TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

FAHAMU JINSI YA KUBADILI MITIZAMO ILI UBADILI NAMNA UNAVYOJIONA...

FAHAMU JINSI YA KUBADILI MITIZAMO ILI UBADILI NAMNA UNAVYOJIONA...
__________________________
Kila mtu yupo hapa duniani kukua ili ayafikie mafanikio, na hakuna mtu ambaye yuko radhi ajione akibaki katika kiwango kilekile ilihali siku  zinazidi kwenda mbele!

Na ifahamike kwamba, kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele kila mtu anaukaribia utu uzima na hakuna ambaye anakua kuelekea utotoni!
Kwa mantiki hiyo huna budi kukuza kiwango chako cha kujiona kipate kukua siku hadi siku.

Mantiki yake ikiwa, kile kiwango ulichokuwa unajiona jana kiwe tofauti na kile kiwango utakachojiona leo!
Na, itafaa zaidi endapo leo utajiona katika kiwango bora zaidi ya kile ulichojiona jana!

Hata hivyo, itakuwa ni ajabu sana kuona mtu anabaki katika kiwango kilekile cha ufahamu wa kujiona ilihali umri wake unazidi kwenda na siku zinazidi kwenda mbele
Hivyo basi ili ubadili namna unavyojiona huna budi kufanya yafuatayo:

1. Badili Fikra Zako
Fikra zako zinaweza kukutoa hatua moja na kukupeleka hatua nyingine kwa sababu fikra ni vitu halisi ijapokuwa hazionekani.

Umekuwa hivyo ulivyo, umefika hapo ulipo na unajiona hivyo ulivyo kwa sababu ya fikra zako  mwenyewe!

Kwanini ubadili fikra zako? 
Unatakiwa ubadili fikra zako kwa sababu kile unachokiwaza na kukifikiri ndicho unachokiumba!
Hivyo basi endapo fikra zako zitakuwa ni duni sana, utajikuta ukijidumaza na kulemaa kabisa!

Na, ndiyo maana yule anayefikiria kuwa anaweza, na yule ambaye anafikiria kuwa hawezi wote wako sahihi, kwani kilicho na mashiko hapo ni kile walichokifikiri!

Hii inamaanisha kwamba, kati ya hao wawili mmoja atajiona anaweza, ilihali mwingine atajiona hawezi!
Kilichopelekea utofauti wao wa namna wanavyojiona ni fikra walizozitengeneza!

Kutokana na hilo huna budi kuwa makini na Fikra zako kwani kile unachokifikiri na kukiwaza ndicho unakiumba!

Mpenzi huhitaji kubadili kingine zaidi ya kubadili fikra zako. 
Badili fikra zako badili maisha yako!

2. Jitamkie Maneno Mazuri
Maneno unayojitamkia kila wakati yana nguvu kubwa sana katika kupima kila kinachotokea katika maisha yako! 

Na, unaweza ukapima kiwango cha kujiona cha mtu fulani kwa kuangalia kauli zake! 
Kwani kimtokacho mtu ndicho kilichomo nafsini mwake!
Na kilichomo nafsini mwake kinategemeana na vile yeye mwenyewe anavyojiona!

Na hii kwa sababu huwezi ukakitamka kitu ambacho hujakiona na wala hujakiamini.
Ubaya unakuja pale unapoona mtu anajitamkia tu kila maneno pasipo kujua nadhara ya maneno hayo dhidi yake!

Friend unatakiwa kujua kwamba, kile unachokitamka ni sawa na unakiumba! 
Na kama unakitamka kitu kibaya kwa ajili yako unajiadhibu mwenyewe kwani kitakutokea mwenyewe kama ulivyojitamkia!

Na ndiyo maana kupitia Neno mbingu na nchi zilifanyika!
Hivi unafikiri Wahenga waliosema: 'maneno huumba" walikuwa wapumbavu?
Hapana kuna cha kujifunza hapo...

Endapo ulikuwa ni mtu wa kujitamkia maneno hasi ninakusihi uyaache kwani, yatakuzuia ushindwe kuuona ule ukuu uliomo ndani ya nafsi yako!

Na, ndiyo maana Ayubu 22:28 Neno la Mungu linasema; “Nawe utakusudia neno nalo litathibitika” 

Hivyo basi huna budi kuwa makini na kile unachojinenea kwani ndicho kitakachokutokea!

3. Badili Matamanio Yako
Huwezi ukajiona katika viwango vya juu ilihali matamanio yako ni hafifu!
Unatakiwa kujua kwamba matamanio yako ndiyo yamekutengeneza na kufanya ujione hivyo unavyojiona!
Hata hivyo itapendeza endapo utajua kwamba hakuna kesho duni au yenye ukomo isipokuwa kuna matamanio yenye ukomo.

Na, ifahamike kwamba kile unachokitamani ndicho kitachochea kiwango chako cha bidii, juhudi, hamasa pamoja na mapambano yako.

Hii inaamanisha kwamba kile unachotamani ndicho kitapima utakachokimiliki maishani mwako.

Sasa basi endapo mataminio yako yatakuwa ni ya kawaida utaishia kujiona kikawaida sana pamoja na kumiliki vitu vya kawaida tu!

Unatakiwa kujua kwamba yule unayemtamani, ndiye unayekuwa! 
Kuna wakati mwingine unajikuta ukipiga hatua ndogo kimaisha siyo kwamba unatakiwa upige hatua ndogo ila ni kwa sababu ukomo wa matamanio yako umeishia hapo!
Badili matamanio yako badili maisha yako!

Ahsante sana kuwa mwanafamilia wa masomo haya!

Mwendelezo wa somo hili utaendelea kwa siku ya Kesho! 

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl, Mwandishi, Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika Endelea hapa 👇

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post