*KAZI ZA NDANI OMAN ZILIVYONIKUTANISHA NA MZIMU WA KIFO*
*SEHEMU YA KWANZA*
_____________________________________
ILIKUWA ni mara ya kwanza katika maisha yangu kupanda ndege, licha ya kuwa na wasiwasi juu ya maisha ninayokwenda kuishi katika nchi ngeni ya kiarabu, nchi yenye utamaduni na sheria tofuati na nchi yangu, hata hivyo, hilo halikunifanya kutoona fahari kuwa ndani ya Fly Emirates Airlines iliyokuwa ikikata mawingu kwa kasi ya ajabu.
Nikiwa nimeketi katika siti ya dirishani nilipotizama nje niliona tupo katikati ya mawingu meupe yaliyozagaa katika anga na kuleta taswira kama shamba la pamba lililomea.
Nilikuwa nimevaa visikilizo vya masikioni (hearphones)nikisikiliza muziki uliokuwa unatokea kwenye walkman yangu ya CD kupitia kwenye visikilizo vya masikio, ilikuwa ni jambo jingine lililoleta buradani nafsini mwangu.
Sikumbuki tulitumia muda gani kusafiri angani, ninachokumbuka baada ya muda mrefu kupita sauti ya mhudumu wa ndege kupitia spika zilizokuwa ndani ya ndege ilisema:
“We are about to land, all passangers of fly Emirates Airlines, make sure your belt is closed” (abiria wote wa fly Emirates Airlines mnatakiwa kufunga mkanda kwani ndege inakaribia kutua) sauti ya mhudumu wa ndege ilisikika kwa Kiingereza na kurudia kwa Kiswahili.
Ni sauti hiyo ndiyo iliyonistua, nikaangalia saa yangu ya mkononi ikanionyesha ilikuwa ni saa mbili usiku, nilifunga mkanda kama tulivyotakiwa, kisha nikatulia kwenye kiti, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi, hofu ikanijaa moyoni
“Wasichana wanaokwenda kufanya kazi Oman, baadhi yao wanabakwa, wanamwagiwa maji ya moto, na hata kuuawa, kubwa kuliko vyote nchi ile inasheria kali dhidi ya makosa mbalimbali” nilikumbuka maneno hayo niliyoambiwa na mama yangu siku moja baada ya kumpa wazo la kutaka kwenda Oman kufanya kazi za ndani.
Taswira ya mandhali ya kijiji cha Nguruka huko mkoa wa Kigoma, ilinijia kichwani, na wakati taswira ya kijiji inapita ubongoni mwangu ilikwenda sanjari na picha halisi ya maisha yangu nikiwa miongoni mwa wenyeji wa kijiji hicho kinachokaliwa zaidi na wakazi wa makabila ya Waha, Wanyamwezi, na walundi wachache waliojipenyeza wakitokea nchi jirani ya Burundi.
Baada ya kumaliza kidato cha nne nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari ya Kibasila iliyoko jijini Dar.
Zilikuwa ni nyakati za furaha maishani mwangu pengine kuliko nyakati nyingine zozote, lakini ni nyakati hizohizo furaha yangu iligeuka na kuwa majonzi yasiyoweza kusahaulika kichwani mwangu.
“Hutuwezi kumudu gharama za kukusomesha mwanangu, shule uliyofaulia ni shule ya kutwa, maana yake ni kwamba, upangishiwe chumba, na upate huduma kama mwanamfunzi, hiyo ni mbali na ada, sizungumzii nauli na mambo mengine ya shule...mji wa Dar wenyewe unausikia tu!. ni mji wenye sifa ya kuwa na gharama kubwa ya maisha kama nini!” mama alinieleza siku moja.
Sikubishana na ukweli wa maneno yale. Alichokisema mama kilikuwa sahihi kabisa, familia yangu ilinuka ufukara, mara kadhaa nilikuwa nikishuhudia tukishinda na kulalia uji usiyokuwa na sukari.
Siyo mara moja kuchekwa nikiwa shuleni, lilikuwa ni jambo la kawaida kudharauliwa, kuzomewa hata kutengwa kwa kuvaa nguo zilizochoka na kuchanikachanika kiasi cha kutoa picha kamili ya kiwango cha ufukara ulionizingira,.
Wala halikuwa jambo la kushangaza kuacha kwenda shule na kuingia porini nikisenya kuni na kuuza kwa watu na pesa kidogo niliyoipata ndiyo niliyotumia kwa kula, kununulia madaftari na sare za shule.
Niliishi maisha ya kifukara tangu nazaliwa hadi nilipokuwa binti mwanamwali. Nikiwa msichana mrembo wa miaka 21 nilikuwa ni mtu mwenye ndoto na matarajio makubwa sana kama vijana wengine, japokuwa nilikuwa natoka kwenye familia masikini.
Nilisumbuliwa na wanaume wakware pale kijijini na baadhi yao, walitumia umasikini wangu kama njia rahisi ya kunipata, lakini ajabu nilikuwa na misimamo isiyoyumba. Niliamini mwanaume pekee atakaye ujua mwili wangu ni yule atakayekuwa mume wangu. Kwakweli nilikuwa ni mwanamke mwenye matarajio makubwa sana, lakini ndoto zote zilizimishwa na ufukara ulio nizingira.
Niliyakumbuka hayo nikiwa nimetulia ndani ya ndege iliyotarajiwa kutua dakika chache katika nchi ya Oman. Nilitokwa na jasho lililotokana na hofu huku nikihisi tumbo likichemka kadri tulivyokuwa tukiusogelea uwanja wa ndege wa Jijini Muscut nchini Oman.
Dakika chache badae, ndege ilikuwa ikiserereka kwa kasi kwenye ardhi ya nchi ya Oman Jijini Muscut. Baada ya kusimama, tulianza kuteremka abiria mmoja mmoja.
Nilipo ikanyaga aridhi ya nchi hiyo, nilijiona nikiwa kiumbe mdogo mithili ya sisimizi, nilijiona ni mtu nisiyekuwa na dira kwenye ulimwengu mpya, utitiri wa magorofa yaliyojichomoza kama uyoga sambamba na barabara za fly over zilinifanya nijione kama ndiyo nakwenda kupotelea katikati ya Jiji hilo.
“Are you Agripina (Wewe ni Agripina?) nilisikia sauti moja akinisemesha, nilipogeuka nilimwona mama mmoja mnene wa umbo, aliyevaa baibui sehemu yote ya mwili wake isipokuwa uso pekee, mkononi akiwa na bango lililoandikwa jina langu.
“Yeah, i’m Agripina, who are you?” (Ndiyo, mimi ni Agripina wewe ni nani?) nilihoji.
“Naitwa Mariamu Rashidi, ninataarifa za ujio wako, mimi ndiye nitakuwa mwenyeji wako hapa Oman” yule mama alisema kwa Kiswahili huku akipokea begi langu la nguo.
“Kumbe unazungumza Kiswahili!.” Niliuliza kwa wahka
“Ndiyo, mimi ni mtanzania kama wewe, tena ni Msambaa wa Milimani, natokea maeneno ya huko Lushoto kijiji cha Makose mkoani Tanga”Alisema.
Kwakweli nilifurahi kukutana na mwanamke yule anayezungumza kiswahili kwenye taifa hilo la kiarabu.
Lakini hata hivyo, kwa muda mchache sana niliotumia kutambuna na yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Rashidi, kuna mambo niliyoyagundua kutoka kwakwe, mambo ambayo yalinitisha vibaya mno.
*SEHEMU YA PILI*
Pamoja na kuwa na wasiwasi dhidi ya yule mtu, sikutaka kabisa kuonesha hali ya hofu waziwazi, wakati wote nilitengeneza uso wenye tabasamu bandia mbele ya macho ya mwanamke yule. Tulitoka nje ya uwanja ule na kuchukua tax kisha tukaanza safari ya kuelekea mahali nisikokujua.
Tulitumia nusu saa kufika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi, ambazo siyo tu hazikujengwa kiramani lakini pia zilikuwa ni nyumba zilizochoka.
“Hapa panaitwa Deira,” Mariamu alisema, tukiwa mbele ya nyumba moja iliyoonekana kuchakaa kwa kukosa ukarabati wa muda mrefu.
“hapa ndipo ninapoishi, lakini kwa sasa tutaishi wote kwa muda wa siku mbili, nitatumia muda huo kukueleza sheria na taratibu za nchii hii kabla ya kwenda kuanza kufanya kazi za ndani.”
“Watu wanasema sheria za hapa uarabuni ni ngumu?” nilimuliza.
“Hapana siyo ngumu, ila inategemeana na wewe utakavyozipokea. Ukizipoea sheria za hapa katika mtazamo wa ugumu, kwakweli utashindwa, lakini ukizichukulia kwa wepesi na ukazitekeleza, huwezi kupata tabu”
Pamoja na maelezo ya Mariamu, bado hayakunifanya kutoogopa, matukio ya mabinti wa kitanzania kubakwa, kuunguzwa kwa maji ya moto wakati mwingine hata kuuawa.
Sambamba na hayo, kila nilivyofikiria familia yangu, familia iliyozingirwa na umasikini wa kupindukia, nilijikuta napata nguvu na hata kutoogopa lolote.
Masaa arobaini na nane badae, mimi na Marimu tulikuwa kwenye tax tukielekea sehemu moja iitwayo Suwaiq kilometa 50 kutoka mjini Muscut, huko ndipo mahali nilipotakiwa kwenda kufanya kazi ni huko ambapo kulikuwa na familia ya tajiri aliyeitwa Abdallah Mustapha ambaye ndiye niliyetakiwa kwenda kuanza kazi nyumbani kwakwe
“Karatasi za majibu yako ya vipimo vya hosptali unazo?” Mariamu aliniuliza wakati gari likikunja kushoto na kuiacha barabara kubwa ya lami na kuingia kwenye barabara iliyokuwa na changarawe nyingi.
“karatasi zipo kwenye begi, kwani majibu ya vipimo, bado yanahitajika hadi huku?”
“Ndiyo” alinijibu kwa ufupi. Nilijiuliza moyoni inaamna huko niendako, wao waajiri hawajui kuwa siwezi kuwa kwenye nchi hiyo pasina kupima, vipi tena wahitaji majibu ya vipimo.
Wakati nikiwa bado najiuliza, gari lilikata kona na kuiacha ile njia yenye changarawe na kuingia kwenye njia nyembamba iliyokuwa na marumaru, pembeni ya njia hiyo kukiwa na miti mingi iliyopandwa kwa mpangilio mzuri.
Gari lilikwenda kwa mwendo wa taratibu, mita kama ishirini tukawa mbele ya nyumba kubwa iliyokuwa na sifa zote za kuitwa nyumba ya kifahari.
Baada ya dereva tax kulipwa ujira wake na kuondoka , tukasogea kwenye geti la jumba lile, Mariamu alibonyeza Swich ya kengele iliyokuwa pale getini na muda mfupi badae, alikuja mvulana wa kisomali kufungua, nilipogonganisha macho na yule mvulana kitu fulani kisichoelezeka lilipita kichwani mwangu. Macho yangu yalinata kwa yule mvulana kwa nukta kadhaa.
Alizungumza na Mariamu kama watu wenye kufahamiana kwa muda mrefu kilichonishangaza zaidi aliongea kwa Kiswahili, alikuwa ni mtu mcheshi na makalimu, Kiswahili chake kilikuwa na lafudhi ya kimombasa, kwakweli alionekana ni mtu mwenye kufurahia maisha wakati wote, baada ya maongezi ya hapa na pale, alitufungulia geti na kuingia ndani.
Ndani ya lile jumba lile kifahari kulikuwa na eneo kubwa la wazi ambalo lilipandwa bustani ya maua na nyasi fupi za kijani kibichi, upande wa kaskazini kukikuwa na bwawa dogo la kuogelea sanjari na viti vichache vya kukalia vilivyokuwa chini ya miavuli midogo mahususi kwa kimvuli, mbele ya nyumba hiyo kulikuwa na magari ya bei mbaya yaliyopaki kwenye parking maalumu iliyojengwa kiustadi.
“Hapa ndipo utakapo fanya kazi” hatimaye Maliamu aliniambia.
“Pazuri sana”
“Ndiyo ni pazuri, hata mshahara utakaolipwa utakuwa mnono, mradi uwe tayari kukabiliana na changamoto zitakazo kukabili” aliposema hayo taswira ya kubakwa, ikanijia.
Wakati huohuo alitokea mwanamke mmoja wa kiarabu aliyekuwa na sifa zote za kuitwa mrembo, pamoja na uzuri wake lakini midomo na macho yake yalinijulisha kuwa mtu yule alikuwa ni mtu wa aina gani. Majivuno na dharau.
“Asalam aleykum” alitusalimia
“Waleykum salama”
“Huyu ndiye yule mtu mweusi kutoka Tanzania?” alisema. kauli ile ilinifanya niendelee kuamini kuhusu fikra zangu juu ya tabia ya yule mwanamke wa kiarabu.
“Ndiye” Mariamu alimjibu.
“Mmepima na mmeona hana Ukimwi”
“Hana?”
“Ebora na Tb je?”
“Hana pia”
“Piteni ndani” alisema yule msichana.
“Huyu anaitwa Zakia Almajidi mke wa Abadallah Mustapha.” Mariamu alininong’oneza tukiwa tunaingia ndani, nilishusha pumzi ndefu na kwa mara ya kwanza nafsi yangu ikikiri kuwa nipo kwenye uwanja wa vita.
Pamoja na kukarahishwa na maswali yale lakini nilivyoingia tu ndani ya lile jumba, akili yangu ikahamia kwenye mandhali ya mule ndani. Niwe mkweli, tangu nizaliwe hadi leo hii, sijawahi kuona sebule nzuri kama sebule la jumba la kifahari la tajiri Abdallah Mustapha lililopo Suwaiq nje kidogo ya Jiji la Muscut nchini Oman.
Macho yangu yalikuwa hayatulii, niligeuza shingo huku na kule, nikivutiwa na fenicha ghari zilizokuwa mule ndani. Nilikuwa mtulivu wakati Marimu akifanya mazungumzo na yule msichana wa Kiaraubu kuhusiana na mchakato wa ajira yangu.
“Shika hii” Yule msichana wa kiarabu alisema.
“ Agripina Soma vizuri huo mkataba wako wa kazi, kisha tia saini hapo chini” alisema Maliamu nikiwa nimeshika ile karatasi niliyopewa na yule mwanamke wa kiarabu. Nilipitia ule mkataba ulioandikwa kwa lugha ya kingereza, sikuamini nilipoona nitalipwa kiasi cha riyal 100 ambayo ilikuwa karibu shilingi laki sita na ushee kwa pesa ya Tanzania.
“Yanii kufanya usafi, kuosha vyombo, kufua na kupika, hivyo tu, nalipwa laki sita na uchafu!” niliwaza, niliona ni pesa nyingi nilizo takiwa kulipwa ukilinganisha na kazi nitakazokuwa nikifanya, niliamini wakati wa kupunguza umasikini kwenye familia yangu ndiyo huo.
Sikutaka kuchelewa, nilimwaga saini kwenye yale makaratasi na nikawa nimeingia mkataba wa miaka miwili Kwa makubaliano ya kuongezewa mkataba endapo mwajiri wangu atakubaliana na utendaji wangu wa kazi.
Muda mfupi badaye, nilielekezwa mazingira ya jumba lile sanjari na kutambulishwa kwa wafanya kazi wenzangu wawili mmoja mwanamke aliyeitwa Fatuma emeke kutoka Liberia na yule mvulana wa kisomali nilitambulishwa kwa jina la Hussein Jabal, baada ya mambo hayo kukamilika Mariamu aliniaga:
“Mimi naondoka”
“Sawa..lakini kuna ajambo nilitaka kukuuliza”
“ ..kuhusu?”
“Kuhusu uvumi wa wasichana wa kazi kufanyiwa ushenzi wakiwa huku ikiwemo kubakwa.”
“Kubakwa ni sehemu ndogo sana ya changamoto zilizopo huku, kwanza ni jambo la kawaida tu, kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuwa tayari kuipokea hali hiyo pale itakapokutokea” Mariamu alisema katika namna ya kuchukulia jambo lile kiwepesi.”
“Niwe tayari kubakwa pale hali hiyo itakapo tokea?”niliuliza nikiwa nimemkazia jicho.
“Siyo uwe tayari kubakwa, uwe tayari kufanya mapenzi kwa hiyari.”
“Sijaja huku kufanya mapenzi na mtu wa aina yeyote, lakini pia, sikuja huku ili ninyanyasike kwa namna yeyote ile.” nilisema kwa sauti kavu lakini yenye viashiria vya kumaanisha kile nilichosema.
“Ngoja nikupe siri moja..” Mariamu alisema, lakini kabla hajamaliza mara Zakia alitokea na kunitaka nianze majukumu yangu. Tuliagana na Mariamu kwa miadi ya kuonana wakati mwingine nikiwa na shauku ya kutaka kujua siri aliyotakiwa kunipa.
*SEHEMU YA TATU*
Nilibaki na mashaka makubwa sana, bado sikuwa na imani na Maliamu, mwanamke yule sikuwa na imani naye tangu siku ya kwanza aliponipokea uwanja wa ndege wa Muscuti.
Nilianza kazi kwa nidhamu na umakini, mwenyeji wangu akiwa ni Fatuma Emeke msichana mweusi na mzuri wa umbo kutoka nchini Liberia. Wiki kadhaa nikiwa ndani ya ile nyumba ya kihafahari kama mfanya kazi wa ndani (house girl) nilibaini jambo jingine jipya.
“Sijaja huku kufanya mapenzi na mtu wa aina yeyote, lakini pia, sikuja huku ili ninyanyasike kwa namna yeyote ile.” nilisema kwa sauti kavu lakini yenye viashiria vya kumaanisha kile nilichosema.
“Ngoja nikupe siri moja..” Mariamu alisema, lakini kabla hajamaliza mara Zakia alitokea na kunitaka nianze majukumu yangu. Tuliagana na Mariamu kwa miadi ya kuonana wakati mwingine nikiwa na shauku ya kutaka kujua siri aliyotakiwa kunipa.
Nilibaki na mashaka makubwa sana, bado sikuwa na imani na Maliamu, mwanamke yule sikuwa na imani naye tangu siku ya kwanza aliponipokea uwanja wa ndege wa Muscuti.
Nilianza kazi kwa nidhamu na umakini, mwenyeji wangu akiwa ni Fatuma Emeke msichana mweusi na mzuri wa umbo kutoka nchini Liberia. Wiki kadhaa nikiwa ndani ya ile nyumba ya kihafahari kama mfanya kazi wa ndani (house girl) nilibaini jambo jingine jipya.
Yule mwanamke wa kiarabu aliyeitwa Zakia Al Majidi mke wa Abdallah Mustapha alikuwa ni mke wa pili wa tajiri mzee Abdallah Mustapha ambaye alikuwa na watoto wawili wa kiume kutoka kwa mke wake mkubwa waliokuwa wakiishi na mama yao katika mji wa Al Jibrih mashariki mwa Jiji la Muscut nchini Oman.
Nilifanya kazi nikiwa ni mtu mwenye mori na ari ya kazi, sikuwahi kukutana na matukio kama yalivyokuwa yakivumishwa nikiwa Tanzania, hapakuwa na mtu aliyewahi kunisumbua kimapenzi aidha kuninyanyasa kwa namna yoyote ile ingawa majivuno ya Zakia sikuwa napendezwa nayo.
Nilimaliza mwezi mmoja salama, nililipwa mshahara wa kwanza vizuri bila tatizo lolote, siku napokea pesa kama malipo ya kazi zangu lilikuwa ni jambo la furaha mno kwenye maisha yangu, niliamini huo ndiyo muda wa kukamilisha ndoto zangu za kupunguza hali ya maisha duni kwenye familia yangu.
Nakumbuka Kila mwisho wa wiki, nilikuwa nikifunga safari hadi Muscut, huko nilipiga simu kwenye vibanda vya simu na kuwasiliana na familia yangu, lakini pia, nilikuwa nikituma pesa nyumbani kwa njia kama mape-xpress, western union na kadhalika.
Katika kipindi chote cha maisha yangu ndani ya nyumba ya tajiri Abdallah Mustafa, mtu wa karibu kwangu alikuwa ni yule mvulana Hussein Jabal, raia wa Somalia, ukiachilia mbali Fatuma ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu wa wa kike tuliyeshirikiana kwenye kazi zote za ndani. Ukaribu wangu na mvulana huyu ulitokana na uwezo wake wa kuzungumza Kiswahili.
Mbali na hilo, Hussein alikuwa ni mtu mcheshi na msikivu, Kila siku baada ya kazi, tulikaa kwenye bustani ya majani na kuzungumza mambo mengi, nilipata kuelewa mambo mengi kuhusu mtu yule, lakini hata yeye alijua mambo kadhaa kuhusu maisha yangu.
Ukaribu wangu na Hussein ulinifanya nimzoe, kumzoea kukazaa hali ya kumuwaza kila wakati. Hali ile ya kumuwaza kila wakati, kukatengeneza hali nyingine ya kummisi hususani pale awapo mbali na mimi.
Taswira ya sura ya Hussein Jabal ilianza kuniganda kichwani mwangu. Sikutaka kujiongopea kabisa kwamba moyo wangu hauvutiwi na uso wenye pua ndefu, macho makubwa sanjari na meno yaliyojipanga vizuri mithili ya punje za muhindi.
Sikutaka kabisa kujifariji kuwa nafsi yangu haikuvutika na umbo kakamavu la yule mvulana.
Lakini hata hivyo, akili yangu haikuwa tayari kuukubali ukweli uliotoka moyoni mwangu, ukweli wenye viashiria vyote vya mapenzi kwa mvulana yule.
Nilijikumbusha na kujionya juu ya msukumo huo. Sauti moja kichwani iliniambia jiepushe na mapenzi yatakuletea matatizo, fuata kilichokuleta, lakini pamoja na hilo, bado moyo wangu ulikumbwa na wazimu dhidi ya mvulana yule.
Bila kutarajia nikajikuta mimi na mvulana yule tunaanzisha mahusiano ya kimapenzi, mapenzi ambayo yalikuja kuleta madhila makubwa mno kwenye maisha yangu hadi leo hii ninapo simulia mkasa huu.
mahusiano ya kimapenzi kati yangu na Hussein yalianza kama mzaha, awali nilichukulia kama nimepitiwa na jinamizi la mahaba na tamaa za mwili kwa bahati mbaya, niliamini mwisho wa penzi lile ni kupotea kama lilivyokuja, lakini kadri siku zilivyokuwa zikiyoyoma ndivyo mapenzi yangu na mtu yule yalivyozidi kustawi na kukua kwa kasi.
Hussein Jabal alikuwa ndiyo mvulana wa kwanza kuujua mwili wangu, nakumbuka siku ya kwanza kugaragara nae kitandani, ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuingia kwenye sayari ya mahaba kunako sita kwa sita , kwakweli siwezi kuisahau siku hii.
“Asante Agripina.” Hussein alisema akiwa amelala chali, kichwa changu kikiwa juu ya kifua chake, tukiwa kama tulivyozaliwa.
“..kwa”
“Kwa penzi tamu...na kwakuwa mwanaume wa kwanza kufungua bikira yako”
“Usijali Hussein, ila jambo moja..”nilisema huku nikigeuza shingo yangu na kumwangalia machoni, tukawa tunatizamana.
“Usiniache tafadhali”
“Siwezi kukuacha Agripina, nataka siku moja tukaishi Mogadishu, huko kwetu Somalia”
“kweli?”
“Kabisa”
Huo ulikuwa ni mwanzo wa mimi kuingia kwenye mambo ya kiutu uzima, Mahusiano kati yangu na mvulana yule yalikuwa ni siri ya watu watatu, kwa maana ya mimi mwenyewe Hussein pamoja Fatuma Emeke ambaye alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu kutoka Liberia.
Usiri wa penzi langu na mvulana yule, raia wa Somalia ulitokana na jambo moja kuu. Tuliogopa Sheria kali ya nchi ya Oman iliyokuwa ikisimamia misingi ya sharia.
Ilikuwa hairuhusu vijana ambao hawajaoana kuwa kwenye mahusiano ya kimapanzi kabla ya ndoa. Adhabu yake ilikuwa ni kuchapwa viboko hadhalani na kufukuzwa nchini humo, hiyo ilikuwa ni kwa wageni.
Tuliendelea kufanya kazi kwa bwana Abdallah Mustapha kwa nidhamu kubwa, huku mahusiano yangu na Hussein yakiendelea kwa kasi lakini yakiwa kwa siri
*SEHEMU YA NNE*
Kila siku usiku nilikuwa nikiondoka ndani ya chumbani na kwenda chumbani kwa Hussein, huko nilifanya nae mapenzi usiku kucha na alfajiri kabla ya adhana, nilirejea chumbani mwangu.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu huko Suwaiq nchini Omani kabla ya siku moja kutokea tukio moja lililobadili dira ya maisha yangu!
**********
“Ta, ta, ta,” sauti ndogo ya mshale wa saa ya ukutani ilisikika. Ilikuwa yapata saa sita na nusu usiku, nilikuwa nimelala chali huku macho yangu yakitizama kwenye dari.
Hakuna kilichosikika zaidi ya sauti ndogo ya saaa ya mshale sanjari na mkoromo mdogo uliokuwa ukitoka kwa Fatuma aliyekuwa kwenye usingizi wa pono.
Nilijinyanyua kitandani na kuketi kitako, macho yangu yalihamia kwenye kipimo cha kupima ujauzito, bado moyo wangu ulishindwa kukubaliana na ukweli kwamba nilikuwa mjamzito. Niliogopa, siyo kwamba sikutaka mtoto, ila muda wa kuwa na mtoto haukuwa sahihi.
Nilivuta pumzi ndefu kwa ndani na kuzitoa kwa mkupuo, nikachukua kanga na kujifunga lubega kisha nikazipiga hatua kuendea mlango, taratibu nikaufungua na kutoka nje, nilinyata kukifuata kibanda alichokuwa akilala Hussein, ndani ya nyumba ile ya tajiri Abdallah Mustapha.
Kulikuwa na ukimya eneo lote la nyumba ile ya kifahari, nilisogea hadi mlangoni mwa chumba cha Hussein na kusukuma mlango, ajabu mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.
Haikuwa kawaida kwa Hussein kufunga mlango hasa kwa kipindi ambacho tunakuwa tumekubaliana kuwa nitakwenda chumbani kwakwe.
Nikasukuma tena, lakini haukufunguka, nikawa natizama huku na kule ili nisionekane, wakati huo akili yangu ikaniambia nimgongee, wakati nataka kugonga mara nikasikia sauti kutokea mule ndani.
Ilikuwa ni sauti ya kilio cha mwanamke, nikapata umakini na kutega sikio, nikaendela kugundua kuwa ilikuwa ni sauti ya kimahaba ya mwanamke aliyekuwa ndani ya chumba cha Hussein Jabal.
Dakika mbili zilitosha kubaini ukweli. Ndani ya chumba kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya mapenzi, Hussein ananisaliti! ndiyo wazo la kwanza kupita kichwani mwangu.
Mwili ukanitetemeka, donge zito likanikaba kooni, nikahisi uchungu wa ndani kwa ndani, wivu ukanivaa, nikaugonga mlango kwa nguvu. Sikujibiwa zaidi ya kuendelea kusikia sauti ya mwanamke aliyekuwa akilia, kilio cha raha.
Kitendo hicho kikazidisha wahaka ndani ya nafsi yangu, akili yangu ikawa na maswali lukuki, ndani ya lile jumba tulikuwa wanawake watatu, kwa maana ya Fatuma Emeke, Zakia ambaye ni mke wa Abdallah Mustapha pamoja na mimi.
Nikaendelea kubaini kuwa kivyovyote vile Hussein ndiye alikuwa akifanya mapenzi na mwanamke mule ndani, lakini swali kuu ni je mwanamke huyo ni nani? Ni Fatuma au ni Zakia, nikaaanzia hapo kutafakari. Fatuma nilimwacha chumbani akikoroma, maana yake ni kwamba siyo Fatuma, nikamfikiria Zakia.
Nilipo muwaza tu mwanamke huyo, hapohapo taswira ya tabia za mwanamke huyo zikanijia akilini,
Mbali ya wivu dhidi ya mumewe, Alikuwa ni mwanamke mwenye dharau na majivuno, mtu mweusi kwakwe alikuwa ni katuni isiyo na maana yoyote, hakupenda kuchangia meza moja ya chakula na watumishi wake wa ndani. Siku zote alimini mtu mweusi yupo duniani kwa ajili ya kuwa mtumwa kwa mtu mweupe. Nilipo waza hilo, nafsi yangu ilikiri kuwa lilikuwa ni tusi zito kwa mwanamke yule kwa kitendo cha kumuhisi kuwa anaweza kuwa ndiye mtu aliye ndani wakifanya mapenzi na Hussein Jabal mvulana asiye na mbele wala nyuma kutoka huko Mogadishu nchini Somalia.
Sasa Hussein anafanya mapenzi na nani? Nilijihoji huku nikijawa na wivu mwingi kifuani kwangu, donge zito lilinikaba kooni kila nilivyozisikia kelele za kilio cha mahaba kutoka mule ndani. “Yanii huyu mwanaharamu anipe mimba halafu kama haitoshi ananisaliti!” kwa nguvu zangu zote niliusukuma mlango na kuingia ndani.
Sikuamini macho yangu
Kwa mwendelezo mpaka Mwisho
Wasiliana Na MWANDISHI
Queen Lizzie
0683944333
Tags
simulizi