MREMBO KIPOFU
SEHEMU YA KWANZA
STORY NA: @MBOGO EDGAR
WHATSAAP 0717924403
Saa nane mchana, ndiyo mida ambao mkasa huu unaanza, mtaa ya bomba mbili darajani, kaskazini mwa mji wa songea uliopo mkoa wa Ruvuma, kwenye barabara kuu iendayo mikoa ya Njombe na iringa, yanaonekana magari nane ya polisi, yakiwa na askari wengi wenye silaha zao zakivita mikononi, huku ving’ola vikipiga kelele, na kufanya magari mengine yasiyo ya polisi, kukaa pembeni ya barabara, yakiyapisha magari hayo yapolisi, ambayo yalikuwa yametanda barabara nzima, raia walishangilia na kupiga mbinja (miluzi) kwa mwendo mkali na mikao ya kupendeza ya polisi hao, kwenye magaro haya ya wazi nyuma, ambayo sasa yalikuwa yana liacha daraja, na kupandisha mlima huu mkali, kuelekea mtaa huu mkubwa sana wa bomba mbili.
Lakini wakati huo huo ndani ya mtaa huo huo, kilomita mbili na nusu, toka darajani, kwenye mtaa mmoja wenye pilika nyingi sana za wanachi, mita chache toka stendi ya barabara kuu, tuna weza kuona uzio mmoja mkubwa sana, wa hotel moja kubwa sana na maarufu ya Kuchile Hotel, yenye hadhi ya juu sana, ambayo mida hii, ndani yake, palionekana kuwa tulivu sana, huku watu wachache wakiwa kwenye vimi zurungi, (midule) au unaweza kusema vibanda vidogo vidogo vilivyo jengwa kwa mtindo wa miamvuli, wakipata vyakula na vinywaji, mbali na wafanyakazi (wahudumu) wengi wao wakiwa ni aschana warembo wenye kati ya umri wa miaka kumi na nane mpaka ishilini na mbili, waliokuwa wanakatiza na huku na huku kuendelea kutoa huduma.
Eneo lilipambwa kwa uzuri wa viunga vilivyo zungukwa na mauwa mazuri nanyasi vupi, yani koka, na kutapakaliwa na harufu nzuri ya vyakula, ikiongozwa na nyama choma, ambayo sehemu zote uwa na kimbele mbele cha kutoa harufu kuwazidi wakina pilau, chips na wengine, huku ndugu ugari akibakia nyuma kabisa, upande wa kushoto wa eneo ilo, mita chache toka kwnye lango la kuinilia kwenye hoteli hii iliyo zungukwa na ukuta mrefu wa mfuti kumi na mbili, palionekana magari ya aina mbali mbali ya kifahari na yakawaida, yakiwa yameegeshwa, ikionekana kuwa wenye magari hayo, walikuwa hotelini hapo, wana pata vinywaji au chakula, na hakika ata watu waliokuwa wame ingia eneo ili wengi wao walikuwa ni watu wenye uwezo mkubwa wakiuchumi.
Lakini utulivu huo aukudumu kwamuda mrefu maana dakika saba baadae, vilianza kusikika ving’ola vya vya polisi, ikifwatia na ngurumbo za magari, ambayo sekunde chache yalisikika alilalamisha mairi kwa kusisima nje ya eneo ilo, huku magari matatu yakipitiliza ndani ya lango ilikubwa na kusimama mbele ya jengo kubwa la ghorofa mbili la hotel hii, huku tayari askari wakiwa wamesha ruka kwenye magari yao, na silaha zao aina ya SMG mikononi mwao, tayari kwa lolote, huku askari wengine toka nje wakiingia kwa fujo, na bunduki zao mkononi.
Yap mlango wa mbele wa gari moja kati ya yale matatu upande wa abilia, ukafunguliwa na akashuka askari mmoja polisi, kijana mwenye kati ya miaka ishilini mbili au ishilini na tatu, mwenye umbo la kimazoezi, mrefu wa wastani, alie jazia kifua, mwenye cheo cha nyota mbili mabegani mwake, yani inspector, licha ya kuwa mwenye sura ya kupendeza kama kijana wa kisasa mwenye kujijari, lakini alionekana kuwa katika sura ya kikazi kweli kweli, “kikundi cha kwanza na cha pili kizunguke nje fensi, kikundi cha tano na sita, kizunguke ndani ya fensi, kikundi cha tatu na sita kiziwie milango yote, na kukagua kila mteja anae ingia na kutoka, kikundi cha nne na cha nane kinifwate mimi” alisema yule insp na kuanza kuufwata mlango wa lile jengo la ghorofa mbili, huku watu waliokuwepo hotelini pale wakishangaa, pasipo kujuwa nini kinaendelea, huku wengi wao wakiingiwa nahofu kubwa, nah ii ni kutokana na mtukio ya mauwaji mfululizo yaliyopata kutokea siku za hivi karibu, ikisemekana kuna mwanamke mmoja, ndie alie fanya hayo mauwaji, ambayo yametikisa na kulizizimisha jiji la songea, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikigongana vichwa juu ya mauwaji hayo, ambayo mpaka sasa tayari kuna viongozi wa jeshi la polisi, polisi wenyewe, pamoja na watu mashuhuri wa hapa mkoani, walisha poteza maisha.
Wakati askari wa vinkundi vingine waki jipanga kama walivyo elekezwa, huku askari kumi wa kikundi cha nne na nane, waliongozana na insp huyu kijana, kuelekea ndani ya hoteli, huku wakipishwa na wahudumu na wateja, walio onekana kujawa na uoga mkubwa sana, “umakini wa hali ya juu unaitajika, hakikisheni leo hatumpotezi” alisisitiza insp ambae mikononi mwake alikuwa na silaha aina ya chines pisto, aliyoishika vyema kwa mikono yake miwili.
Huyu anaitwa Insp Elvis Eric, ambae kiukweli licha ya kuwa na uwezo kubwa sana wakupigana lakini kwa kutumia mikono mitupu, lakini mbele ya muuwaji huyu, waliekuwa wanamsaka, akuwa na ujasiri wa namna hiyo, sababu anaijuwa kazi yake vyema kabisa, maana alisha wai kukutana nae mala kadhaa, na malazote, aliambulia kipigo, kisha muuwaji kuondoka zake.
Naam kikundi kilipandisha ngazi, huku insp Elvis akiongoza, mpaka walipo ifikia ngazi ya mwisho, ili waingie kolidoni, hapo insp akajibanza kwenye kiambaza cha ngazi ya mwisho na kusimama, kisha akaonyesha ishala kwa kuinua mkono wa kushoto, juu na kunyoosha vidole viwili, kisha akavielekezea mbele, hapo kwatahadhari wakachomoka askari wawili, na kumpita yeye, wakachungulia kwenye kolido, kisha waka jitokeza, ikionyesha akukuwa na hatari yoyote, hapo insp akaonyesha tena vidole viwili, wakapita wawili, na yeye akafuatia, huku wakionyesha ishala kwa wale sita walio bakia.
Yap! kwenye kolido akukuwa na dalili ya muuwaji zaidi ya wahudumu wawili wakike, waliokuwa wanaendelea nashuguli zao, mmoja akiwa amebeba shuka na tauro anapeleka kwenye moja ya vyumba, kati ya vingi vilivyomo mle ndani, huku mwingine, alikuwa anaburuza lile dude la kuwekea nguo chafu, lililo onekana lime jawa na nguo chafu, akielekea kwenye ngazi, insp Elvis alimtazama kwa umakini mkubwa sana mschana huyu mwenye kubuluza toroli la nguo chafu, sababu alionekana tofauti na wale aliopishana nao, ukiachilia wasi wasi ambao ata wenzake walikuwa nao, yeye alikuwa anatoka jacho maeneo ya mashavuni na kwenye paji la uso, alafu alikuwa anajitaidi kukwepesha macho yake yasikutane na macho insp, lakini akaachana nae, sababu umbo la mschana huyu, lilikuwa tofauti na umbo la muuwaji, maana insp Elvis, alikuwa analifahamu umbo la muuwaji kutokana na kukutana nae mala kwa mala, muuwaji alikuwa ni mrefu wa wastani, ambae yeye alikuwa anapenda sana kumfananisha na rafiki yake Thensia, mschana ambae anaishi nae nyumba kwenye nyumba za polisi, (polisi quarters) au line polisi, kama wengine wanavyopenda kuita, ata maumbo yao yalikuwa yanaenda kidogo, makalio ya wastan, hips za watan, kifua kilicho kaa vyema, maana kifua cha Thensia mala nyingi, amekuwa anakimezea mate, nakutamani kuwa, japo siku moja ange pata nafasi ya kukigusa na kucnezea chuchu za mschana yule ambae siyo ndugu yake wala mpenzi, wake, ila tu aliamua kumsaidia baada ya kuona kuwa anatatizo la kuto kuweza kuona, (kipofu)
Insp Elvis aliachana na dada yule na kuendelea na safari yakukifwata chumba ambacho waliambiwa kuna tukio linataka kutokea, nasasa walikuwa wanatembea kwa tahadhari kubwa sana, “leo lazima nikupate we mshenzi” aliwaza insp huku wakizidi kukisogelea chumba na alobaini, huku akiwa na hamu ya kumkamata mschana huyu muuwaji, ambae alitamani sana kuiona sura yake, kutokana na siri ambayo alikuwa nayo kichwani mwake, siri ambayo akuwai kumweleza mtu yoyote, “inabidi uwe makini sana, ujuwe ata kuku akijuwa anawindwa anakuwa mkali” Evis alikumbuka maneno ya rafiki yake Thensia, ambae toka alipo mkaribisha nyumbani kwake, akutamani tena aondoke, maana ukiachilia ukipofu wake, lakini alikuwa mrembo, na mcheshi.
Hapo insp akaonyesha ishara ya kuwa askari wasimame, nao wakasimama, kisha akaonyesha ishra kwa wale askari wawili wambele wasogelee mlango wa chumba namba alobaini, kisha wafungue na kuingia ndani, na ikawa hivyo askari wanne waliotangulia, wakausogelea mlango na kufungua kwa nguvu, japo ulifunguka kilahisi ukionyesha kuwa aukuwa umefungwa na funguo wala komeo.
Hapo kika pita kimya kifupi, kwa sekunde kama ishilini hivi, alafu akachomoza askari mmoja, afande tayari ASP Kachinga ame uwawa, na muuwaji ayupo” alisema yule askari, taharifa ambayo ilimshangaza kila mmoja, kuwa ASP Kachinga anausikaje katika mkasa ule, japo kwa insp Elvis aikuwa ajabu, sababu alisha juwa kuwa ASP Kachinga ni mmoja kati ya watu wakao uwawa,
Hapo insp Elvis akakimbilia mle ndani, akiongozana na wale askari wake sita waliobakia, na alicho kikuta kule ndani, ndiyo kilicho muacha mdomo wazi, japo aikuwa mala ya kwanza kukuta vile, katikati mfululizo wa mauwaji ya mschana huyu, ambae yeye alimwita mrembo karatasi, kutokana wepesi wake, ila ilimhuzunisha sana, maana alikuta mwili wa afande wake ASP Alois Kachinga, ukiwa umelala sakafuni, kwenye bwawa la damu, zilizo kuwa zinatokea shigoni mwake, kwenye jeleha kubwa, ambalo lilionyesha wazi kuwa ni kisu ndicho kilicho pita sehemu hiyo, tena ni muda mfupi sana uliopita, maana damu bado zilikuwa zina ruka.
Naam kutokana na uzowefu wake juu ya muuwaji huyu, insp akatazama ukutani, na kuona maandishi yaliyo andikwa ANASTAILI KIFO, ikionyesha muuwaji aliandika kwa kidole alicho chovya kwenye damu, tena damu mbichi kabisa, kwa kifupi kila kitu kilionyesha kuwa mauwaji yana muda mfupi sana toka yametokea, hivyo muuwaji wamepishana nae muda mfupi uliopita, hapo insp akakumbuka mwonekano wa yule mhudumu alie kuwa anaburuza lile toroli la nguo chafu, “pumbavu, wanje haraka” alisema insp huku anakimbia kutoka nje ya chumba, akifwatiwa na askari wake, “namba nane wabakie hapa kwenye kolido, hakikisha atoki mtu vyumbani, nammba nne nifwateni, tumuwai yule mschana mwenye toroli, la nguo chafu” alisema insp huku anakimbilia kwenye ngazi, na wale askari wakajigawa haraka, na wengine wakamfwata insp, ambae kiukweli alikabidhiwa jukumu ili la kuhakikisha anamkamata mschana huyu hatari, miezi kadhaa iliyopita, akiaminiwa kuwa yeye ndie mwenye uwezo wakufanya hivyo, kutokana na juhudi zake kwenye kazi.
Naam ile wanafika kwenye ngazi ndio kwanza waliona toroli likiwa lime achwa katikati ya ngazi, huku mschana yule alie kuwana liburuza akiwa amelala chini ana galagala akionyesha amefungwa kamba mikononi na miguuni, na mdomoni, “shenzi, wai nje mkamzuwie mshenzi huyo” alipiga kelele insp, ambae katika moyo wake alikuwa anatamani kumjuwa mschana ambae licha kuwai kuingia kwenye mikono ya muuwaji huyo na kuachiwa uhai wake, lakini pia mschana huyo muuwaji alisha wai kuyaokoa maisha yake mala kdhaa, kitu mbacho nisiri yake peke yake, na ajawai kumweleza mtu yoyote, wala kuandika katika report yake ya uchunguzi.
Askari wawili walikimbilia nje ya jengo lile la hotel, na kuwakuta wenzao wanaendelea kuwa kagua raia na wahudumu, kisha kuwa toa nje, ili ikitokea majibazo ya risasi, kama ilivyo wai kutokea siku za nyuma, wasidhurike, wakiwaacha insp na askari watatu, wanamfungulia yule mhudumu, huku wanapkuwa lile toroli, ambalo sasa likuwa lime pwaya, “ameondoka, amechukuwa sale chafu zilizokuwepo humu” alisema yule mhudumu, huku anaonyesha, kwenye lile toroli, ni baada yakuwa amesha funguliwa, “afande kuna kisu kilicho lowa damu” alisema askari alie kuwa anakagua toroli, hapo insp akuwa amesikiliza, juu ya kisu kilicho lowa damu, mana alisha toka mbio kuelekea nje, alipofika pale akadakwa na wale askari wawli waliotangulia, “afande mpaka sasa akuna dalili ya mschana yule mwenye nguo nyeusi” alisema mmoja wa askari kai ya wale waliotangulia, kwenda kumzuwia, hapo insp akatazama gate, akaliona likiwa wazi, kama walivyo likuta huku watu waliokaguliwa wakiondoka zao, hivyo akatoka nje haraka, na kutazama pande zote mbili kushoto nakulia, yani barabara za mtaa, ambao kwa nje ya hotel kiukweli ilikuwa imechangamka vibaya sana, na sasa uliongezeka watu waliokuwa wanashangaa ujio wa magari ya polisi, wengi wakiwa wamekaa vikundi vikundi, wakijadiri ili nalile, ata wale waliotoka mle ndani pia walionekana wakijadiri ili na lile, huku baadhi ya polisi wa kundi la kwanza wakiwa sogeza watu nyuma ili wasijae pale kwenye eneo la mlango, yani getini.
Naam wakati insp anataka kukata tamaa, ya kumwona muuwaji wake, sijuwi kilimtuma kitu gani, maana wakati anageuka, akatazama upande wa kusini wa eneo lile, na hapo basi umbali wa mita kama mia mbili au zaidi, akamwona mschana mmoja alie valia sale za wa hudumu wa ile hoteli Kuchile, yani suluali nyeusi na shati jeupe, mrefu mwenye umbo zuri la kutamanisha mwaume lijari, yani lililo kamilika kila idara, ambae akudumu sana kwenye ile barabara ya vumbi, aka kata kona upande wakushoto, na kuzama kwenye chochoro za mtaa, ambao nyumba zilikuwa zime banana kweli kweli, japo kilikuwa vijinjia vya kupita watu, “kikundi cha tatu na sita na nne kinifwate haraka” alipiga kelele insp huku anaanza kutoka mbio kuelekea upande ule ambao alimwona yule mschana ambae kiukweli alikuwa na mwonekana kama wa muuwaji ambae ata akitoka usingizini asinge weza kupoteza taswila ya mwonekano wake.
Hapo baadhi ya polisi waliingia haraka kwenye gari, na kumfwata kamanda wao, huku wengine wakija kwamigumuu kumkimbilia kamanda wao, ambaealikuwa mita kama mia mbili mbele yao, ambapo walimwona akihepuka na kuingia kwenye chochoro za nyumba za upande wakushoto akiwa mbio mbio na bastora yake mkononi, na wao wakaongeza mwendo ili kumuwai.
Yap insp Elvis toka kitengo cha upelelezi mkoa wa Ruvuma aliona bola aingie kwenye chochoro hiyo ili amuwa muuwaji kwenye mtaa wapili, yani kule alikoelekea, huku wale waliokuwa kwenye magari, wakizunguka upande wapili, ambako kwa vyovyote muuwaji asingeweza kutokea, akiofia kugeuzwa chekecheo kwa kumiminiwa risasi, na askari hao.
Naam kwa uharaka wa hajabu, insp Elvis Eric alitokea kwenye chochoro ya katikati iliyo nyooka, chochoro ilitengenezwa kwa nyumba zilizo peana migongo, akitegemea kumwona muwaji akikatiza au kuambaa ambaa na chochoro hiyo, lakini cha kushangaza akumwona muuwaji wala dalili ya muuwaji, hivyo akazidi kukimbia kusonga mbele, kufwata usawa ambao muuwaji yule wakike aliingilia, huku bastora yake ikiwa mkononi, maana tayari magari ya pilisi yalisha anza kusikika upande wapili, wa mtaa, hivyo aliamini kuwa muuwaji awezi kuelekea upande ule, wakati mtaa waliotoka tayari kulikuwa na askari wengine waliokuwa wana tembea kwa miguu, hivyo muuwaji asinge weza kurudi alikotokea.
Lakini basi insp baada yakutembea kwa hatua kama mia moja mbele, mala ghafla akashtuka kuliona shati jeupe, likiwa chini, akainama na kuliokota lile shati kwa mkono wa kulia huku bastora yake aina chines pisto, akiwa ameishika kwa mkono wa wakushoto, akalitazama vizuri lile shati, “pumbavu amesha badirika” alisema insp, huku anatupa lile shati chini, lilikuwa ni shati ambalo linatumika kama sale za wahudumu wa Kuchile Hotel.
Insp Elvis akatazama mbele, kama ange mwona mschana yule muuwaji, mrembo karatasi, akama alivyo penda kumwita, kutokana wepesi wake, lakini akukuwa na dalili ya uwepo wa mschana huyo, “ukimwona nyoka amejikunja usizanie anakuogopa, ujuwe anajiandaa kukurukia” maneno hayo yali mjia kichwani insp Elvis Eric, wakati ana tazama kule alikotokea ambako nako akukuwa na dalili ya muuwaji, maneno ayo ambayo aliwai kuambiwa na rafiki yake Thensia, ambae yeye upenda kumwita mrembo kipofu, kutokana na tatizo lake la macho, nidyo yaliyo mkubusha kuwa akutakiwa kuzubaa eneo lile.
Hapo insp aka kumbuka kuwa alikuwa ameshika bastora kwa mkono mmoja, akageuka haraka na kutazama huku anashika tena bastora yake kwa mikono miwili, hamad mbele yake tayari kulikuwa na mtu, ambae muda huo alikuwa anarusha teke kuipiga ile bastora, mkono mwa insp, kwa wepesi wa ajabu, insp akakwepesha mikono yake na yumbia pembeni, “tulia hivyo hivyo, la sivyo utafikishwa kituoni ukiwa marehemu” alisema insp kwa sauti kali ya kikakamavu, hapo akamwona mtu yule ambae ni mschana alie jiziba kitambaa cheusi, kwenye uso wake, usawa wa pua mdomo na kidevu, na kichwani mwake kukiwa na nywele bandia (wigi) akionekana wazi anatabasamu, sababu macho yake yali onyesha hivyo, “leo umekuwa mjanja kidogo” kwa mala ya kwanza insp Elvis alihisikia saui harisi ya mschana huyu, na kumstua vibaya sana, sababu sauti hii akuwa ngeni masikioni mwake, akatoa macho kwa mshangao, na kutazama mschana huyu, ambae alikuwa ametulia kama vile akukuwa na hatari yoyote mbele yake, “mungu wangu, hii ni ndoto ya aina gani?” alisema insp kwa sauti iliyo jaa mshangao, maana alihisi kumfahamu muwaji huyu, alie msaka kwa muda mrefu, “najuwa auta amini, ila ni mimi” alisema yule mschana, huku akimtazama insp Elvis, wakati huo ving’ora vya magario vikiendelea kulindima upande wapili wa mtaa.
Ukweli insp Elvis nikama alishikwa na gazi, akajikuta anamsogelea yule mschana anae mwita mrembo karatasi, na kupeleka mkono wake kwenye kile kitambaa cha usoni, lakini ile anakishika ili akivute, kwa wepesi wa ajabu, wa mrembo karatasi, akashtuka akipolwa batora na kuwekewa kwenye paji la uso, lakini insp akuonekana kuacha mpango wake, nazani alikumbuka kuwa alisha wai kuingia mala kadhaa kwenye mikono ya mschana huyu, na kutoka salama, akiachiwa kwa makusudi kabisa, na wakati mwingine alimwokoa kwenye hatari ya kifo, hivyo leo asinge weza kumuuwa.
Hapo insp Elvis Eric, akakamata kile kimask cheusi, mfano wa vile vimaski vya watu wa saloon, na kukishusha kwa chini, Naam hapo insp alijikuta anatamani kuzimia, kwa kile alicho kiona, “Thensia?” aliuliza insp kwa mshangao, akuamini kama yule mschana ambae alikuwa anaishi nae kwa miezi kadhaa, akimshulia kama kipofu, huku akimsaidia kwa mambo mengi ambayo kutokana na ukipofu asingeweza kuyafanya mwenyewe, wakati mwingine alikuwa akijiiba kumchungulia, kwa tamaa za kuuona mwili wa mschana huyu mrembo kipofu, ata wakati mwingine insp Elvis alikuwa ana badiri nguo mbele ya mschana huyu, na kubakia uchikabisa akiamini kuwa ni kipofu, alisha msimulia baadhi ya mipango yake ya kazi, ya kumsaka muuwaji mrembo karatasi, “kumbe siyo kipofu, na wewe ndiyo muuwaji” alisema insp kwa sauti ya chini iliyo tawaliwa na mshangao mkubwa sambamba na kuajicheka kidogo, huku akimtazama Thensia, ambae alikuwa anatabasamu, “wengine zungukeni kwa mbele” ilisikika sauti ya mmoja wa askari, akitoa amri kwa wenzake……….naam huo ndio mwanzo wa simulizi hii mpya ya Mrembo kipofu, ukiachilia hapa walipo itakuwa, je unazani ni nini kilitokea mpaka mschana Thensia akaamua kuya fanya haya yote, je ata fanikiwa kutoka hapa alipo, basi endelea kufwatailia mkasa huu hapa hapa kwa @Hadithi ZA MBOGO EDGAR au jinunge kwenye group la @HADITHI ZA MBOGO EDGAR, ilikuipata kila siku simulizi hii na nyingine.
MREMBO KIPOFU
SEHEMU YA PILI
STORY NA: @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: huku akimsaidia kwa mambo mengi ambayo kutokana na ukipofu asingeweza kuyafanya mwenyewe, wakati mwingine alikuwa akijiiba kumchungulia, kwa tamaa za kuuona mwili wa mschana huyu mrembo kipofu, ata wakati mwingine insp Elvis alikuwa ana badiri nguo mbele ya mschana huyu, na kubakia uchikabisa akiamini kuwa ni kipofu, alisha msimulia baadhi ya mipango yake ya kazi, ya kumsaka muuwaji mrembo karatasi, “kumbe siyo kipofu, na wewe ndiyo muuwaji” alisema insp kwa sauti ya chini iliyo tawaliwa na mshangao mkubwa sambamba na kuajicheka kidogo, huku akimtazama Thensia, ambae alikuwa anatabasamu, “wengine zungukeni kwa mbele” ilisikika sauti ya mmoja wa askari, akitoa amri kwa wenzake……….ENDELEA………
Hapo insp Elvis akamtazama Thensia, kama vile ana jiuliza kitu, akakumbuka jinsi, alivyo mfundisha kupika, na kutumia jiko la umeme, akimwelekeza sehemu vitu na jiko ilo lilipo, na mschana huyu kuelewa mapema, “kumbe siyo kipofu” aliwaza Elvis, hukuanacheka, na kushusha pumzi ndefu, wakati huo vishindo vya askari vikizidi kusogea upande wao vikitokea barabara ya mbele ya mtaa, “najuwa unaweza kuondoka bila kukamatwa” alisema insp Elvis, kwa sauti ya chini.******
Upande wa pili tayari polisi, wenye silaha zao walikuwa wamesha zunguka eneo lile, ambalo walimwona insp Elvis akiingia, huku kundi lililo ongozwa na sajent Baraka Magesa, lililokuwa limesha ingia kwenye chochoro za mitaa mle ule, ambao walimwona afande wao akiingia, lilizidi kusogea ndani wakiwa wamegawana vikundi vidogo vidogo, na kusambaa kwenye chochoro kadhaa, “kumbuka shati jeupe na suruali nyeusi nywele ndefu, kitambaa cheusi usoni” ilisikika sauti ya insp Elvis mbele yao, hapo askari wote wakajuwa kuwa afande wao alikuwa karibu na naeneo ilo, hivyo waka zidi kusogelea kwenye chochoro ya kati, “angalia raia wanao katiza wasidhurike” alisema insp Elvis wakati wale askari wanatokea, huku wanapishana na mschana mmoja mwenye nywele fupi, japo alikuwa mrefu mwenye umbo zuri la kike, lakini alikuwa amevalia suruali nyeusi na tishet jeusi, mwenye uso wa kuogopa, nazani nikawaida kwa raia asa wakike, kuogopa polisi, tena wenye silaha “ondoka huku haraka kuna hatari huku” alisema sajent Baraka, huku ana msindikiza yule mschana kumtoa eneo lile, huku askari wengine wakimfwata insp Elvis, alie kuwa anazidi kusonga mbele, na bastora yake mkononi.
Naam dakika kumi baadae tayari walisha saka eneo lote bila mafanikio, wala dalili ya kumwona muuwaji, insp Elvis aka toa taalifa makao makuu ya polisi mkoa wa Ruvuma, juu ya kifo cha RCO, Alois Kachinga, kisha wakauchukuwa mwili wa ASP Alois kachinga, na kuupeleka hospital.
Saa kumi na mbili za jioni, insp Elvis ambae alikuwa amechanganyikiwa nakujawa na mawazo mengi sana, juu ya kile alicho kiona leo, akiwa na wasi wasi na maswali mengi kichwani mwake, juu ya kile alicho kiona leo, alienda moja kwamoja mpaka nyumbani kwake kwenye makazi ya polisi, ambako moja kwa moja alifikia nje na kukaa kwenye ngazi, kama vile ana jiwazia kuyingia ndani, “unafanya nini?” alikumbuka ili swali insp Elvis Eric, lilotoka kwa mschana Thensia, ukweli Elvis alijikuta anacheka, sababu siku aliyo ulizwa swali hilo, alikuwa amesimama uchi wa mnyama mbele ya kioo, chumbani kwake, anabadiri nguo, wakati huo Thensia alikuwa mle mle chumbani, “nabadiri nguo, yani unge niona hapa nazani unge pofuka macho kwa mala ya pili” ilo ndilo jibu alilo litoa Elvis, “khaaa! kumbe alikuwa ananinona mshenzi huyu” aliwaza Elvis huku anacheka, kisha akaanza kufungua kamba za buti zake za kijeshi, mala akasikia mlango wa nyumba ile unafunguliwa, “kumbe umesha rudi” ilisikika sauti ya Thensia toka nyuma ya Elvis, ambae aligeuka na kumtazama rafiki yake huyu, ambae ungepata nafasi ya kumwona mida hii, usinge amini kama ndie yule ambae masaa machache yaliyopita ametoka kufanya mauwaji, alikuwa amejitanda kanga vizuri, amevalia miwani meusi, mkononi alikuwa ana fimbo moja ndefu, na pana kiasi cha sentmeta nne, siyo mkongojo, ilikuwa ime nyooka kama fimbo ya kawaida, ambayo ukiitazama kwa haraka ungejuwa ni kipande cha mti kilicho chukuliwa bila kuwekewa urembo wowote, “hooo! mrembo wangu kipofu, nimekuja sasa hivi” alijibu Elvis, kisha akaendelea kuvua viatu vyake, “pole na kazi kamanda kijana” ndivyo alivyo penda kumuita Elvis, ambae alicheka kidogo, “vipi, umepika chochote?” niswali ambalo, kikawaida ni vingumu sana, kumwuliza kipofu, lakini kwao ilikuwa kawaida, kwa mrembo kipofu kuandaaa chakula, au kushilikiana kuandaa chakula wote wawili, midaa hii wote walicheka, ni mala bada ya Elvis kuuliza swali ilo, “kwanini nisipike polisi kijana, wakati umenifundisha wewe mwenyewe” alisema Thensia, huku wakiendelea kucheka.
Elvis alimaliza kuvua viatu kisha wakaingia ndani, na Elvis akakuta chakula mezani, chakula hiki ilibidi Elvis akile mchana, lakini Elvis akuwa amekuja nyumbani mchana huo, kutokana na majukumu aliyo kuwa nayo, Elvis alikaa mezani na kutaka kuanza kula, lakini ukweli chakula singe pita shngoni, maana kila alichokuwa anakifanya mbele ya Thensia, nikama alikuwa anajilazimisha, ukweli ukiachilia wasi wasi, aliokuwa nao, pia alikuwa anamaswali mengi sana kichwani mwake, “Elvis najuwa kuna vitu vinakusumbua kichwani, mimi naomba uondoe wasi wasi, kifupi nimesha maliza kazi yangu, nilikuwa na kusubiri nikuage, maana naitaji kuondoka na kuanza maisha mapya, cha msingi nashukuru sana kwa msaadawako, na mambo yote uliyo nifanyia na uliyopanga kunifanyia, hakika umekuwa rafiki mwema kwangu” alisema Thensia, lakini Elvis akashtuka kidogo, kisha aka tazama chini kwa udhuni, kabla aja ingiza mkono kwenye maji ya kunawa, muda wote Thensia alikuwa anamtazama, na alisha gundua kuwa rfiki yake na mwenyeji wake huyu, amenyongea ghafla, “Thensia, kabla ujaondoka nina mambo mawili nayataka kutoka kwako” alisema Elvis huku akimtazama Thensia kwa umakini, “nakusikiliza Elvis” alisema Thensia na hapo Elivs akatulia kidogo, kama vile anawaza aanze na lipi, “lakwanza, nazani huu ni wakati mzuri wa wewe kunieleza uliyafanya haya kwa maana hipi, na sababu ilikuwa nini japo mengine nina fahamu, lakini kuna watu sijajuwa sababu, ya vifo vyao” alisema Elvis na hapo Thensia akatabasamu kidogo, hakuna tatizo, nitakuelezea japo kwa sasa ainamaana tena sababu yamesha pita” alisema Thensia, na kutulia kidogo, huku akiwa amevalia miwani yake kubwa nyeusi, na fimbo mkononi, amekaa kwa utulivu kabisa kwenye kochi lililotazamana na lile la Elvis, kama vile kipofu kweli kweli, “Elvis chakwanza unatakiwa uamini kuwa, mimi niliwauwa maadui zangu na watu waliojaribu kukuuwa wewe na mimi mwenyewe, hivyo nili kuwa na kulinda kwa muda mrefu, na pia walio kufa wali stahili kifo, kutokana na uovu wwalio ifanyia familia yangu” alisema Thensia na kutulia kidogo.********
Turudi nyuma mpaka mwaka 1995, kilipo anzia kisa chetu, ulikuwa ni mwezi wa kumi, siku ya Ijumaa, ilikuwa siku tulivu sana, mwishoni mwa mwezi huo wa kumi, majira ya saa moja kasoro za jioni, kusini magharibi mwa mji wa songea, kilomita kama sita hivi toka stendi kuu ya kipindi hicho, pembezoni mwa kijiji cha Ruvuma, ambacho kipo sehemu ambayo mji na mkoa wa Ruvuma ulianzia hapo, kabla wageni awaja jenga nyumba za kisasa, sehemu ambayo sasa ndio kuna mji wenyewe, ndani ya majengo ya shule ya shule ya sekondali, mchanganyiko, iliyopo pembezoni mwa kijiji hicho, walionekana wanafunzi wawili wakike na wakiume, wakitoka pale shule shuleni wakiongozana na wenzao, sambamba na wenzao, wakiwa wanavalia uniform zao mashati meupe, na skert na suruali nyeusi.
Tofauti na wanafunzi wenzao waliokuwanao mida hii, wakitoka kujisomea, kwaajili ya kujiandaa na mitihani ya mwisho ya kuitimu kidato cha nne, wao walionekana, kutembea taratibu, wakiwa wawili, kama kumbi kumbi, pia wawili awa walionekana wenye sura za kinyonge sana, ni wazi kuna jambo lilikuwa lina wasumbua, zaidi ya ilo, pia wanafunzi awa wakike na wakiume, licha ya kuonekana ni wapenzi, lakini walionekana kuwa na utofauti mkubwa wa hali za maisha yao, yani wakati yule wakike akionekana kuvalia uniform maridadi, ungezania za mwanafunzi mpya wakidato cha kwanza, kwa upya wake, huku yule wakiume, akionekana kuvaa uniform chakavu ungesema ni mlinzi wa shule.
Giza lilikuwa ndio linaanza kutanda, maana tayari jua lilisha fichwa na mawingu ya magharibi, juu walionekana kunguru wengi wakivamia miti, na kujishikiza kwenye viota vyao, walivyo vijenga kwenye matawi ya miti mikubwa ya misuku na miembe, “mimi naona tuitoe hii mimba” alisema yule mwanafunzi wa kike, kwa sauti flani ya upole na yakukata tamaa, huku akitembea taratibu kuelekea upande wakijiji, wakiwa nyuma kabisa ya wenzao, ambao walisha waacha kwa umbali wa mita kama mia moja au mia na hamsini, wote wakiwa wamekumbatia daftari mikononi mwao, “lakini Neema, una wasi wasi gani, wakati week ijayo tunaanza mitihani?, ni bola uiache tu! kutoa mimba ni hatari sana” alisisitiza yule mwanafunzi wa kiume, huku akishika daftari kwa mkono wa kulia, na kumkono wa kushoto akamshika mwenzie wakike, ambae pia aliamishia daftari kwenye mkono wa kushoto, na kuudaka mkono wa mwenzie “mitihani siyo tatizo Khamis, tatizo mjomba akijuwa, anaweza ata kuni uwa, au kukupeleka polisi” alisema Neema kwa sauti ya upole, iliyojaa unyonge wa hali ya juu, “haaaaa! Neema, mbona mjomba wako anaonekana nimpole sana, tatizo uwezi kujuwa madhara yatakayo tokea wakati wa kutoa, nimesha sikia watu wanakufaga” alisema Khamis, ambae kiukweli ukiachilia, uduni wa maisha yake na familia yake, lakini pale shule alikuwa anasifa ya nidhamu, na heshima kwa kila mtu, japo darasani akuwa vizuri sana, na tabia zake njema ndizo zilizo mfanya Neema avutiwe nae, na kumkubalia kiulahisi pindi alipo mtongoza, na kilicho wa pelekea kuwa na ukaribu wa mnzo ni ujirani wao huko mtaani, “Khamis ili linaweza kuwa tatizo kwako, pindi mjomba atakaposikia kuwa mimi ni mjamzito, na mimba ni yako, utasahau kuwa ni mpole, na alikuwa anakuchukulia kama mtu wakaribu wa familia, kwa kitu atakacho kufanyia” alisema yule mschana, ambae kwa mwonekano ni mschana mrembo kweli kweli, maana ata kwa wale wenzie waliotangulia mbele yao, akuna alie msogelea kwa uzuri, wa sura na umbo, “Neema nipo tayari kwa lolote, bola ni ghalimike kwa mateso yoyote, kuliko wewe kuhatarisha maisha yako kwa kutoa ujauzito huo?” alisema Khamis kwa sauti ya upole iliyo maanisha, huku wakiwa bado wameshikana mikono, wanatembea taratibu, kuelekea upande wa kijiji cha Ruvuma, kilicho pakana na mtaa wa majengo, kwa kutenganishwa na mto unao julikana kama Ruvuma mdogo, mto unao mwaga maji yake kwenye mto Ruvuma, “lakini Khamis, kumbuka kuwa atujajiandaa kuishi pamoja, atuna fedha za kumtunza mtoto, unazani tutaishije kama nitafukuzwa nyumbani?” aliuliza Neema, ambae alikuwa na haki ya kusema hivyo sababu, ukiachilia yeye kulelewa na mjomba wake, ambae katika ukoo wao, ndie mtu mwenye uwezo, wa kifedha, anae tegemea kazi yake, ya udereva wa magari makubwa ya mizigo, akukuwa na mtu mwingine mwenye uwezo wa kujipatia angalau fedha ya kueleweka, mama yake alizalia nyumbani, na sasa yupo kijijini Mpingi, kilomita nyingi sana toka Songea mjini, ambako ndiko chimbuko la ukoo wao, na wote walikuwa wanaishi kwa kumtegemea mjomba, na sema Neema alikuwa na haki ya kusema hivyo, sababu Khamis nae licha ya kuwa alikuwa anaishi na mama yake na baba yake, jirani na kwakina Neema kule matogoro, lakini wazazi wake walikuwa na hali duni ya kimaisha, waliishi kwa kutemegea kilimo, cha kawaida cha jembe la mkono, na biashara ya mifagio, ambayo baba yake Khamis alikuwa ana ifanya kila siku za jumapili, na wateja wake wakubwa wakiwa ni wahumini wa kanisa la kikatoriki, la mt Telasia wa mtoto yesu, lilipo huko huko Matogoro, biashara iliyo mpatia jina la utani baba yake Khamis, ambae alikuwa anajulikana kwa jina la Komba Mafagio, ata Khamis pia alikuwa ana tambuliwa kama, mtoto wa Komba Mafagio, kwa biashara hii mzee Komba akuweza kumpatia fedha za ziada kijana wake, ambae kwa miaka hiyo ya 1999, alikuwa na miaka kumi na Tisa, akipishana mwaka mmoja na Neema alie kuwa na miaka kumi na nane, ambae ndie alikuwa kama mkombozi wake, kwa mambo madogo madogo, kama vile fedha ya nauri, na ile ya kutumia mida ya mapumziko, yani saa nne na chakula cha mchana, “ilo siyo tatizo Neema, siyo kwamba nitakuwa masikini kila siku, ipo siku nita pata fedha ya kuweza kukulea wewe na mtoto” alisema Khamis, kwa sauti ya upole iliyo kuwa na sifa zote za kubembeleza, na kutafadharisha, hapo kikapita kimya kidogo, huku wote wakionekana kutafakari jambo, macho yao yakitazama kule walikokuwa wanaelekea, ambako awakuweza kuona mbali, maana tayari giza lilisha anza kutanda.
Neema akauachia mkono wa Khamis na kuulaza mkono wake begani kwa Khamis, huku akijipachika kwenye ubavu wa Kijana huyu alie mpenza kweli kweli, ambae akuwa tayari kumsaliti kwa ghalama yoyote, maana alisha shawishiwa na vijana wengi sana, wa mtaani na wafunzi wenzake, wengi wao wakiwa ni wenye fedha nyingi sana, yani watu wenye matajiri kwa watoto wa matajiri, lakini Neema akuwa tayari kugawa kitumbua chake kwa mtu mwingine zaidi ya mpenzi wake Khamis, “basi Khamis tuamue kuwa kitu kimoja, tukisha maliza mitihani, niage kwa mjomba na enda kijijini, alafu tuenda kuishi mpingi” alisema Neema, kwa sauti ya kudeka, huku amitazama Khamis, wote wawili wakiwa wamejawa tabasamu kwenye nyuso zao, awakujuwa kitu kinachoenda kutokea muda mfupi ujao, “yani hapo Neema ume nielekwa vizuri sana, tukirudi huko, tutakuwa tumesha fanikiwa kimaisha, yani akuna kuzubaa, ni kuchakalika mpaka tuwe matajiri” alisema Khamis huku wana chepuka upande wakulia, kuifwata njia moja nymbamba inayoelekea mtoni, ikiwa ndiyo njia mbayo utumika kama njia ya mkato, kwenda kutokea majengo, ambako wangepata daladala za kwenda matogoro.
Wawili awa walitembea taratibu, kwenye chochoro hiyo liyo anza kumezwa na matete mengi yaliyo stawishwa na unyevu unyevu wa mto wa Ruvuma, huku waki peana matumaini ya kitoto, kwa ndoto, za mchana, za kuwa wataenda kufanikiwa huko kijijini, kupitia kilimo, na mifungo.
Naam wakiwa wenye furaha na matumaini mapya, walifika mtoni, na kuvuka mto, sasa walikuwa wametengana na makazi ya watu, zaidi walikuwa wana sikia sauti za vyura wa mtoni, na maji yaliyosikika kwa mvumo wake, akuna alie ogopa giza na ukimya wa vile vichaka, walitembea taratibu kuelekea majengo, wakifuata kijinjia kile, Khamis akitangulia na Neema akifwatia nyuma.
Mala ghafla Khamis akasimama, huku akivuta harufu, kama vile kuna harufu flani aliisikia, ambayo aikuwa ya kawaida, “vipi unasikia harufu ya nini?” aliuliza Neema ambae pia alikuwa amesimama nyuma ya Khamanis, lakini kwa ukaribu mkubwa sana, “we usikii harufu ya bang….” kabla Khamis ajamaza kuongea mala waka shangaa kuona kuna watu wana ibuka toka kwenye vichaka, idadi yao kwa haraka ilikuwa ni vigumu kuitambua, lakini baadhi yao walikuwa wameshika sigara yenye harufu kali sana………….. Naam Thensia anasimulia kisa cha yeye kuamua kufanya mauwaji, je nini kilitokea hapo?. Tukutane kwenye sehemu ya tatu ya mkasa huu wa MREMBO KIPOFU, hapa hapa kwa HADITHI ZA MBOGO EDGAR.
03
MREMBO KIPOFU
SEHEMU YA TATU
STORY NA: @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Mala ghafla Khamis akasimama, huku akivuta harufu, kama vile kuna harufu flani aliisikia, ambayo aikuwa ya kawaida, “vipi unasikia harufu ya nini?” aliuliza Neema ambae pia alikuwa amesimama nyuma ya Khamanis, lakini kwa ukaribu mkubwa sana, “we usikii harufu ya bang….” kabla Khamis ajamaza kuongea mala waka shangaa kuona kuna watu wana ibuka toka kwenye vichaka, idadi yao kwa haraka ilikuwa ni vigumu kuitambua, lakini baadhi yao walikuwa wameshika sigara yenye harufu kali sana………ENDELEA…………
“ha haaaaaaaa! leo tume kuotea wewe demu, unajifanya mjanja sana” alisema mmoja wa wale vijana, ambao pia walikuwa wamevalia uniform (sale za shule) kama walizo vaa wakina Khamis, yani shati jeupe, na suruali nyeusi, hapo Neema alimshika Khamis kwa nguvu sana, huku akionekana kuogopa wazi wazi, “dah, kama zali vile, nilikuwa namtamani kinoma huyu demu” alisema mwingine, huku wakizidi kuziba kile kinjia, na wengine kuwa zungukia kwa nyuma na kuwaweka kati kati yao, Khamis aliwatzama wanafunzi wenzake awa kwa macho tulivu, japo alionyesha wasi wasi usoni mwake, sababu alikuwa ana wajuwa vizuri vijana awa kuwa ni wakotofi sana, na ata kama ukiwa tolea taalifa shuleni ni kazi bule, maana wazi wao walikuwa ni watu wwakubwa sana pale mkoani, “samahani jamani, sisi atutaki matatizo na nyie, tunaiomba mtupishe tuondoke zetu” alisema Khamis kwa sauti iliyo jaa wasi wasi na kitetemeshi, huku anawatazama wale jamaa, ambao idadi yao walikuwa watano, “kwani umesikia sisi tunakuitaji wewe?, we! nenda zao tuachie huyu demu” alisema mmoja wao ambae alionekana kuwa ndie kama msemaji wao mkuu, “George tuacheni tupite, na kesho ninakusemea kwa mwalimu” alisema Neema kwa sauti ya ukali, lakini kitu cha hajabu, vijana wale watano, yani wakina George, waka cheka kwa dharau, “kwanza njoo hapa, unajifanyaga mgumu sana wewe” alisema mmoja wao, siyo George, huku ana mshika Neema mkono, na kumvutia kwake, “Seifu niache bwana” alisema Neema huku ana akijaribu kujipapatua toka kwa huyo Seifu, ambae alionekana kumshika kwanguvu Neema, licha ya hivyo akaongezeka mwingine na kumsaidia Seifu kumthibiti Neema.
Hapo Khamis akaona akizubaa, anaweza kushuhudia mwanamke anae mpenda akifanyiwa kitu kibaya sana, maana alikuwa anawafahamu vyema vijana awa, ambao ni wanafunzi wenzao waliokuwa vidato, tofauti tofauti, kuanzia kidato cha pili mpaka cha cha nne, ni watoto maarufu sana siyo tu! shuleni kwao, pia ata shule za jirani, kama Luhuwiko na songea boyz, wwalifahamika, kwa utukutu wao, na kushiriki katika matukio mengi ya uovu, matukio ambayo kwa hakika walistahili adhabu kali, ambayo siyo tu kufukuzwa shule, laiti kama wange kuwa ni watoto toka kwenye familia kama za Khamisi Kom,ba mafagio, basi wange fungwa miaka mingi jela, lakini kutokana na utajiri na umaarufu, wa wazazi wao, waliishia kupewa onyo kali, kisha kuendelea na masomo, ambayo awa kuyazingatia ata kidogo, na kusababisha kushika namba za mwisho kwenye mitihani yao.
Khamis kuona tayari wamesha mkamata Neema, akamtazama George ambae wanasoma darasa moja, akamwona anamtazama kwa macho ya dharau, yaliyo regea kwa ajili ya bangi alizo kuwa amtoka kuzivuta, kitendo bila kuchelewa Khamis aliachia ngumi moja nzito, iliyotuwa usoni kwa George, ambae kiukweli akuwa ametarajia tukio lile, ile anapeleka mkono kujishika usoni, tayari alisha ongezewa nyingine ya chembe ya moyo, ambayo ilimkata pumzi kwa sekunde kadhaa, na kumfanya ainame huku akijishika sehemu ile, kwa maumivu makali aliyo yasikia, lakini aikuwa bahati ya Khamis, ambae alipotaka kumwongeza teke la uso, kijana George, akashtuka akizolewa migguu yake yote miwili, kwa mtama toka nyuma yake, na kujibwaga chini, kama kiroba, na kutulia akisikilizia maumivu, na ilo lilikuwa kosa kubwa sana kwa kijana Khamis Komba Mafagio.
Hapo wanafunzi wawili, kati ya wale watano watukutu, walimvamia Khamis pale chini, na kuanza kumshushia kipigo cha mwizi, Khamis kila alipojaribu kujitetea akuweza, maana jamaa walikuwa wana mshushia mvua ya kipido, pasipo kushagua sehemu ya kupiga, Neema akashuhudia kipigo kikali kikimshukia mpenzi wake, ambae akuwa na uwezo wa kumsaidia, zaidi ya kuangua kilio, huku akiomba mpenzi wake aachiwe, lakini maombi na kilio hicho akikusaidia, ndio kwanza kama kilizidi kutia chachu kwa wale vijana watukutu, wazidi kumshambulia Khamis, huku George nae akiwa ame chuchumaa anasikilizia maumivu kwenye chembe ya moyo, mpaka alipoona sasa amekaa sawa, akainuka na kujipapasa kiunoni mwake, akaibuka na bisi bisi, ndefu iliyo chingoka mbele, moja ya vitu ambavyo vijana awa usinge wakosa navyo ata wakiwa darasani, George akawasogelea wale waliokuwa wanampiga Khamis, aka wapangua kama vile anawaondoa wasiendelee kumwadhibu Khamis.
Nikweli aliwasukuma na wao wakasukumika na kuachia nafasi na kumwacha Kahamis peke yake, ndio wakati Khamis alipopata nafasi ya kuinuka pale chini haraka, akijuwa huo ndio wakati wa kuanza kupambana ili umwokoa mpenzi wake.
Naam Neema akaweza kushuhudia, mpenzi wake Khamis anainuka na kukaa sawa, lakini ile anataka kupiga hatua kumfwata pale aliposhikiliwa na wakina Seif, ghafla George nae kwa haraka na ghafla, akausukuma mbele mkono wake wakulia, usawa wa shingo ya Khamis, huku ameshika kitu chenye mwonekano wa chuma chembamba, kwa jinsi likivyo ng’aa, na mkono uka jikita usawa wa koo la Khamis, hapo kikaonekana kitu mfano wa msumari mrefu, kikipenya kwenye shingo ya Khamis, na kuzama chote, kiasi cha kugota kwenye mpini wake, alioushikila George, alafu akakichomoa kwanguvu, ikifwatia na mchuruziko wa damu, huku Khamis akionekana kuyumba yumba kama mlevi, na kujibwana chini kwanye kichaka cha matete, huku akiendelea kutatalika kwa kurusha rusha miguu, huku Neema akishikwa na mstuko mkubwa sana, akijihisi mwili unakosa nguvu, kwa kile alicho kishuhudia, akajaribu kupiga kelele za kuomba msaada, lakini wakina seif wakamziba mdomo.
Naam taratibu Neema akajiona anaanza kuregea na kupoteza nguvu, akawaona wale vijana wakimchukuwa na kuingia nae kwenye vichaka vya matete, na akiwa anazidi kulegea na kupoteza nuru ya macho yake na kuanza kuona giza lina tanda machoni mwake, kwambali akaona wale vijana wanamlaza chini na kuanza kumvua nguo, kwa kuzichana, kisha waka mtanua mapaja, na mmoja wao alie kuwa ametoa dudu yake iliyo simama, aka sogea mbele yake na kupiga magoto mbele yake, kisha aka jiweka sawa na kuiweka dudu kwenye kitumbua chake, Hapo Neema akahisi dudu ya yule kijana ambae alihisi kuwa ni George, ikiingia kwenye kitumbua chake, huku yeye akizidi kupoteza nguvu na mwisho kiza kikatanda usoni mwake, akujuwa kilichoendelea.
Naam Neema alishtuka nakujikuta akiwa amelala kwenye kitanda cha hospital, huku shangazi yake akiwa pembeni yake, Neema alihisi maumivu makali sana sehemu zake za siri, “shangazi, Khamis yupo wapi?” lilikuwa swali la kwanza, kwa Neema mala baada ya kuzinduka, huku akijaribu kuinuka toka kitandani, “tulia kwanza Neema, mwenzio Khamis, pia amelazwa nae ameumia sana” alijibu shangazi, kwa sauti flani iliyo jaa majonzi, “nataka nikamwone shangazi, nilizania ata poteza maisha, maana George alimchoma shingoni” alisema Neema ambae alikuwa ametundikwa drip kwenye mkono wake wakulia, “subiri kwanza uonane na doctor, kisha utaenda kumwona Khamis” alisema shangazi yake Neema huku anainainuka nakwenda kuwaita madoctor.
Madoctor walikuja mala moja, baada ya kuitwa na shangazi yake Neema, na kuanza kumkagua Neema, wakampima mapigo ya moyo na vitu vingine, ukweli Neema alikuwa amelazwa kwa siku tatu pale hospital ya mkoa, akiwa amepoteza fahamu, na Khamis, akuwa amelazwa kama shangazi alivyo sema, ukweli ni kwamba siku ambayo Neema alizinduka ndiyo siku ambayo, Khamis alikuwa amezikwa masaa machache yaliyopita, ni baada ya polisi kuufanyia uchunguzi, na kutoa luska ya kuzikwa kwa mwili ule.
Licha ya kuonekana kuwa alikuwa anaendelea vizuri, baada ya kubakwa na watu zaidi ya mmoja, lakini akuwa na mahambukizi yoyote ya magonjwa ya zinaa, pia madoctor walithibitisha kuwa Neema ata ujauzito wake wa miezi mitatu ulikuwa salama, ukweli taarifa hii ya madoctor, ilikuwa ni pigo jingine kubwa sana, kwa shangazi na mjomba wa binti huyu, yani Neema alie kili kuwa ujauzito ule ulikuwa ni Khamis Komba Mafagio, mjomba na shangazi awakuwa na lakufanya, zaidi walipanga kumalizia hasira zao kwa mtu alie mbaka Neema.
lakini mambo yalianza kubadirika muda mfupi ujao, ni mala baada ya insp wa jeshi la polisi, toka kitengo cha upelelezi, kuja kumhoji Neema, “binti utakiwi kuficha lolote, itatusaidia sisi, kufanya kazi yetu na kumkamata mtu alie kufanyia hivyo, ili achukuliwa hatua kali za kisheria, sababu alie fanya hivyo, ndie alie muuwa rafiki yako Khamis” aliongea insp Alois Kachinga, kwa sauti kavu ya nzito pasipo kubembeleza, katika mahojiano yaliyofanyika ndani ya ofisi ya doctor mkuu wa hospital ya mkoa, na hapo ndipo Neema alipo juwa kuwa, Khamis amesha fariki.
Kwanza Neema alianza na kilio cha kwikwi, “binti ukiendelea kulia, tutashindwa kumaliza mahojiano yetu” alisema Insp Kachinga, kwa sauti ya kikamanda, hapo Neema aka nyamaza na kuanza kueleza ilivyo kuwa, huku akiwataja, kwa majina waliomfanyia huovu huo, pamoja na kuondoa uhai wa Khamis, ambae ndie mama wa mtoto alie mbeba tumboni mwake, huku insp Kachinga, akiandika baadhi ya maneno ya mahojiano yao, “umesema waliofanya hivyo ni wanafunzi wenzenu?” aliuliza insp kwasauti ya ile ile kavu ya kuogofya, huku akimkazia macho Neema, “ndiyo nina wafahamu, alikuwepo George Keneth Mango, Seif Idd Mtumbuka, Chiza Kajoro Brazio, Justin Inocent Machiba, na Kulwa Philipo Ngaga” alisema Neema, na hapo insp Alois Kachinga akaonekana kushtuka, na kumtolea macho Neema, “we binti, ume sema hao vijana ni George Keneth Mango, Seif Idd Mtumbuka, Chiza Kajoro Brazio, Justin Inocent Machiba, na Kulwa Philipo Ngaga?” aliuliza insp Kachinga kwa sauti flani, ya ukali iliyo jaa mshangao na mshaka, “ndiyo, nihao hao, wanafunzi wenzetu, tunasoma nao Ruvuma day” alijibu Neema kwa msisitizo, hapo insp Kachinga, alitulia kwa sekunde kadhaa, kama vile anawaza jambo, kablaajainua usowake na kumkazia macho Neema, “mh! ebu sikia Neema, iliswawla usimwambie mtu yoyote, sababu tayari lipo polisi, pili ni hatari kwako aitakiwi vijana wale wajuwe kama umewatambua” alisema insp Alois, safari hii kwa sauti ya upole na tulivu, huku akimkazia macho Neema.
Ukweli ni kwamba hapo ndipo mahojiano yalipo ishia, insp Alois Kachinga, aliondoka zake, akionekana mwenye mawazo mengi, japo alijaribu kuficha hali yake isionekane usoni mwake, mjomba na shangazi walimwuliza Neema alichoongea na insp, nae akaeleza kama alivyo ulizwa na majibu yake yalivyo kuwa, “kwahiyo Neema una uhakika kuwa waliokufanyia hivyo ni hao watoto?” aliuliza mjomba kwa sauti yenye mshangao mkubwa, ikionyesha kuwa anawafahamu watoto hao na wazazi wao.
Labda msomaji ni kwambie kitu, kwa kifupi, ni kwamba watoto awa watano, walikuwa ni watoto wa kati ya watu matajiri wakubwa sana pale songea mjini, kwa kipindi hicho, tena matajiri wakubwa, ambao ni tegemeo la uchumi wa mkoa Ruvuma, iwe kwa misaada na kujitolea kwenye shughuri mbali mbali za kijamii, au shuguri inafsi za watu nazo ziliwategemea watu hao, ukiachia vyombo vya usafiri walivyo kuwa wanamiliki, ambavyo vilitegemewa kwa usafiri wa ndani nan je ya mkoa, pia walikuwa wanamiliki maduka makubwa ya pembejeo, na madawa ya mifugo na wanyama, pia maduka ya nguo na vyakula, bila kusahau kuwa wao ndio walikuwa wanunuzi wakubwa wa nafaka na mazao mengine toka kwa wakulima, “lakini aitazuwia wao kulipia hiki walicho kifanya, nitahakikisha wana fikishwa mahakamani” alisema mjomba akionekana kuwa, ana asira na machungu sana juu ya kilicho tokea, na ameamua kwa dhati, kusimamia jambo lile.
Lakini kama ujuwavyo, ata wahenga walisha sema, MASKINI ANAGA KIAPO, jioni ya siku ile Neema alipewa luhusa ya kurudi nyumbani, ambako alikuta kwa jirani yao, yani kwa Komba mafagio, kuna kila dalili ya kuwa palikuwa na msiba, hivyo alijifungia chumbani kwake akiendelea kulia, mpaka alipopitiwa na usingizi, na kuja kushtuliwa mida ya saa mbili za usiku, alipokuja kuitwa na dada wao wakazi ambae kwa umri nikama wanaendana, kuwa anaitajika sebuleni, kuna wageni wanaitaji kuongea nae, Neema akajizoa zoa na kuelekea sebuleni ambako aliwakuta shangazi na mjomba, wakiwa na watu wawili, mmoja akiwa ni mzee mtu mzima, na mmoja ni yule insp alie muhoji kule hospital, yani ni insp Alois Kachinga…….Naam tunazidi kusonga, na simulizi yetu ambayo ndio kwanza inaanza, tukutane kesho ili kujuwa huyu mzee ninani na hapa ame fwata nini, cha msingi tunza kumbu kumbu ya majina, na matukio. endelea kufwatilia kisa hiki, hapa hapa kwa @Hadithi ZA MBOGO EDGAR.
MREMBO KIPOFU
SEHEMU YA NNE
STORY NA: @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: Lakini kama ujuwavyo, ata wahenga walisha sema, MASKINI ANAGA KIAPO, jioni ya siku ile Neema alipewa luhusa ya kurudi nyumbani, ambako alikuta kwa jirani yao, yani kwa Komba mafagio, kuna kila dalili ya kuwa palikuwa na msiba, hivyo alijifungia chumbani kwake akiendelea kulia, mpaka alipopitiwa na usingizi, na kuja kushtuliwa mida ya saa mbili za usiku, alipokuja kuitwa na dada wao wakazi ambae kwa umri nikama wanaendana, kuwa anaitajika sebuleni, kuna wageni wanaitaji kuongea nae, Neema akajizoa zoa na kuelekea sebuleni ambako aliwakuta shangazi na mjomba, wakiwa na watu wawili, mmoja akiwa ni mzee mtu mzima, na mmoja ni yule insp alie muhoji kule hospital, yani ni insp Alois Kachinga…….ENDELEA…….
Neema alikaa kwenye moja ya kochi kati ya seti mmoja ya makochi yaliyokuwepo mlendani, huku ana zisoma sura za watu aliowakuta yani mjomba wake shangazi yake, pia yuyle insp Alois Kachinga, na huyu mgeni mwingne aliie kuja nae, “shikamoo” alisalimia Neema akimtazama yule mzee wamakamo, ambae alikuwa katika sura ya tabasamu, la kawaida kama mwenzie kachinga, tofauti na mjomba alie kuwa katika hali flani kama vile ya kuchukizwa na jambo flani, kama alivyo kuwa shangazi pia. “marahaba Neema na pole sana” alisema yule mzee na hapo Neema akaitikia kwa kichwa, kisha maongezi ambayo yalionekana kuwa yalishaanza muda mfupi uliopita, yakaendelea, japo Neema alishangazwa na hali aliyo ikuta pale sebuleni, ya kuwa watu walikuwa na sura za mionekanao tofauti, lakini akatulia kumsikiliza yule mzee ambae alianza kuongea, “nazani unifahamu Neema, mimi naitwa ASP Jacob Mhando, ni mkuu wa jeshi la polisi, katika kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai hapa mkoani, alijitambulisha yule mzee, huku Neema akimsikiliza kwa umakini, na sasa alijuwa kuwa walikuja kwaajili ya kuchukuwa maelezo yake zaidi, “na huyu ni mmoja wa wapelelezi wangu” alisema yule Mzee Mhando huku akimshika bega insp Alois Kachinga, “tume kuja hapa usiku huu, tuna jambo moja muhimu tuna taka tukiongee na kukubariana, na ili ni kwa ajili yako, na maisha ya mtoto ulie nae tumboni, maana na ata wewe unajuwa ni kosa kwa mwanafunzi kuwa na mimba, hivyo tume kuja kukusaidia ili uwe na maisha mazuri, na uweze kumaliza mitihani yako” alisema yule mzee, hapo Neema akamtazama mjomba wake, akiamini kuwa anakuwa kinachotaka kuzungumzwa na mzee Mhando, lakini akaona wazi kuwa mjomba na shangazi walikuwa na nyuso za kipingamizi.
Nikweli maana ata kabla yule mzee ajaongea tena, tayari mjomba wa Neema alisha dakia, “lakini mzee kumbuka kuwa mimi ndie, mlezi wa Neema, huyu ni mtoto awezi kutoa maamuzi juu ya swala ili, maamuzi ni yale niliyo yatoa mimi, kuwa akuna kitakacho badirishwa jamaii aito nielewa, nachoomba wale watoto wakamtwe na washtakiwe, wapewa adhabu kwa walicho kifanya” alisema mjomba wake Neema, hapo insp Kachunga na mzee Mhando, wakatazamana, kisha wakatabasamu lile tabasamu la dharau, huku wanatazama chini.
Insp na ASP wali tulia kwa sekunde kadhaa kisha yule mzee akamtazama mjomba, “kijana sizani kama unakijuwa unachokifanya, kumbuka ukaidi wako auwezi kukusaidia kitu” alisema yule mzee kwa sauti tulivu, huku bado dalili ya tabasamu la dharau likiwa usoni mwake, “lakini mzee wewe ndie msimamizi wa sheria, sasa kwanini tumsingizie marehemukuwa mbakaji, wakati waliofanya hivyo wanajulikana?” aliuliza mjomba kwa sauti ile ile ya hamaki, “hiyo ni kwaajili ya kuondoa usumbufu na kashfa kwa waheshimiwa, isitoshe wame aidi kukulipa kiasi kikubwa cha fedha, ambacho kita msaidia huyu binti yako, pamoja na kumsaidia kumaliza shule” alisema yule mzee wakati huo wengine wote walikuwa wametulia, wakiwasikiliza wawili hao “ kwahiyo waende wakawabake na kuwauwa watoto wengine kwaajili ya kulinda heshima za wazazi wao?” aliuliza mjomba na hapo yule mzee akatulia kidogo, akiinamisha kichwa chini, kama vile anatafakari jambo flani, kisha akainua uso na kumtazama insp, “Kachinga nazani huyu bwana atuelewi, na hapa tuna poteza muda tu! bola mpango wapili utumike” alisema yule mzee ambae jina lake ni bwana Jacob Mhando, huku anasimama na na kuufwata mlango wa kutokea nje, akifwatiwa na insp.
Na walipoufikia mlango, yule mzee akasimama nakugeuka uande wa sebuleni, akamtazama mjomba wake Neema, alie kuwa anawasindikiza kwa macho, kama aliyo fanya shangazi na Neema mwenyewe, ambae sasa nikama alikuwa anaelewa kinacho endelea, “lakini kijana inabidi ukubaliane na matokeo, maana siku zote mtoto alali na fedha” alisema bwana Mhando, kisha akatoka nje ya nyumba ile, na hapo ndipo Neema alipo gundua kuwa Mzee Mhando na mwenzake, walikuja na magari mawili, maana yalisikika yakiwashwa, na kuanza kuondoka, na yeye akainuka kwenye kwenykochi na kuelekea mlangoni, ambako alichungulia nje na kuona magari mawili ya polisi, yenye askari kasha nyuma yake, yakiondoka, eneo lile la nyumbani kwao, na kupitia upande wa kushoto, ambao ni upande wa kusini wa wa mji wa songea, kisha yakipotelea upande wa pili wa kanisa la Matogoro.
Yap! Neema alisimama kwa sekunde kadhaa pale mlangoni kwao, huku akifikilia kilichotokea dakika chache zilizo pita, akuelewa ni kwanini wale wale wakubwa wa polisi walikuwa wanataka kumsingizia marehemu Kahamis kuwa ndie alie mbaka, “wanataka kuwatetea wakina George” ilo ndilo jibu ambalo Neema alilipata, jibu ambalo ni kama lilimkumbusha mpenzi wake na tukio zima la pale mtoni, jinsi mpenzi wake Khamis alivyo uwawa kwa kuchomwa na bisi bisi.
Taratibu machozi yakaanza kumtoka machoni mwake, akageuka kutazama sebuleni, ambako aliwaacha shangazi na mjomba, akawaona walikuwa wanaeleka vyumbani mwao, huku mjomba akiongea kwa kuwalahumu wale wakuu wa jeshi la polisi, “hii yote ni kujali maslai yao, na mimi siwezi kukubari upuuzi kama huo” alisema mjomba wake Neema, huku wanapotelea upande wa vyumbani, Neema aka geukia upande wanje, na kupiga hatua mbili kuelekea upande huo, na kujikuta yupo nje kabisa ya nyumba, akatazama juu wingu, giza lilikuwa lime tanda kweli kweli, akakumbuka kuwa mida kama hii, ndio mida ambayo alikuwa ana kutana na Khamis, roho ilimuuma sana, kwa kukumbuka kuwa asingeweza kuonana tena na Khamis.
Neema akatazama upande wa nyumba ya mzee Komba mafagio, akaona papo kimya kabisa, na giza lile tanda eneo ilo, sababu nyumba yam zee huyu aikuwa na na umeme, wala nishati yoyote inayofanana na hiyo, Neema akiwa ameacha mlango wazi, akaanza kutembea taratibu kuelekea upande wa nyuma wa nyumba yao, ungesema anaenda upande wa mabanda ya uwani, au kwenye choo cha nje, lakini aikuwa hivyo, alitembea taratibu akipita eneo la banda ya uwani, na kuelekea upande wa kulia kwake, ambako kuna nyumba ya kina Khamis, na kufwata mti moja mdogo wa muembe, na alipofika chini yake ambapo palikuwa na kitu kama benchi, aka kaa kwenye lile benchi na kutulia kimya kama vile alikuwa anamsubiri mtu, sekunde chache baadae akaaza kuangua kilio cha chini chini, maana alivuta kumbu kumbu ya kuwa mida hii maali hapa ange kuwa na Khamis.
Nikweli hii ndiyo sehemu waliyo kuwa wanaitumia yeye na Khamis kama sehemu ya makutano yao, nisku chache sana ambazo awa kuja sehemu hii, lakini karibu kila, ilikuwa ni lazima wakutane mahali hapa ambapo wangekaa mpaka saa sita za usiku, kisha kila mmoja kuingia kwao, kwenda kulala, “na usiku huo ndipo lilitokea tukio kubwa jingine ambalo nisingeweza kuacha kuwafanya wakina Mahando na Kachinga” alisema Thensia, alie kuwa ana simulia kisha cha yeye kuamua kufanya aliyo ya fanya.
Mschana Thensia alipofika hapo alitulia kidogo, “ebu ngoja kwanza” alisema Thensia, kisha akainuka na kutembea kuelekea chumbani ambako toka ameingia ndani ya nyumba hii, amekuwa analala pamoja na insp Elvis Eric, ambae alijuwa mschana huyu ni kipofu, na kule chumbani Thensia alietembea kama mtu anae ona, yani siyo kipofu kama alivyo jifanya kwa miezi kadhaa, akutumia muda mrefu alirudi akiwa na magezeti mawili, japo mwonekano wake ulionekana wa kawaida, ungesema alinunua jana au juzi, lakini alipo mwokabidhi insp Elvis alishangaa na roho yake, mala baada ya kusoma tarehe usika ya gazeti lile, lililo toka mwishoni mwa mwaka 1995, “gazeti ili lilitoka asubuhi ya siku ya pili ya” alisema Neema huku akionyesha gazeti la kwanza na kisha akaonyesha la pili, “na ili lilifwatia siku iliyofuata, unaweza kusoma kilicho andikwa” hapo insp akaanza kusoma lile la kwanza, ambalo lilikuwa na kichwa cha habari kikubwa chenye maandishi meusi ya elufu kubwa, “MWANAFUNZI AFARIKI AKIJARIBU KUBAKA” hapo insp Elvis alibadirika uso kwa mshtuko, inamana afande Kachinga alifanya mchezo wa kubadiri tukio?” aliuliza insp Elvis huku anamtazama Thensia, mimi na wewe atukuwepo, nazani nivyema ukisoma maelezo ya kichwa hicho cha habari” alishauri Thensia, na hapo insp Elvis Eric, aka funua kurasa ambayo ilielekezwa kuwa ina habari hiyo, “mwanafunzi Khamis amewawa wakati akitekeleza tukio la ubakaji kwa mschana Neema ambae ni mwanafunzi mwenzake, katika shule ya sekindali ya Ruvuma, tukiongea na kamnda wa upelelezi wamakosa ya jinai wa mkoa, wa Ruvma, amesema kuwa, maelezo ya mschana Neema, mwenye umri wa miaka kumi na nane, alifanyiwa kitendo hicho na marehemu Khamis, wakati wakiwa njiani wanatoka shuleni, nakatika hali ya kujiokoa toka kwa mbakaji huyo, ndipo alipo msukuma na kukusababisha Khamis, alie kuwa anatekeleza ubaki, aangukie kisiki na kujichoma shingoni, kitu kilicho pelekea kijana huyo kupoteza damu nyingi na hatimae kufariki hapo hapo” alimaliza kusoma insp Elvis, “ninani alikupatia ili gazeti na wakati kipindi hicho sisi atukuwa tumezaliwa?” aliuliza insp Elvis, huku anachukuwa gazeti la pili, “alinipa huyo schana alie bakwa yani Neema” alisema Thensia, huku akimtazama Elvis alie kuwa anatazama kurasa ya mbele ya gazeti la pili, ambayo yalipishana siku moja kutoka.
“FAMILIA YA BINTI ALIE BAKWA YAJINYONGA KWA KUKWEPA AIBU” hicho ndicho kichwa cha habari kilicho onekana kwenye gazeti la pili, “kwanini walifanya hivi awa wanafamilia” alijisemea mwenyewe insp Elvis uku ana pekuwa kurasa yenye maelezo kamili, “watu watatu wanao semekana kuwa ni familia ya mschana Neema alie bakwa siku chache zilizopita, wame kutwa wame kufa kwa kijiuwa na kinywaji kinacho sadikiwa kuwa ni sumu, kwa kile kilicho bainika kuwa ni kukwepa aibu, juu ya kile kilichotokea, kati yao waliokutwa wamekufa, ni mjomba na shangazi, ambao ni walezi wa mschana, Neema na Neema mwenyewe” alimaliza kusoma insp Elvis, ambae nikama alishajuwa kilichtokea, mana ata usowake ilijawa na uzuni, “sasa wewe ni nani na usika vipi juu ya ili, na kama neema alisha kufa aligeavipi iligazeti?” aliuliza insp kwa sauti iliyo jaa mshangao, lakini Thensia akatabasamu kidogo, “mimi ni mtoto wa Neema na Khamis, na Neema akufa kama ilivyo andikwa, tena mpaka leo anaishi na anaendelea vizuri kabisa, alie kufa alikuwa ni dada wakazi na siyo Neema” alijibu Thensia, kwa sauti tulivu, nini kilitokea mpaka mjomba na shangazi waka jiuwa?” aliuliza Elvis, kwa sauti ya mshangao, huku anaweka gazeti mezani, “kwanza kabisa lazima ufahamu kuwa mjomba na shangazi awakujiuwa, ila wali uwawa” alisema Thensia, kisha akaendelea kusimulia kilicho tokea.*******
Ilikuwa hivi, mida saa sita kasoro za usiku, Neema akiwa bado amekaa chini ya mti, karibu na nyumba ya kina Khamis, akawaona watu kadhaa waliovalia sale za polisi, wakitembea kwa kuvizia kuelekea kwenye nyumba yao, na kwa bahati mbaya akuwa amefunga mlango, sababu akuegemea kuwa yange tokea yale yaliyotokea usiku ule, mwanzo Neema alizania kuwa watu wale, ni wageni wao, nao wanakuja kuhoji kuhusu tukio la kubakwa kwake, lakini alipozingatia muda na mwendo waliokuwa wanatembea wageni wale walio fikia idadi yao, kama kumi hivi, aliwatilia mashaka, na kuamua kutulia pale pale, ilikusikilizia kinachoendelea………. endelea…………. kufwatilia kisa hiki, hapa hapa kwa @Hadithi ZA MBOGO EDGAR.
Tags
simulizi