TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

LIVIA 04

Story.... *LIVIA* 

SEHEMU YA 4


Uwiii  mkojo ulinitoka kidogo sikuamin kumuonamama pale,miongoni mwa wababa aliokuja nao mmoja alivaa kibarakashia na kanzu,mama akasema liv haya ndio maisha ulioamua si ndio?Umeacha duka langu wazi watu wananifungia hukujali kabisa kuwa ndio sehemu unakula sababu ya hiki kijanaume kinachoishi uswahilini?nilidhani umejitunza sababu una malengo yako lkn kumbe umeaona uje utupe ujana wako kwa mwanaume kama huyu kweli?umeniskitisha san asana we binti,nimeshawapigia simu kwenu kuwa kuanzia sasa hautokua na mm tena mana nilishakuonya hukuskia uliomba msamaha na kusema hutorudia lkn ni wazi mapenzi yamekulevya sasa basi kijana si umeamua kunipanda kichwani huyu ni mkeo kuanzia sasa,shehe fanya mambo yako hapo, waozeshe mana hatuchukui ahta sh 10nyake najua hana,na liv utakua mke wa huyu anaekuchezea na kukufaidi bure,msichana mzuri lkn akili hakuna si unaitaka ndoa umeipata,sikuamini kinachotokea na mm kwtu sikuwahi ona ndoa za dizaini io,tulifungishwa ndoa pale pale mm na hakeem kisha ikaisha nikaambiwa mm rasmi n mke wa rahim na rahim alikubali kabisa,watu walijaa hapo kushangaa mana ni tukio na wapangaji ni wambea hivo waliambizana watu wakajaa barazani,mama crey alienda kwenye gari lake akabeba begi langu kubwa la nguo,akaleta mlangoni akaenda tena akashusha mashangazi kaja manne alisaidiawa na vijana sikujua ameweka nini akaniekea mlangoni akasema mm na wewe hatujuani tena kama kuna changamoto wapigie kwenu kwaheri.akapiga ahatua akarudi akasimama akarudi tena akafungua pochi yake akatoa pesa akasema hii ni pesa yako ya mwezi huu,hunidai sikudi,akaondoka zake sasa,nilikosa pozi yani kweli nimeolewa?moyo wnagu uliniuma kuondoka vile kwa mama crey lkn ndio basi tena,hakeem alianza kuingiza vile vitu nje huku wambea wakiwa wanasemezana na kupiga vigelegele,kushangilia ndoa et,nilikaa ndani hakeem akasema liv ww udhakua mke wangu,nah ii ni ndoa halali kabisa usiwe na wasiwasi sawa mm nitafanya kazi kwa bidii na tutayamudu haya maisha,nikasema sawa lkn sikupenda kuondoka hivi kwa mama creay amenijali sana,hakeem akasema sasa Yule sio mama yako ingetokea tu siku ungeondoka achana na mawazo hayo sasa iv fikiria kunitunza mme wako sawa,nikasema sawa,akasema nitawajuza nyumbn kuhusu hili kisha tutaenda sawa mke wangu,nikasema sawa.akasema acha nijiandae basi niwahi kazini,nikasema sawa,nilimuandalia maji bafuni huku wapangaji wenzie wakisema hayo ndo mambo sasa hakeem unaona sasa kiulaini umechukua chombo tena chombo kikali daaaaaah,hakeem anajichekesha tu.nilianza kufungua yale mashangazi kaja,mcuko mmoja ulikua na masufuria mazuri sana mazito sikuyanunua mm,nilijua mama crey amenipa,humo kulikua na flampeni pia,vijiko vizuri sana vvikubwa,mfuko mwingine ulikua na sahani nzuri na mabakuli vikombe vya udogo na vijiko pia hotpot nzuri sana,mfuko mwingine ulikua na vitu nilivokua nanunua mm mwenyewe mashuka na vingine na mfuko mwingine ulikua na mapazia mazuri mashuka mazur ya gharama na vitenge dot kadhaa,nililia mama cray hakuniaxcha hiv hivi alinipa zawadi,nilishika simu nikamtumia msg ya msamaha na shukrani ilienda lkn hakujibu.nilianza maisha hivo na hakeem kama mme wangu na mm mke wake.nilikaa mwezi akanipeleka kwao kabisa bagamoyo huko ambako ndiko wazazi wake wapo na wadogo zake wakike na ni mashangingi balaa,walinipokea vizuri tu lkn maisha yao ni ya Kiswahili mnoo,kila muda kusema watu na kubeza watu,nikasema hapa nimepatikana sasa,nilijitahidi kufanya kazi ukweni tulikaa wiki lkn niliona kama mwezi kwa mambo yaliokua yakiendelea pale,mana ni watu wa ngoma wavivu na maneno pia kuchambana na watu ndio zao,sikuyaweza mana mm hata kuongea sikuwa muongeaji sana,nilirudi msimbazi kwangu na kuendelea na maisha,miezi sita ilipita bila mm kushika mimba ,pia mme wangu alianza tabia ya kubana sana pesa akawa hanipi wala hanihudumii ipasavyo,nikitaka kutafuta kazi ananikataza anasema nataka kwenda kufanya umalaya basi maisha yaliniwiamagumu sana,kuna siku naweza kula mara moja tu kwa siku au nikashindia kipande cha muhogo kitu ambacho kilinifanya sasa niamze kuchakaa,pesa yote niliokua nayo niliitoa kwa matumizi madogomadogo ya ndani kitu ambacho kilikua kinamfanya mme wangu ajue mm nina pesa kumbe maskini ya Mungu sina.miezi nane ikapita mambo yakazidi kuwa magumu mme wangu akawa analalamika sana kuwa mm simzalii anataka kuitwa baba kwa nn sizai au nakunywa madawa sitaki mzalia,mm nikasema hapana mme wangu sijawahi kunywa madawa na ninywe sababu gani wakati na mm nataka kuitwa mama?akasema mm nachotaka mtoto tu nimechoka kukuona ww tu kila siku mtu mzima nataka mtoto.bai nikawa nakosa sana raha,nilijaribu kuuliza kwa wenzxangu njia ya kufanya nipate mtoto,nikawa naambiwa kuhusu kalenda basi nafata zile siku hatari namwambia mme wangu tufanye tunafanya zote lkn hola,nikawa naoneshwa majani ya kunywa nakunywa wapi,akinipa vipesa vya matumizi nabana naenda nunua vidonge wanavonishauri vya kurutubisha lkn wapiiiii,mmh mm ina mana mm ni tasa?Mbona mzunguko wnagu uko sawa tena wa siku 28 kwa nn sipati mimba sasa?nilikua nakosa sana raha,basi nikaona ni kumuachia MUngu tu.mme wangu alikua anataka mm niwe navaa kiislam kabisa hataki nionekane sijui mikono au miguu kwa watu wala kichwa hivo nikawa mtu wa hijab na nikawa nazipenda sababu ni mavazi ya heshima sana,na uzuri alikua ananinunulia japo sio mara kwa mara.lkn mpango wa kunipa pesa ukawa hakuna kabisa.katika kuishi nilipata rafiki dada mmoja alikua ameolewa na mkaka  wa bodaboda alikua anaishi jirani jina lake arafa,tulipendana baada ya kuona maisha yetu yanaendana wote wanaume majipu pesa za matumizi kwa nadra basi tukawa tunapeana kampan yy akiachiwa pesa mm sina anapika naenda kula,na mm nikiachiwa voivo hivo basi tukaivaa sana,siku moja arafa alikuja nyumbn kwangu akasema dia hivi tutaishihiv hadi lini?kwa nini tusianze biashara za hapahapa nyumbn hata kupika maandazi au kukaanga sambusa kuliko kukaa hivi we unaonaje lkn?nikasema mmh hilo ni wazo zuri my dia mm nadhani tufanye hivo lkn sasa mtaji shoga angu tutafanyaje?akasema wewe kwan unaweza kupika nn?nikasema mm mandazi nayapika malaini mazuriii sana nilifundishwa na masista lkn mama crey alikazia maarifa,akasema  sawa ww pika hivo ila mm hata sijui kupika kitu shiga angu sijui nafanyaje,nikasema ww pika sambusa za viazi nitakufundisha akasema sawa asante dia,akasema nakupa mtaji dia nakopa kwa mtu sh elf 30 mm 15 na ww 15,nikasema asante sana dia.arafa alitafuta hio pesa akaniapa,tukaenda nunua vifaa kisha tukaamshana saa 11 asubuhi kisha tukaanza kupika huku nikimuelekeza cha kufanya mana kutengeneza manda alikua anajua.,tulikanda na kuanz akupika watu wanaamka sie tuko nje na videl vyetu na vigoda maandazi yamoto tunaitia itia,majirani walitucheka hawakutaka kutuunga mkono ila uzuri tunapoishi hupita wanafunzi mara wakawa wanapita kama watano hivi arafa akasema karibuni watoto wazuri mandazi matam na sambusa tamu tena zamotooo,watoto wale wakapitia wakanunua mandazi na sambusa wakaanza kula,walinunua sambusa mbili na mandazi mawili wakagawana huku wanenda mara wakarudi wakaongeza wanasifia mnoo,ndipo watu wengine wakaskia wakaanz akuja et tuone,haikuchukua mudamandazi yangu yakaisha na sambusa zikaisha,biashara ikanoga,tukawa tunaamka na kupika tena mara ingine tunapika hadi n jioni mana wanafunzi walikua wanataka sana muda wa kutoka shuleni,maisha yakaanza kuwa na kaunafuu kidogo sikosi mboga lkn mume wangu alikua anarudi kwa kuchelewa sana na analewa sana.siku moja nilikua nafua pale nje kuna mpangaji wa chumba kinachofata baada ya chetu alihama hivo siku hio akawa anakuja mwingine,alikua ni mkaka mtanashat tu,akanisalimia kisha akaingia ndani,alitoka mdada mmoja mpangaji mwenzetu anaitwa zaitini akasema we livia huyo mkaka ndio mpangaji mpya?Nikasema sijui ila kaingia humo,akasema mmh nimeona gari apo nje ina vitu kweli kweli anaonesha mambo si haba huyo sio pangu pakavu kama sisi,nikasema mmh zai umbea tuuu khaa,akasema si utaona?kabla hatujaendelea kweli lilishusshwa kapet fln zuri la unyoya fln,likapelekwa ndani kisha sofa mbili zawatu wawili na moja la mtu mmoja,kikashushwa kitanda kilikua kimefunguliwa lkn ni bomba.mara tv mara mredio na sabufa zake,mmmh zai ananikata jicho anasema unaonaaaaaaa,mm nacheka tu,alishusha vitu vitu mm nikamaliza kufua nikaingia zangu ndani.niliendelea na kazi yangu ya kupika mandazi mpangaji mpya sasa ambaye ni jirani yangu zaidi akawa mteja wa mandazi yangu,.alikaa wiki siku moja nikiwa nje napaa samaki niko na arafa tushafanya biashara hapo akatoka ndnai kwake hapo sijui anafanya kazi gani ila siku zingine anaondoka asubuh anarudi jioni,zingine mchana anarudi sijui saa ngapi lkn siku zingine yupo tu anapiga mziki wake basi.siku hio alitoka akanisalimia nikaitika akasema samahani nauliza kama kuna mtu unamfahamu anafua nguo kwa kulipwa nina nguo anifulie,arafa akasema ndio huyo unaemuliza anafua,nilistuka nikamtizama arafa ,Yule kaka akasema ahaa basi naomba unifulie kabla hata sijajibu akaingia ndnai akatoka na suruali za jeanz nne na tshat mbili na mashat matatu soksi pia,akasema bei gani?nikasema nitakujuza zikikauka,akasemasawa basi mm natoka nikirudi nitakulipa nikasemasawa,akafunga mlango wake akatoka,nikasema we arafa una kichaa toka lini mm dobi?akasema kuanzia leo,hio ni pesa isio na mtaji shoga ebu fua tupate pesa,nikacheka,alisema acaha nimalizie kupaa samaki ww kafue,nikasema sawa,nilitoa madishi nikapekua mifukoni nikakutana n ash elf 10 not mfuko mmoja wa suruali,na suruali ingine ilikua n ash elf 5,arafa akasema unaona marupurupu hayo,nikasema nitarudisha,ilibidi ninunue sabuni nikafua zile nguo,jion alirudi nikampa pesa yake akasema niichukue ni bahati yangu kisha akanipa n ash elf 6 kama ujira wangu,nilkataa akasema naomba uchukue nikasema asante,kazi hio niliona ni bora pia hivo nikaanz akuifanya kama kazi sasa asubuhi mandazi kunzia saa tatu nafua na vile mme walikua harudi mchana kula basi burudani hapo n mm na arafa wangu.siku moja nilipumzika tu jumapili mana nilijipangia jpil ni siku ya mapumziko,mara nikaskia ngoma ngoma na shangwe nje mmh ni wapi huko?nikamtumia msg arafa akasema kuna mtu anaolewa mtaa wa pili,nikasema ndoa ya kiislam hio akasema ndio,nikasema hongera zao,nikaendelea kujipumzisha baada ya muda alikuja mme wangu akiwa na kanzu nzuri na kilemba pia na lile kama panga kiunoni nilistuka mana ndivo wanavovaa waislam wanapooa,nikasema vipi mme wangu mbona hivo,akasema nimekuja mara moja kufata nguo mm nimeoa nimemuoa esma hapo mtaa wa pili,nilistuka nikasema unasemaje?akasema ndio hivo ww si hukutaka nizalia sasa nimempa mimba esma nimeamua kumuoa mke wa pili na ataishi mtaa wa pili pale pale sitaki vurugu jua esma ni mke wangu kuanzia sasa,nilikosa nguvu huyo  esma ni mcharuko na alikua anajifanya kunipenda sana na ni mkubwa kwangu lkn alikua anajifanya kuniita dada kumbe dada enyewe ndio hii?nikasema mme wangu kwa nn umenifanyia hivo lkn?akasema bana weweeeeee usiniletee za kuleta bana weee hapo angekua analia mtoto ningeelewa sio ww jitu zima unajiliza huoni aibu?umezeeka wewe ebu nenda huko tupishe watu tunaenda honeymoon sehemu ambazo tunatia na matunda yanaonekana sio kwako namaliza nguvu nakutia mpaka naskia kizunguzungu halafu hakuna matunda mfyuuuuuu tokaaa zako,esma ndio habari ya mjini,akanisukuma nikaanguka chini akaanza kutoka na kibegi chake……

🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post