CHOMBEZO : MASSAGE ROOOM!
..............................(Chumba Cha Masaji)
Umri........................🔞
SEHEMU YA 1🌷
Jogoo alishawika mara kadhaa, akachoka na kwenda zake kutafuta michepuko, jua likachomoza mpaka likaisha la vitamin, likaja lile la kuchoma. Lile ambalo ukimuona mtu amekaa juani basi mgonjwa huyo muwahisheni hospitali!
Ndani ya chumba kimoja kikubwa kiasi, chumba Cha kawaida kabisa maeneo ya Kinondoni B!
Walikuwa wamelala watu wawili, jinsia mbili tofauti, ungewaona ungepata tabu kujua wale ni wapenzi au mtu na kaka yake.
Kidogoro Chao Cha nne kwa sita kilichoisha kwa kutumika siku nyingi, bado hakikuwafanya wagusane au wasogeleane kabisa!
Wangepata wapi huo ujasiri? kwa hili joto la Dar! Wangepata hamu sangapi ya kukumbatiana ndani ya chumba kile Cha giza, hakuna umeme wala feni ya kuwapa matumaini!
Mmoja alikuwa amelala mashariki na mwingine magharibi ya mbali, mwanaume alikuwa anakoroma lakini mwanamke alikuwa macho anahesabu Marinda ya bati ambalo mvua ikinyesha basi wanaanza kutafuta upande usiovujia!
Pembeni kulikuwa na sahani ya mihogo waliokula usiku wa jana kupoza njaa wakalalia!
Kichwani alikuwa akiwaza binti Yule ambaye kwa hakika alikuwa mrembo sana tu, lakini urembo wake ulifichwa na umaskini na maisha magumu anayopitia.
"Maisha haya mpaka lini?mbona kila siku sisi tu?" aliwaza na kuwazua mwisho akainuka na kuitupia kanga yake nyepesi iliyoandikwa maneno yaliyosomeka, 'Yarabi nikumbuke mja wako!'
Alitoka na kuchukua ndoo akaenda msalani, umaskini wake bado haukuwa sababu ya kumpotezea umbo lake matata, alikonda mwili tu ila huku nyuma mashallah alijaliwa Mwantum!
Aliingia msalani akafanya yake kisha akatoka, akashangaa anavutwa kwenye mlango wa jirani yake, ilikuwa ni ghafla sana hakuweza kujitetea akaingia ndani.
"Una nini Mchopanga?nilishakuambia sipendi Mambo yako!" alifoka Mwantum!
"Sikia binti mrembo, we unakaaje na yule boya?acha kujitesa njoo nikupe maisha mazuri eeh, cheki pesa hizi!"
Mchopanga alijipigia debe na kumuonyesha Mwantum noti za elfu hamsini!
"Mchopanga ebhu achana na mimi, niliye naye ananitosha sana!"
"Acha ushamba wewe unakuwaje na kapuku!"
"Hivi Mchopanga unajiona kweli una hela wewe, wenye hela wanakaa kwenye kijumba Kama hiki? wanalalia kitanda Cha chuma Kama hicho kuumiza mbavu zao, ebhu niache na usinizoee, nampenda sana Mkama, tena ukome kunivutia kwenye chumba chako mbwa wewe!"
Mwantum alimshushua kijana Yule Kisha akatoka na kuingia chumbani kwao, akamkuta Mkama au Mk Kama wanavyomuita ameamka na yeye anahesabu mabati na kuangalia wapi fundi alikosea!
"Mmh! mshkaji umeamka?" aliuliza Mwantum!
"Ndiyo, hapa nawaza Yule jamaa sijui hata namtafutaje sina simu!" alisema Mk!
"Duh! Na Mimi ndiyo ivyo kiswaswadu changu kimegoma tangu juzi hakiwaki kabisa!"
"Inabidi nimfuate, hiyo pesa siwezi kuiacha!"
"Kwani anakulipa shingapi?"
"25000!"
"Dah! Amka baba changamka, mie mwenyewe nina kibarua Cha kwenda kufua kwa mama Asia!"
"Duh! ngoja niamke!"
Alijikaza Mk akaamka na kutupia nguo zake ambazo zingekuwa na uwezo wa kuongea basi, zingemwambia 'Baba tupumzishe tumechoka!'
Mwantum alimuangalia mwanaume wake, ambaye wana mwaka na nusu Sasa tangu waanze kuishi pamoja,!
Anampenda sana Mk, na alikuwa radhi kuvumilia Yale maisha kutokana na jinsi mwanaume Yule alivyomsaidia wakati anahitaji sana msaada!
Mwantum alikutana na Mk stendi ya mabasi Mbezi, akiwa hana pa kwenda wala pakulala!
Mtu aliyemuita Dar akimuahidi atakuja kumpa kazi ya mama ntilie alimzimia simu siku ya tatu mfululizo!
Ndipo kijana Mk akajitolea kumchukua na kwenda kumhifadhi kwake, ambako maisha ndiyo kama hayo!
Mk na Mwantum wakijikuta wamekuwa wapenzi, basi wakaanza kuishi pamoja kuanzia kipindi hicho mpaka Sasa!
Mk alimaliza kuvaa akachukua mswaki wake na chumvi akatoka,(watoto wa kishua hawajawahi kujua kuwa chumvi ni dawa ya meno, mtupishe kidogo)
Alirudi akamuaga Mwantum ili aondoke zake!
"Oyah!mi nasepa baadae basi!"
"Poa basi!" alisema Mwantum akenda kumkumbatia mshikaji wake Kisha akampa busu zito!
"Mmh! Mwantum!Mwantum! chonde mama usije ukanirudisha kitandani na hii njaa utaniulia kifuani, na hili joto sasa!"
"Hahahahhaha! tafuta pesa baba Dar hamna joto!"
"Hahahahah! chizi wewe!"
"Na leo nataka chipsi kuku!"
"Yani hapo kwenye elfu ishirini na tano, ushakata elfu tano!"
"Bhana niletee!"
"Sawa mama! mi nikikuta ugali dagaa mbona saaafiiiiii mwanangu!"
"Usijali mshikaji wangu, we ngoja niamkie nikafue vichupi vya Mama Asia nikupikie dagaa!"
"Poa mwanangu!"
Mk aliondoka akamuacha Mwantum naye anajiandaa kutoka lakini ghafla akapata mgeni!
Mlango wake uligongwa akawahi kumpokea mgongaji maana alihisi ataubomoa muda si mrefu.
"Eeeh!nani tena jamani!taratibu utatubomolea mlango!"
"We Mwantum ni mimi Mwanaisha bhana!"
"Kumbe ni wewe chizi, haya njoo ndani!"
"We thubutu! humo ndani siingii kwa hili joto shoga yangu we toka nje Malaika wakuone!"
"Malaika gani shoga, mtoa roho au mtakafujo?"
"Wahi shoga! wahi ni dili la pesa !"
Mwantum alitoka akiufungua mlango kwa tahadhari usije ukamuangukia!
"Nambie shoga yangu maana si kwa dili Hilo la asubuhi asubuhi, mpaka ukanikumbuka shoga yako!"
"Nisikukumbuke wewe tena, shoga yangu, msiri wangu nimkumbuke nani Mwanaisha miye!"
"Aya nambie dili gani shoga!"
"Shoga yani nakuambia kwa hilo dili umaskini basi, yani utajiri uleee!"
"Weeeh! usinambie ujue nimelalia mihogo na msela wangu!"
"Tulia nikupashe shoga tulia!"
Mwanaisha alikuja na habari njema kwa Mwantum, Mwantum akashika na kiuno kupokea habari zile ambazo kwa hakika zilikuwa na mashiko sana kwake!
"Nambie shoga yangu dili gani tena Hilo!"
"Tulia nikupashe shoga yangu, wewe si unazubaa mie ndiyo Mwanaisha mtoto wa mjini!"
"Shoga nambie acha kuzunguka!"
"Ni hivi shoga Kuna kazi!"
"Kazi gani?"
"Tulia mbona una haraka Kama unaoga nje?kwanza mshahara unajua shingapi?"
"Eeh! nambie!"
"Laki moja kwa siku!"
"Mmh! ebhu subiri, ina maana kwa siku laki, kwa wiki laki saba, kwa mwezi ni, mmmhhh! we Mwanaisha kazi gani hiyo ya kuingiza milioni tatu kwa mwezi!"
"Hata tano unaingiza shoga yangu inategemea na kujiongeza kwako!"
"Mmh! shoga au tunaenda kuuza Figo, maana zina dili siku hizi!"
"We Kama uko tayari nambie, kwanza nimekuchagua wewe sababu unalipa, halafu unajua we mzuri sema tu hujapata matunzo, ukipata hela utajitunza na huyo bwana ako utamgeuza kibenteni upo!"
"Hahahahah! Mwanaisha ebhu niache Mimi!"
"Siyo nikuache, sema kama uko tayari twende au nikatafute mwingine!"
"We na wewe nani wa kukataa dili Kama hilo, hapa penyewe kwa jinsi nilivyofulia ukinambia kuuza Figo nauza fresh tu!"
"Basi jiandae mi nakuja kukupitia!"
"Powah! ngoja nikaoge!"
Mwanaisha aliondoka na kwenda zake kujiandaa akamuacha Mwantumu naye akianza kujiandaa tayari kwa kupelekwa huko kwenye kazi!
"Mmh!mbona ndoto hii, laki moja mmmh!"
Alijisemea Mwantumu muda huo kachukua maji anaenda zake bafuni na kanga yake!
Maisha magumu bado hayakuweza kuliathiri shepu lake la kuvunjia chaga, kanga moja aliyoivaa ilimfanya aache matetemeko mpaka wapangaji wenzake wakaanza kumsema, hasa wanawake.
"Huyu naye atatuibia wanaume zetu, ndiyo nini makusudi tu chefuuuuu!"
"Tena kajibinua makusudi kabisa, tuchunge waume zetu kwa kweli!"
"Mmmh! mi akimchukua wangu namroga, hiyo papuchi yake inahamia usoni!"
"Na hushindwi wewe, hahahahahha!"
Mwantumu alitoka bafuni muda huo sasa hali imekuwa mbaya zaidi, maji yalimganda mwilini na kuanzisha tetemeko lenye balaa zaidi!
Alikuwa hana habari, hakujua huku anatengeneza makasiriko yasiyo ya lazima!
Mpangaji mmoja akashindwa kuvumilia, huyu anaitwa mama Juma akasimama na kumfuata Mwantumu, kabla hajaingia ndani akashikwa mkono!
"We Mwantumu!" aligeuka maana hakutegemea wito ule!
"Abee!"
"Ndiyo nini unafanya?"
"Nimefanya nini Mama Juma!?"
"Unatokaje na kanga moja unataka kutuibia waume zetu!"
"Mmh! Mama Juma nakuheshimu hii nchi ya amani na Uhuru, we ukiona nimetoka na kanga toka na chupi!" Mwantumu naye hakuwa haba ukijaa kwenye kumi na nane zake!
"Kwahiyo una kiburi eeeh!?"
"Ebhu niache mama weeh! hamsini zako hamsini zangu, una mume nina mume tuheshimiane!"
"Unataka Vita eeh!unataka Vita eeh!"
Mama Juma aliwaka Mwantumu akamuangalia kuanzia chini mpaka juu, akampandisha na kumshusha kisha akaachia msunyo mkali huo balaa!
"Msyuuuuuuuuu!"
"Unajifanya jeuri!"
"Mi maskini jeuri, sijawahi kuja kukuomba chumvi Bibi upo, tuheshimiane ukizingua nakuzingua, nikuogope wewe unanikojoza?namuheshimu aliyeniweka ndani upo, anayenivua chupi na kunifanya atakavyo!"
"Jamani Kuna nini?" Mwanaisha alikuja akakuta vagi, na huyu ndiyo kichaa sasa!
"Si huyu kikaragosi ananipangia maisha!"
"Anasemaje tena? ebhu nambie nimemiss kupigana jamani, nimemiss kulala polisi Mimi uwiiiiiih!" alisema Mwanaisha akitaka kuinunua kesi Ile kwa gharama yoyote!
"Eti natoka zangu bafuni ananifuata, eti nyonyonyo! kanga moja nyenyenye! waume zetu nyoooo! chefuuuuuu!"
"Kumbe wana hasira za maumbile, hahahahahha!" alisema Mwanaisha!
"Hahahahahh!mbona maumbile ....maumbile kwiyooooo!"
"Mwambie aende uturuki, akafanyiwe surgery na sijui kama itakubali, maana ana umbo kama sahani ya bati!"
"Hahahahah! shoga ebhu niache miye!"
Mama Juma uso ulimshuka akakosa la kusema, maana aliona kabisa kuna kupigwa pia!
Alipoona maji yamezidi unga akaondoka akiwa na aibu maana hata waliokuwa wanamsema Mwantumu pamoja hawakuingilia, akashushuliwa yeye tu wenzie wakawa wanamcheka kichinichini!
Mwantumu na shoga yake wakaingia ndani, huko akajiandaa Mwantumu akavaa kijora chake cha msomali!
"Shoga nina tako ila wewe kiboko!",alisema Mwanaisha maana akijiangalia pamoja na umbo lake matata lakini kwa Mwantumu hafiki kabisa anaishia mbali huko!
"Hahahah! Mwanaisha bhana au na wewe una hasira za maumbile?"
"Weeeh! si bora mimi naweza kusimama na wewe tukashindana japo najua nitashindwa, sasa yule je mwenye umbo kama boksi la kiberiti!"
"Hahahahahh! shoga una dhambi wewe, Aya tuondoke!"
"Na hivi vijora vyetu jamani mpaka aibu, ila twende bhana watajua huko huko!"
"Hahahahahah!"
Waliondoka wakapanda gari za Kawe wakashukia Mikocheni B, hapo Mwanaisha akatoa simu akapiga maana hata yeye hakuwa akifahamu!
"Eeh!tumefika!" simu ilikatwa wakakaa kusubiri huyo anayewafuata ili wakaione sehemu ya kazi.
JE NI KAZI GANI HIYO?USIKOSE MWENDELEZO!
Tags
Simulizi 🔞