba wa Watoto wangu sio huyu niliyeondoka naye Wala huyo aliyekuwa tumboni' basi nikalia mwisho nikakubal kuwa bahati sio yangu' nilihangaika Sana na maisha hayakuwa rahisi upande wangu nikajifungua kwa shida mtoto wa kike yule mtoto ni Kama alikuja na bahati yake alipofika miezi 6 tu nami nikaitwa kazini kweli ilikua ni kazi nzuri Sana na mshahara ulikua mkubwa kwakweli maisha yangu yalibadilika mno miaka ikapita Kama mitatu hivi nikampigia Tena mwanaume simu labda atakuwa na Upendo basi na watoto lakini hajali Wala nini 🤔 nikaendelea na maisha yangu ikafika mahali nikaona nahitaji kuwa na familia nami niwe na mume kwani naishi maisha ya kujificha Sana na sio kwamba sikuwa na Mahusiano lah! Nilikuwa nayo isipokuwa sikuruhusu mwanaume kuja nyumbani kwangu au watoto wangu wamjue na hii ni kutokana na kuwa kila mahisiano niliyokua naingia mwisho nakuja kugundua mtu anafamilia yake hivyo naamua kuachana naye kwani Mimi nahitaji mwanaume wa kuishi naye na wanangu wamtambue Kama baba' nakumbuka mwaka Jana mwezi wa 10 nilikua natoka Ofisini gafla ilisimama gari mbele yangu akashuka kijana mmoja hivi yule Kaka alinichangamkia Sana Kama ananifahamu siku nyingi' alinisalimia nikaitikia akaniuliza Kama namkumbuka kwakweli nilikua sikumbuki chochote kuhusu yeye' mkaka ni mzuri jamani mzuri mwisho alivaa suti ya Dark Blue imekaa' mahali pake af mchangamfu kupitiliza alipoona Sina dalili zozote za kumkumbuka akaniambia anyways ninasafari ya haraka nawahi kwenye kikao akaniambia nitajie namba yako nikamtajia akanibipu akasema isave Yuzo Kisha huto akangia kwenye gari ilikuwa ni gari ya serikali yale macruser makubwa mie nikabaki nimesimama najiuliza hivi nimemuona wapi huyu Kaka nikakosa kumbukumbu kabisaaa nikamuua kujiondokea zangu' jioni nikiwa home akapiga video call nikaikata maana hakuna kitu sipendi Kama video call sipendi haswaa' nilipokata akaandika sms Whatsapp mambo' nikamjibu poa' afu hata sijajua jina lako mumy' nikamwambia naitwa Angle( sio jina langu halisi) akajibu waao jina zuri sana... Unaishi wapi? Nikamwambia akasema waooo unaishi mitaa ya vigogo' nikamjibu hamna ni kawaida tu' Basi tukaendelea kuchati pale ananiuliza Kama nimeolewa nikamjibu hapana ila nina watoto' akasema baba yao yuko wapi nikamwambia yupo sehemu fulani nikamtajia mkoa' akasema mnamawasiliano? Nikamwambia kwakweli sijui chochote kinachoendelea kwenye maisha yake kwa sasa... Basi tukachati weee mwisho wa siku akanitakia usiku mwema nikalala.....
YUZO 👌👌
*SEHEMU YA PILI*
Asubuh saa 12 nikasikia simu inaita nikaichukua kivivu kutazama ni Yuzo nikaipokea 'Vipi mamiloo hujaamka tu au Leo huendi kazini' nikamjibu naenda akasema basi amka ujuandae' mie Tena nashangaa anaanzaje kunipigia simu za kuniamsha asubhu asubuh wal sikujali Sana nikaamka nikaingia bafuni nikajiandaa nikaenda zangu kazini' siku zikapita mawasiliano yakazidi salamu nyingi muda wote ni simu' anawajulia watoto hali.. Sasa nakumbuka kabla ya Krismass nilisafiri kikazi nikiwa njiani alinipigia simu nikamwambia nipo safarini naelekea Dar kikazi nitarudi baada ya wiki moja akaniambia oooh nilikuwa na mazungumzo muhimu Sana na wewe siku ya leo nilikupigia simu ili nikuombe leo nikutoe lunch ili tuzungumze' nikamwambia labda wakati mwingine... Niliendelea na Safari tulipofika morogoro akanipigia simu Tena umefika wapi' nikamjibu Morogoro' akauliza utakuwa umechoka eeh? Nikamwambia kawaida' umekula mumy? Mie tena bado sijala Hadi nikifika ndio ntakula sipendi kula njiani' akaniambia unafikia hoteli gani' nikamwambia hata sijajua nitajua nikifika' akasema basi mimi naomba nikuchukulie hotel Kama hutajali ila naomba usikatae tafadhali' kweli nikakubali akaniambia ukifika stendi mbezi niambie nina kijana wangu wa Uba atakuja kukufata' mie Tena Asante😀 Safari iliendelea nikakafika mbezi nilipofika tu nikamwambia nimefika akaniambia Kuna mtu atakuja kukuchukua nimempa namba yako tafuta mahali upumzike' nikatafuta mahali kweli nikakaa nikaagiza juice zikapita Kama dakika 20 hivi simu yangu ikaita nikaipokea 'wewe ndio fulani? Mie ndio akasema nimepewa namba yako na Braza Yuzzo nije nikuchukue' nikajibu sawa Basi akanielekeza alipopaki mie nikaenda nikaingia kwenye gari Safari ya mjini ikaanza tulipokaribia ubungo akaniambia nimeambiwa nikupeleke Moveck Hoteli hii hotel ipo ubungo maziwa nyuma ya Tanesco kweli nikapelekwa ni Hoteli nzuri kwakweli nikaagana na yule Uba akaondoka' nikaingia room wakati naingia tu simu ikaanza kuita kutazama ni Yuzzo nikaipokea 'Mamiloo pole na uchovu nikamjibu Asante 'naamini utapapenda hapo' nikamwambia ni pazuri nimepapenda ni pazuri' ok Basi jimwagie maji ukapate chakula bili ya kila kitu nitaclia Mimi nakutumia hela ya chakula soon' mmh nikaanza kujiliza kwani inakuwaje ameambiwa mimi siwezi kujigaramia na nimekuia safari ya kazi si nitalipwa hela ya kujikimu? Nikakosa majibu ilikua kwenye saa kumi hivi nikaona nioge nipumzike kidogo ikifika saa moja nitoke nipate chakula uzuri ile hoteli inaupande wa bar kila kitu kipo.. nikaoga nikapanda kitandani nilale kidoho hee Mara Yuzzo anapiga ... vipi mamiloo nimekutumia hela ya chakula nikamjibu asante' tukaanza kuchati pale kama kawaida ni mtu wa maswali kibao unauliza hili ukijibu unaulizwa jingine had anakera ila sikua na jinsi kwakweli' Mimi sikumuuliza hata swali moja ni kujibu maswali yake tu nikajikuta saa moja hii hapa nikaona nishuke nikatafute chakula' nilala nikarudi zangu kulala maana mbilinge mbilinge za usafiri wa Dar asubuh inanibidi niwahi kuamka nkarudi zangu room nikapanda kulala nipo kwa bedi simu inaita 😏kutazama ni Yuzoo nikajisemea huyu naye anakera sasa Kama ni kihela chake kisinisumbue Mimi mwenyewe ninazo nikapokea
YUZO 👌👌
*SEHEMU YA TATU*
Basi nikapokea 'Vipi mamiloo umeshapata msosi? Ndio nimeshakula ndio Nataka nilale' ok Sasa shughuli yenu ya kazi mnafanyia wapi? Nikamuelekeza 'vennue itakuwa mikocheni B' nikamuelekeza na eneo tunalofanyia semina akasema basi yule kijana atakuja kukuchukua asubuh akupeleke na atakurudisha jiono🙄 nikabaki natoa macho najiuliza Sasa nitakuwa sina Uhuru wangu huyu mkaka Vipi🤔 nikajibu sawa Asante nashukuru Sana' Usijali mamiloo ni jukumu langu kuhakikisha haupati dhoruba yoyote ukiwa huko mbali🤣Mimi Tena haya Asante' nikakata simu... Kiukweli hakuniingis kabisaa Yani hata kuwaza kuwa ninaweza kumkubalia sikubakinitongoza sikuwaza nikatupa simu pembeni nikajilaza niutafute usingizi' Asubuh na mapema simu inaita Yani nakereka haswaa maana Kwanza maisha ya simu simu sijazoea' kuulizwa uko wapi unafanya nini' amka ujiandae sijazoea kabisaa Mara sijui umekula nini nilishasahau tangu uchumba wa yule mwendawazimu aliyeniachia watoto ni zaidi ya miaka 4 najiishia kijeshi Yani nile nisile nioge nisioge yote sawa tu nikizima simu nikiwasha hakuna Cha kutafutwa Wala sms😀Sasa saiz hadi kuzima simu nawaza maana ntakutana na uko wapi? Unafanya nini' ilikuwaje ukazima simu' mtu mwenyewe hata kunitongoza bado halafu upande wa pili bado nina ile Hali ya kuwa mwanamke akishazalishwa akachwa kupendwa tena ni mtihani pia nikawa nahisi hata huyu nikimkubalia siwezi kumuweka akilini maana anaweza kuwa na familia yake means sio aina ya mwanaume ninayemuhitaji Mimi kwa wakati huu nahitaji mwanaume wa kuishi naye watoto wangu wamtambue Kama baba kwa kuwa baba yao Hana mpango nao hivyo nayamani mwanaume wakusaidiana naye malezi' sio kwamba anisaidie Kodi ya nyumba au ada za watoto' hapana!! Nataka mwanaume wakuishi naye mengine tutasaidiana huko huko ndani ya nyumba na kwa kuwa ni singo mama nilijua kabisa kumpata mwanaume Fresh ambae hajawah kuoa Wala kuwa na mtoto atanisumbua na anaweza asiwapende watoto wangu huvyo nilijiwekea vigezo vya nahitaji mwanaume aidha kafiwa na mke wake au wameachana na yeye awe na watoto tukikubaliana tutazaa mtoto wetu mmoja wakutuunganisha basi maisha yaende hivyo huyu sikumuweka akilini kabisa na jinsi nilivyomuona ile siku ya Kwanza akili zake zilivyo mawenge nikajisemea hapa nitatongozwa nitakubali sawa lakini nitaliwa nitaachwa🤔 muda wote huo nawaza nipo kitandani simu imeita Hadi imekata ikaanza kuita tena nikapokea' vipi umeshajiandaa nikamwambia ndio Nataka kujiandaa akasema basi fanya haraka maana jamaa yupo njiani anakuja' nikajibu sawa' watoto je umewasiliana nao? hapana' kwanini? Unapataje amani umelala mbali na nyumbani halafu hujawajulia hali? Nikaambia ndio nilikua nataka niwapigie ndio simu yako ikaingia nikimaliza kuongea na wewe nitawapigia' akajibu 'Sawa ukiongea nao utanijulisha Kama wapo salama' akakata simu... Yani nilijikuta nasimama kwenye kioo maana haya mapenzi sijapata kuyaona afu nikaanza kumsoma ni mkali ana amri' mmh anyways kweli nahitaji Sana kuwa na mtu haswa umri wangu ulipofikia nisipokua makini hapa nitajikuta nabaki singo mama milele... Nikanyanyuka kivivu nikaingia bafuni kuoga nikajiandaa haraka haraka maana muda ulikua umeshaenda na Uba tayari alishafika nikabeba mkoba wangu huyo nikashuka nikakabidhi kadi reception nikaingia kwenye Uba tukaanza safari' by saa mbili nikawa nimeshafika Mikocheni mahali Vennue ilipo nikaingia tukajumuika na wenzangu nikakumbuka sijaongea na watoto nikampigia binti wa kazi nikaongea nao nikaona Sasa nizime Sim muda wa session umefika
YUZO 👌👌
*SEHEMU YA NNE*
Kabla sijazima simu nikakumbuka Yuzzo atapiga simu muda wowote ngoja nimtumie sms kuwa karibu naanza session hivyo tunawasiliana kwa sms' nilipotuma tunakajibu muda huo huo "usijali mamiloo nami nipo ofisini saizi" nikajibu poa' tulimaliza session salama' kwenye saa kumi hivi yule Uba akanifata tukiwa njiani akaniambia Braza amesema Kama Kuna sehemu unajitaji kwenda uwe huru kuniambia nikupeleke mmh nikawaza Sasa kwanini kila mahali nipelekwe na uba au ananichunguza🙄 nikajibu "sawa" tukafika Hotelini nikashuka Uba akaondoka zake nikaona kabla sijafanya chochote nimpigie huyu mtu nimwambie Asante nimerudi salama' lakini kila ninapofikiri kufanya hivyo unakuta yeye anapiga hata kabla Mimi sijapiga.. simu inaita nikapokea' "mamiloo pole na joto la mji wa watu" "Asante vipi umeshindaje" akajibu "poa" basi tukaongea pale akasema atanipigia saa moja usiku kuda ule anaenda mazoezini nikakata simu nikaingia kuoga nikarudi zangu nipumzike maana nilishachoka na jioni ikawa imefika nilipiga simu jikoni niletewe chakula room ili nisitoke' siku zilienda Hatimaye Semina iliisha zikawa zimebakia siku chache kufika xmass hapo najiandaa kesho yake nianze Safari ya kurudi mkoani kwangu na ilikua ijumaa jioni akanipigia simu kuniuliza kesho naondoka saa ngapi nikamwambia nimekata gari za Asubuhi Sana Nataka niwahi kufika nimewamiss Sana wanangu akaniambia " unajua siku zimebaki chache kufika Xmass na huko Dar vitu ni rahis Sana kwanini usiwafanyie shopping huko huko watoto?" Nikakaa kimya ananiambia Mimi Habari ya Shopping wakati nilishapanga Xmass hii Mimi sinunui nguo Wala nini maana Kama ni nguo wanazo nzuri tu kwa kuwa Mimi nikukutanaga na nguo nzuri muda wowote ule nanunua lakini pia saiz bajeti yangu haitoshi maana na huyu mtoto mdogo naye ndio anaenda kuanza shule sasa nitakuwa natakiwa ada za watoto wote wawili' mahitaji na Fedha ya usafiri kwa hesabu nilizopiga natakiwa niwe na milioni na ushee ili January hii watoto wote wawili waende shule... Mwenyewe nilishapiga bajeti mshahara ukiingia nikimix na hela hii ya semina January wanangu wanaenda shule kipapaa🤣 Sasa huyu vipi tena anataka kunivurugia bajet kwani hajui Mimi nu singo mama kila kitu nafanya mwenyewe 🤔 wakati huo siku bado ipo hewani nawaza nimpe jibu gani' Mara akasema namuagiza yule Uba aje akuchukue akuwahishe kariakoo saiz ni jioni usije ukachelewa kurudi😫nikahisi kuchoka maana Sasa kahela kangu naenda kukatoa lakini nikawaza sijalipa hoteli' sijalipa chakula na nimepewa hela hafi ya hoteli nimelipwa Sasa ubahili wa nini 🤔 nitatia aibu ngoja tu niende... Nikajibu sawa' akakata simu nikawa najiandaa ili uba akifika asinisubiri Sana Mara Sms ikaingia kwa simu kuchek ni Halopesa😜laki na sabini mie Tena nikapanda hewani nikamshukuru tukaondoka zetu na uba wangu kwenda kariakoo nikaona hapa niongeze na hela yangu nifanye manunuzi kamili hadi ya viatu na begi za shule pamoja na hizo nguo za sikukuu nikamaliza nikarudi zangu hotelini' Asubuh kulikucha nikawah shekilango kupanda gari za kwetu nikajirudia zangu mkoani ila jamaa ni mtu wa simu' sms muda wote umefika wapi' hatimaye tukafika alinifata stendi tukapitia Ice cream za watoto akanipeleka nyumbani njiani nikawa nawaza asije analazimisha kuingia kwangu wanangu wakamjua sipendi hii tabia itakuwaje lakini uzuri aliishia getini nikashusha mizigi akasema "wasalimie machalii" nikaingia zangu ndani wanangu walifurahi Sana kuniona kesho yake ilikua j2 tuliwasiliana Kama kawaida j3 Asubuh alikuja nyumbani kunifata akanipeleka kazini' ikawa ndio ratiba asiponipeleka asubuh basi jioni atanirudisha nikajikuta kidogo anaanza kuniingia moyoni maana udhaifu wangu Mimi ni watoto wangu na vile niliona anawajali kwakweli nilijikuta naanza kumuwaza nikikaa nikitulia mawazo yote yapi kwake asiponipigia simu nakosa raha akaniingia gafla sana' Kuna muda ikikaa nawaza navuta picha kuwa wanangu watafurahi na wao kujua kuwa tuna baba' ila Kuna saa Tena nikiwaza je Kama ana mke wake itakuwaje? Au alinitamani tu akijua Sina watoto Sasa amejua ananipumbaza ili anilale ananidump🤨 yani nilikua na mawazo mengi mno kumpenda nimeshampenda nasubiri tu aniambie ananipenda nimjibu "ndiyo" lakini baada ya hapo itakuwaje?🤔 Vipi nikijua ana mke😥 sikua sawa kwakweli' najua singo mama wenzangu mnaielewa hii hali haswa ikifika mahali umependa halafu ni lazima ufanye maamuzi ambayo hayatawaathiri watoto wako' nilijikuta hata nikikaa Ofisini nakuwa mtulivu mno "mapenzi" jamani yananisumbua... Nikarecall matukio ya nyuma wakati ndio narudi nyumbani nimeachika Sina mbele Wala nyuma nina mtoto wa miaka 2 na mimba juu mama yangu mdogo aliwah kuniita akasema "Angel saiz una mtoto na siku si nyingi utakuwa na mtoto mwingine kwa maana ya watoto wawili' hauna mume na wewe sio Mbaya utakuja kupendeza na kurudis uzuri wako wanaume watakupenda na kukutamani pia🤨hiyo hali huwezi kuikwepa 'utapenda tena' lakini wakati huo utapenda kulingana na watoto wako licha ya kua kiongozi ni moyo wako......
Nitarudi 💃💃💃💃💃
YUZO 👌👌
*SEHEMU YA TANO*
Licha ya kua kiongozi ni moyo wako lakini waamuzi wa ni aina gani ya mwanaume uwe nae ni ya watoto wako... Mwanamke mwenye watoto anatakiwa kufikiri Mara mbili mbili kabls hajaingia kwenye Mahusiano yoyote" niliyakumbuka hayo maneno ya mamdogo akili ikastaki maana naumia jamani hapo nimeshakaa mwaka mzima Sina Mahusiano Wala mwanaume yoyote maana nilichoka ile hali unatoka na mtu ambaye huna uhakika naye inabidi muende Logde siku ya mdinyo mie nina watoto ili nipate muda mzuri wa kuwa na mtu najikuta naaga watoto kuwa ninasafiri kikazi naenda nalala huko asubuh ukirudi unakutana na maswali ya watoto "mama mbona umerudi asubuh watu wakisafiri wanarudi jioni😂 Yani singo mama tunashida Sana Mimi huwa nakutana na maswali mazito kutoka kwa wanangu.... Sasa nikiwaza Hilo tu nakuta akili inagoma kabisa nipo katikati ya mapenzi na watoto afu ndio nishapenda na mwili nao unahitaji🙊 nyie jamani ukitaka kujua mapenzi yanatesa uwe singo mama ndio utajua ujui😂😂... Niliwaza Sana mwishoni nikasema nitamkubali akinitongoza ila sitamleta kwangu hadi nijue ni muoaji ama la na Kama ni muoaji tufunge ndoa ya 12 asubuh life lianze😂😂 ilifika siku nikaanza likizo ya siku kuu ilikua j5 ya tar 22 Yuzzo alinipigia simu ndio nilikua najiandaa kurudi nyumbani nikapokea akasema uko wapi nikamjibu "Ofisini lakini ndio najiandaa kurudu nyumbani" akasema nakufata kweli alikuja Ofisini kwangu Safari hii hakuwa akiendeshwa na gari ya ofisi alikua na gari yake ( Subaru Impreza nyeusi) nikatoka tukaondoka' namkata jicho la wizi kapendeza hatari Kaka ananukia suti imekolea pasi jamani huyu Kaka kumbe mzuri hivi mbona anachelewa kunitongoza jamani ili nimpe condition zangu😂kwakweli Kaka ni smart tukapita sokoni ananiuliza watoto wanakula nini mie hata sijui chochote tu nitanunua "aa wewe sema watoto wanakula nini bana" mie hata Sina jibu maana najua home Kuna maharage kikubwa hapo nirudi na nazi na Matunda basi' nikaona jamaa anaingia kwenye bucha ya samaki akapaki gari akashuka aliporudi kaja na Mfuko unakuku ndani samaki Kama kg mbili hivi na pakti ya soseji😂 tukatoka hapo tukaingia sokoni akanunua mazaga mifuko miwili mmoja wake mmoja wangu akanipelea nyumbani akarudi zake... Ila ile siku kwangu ilikua ndefu Sana kila nikifumba macho nahisi Kama namuona navuta picha Kaka ana rangi ya mtume😜 nikaona hapa isiwe shida nina Rafiki yangu wa Rohoni lake langu na langu lake tumepanga jirani nikampigia simu aje ili nimueleze anisaidie nifanyaje na yeye ni singo mama mwenzangu ingawa yeye ni Kama wapo kwenye kurudisha ndoa yao maana mume ameshajirudi ni yeye tu hataki kurudi kwake, nikamuita Debby akaja home nikamuelezea situation yote tangu siku nimekutana na yuzo hadi hapo nilipofikia nikamuonesha na picha ya Yuzzo' Debby akaniambia Sasa huyu ndio mwanaume Yani hapa shikilia na usichomoke kirahisi hakuna mwanamke anapenda kulea watoto peke yake Mimi tu hapa nataka kurudi kwangu hivyo shikilia rafiki yangu' kwanza mwanau mwenyewe kisu' anaonekana hela ipo' anakujali na uneshamwambia una watoto anaonekana bado anakuhitaji acha ujinga siku hizi wanaume wanatafutwa Kama almasi watu wanakesha makanisani kuomba MUNGU awape wanaume wewe umeletewa mdomoni kabisaa 😂😂 Debby aliongea hadi nikaishiwa pozi' wakati tunaongea yuzo akapiga simu nikapokea "mamiloo umelala?" Mie hapana "ok kabla hujalala unicheki basi mamaa" nikamjibu sawa
..... Narudi💃💃💃💃💃
Kwa mwendelezo Wasiliana Na MWANDISHI
Queen Lizzie
0683944333
Tags
simulizi