( 1-5 )
SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAAðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ—£️
EP: 01.
Ilikuwa ni Jumamosi ambayo Mama Bry aliamka furaha tele baada ya mwanae wa kiume, Bryton ambaye anasoma huko Texas nchini Marekani kumpigia simu kwa njia ya Whatsapp video na kumtaarifu kwamba anakuja nyumbani, yupo uwanja wa ndege nchini Marekani na sio muda ataianza Safari.
Mama Bry alifurahi sana na kuamua kuandaa hafla fupi (🎉 party) kwa ajili ya mwanae.
Majira ya saa tisa alasiri, Bryton aliwasili uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere na kuchukua Taxi ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka nyumbani. Alipokelewa kwa shangwe kubwa huku ndugu zake waliokuwepo hapo nyumbani wakimkumbatia Bryton kwa furaha sana.
"Oooh karibu Bryton jisikie upo nyumbani kipenzi" Mama Bryton alimwambia mwanae "Ahsante sana yani mimi ugonjwa wangu ulikuwa ni kuwami-ss tu jamani hakika sasa tiba yangu imepatikana" Aliongea Bryton kwa kiswahili kinachotaka kufanana na kiswahili cha kizungu!
Party ilifanyika siku hiyo lakini Rabia dada wa kazi ambaye alikuwa ni mkubwa kiumri kuwashinda watoto wa mama Bryton alifungiwa chumbani muda wote Party ilipokuwa inaendelea. Mziki ulidunda sio poa, huku watu wakila na kusaza, baadae yani jioni sasa Bryton alienda mjini na kununua kreti nne za soda, alipozileta nyumbani akaona aziweke kwenye kile chumba anacholala Rabia, hakujua kuwa kuna mtu ndani ya kile chumba yeye alichujua ni kwamba kile chumba kilikuwa ni stoo ya kuwekea chakula na vitu vinginevyo.
Alipofungua mlango, mara akashtukia kumuona Rabia akiwa amelala kwenye mabox huku akilia kwa kulishika tumbo lake kuonyesha kuwa anahisi njaa. "Wewe ni nani?" Aliuliza Bryton mara mama Bryton akatokea. "Achana naye huyo ni Rabia dada wa kazi funga mlango uje huku sebuleni baba yako anataka kuongea na wewe" Alisema mama Bryton.
"Mh sasa kama ni mmoja wa Familia hii kwanini tusijumiike naye, halafu....halafu anaonekana ana njaa sana huyu" Aliongea Bryton kwa huruma. Mama yake akamsogelea karibu na kumwambia. "Huyu achana naye hana nguo za kuvaa ana nguo moja tu hiyo aliyovaa atatia aibu kwa wageni, kingine anajikuna sana sijui ana chawa yani ni mchafu huyu binti kama ni chakula aletewe ale mwenyewe maana hata hivyo anakulaga mwenyewe baada ya sisi kushiba" Alisema mama Bryton, mara akashangaa Bryton anatokwa na machozi. "Sasa unalia nini na wewe" . "Hapana mama, mimi kama ni chakula changu nileteeni huku chumbani nitakula na Rabia" alisema Bryton huku akifuta machozi yake kwa leso. "Huyu binti ni mgonjwa Bryton mbona huelewi, huoni vidonda hivyo mwilini, ana ukimwi sio wa kukaa naye karibu, anatakiwa ale peke yake na alale peke yake...." Alisema mama Bryton. Lakini akashangaa Bryton aki......
HUO NDIO MWANZO WA SIMULIZI HII YA SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAA! JE IENDELEEE?????? SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAAðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ—£️
EP 02
"Huyu binti ni mgonjwa Bryton mbona huelewi, au huoni vidonda hivyo mwilini, ana ukimwi sio wa kukaa naye karibu anatakiwa ale peke yake na alale peke yake" Alisema mama Bryton.
ENDELEA SASA...
"Mama maisha hayapo hivyo ukimwi sio Corona kusema kwamba kama anao ataambukiza wengine kwa njia ya hewa na sio wote waliopata ukimwi kwa kufanya zinaa wengine walizaliwa nao hivyo tusiwanyanyapae wagonjwa wa ukimwi" Bryton alimwambia mama yake. "We shauri yako unajifanya unamjua huyu binti kuliko sisi ambaye tuko naye siku zote haya endelea" alisema mama Bryton lakini Bryton hakuwa na muda huo wa kumsikiliza alichukua sahani mbili za chakula akazijaza chakula na kwenda kwenye kile chumba alipo Tabia akaanza kula naye.
"Ahsante kaka tangu nifike nyumba hii wewe ni mtu wa kwanza kuniona nina thamani, siku nyingine nakula baada ya wenzangu kushiba, makombo yanayobaki ndio nakula mimi ahsante kaka Bryton uwepo wako kwangu umekuwa na maana kubwa sana" Alishukuru Rabia kila mara huku akiendelea kula. Bryton alibaki analia tu.
Mara akaingia mama Bryton akaokota sahani ya Rabia ambayo ilikuwa bado ina chakula, akammwagia Rabia usoni wali wenye michuzi. "We mbwa! Unamueleza nini mwanangu mpaka analia mda wote, katoka Marekani akiwa na furaha unataka kumfanya awe na huzuni kwasababu yako mbwa usiye na wazazi" alifoka mama Bryton.
"Mama Mungu hapendi hivyo. Isitoshe kila siku upo mstari wa mbele kwenda kanisani hivi huko kanisani mnafundishwa kunyanyapaa wengine ah! Nyumba hii sijui ina laana gani kwa kweli" alisema Bryton muda huo Rabia alikuwa anajifuta michuzi ya wali usoni huku akibubujikwa na machozi.
*
Siku iliyofuata Bryton aldamka asubuhi na kumsaidia Rabia kazi zote, walifagia pamoja, kupika, na kufanya kila kitu kitendo ambacho kilimuuma sana mama Bryton. "Nisikilize Bryton mwanangu huyu binti leo nataka nimfukuze maana ataleta mifarakano kwenye familia kwani tangu uje wewe naona mbwa huyu ana kiburi sana," alisema mama Bryton. "Rabia kaoge twende zetu mjini maana kazi tushamaliza" Bryton alimwambia Rabia na wala hakutaka kumsikiliza mama yake.
Rabia alioga na kuvaa masembere yake wakatoka na Bryton. Walienda shopping centre Bryton akamnunulia Rabia nguo nyingi na zawadi kemkem. "Rabia na wewe ni mtu hivyo unahitaji kuthaminiwa hebu nikuulize ni kweli una ugonjwa wa ukimwi!" Bryton alimwambia Rabia . "Hapana kaka sina ugonjwa! Ila kwa jinsi nilivyokonda mama ananitangaza kwa watu kuwa nimeathirika hivyo wakae mbali na mimi, watu wengi wamenitenga kaka lakini nashangaa wewe upo karibu na mimi"alisema Rabia huku akilia. "Pole! Hebu tupirue hospitali ukapime ili uwe na uhakika kama umeathirika uanze kutumia dawa! Usiogope twende Rabia!" Bryton alimwambia Rabia huku wakielekea hospitali!
JE RABIA ATAKUTWA NA VIRUSI VYA UKIMWI? NA ITAKUWAJE KAMA ATAKUTWA HAIJAATHIRIKA? JE NA ITAKUWAJE MAMA BRYTON AKIJUA RABIA NI UZAO WAKE WA KWANZA ILE HALI ALIMTESA SANA NA KUMNYANYAPAA! WEEE CHUNGA SANA HAKIKA USIKOSEE SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAAðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ—£️
EP 03.
Bright na Rabia walipitia hospitali ambapo daktari alichukua damu ya Rabia na kuwaambia wakae nje wasubiri majibu!, Punde tu daktari aliwaita na kuwapa majibu "Binti hongera sana, afya yako ipo safi endelea kujilinda hivyohivyo!" Alisema daktari na palepale Bryton akimkumbatia Rabia kwa furaha kubwa kisha akambusu mdomoni. Rabia alijisikia fahari sana kwa namna ambavyo Bryton alikuwa akimjali.
Walitoka pale hospitalini na kupitia Saloon, Bryton alitoa 30000 kwa msusi ili Rabia asukwe nywele, Zoezi hilo lilifanyika kwa haraka huku Bryton akimsubiria Rabia, alipomaliza kusukwa walitoka pale na kupitia hotelini. "Kula kabisa ushibe huku huku maana chakula cha nyumbani ni cha masimango na siku zote chakula cha masimango hakishibishi" " Bryton alimwambia Rabia. Walikula na walipomaliza walianza safari ya kwenda nyumbani!
Walipofika nyumbani Bryton alimsalimia mama yake lakini mama Bryton hakumuitikia zaidi ya kumtizama vibaya Rabia.
*
Ilipofika usiku sasa, Bryton alimuaga mama yake kuwa anaenda kuangalia mpira, mama yake hakumuitikia bado alikuwa amemnunia hata hivyo Bryton hakujali aliondoka zake na kwenda mpirani. Alipoondoka tu mama Bryton alimfuata Rabia kule chumbani kwake akiwa na kisu. "Unapenda urembo sana eti, sasa ngoja nikuonyeshe" alisema mama Bryton huku akizishika zile nywele za Rabia na kuanza kumnyoa na kisu, Rabia alipiga kelele lakini haikusaidia kutokana na nyumba ile kujengwa kwa mfumo wa kisasa zaidi kiasi kwamba ukipiga kelele ndani aliye nje hawezi kusikia. Kabla hata jamalizia kumnyoa, Rabia alidondoka chini na kupoteza fahamu. "Na ukome!" Alisema mama Bryton huku akizishika nguo za thamani alizonunuliwa Rabia na kuanza kuzichana chana na kisu alipomaliza akafungia Rabia kule chumbani akabeba funguo na kwenda kulala nayo.
Bryton aliporudi mpirani aliingia moja kwa moja chumbani kwake kulala kwani muda ulikuwa umeisha, hakujua chochote kitu kilichotokea. Usiku wa manane sasa alishtuka usingizini baada ya kusikia mama yake akipiga kelele chumbani kwake. "Niacheee nimekoma uuuuwwii niache jamani" Haraka Bryton alikimbilia chumban kwa mama yake, ile tu kufungua mlango mama yake akashtuka!
"Ah huu ndoto ni mbaya sana" Alisema mama Bryton huku akihema sana. "Ndoto gani mama" Bryton aliuliza. "Marehemu bibi yako amenitokea kwenye Njozi na kuanza kunitandika sana huku akidai namtesa bila kujua kwa kitendo cha kumpiga Rabia ni sawa na namtesa yeye kwani Rabia ni mwanangu wa kumzaa kabisa, yani hata sielewi inakuwaje Rabia awe mwanangu, hapa nilipo mwili mzima unaniuma kwa maumivu!"
"Kwani mama Kabla ya hapo uliwahi kuzaa" Bryton alimuuliza mama yake. "Ndio lakini ni historia ndefu mwanangu" Alisema mama Bryton huku akilia.
"Mh mi naona tumchukue Rabia usiku huu tukafanye vipimo vya DNA maana ukisubiri mpaka pakuche mizimu itakutoa roho, twende hapo Manundu Hospital maana wao wanafanya kazi masaa 24" Alisema Bryton ilibidi mama yake akubali maana kipigo alichopata hakutamani kimrudie tena! Mama Bryton alimpa funguo Bryton ili akamfungulie Rabia. "Mh yani mama ulimfungia mtoto wawatu, sasa akitaka kujisaidia? Ama kweli wewe ni shetani wa mguu mmoja" Alisema Bryton huku akielekea chumbani kwa Rabia, bado alikuwa hajajua kilichompata Rabia. JE ITAKUWAJE SASA BRYTON AKIFUNGUA CHUMBA CHA RABIA?" MAMBO NDIO KWANZA YANAANZA KULE WHATSAP
SIKUJUA HOUSE GIRL NILIYEMTESA NI BINTI YANGU WA KUMZAAðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ—£️
EP 04 & 05
Bryton alipofungua mlango wa chumba cha Rabia alishtuka sana kumkuta Rabia akiwa amelala chini hana fahamu na zaidi alikuwa amenyolewa nywele kichwani kwa kisu kitendo ambacho kilisababisha atokwe na damu nyingi kichwani zilizogandiana.Bryton alitetemeka kwa woga sana akarudi chumbani kwa mama yake na kuanza kumgombeza. "Mama hivi ni unyama gani ule uliotendea yule binti ni unyama wa aina gani lakini" Wakati Bryton anaendelea kumgombeza mama yake, Rabia alizinduka kule chumbani kwake, taratibu akatoka nje na kuamua kutoroka!, Aliona ni bora akaendelee kuishi katika maisha duni yenye amani kuliko kuishi sehemu ambayo hata chakula ni cha masengenyo, aliona ni bora akaendelee kula dampo kama ilivyokuwa hapo awali lakini moyo wake uwe na amani.
"Haraka sana twende tukamchukue yule binti tumpeleke hospitali laa sivyo nitaenda kukukabidhisha kwenye mikono ya sheria" Bryton alimwambia mama, wakatoka na kwenda chumbani kwa Rabia lakini Rabia hakuwepo. Mara mama Bryton akaanza kupiga yowe huku akigaragara chini, alikuwa anachapwa na mtu ambaye hamuoni, alichapwa sana mpaka akapoteza fahamu. Asubuhi waliamua kumpeleka kwa mganga, mganga alimwambia mama Bryton kuwa mizimu imekasirika sana na kitendo ambacho alikuwa akimfanyia Rabia na hivyo imempa adhabu ya kutokwa na Blidi maisha yake yote na viungo vya mwili kulegea, ataweza kupona endapo tu atamtafuta Rabia amuombe msamaha! . Kweli Mama Bryton alishangaa akiwa palepale kwa mganga anaanza kutokea na damu nyingi sehemu za siri ambayo ilitoa harufu mbaya sana, na zaidi viungo vyake vya mwili vilikuwa kama vimeparalaizi.
Bryton alimrudisha nyumbani ili aanze kazi ya kumtafuta Rabia maana mama yake alikuwa ni mtu wa kujisaidia hapohapo hadi kula alilishwa. ",Unaona mama haya ndio malipo yako yani huwezi kupanda mahindi ukavuna maharage, ukipanda mahindi utavuna mahindi, ulipandikiza mbegu ya ubaya na haya ndio malipo ya pando ulilopandikiza, nimezunguka kila kona ya mji,nimetafuta mpaka kwenye majengo ambayo hayajaisha lakini sijamuona Rabia" Bryton alimwambia mama yake.
"Ahh basi nipeni hata sumu nife tu kama Rabia haonekani maana haya mateso ni makali mno" Alisema mama Bryton lakini hakuna aliyeweza kumsikiliza.
***
Rabia alipotoka pale kwa mama Bryton usiku ule alienda kulala nje ya nyumba moja ya kifahari, alilala kwenye kibaraza na asubuhi tajiri wa nyumba hiyo aliweza kumuona, tajiri alitetemeka kwa woga baada ya kuona damu nyingi ikiwa imegandiana kichwani kwa Rabia, alimuamsha, alimpeleleza, Rabia alimuelezea kila kitu, tajiri yule aliumia sana alimpeleka hospitali, Rabia alitibiwa. "Pole sana binti hakuna haja ya kusema ukashtaki polisi wala kukumbuka mabaya uliyofanyiwa, sahau kabisa kwani Mungu ndiye hakimu wa haki, mimi nitakusaidia mtaji, nitakufungulia duka ujiendeleze mwenyewe"Tajiri yule alimwambia Rabia.
Rabia alifurahi sana, siku tatu baadae Rabia alifunguliwa duka kubwa la jumla na kukabidhiwa, hapo alianza maisha mapya na Mungu si athumani alimbariki kwa kiwango kikubwa kwani baada ya miaka minne Rabia aliweza kujenga nyumba yake mwenyewe ya kifahari, hakuwa wa kutembea tena kwa miguu alitembelea gari, na zaidi alifungua hoteli kubwa sana ya kifahari mjini Arusha!.( RABIA HOTEL VIEW PACK,) Hakika Mungu alifanya njia pasipo na njia!
**
Bryton alisumbuka sana na mama yake kwa miaka minne bila mafanikio, waliuza kila kitu walitembea kwa waganga lakini hawakufanikiwa, mama yake alikonda kiasi kwamba mikono ilikuwa kama ile fimbo ya mwamvuli, Maisha ya Bryton yalibadilika hakuweza kufanya kazi kwasababu ya mama yake, yeye ndiye alikuwa wa kumlisha, kumuogesha kwani ndugu wengine walimsusia.
Siku moja Bryton aliingia hotelini mjini Arusha, aliagiza chakula na kuanza kula huku akiwa na mawazo sana, mara akaguswa kwa nyuma kisha akageuka. "Samahani kaka nimekuona mda mrefu sana toka ulipoingia hapa hotelini nikawa kama nakufananisha hivi, sijui ni wewe au laaah" Rabia alimwambia Bryton. Lakini kwa namna Rabia alivyokuwa amebadilika Bryton hakuweza kumkumbuka hata kidogo. "Hebu niambie dada unanifananisha na nani maana mimi ni mtembeaji sana pengine tulishawahi kuonana kabla ya hapa!" Alisema Bryton.!
JE NINI KILIENDELEA SASA? ITAKUWAJE BAADA YA BRYTON KUJUA KWAMBA DADA ALIYEVALIA MAVAZI YA THAMANI NI RABIA? ITAKUWAJE?
MAMBO NI 🔥🔥🔥🔥🔥🔥 MoTo.....
Tags
simulizi