TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MASSAGE ROOOM 02

CHOMBEZO : MASSAGE ROOOM!
..............................(Chumba Cha Masaji)
Umri........................🔞

SEHEMU YA 2🌷
ILIPOISHIA...... 

Waliondoka wakapanda gari za Kawe wakashukia Mikocheni B, hapo Mwanaisha akatoa simu akapiga maana hata yeye hakuwa akifahamu!
"Eeh!tumefika!" simu ilikatwa wakakaa kusubiri huyo anayewafuata ili wakaione sehemu ya kazi. 

ENDELEA NAYO...... 

Walisimama kwa dakika Kadhaa wakimsubiri huyo anayewafuata kuwapeleka kazini. 

"Jamani wapendwa ni nyie?" waligeuka wakamkuta binti mmoja aliyevalia mavazi ya kileo amependeza haswa. 

"Ndiyo ni sisi, wewe si ndiyo dada Joyce?" aliuliza Mwanaisha!
"Hapana mimi ni mfanyakazi wake tu, yupo ofisini anawasubiri!"
"Ooh!sawa!"
"Nifuateni!"

Mwantumu na Mwanaisha waliangaliana kisha wakaongozana kumfuata yule binti. 

Vichwani kwao walianza kujenga taswira ya sehemu wanayoenda kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa Yule binti! Alikuwa amevaa haswa! siyo wao waliotupia nguo mwilini tu, tena vijora kama wanaenda kwenye harusi Mbagala. 

Vichwa vyao vilifunikwa na mawigi ya kariakoo, mwanzo walijiona wamependeza ila walipomuona Yule binti alivyosuka nywele za gharama wakajua hawajui. 

Safari yao iliishia kwenye jengo moja kubwa sana, hapo ndipo zilipokuwa ofisi za kazi wanayoenda kufanya, ambayo hawakujua bado ni kazi gani. 

"Karibuni sana!"
"Ahsante!",waliitikia wakataka kuvua visendo vyao vya manyoya mlangoni.
"Hapana msivue, piteni navyo!" alisema Yule dada. 

Waliingia ndani wakakutana na ofisi kubwa sana, kwenye kiti alikaa mwanamke mnene kiasi, alikua amevaa nguo za gharama, cheni za dhahabu zilining'inia shingoni, saa ya gharama na Pete ya Tanzanite. 

Kulikuwa na wadada wamekaa kwenye masofa yaliyokuwa mle ndani Kama watano na wote walikuwa wanachati na simu zao tu hawana habari na mtu!
Wote walikuwa wamependeza haswa!Nguo za gharama na misuko ya gharama ilikuwa kichwani kwao imetulia. 

"Karibuni!", alisema Yule mwanamke ambaye alionekana ndio boss pale. 

"Ahsante!" waliitikia Mwantumu na shoga yake muda huo wamekaa kwenye masofa hawajiamini amini!"

"Ka....!" alitaka kuongea yule boss lakini akasita baada ya mlango uliokuwa karibu kabisa na sofa walikokaa kina Mwantumu kufunguka!
Alitoka mwanaume mmoja akiwa anaweka vizuri tai Yake, alikuwa mbaba mtu mzima kabisa. 

"Madame Joyce!" aliita Yule mwanaume!
"Abee boss!" aliitikia yule mwanamke!
"Nimeenjoi Sana, nahisi mwili wangu uko sawa sasa!", aliongea huku anawaangalia kwa macho ya matamanio Mwantumu na mwenzake. 

"Hahahhaa!Karibu sana!"
"Hapa ni nyumbani nitarudi tena!"
"Karibu sana!"

Aliondoka yule baba, lakini mlangoni akapishana na kijana mwingine wa umri wetu tu anaingia! Alifika moja kwa moja mpaka kwenye meza ya Madame Joyce akasalimiana naye kisha akatoa waleti yake akahesabu laki nzima akamkabidhi kisha Madame akamuita binti mmoja. 

"Rose!"
"Abee Madame!"
"Muhudumie mteja!"
"Sawa!"

Yule binti mrembo aliinuka akaongozana naye Yule Kaka wakaingia kwenye ule mlango aliotoka Yule mbaba.

Mwantumu na mwenzie bado hawakujua ni kazi gani hiyo, walibaki na maswali mengi mno!

"Ooh!sorry karibuni sana!"
"Ahsante Sana Madame!"
"Naitwa Madame Joyce, nadhani mmoja wenu niliongea naye!"
"Ni Mimi hapa, naitwa Mwanaisha na huyu shoga yangu anaitwa Mwatumu!"
"Aaah!okay basi karibuni sana, mnataka kazi eeh!?"
"Ndiyo tunataka kazi!"
"Kweli mnataka kazi?"
"Ndiyo Madame!" walijibu kwa pamoja!"
"Sawa, basi vizuri hapa sisi kazi zetu ni masaji, kama unavyoona wanaume wanakuja hapa na kufanyiwa huduma!
Huduma zetu sisi sana ni kwa wanaume, hao ndiyo wateja wetu wakubwa Sana. 

Huwa tunatoa huduma hapa ofisini lakini pia huwa tuna huduma ya kuwafuata wateja nyumbani!
Mpaka hapo tunaelewana shoga zangu?",aliwauliza!
"Ndiyo Madame !"
"Basi mengine mtajifunza taratibu taratibu kwahiyo nyie Kama mnataka kazi,mtaelekezwa leo kesho mje muanze kazi!"
"Sawa Madame!"

Mwantumu na Mwanaisha walichukuliwa na mmoja wa wale wadada akawapeleka kwenye chumba kimoja wapo Kati ya vyumba vitano!
Ndani kulikuwa na vyumba vitano, walipita kwenye chumba kimoja sauti walizosikia ziliwachanganya. 

"Ashiiiihhh! ooohhhh!oooohh!" ilikuwa sauti ya mdada, Sasa wakajiuliza ile nayo ni masaji au mengineyo?

"Twendeni jamani acheni watu wafanye kazi!" alisema Yule dada anayewaongoza!
Waliingia kwenye chumba kimoja, wakakuta Kuna kitanda na Kuna mdori wa kiume ukiwa mtupu. 

"Jamani mafunzo yanaanza muwe makini sana, hii kazi inataka umakini mkubwa, ni kazi rahisi lakini siyo kila mtu anaweza kufanya! Ndiyo maana watu wanaacha wake zao wanakuja kupata huduma zetu hapa!"

Mafunzo yalianza kwa kumtumia yule mdoli basi wakaelekezwa kila kitu kwa vitendo na wakaanza kufanya kwa vitendo pia!
"Safi sana unaona mwenzako anafanya vizuri na wewe fanya Kama hivyo, eeh unamshika hapo unaminya hivi, siyo kwa kutumia nguvu, hapa tunatumia nguvu kidogo akili nyingi!", Yule dada alimsifia Mwantumu maana alionesha bidii kubwa katika kujua mambo.

Mafunzo yalichukua masaa matatu, hapo wakatoka wameelewa walau robo tatu ya ufanyaji wa masaji!
Walirudi wakamkuta Madame Jayce anakunywa zake wine taratibu hana habari!Maisha yanataka nini zaidi? pesa inagia tu kila dakika. 

"Mmeona eeh siyo kazi ngumu, pesa mnapata kirahisi Sana, kesho mje muanze kazi!"
"Sawa Madame!"

Madame alifungua droo akatoa noti nne akawapa kila mtu elfu ishirini ishirini!
"Hizo nauli eeh! kesho muwahi Sana!"
"Sawa Madame, ahsante jamani Madame!"

Waliondoka wakiwa na tabasamu pana sana, walijiuliza kama ile tu ni nauli je wakianza kazi inakuwaje?

"Shoga yani najiona Mwanaisha mwingine, watanikoma mtaani nikianza kazi watanikoma!"
"Lakini shoga hivi hukusikia yule dada aliyekuwa analia chumbani, ile ni masaji kweli?"
"Aaaaah! hayo hayatuhusu shoga tufanye kazi!"
"Lakini alikuwa anafanywa yule dada ujue!"
"Kwani kufanywa shingapi? We unafanywa na Mk anakupa shingapi?sembuse unafanywa na unapewa laki moja!"
"Mmmmmh!"

Wasiwasi wa Mwantum ulikuwa kwenye ile sauti aliyoisikia inatokea chumbani, akamueleza shoga yake ambaye hakujali wala nini, yeye alichotaka wakati ule ni kuanza kazi wapate pesa!!

Walipanda daladala na pesa zao kibindoni, matarajio ya kuuaga umaskini yalikuwa makubwa mno kwao!
"Yani shoga hapa nikianza kazi tu mwezi mmoja nahamia kwenye nyumba kali, nataka gheto langu liwe kama pa supastaa!",alijinadi Mwanaisha!
"Mmh!shoga we mwezi wote huo, mie hapo napiga wiki moja tu ya pili sipo kwenye ile nyumba, nyumba yenyewe mbaya maneno mengi!"
"Kwahiyo unamuacha Mk hapo?"
"Weeeeh! thubutu!nimuachie nani? ule mkoba wangu shoga popote ninao!"
"Inaonekana unampenda sana Mk!"
"Sanaaaa! Yule kaka tukiacha Mambo mengine, ila kanisaidia Sana, bila yeye sijui ningekuwa wapi?"
"Hahahahah! ungekuwa kwenu!"
"Kwetu sirudi!"

Walipiga story mwisho wakashushwa Kinondoni B, hapo Mwanaisha akanunua chips kuku kwa ile pesa ya nauli waliyopewa, lakini Mwantumu yeye akanunua kidari na paja lake, akapita dukani akanunua mchele akapike nyumbani!

"Kama namuona baba Chanja wako leo!"
"Muache mume wangu ale anenepe, ameshanilisha Sana!"
"Hahahahahah!wapendanao!"

Waliagana Mwanaisha akaenda kwao na Mwantum akaenda kwake! Kigiza kilikuwa kimeshaanza kubisha hodi, akaenda kununua mkaa na mafuta maana ndani kulikuwa hamna chochote!

Aliwasha jiko akaanza kupika mpaka akamaliza, bado Mk hakuwa amerudi nyumbani!
Njaa alikuwa nayo sana tu, lakini kwa upendo hakula akamsubiri Mk ambaye aliingia mida ya saa mbili usiku!
Harufu ya chakula kitamu kilichopikwa kwake ndiyo iliyompokea Mk!

"Wow mume wangu!"nalisimama Mwantum na kumlaki kijana yule ambaye alionyesha kuchoka Sana kwa kazi nzito alizofanya!"
"Karibu mume wangu!", alimpokea kwa mabusu mazito!
"Ahsante Mwantum!"
"Mume wangu ukaoge Sasa uje nimekupikia chakula kizuri sana!"
Alimuwekea maji bafuni akaenda kuoga, huku akaanza kupasha mboga!

Mk alikuwa na maswali mengi mno, chakula kilichopikwa nyumbani kilimfanya ajiulize maswali mengi mno!

"Huyu mwanamke katoa wapi hizi pesa Au kaanza kuchepuka? mmmh!nitajua tu, alisema anaenda kufana kazi ya kufua lakini ile siyo ya malipo Yale kabisa!"

Maswali yalikuwa mengi kwa Mk lakini yalikosa majibu yake, alibaki tu njia panda akijipa majibu ambayo alihisi ni sahihi kwake!

Alimaliza kuoga akarudi ndani, Mwantum akapakuwa chakula akaweka juu ya ndoo za maji, hizo ndiyo meza zao. 

"Karibu mume wangu!"
"Ahsante Mwantum lakini roho yangu itafunguka ukinambia hiki chakula umetoa wapi pesa?" 
"Mmh! jamani Mk unadhani nimetoa wapi baba?"
"Ndiyo unambie, sababu kutoka kula mihogo jana tu, na leo kula pilau kuku ni hatua kubwa mno!
"Okay!okay! Mk nimepata kazi, na huko nimeenda leo na Mwanaisha, kwahiyo tumepewa pesa za nauli ila kesho tunaanza kazi rasmi!"
"Umepata kazi???"
"Ndiyo baba!"
"Kazi gani?"
"Ni kazi ya Masaji mume wangu, na wamesema watakuwa wanatulipa pesa nzuri!"
"Masajiiiii!!" alishtuka Mk!
"Ndiyo baba!"
"Ooh! kwahiyo wamesema wanawalipa shingapi?"
"Elfu thelathini mpaka elfu hamsini kwa siku kutegemeana na wateja ila ikiwa mbaya ni kuanzia elfu thelathini!"
"Elfu thelathini kwa siku!?"
"Ndiyo, na pesa ya nauli wanatupa na chakula tunakula nje ya hiyo pesa!"
"Duh! kwani siwezi nikapata na mimi!"
"Hahahahha! mume wangu bhana pale wanatakiwa wanawake tu!"
"Mmh! kwahiyo mnaanza lini?"
"Kesho baba yangu, yaani nataka tubadilishe maisha babe nimechoka haya maisha mwenzio!"

Mk hakuwa na namna ilibidi akubali japo kishingo upande, pesa ilikuwa kama mvua isiyonyesha kabisa kwao, kila siku walilia na ukame wakahisi Mungu amewasahau!

Kitendo cha kusikia elfu thelathini kwa siku, alipagawa bila kujua kuwa hapo Mwantumu amepunguza zaidi ya elfu sabini nzima!
Pesa ya malipo ni laki kwa siku, lakini kamwambia mume wake ni elfu thelathini, wanawake Mungu anawaona.

Walikula chakula kigeni siku ile, ilipita muda sana hawajala pilau kuku, hata minyoo tumboni siku hiyo waliisikia ikishangiria kwa nguvu kwa kupokea ladha mpya, Chakula kitamu siku ile kiliwafanya wapandishe mizuka ya kufanya mapenzi, Sasa mtu unakula mihogo na maji unapataje nyege kweli jamani. 

Mk alimrukia Mwantum na kuanza kumpapasa kwa hisia sana, mikono Yake ilitambaa kwenye mwili wa Mwantum na kumfanya azivute pumzi na kuzishusha kwa nguvu sana. 

"Ooooshhhh!Mkaaaamaaaa!"
Alijipinda kama nyoka na kukiinua kiuno juu akionyesha kukubali kazi nzuri ya Mk!

Ndimi zao zilivutana na kuongea hisia kali Kati yao! Mk akautoa ulimi wake na kuutupia sikioni hapo Mwantum akafumba macho na kutamani kupiga yowe akakumbuka nyumba haijazibwa juu atawapa faida majirani!

"Mk nifanyeee basiiiii ooohh!nimerowa tayariiiiiiiii!"
"Nakufanya mke wangu subiri!",alisema Mk hapo akainyanyua mikono ya Mwantum na kuzama kwenye kwapa zake!"
"Babababababaaaa!babaaaaaa!unaniuaaaaaah!"

JE NINI KITAENDELEA ?MK FUNDI MAJUMBA ANAPANGA MATOFALI ITAKUWAJE?

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post