TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

BUSARA NA UAMINIFU (Vilimfanya Aishi Maisha Ya Kifalme)

𝐒𝐨𝐦𝐚 𝐊𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐔𝐣𝐢𝐟𝐮𝐧𝐳𝐞.
Kijana mmoja mwenye busara zake alikwenda msituni kukata kuni na shoka lake. Ghafla akiwa njiani darajani akadondosha shoka lake likadumbukia mtoni. Akasikitika sana kutokana na umuhimu wa shoka lile,

"Dah mbona hii ni kama nuksi shoka langu ndio linalolisha familia yangu sijui nitamweleza nn mama watoto nikirudi bila kitoweo."

Wakati akiendelea kuongea peke yake Mara akatokewa na Malaika kwa nyuma bila kujua na kuguswa begani kitendo kilichomfanya ageuke. 

"Nini kimekupata kijana?" 

Malaika alimuuliza yule kijana na ndipo akamuelezea kilichomkuta kuhusu shoka lake. Malaika akamuonea huruma akaingia mtoni na kutoa shoka la dhahabu kisha akamuuliza Yule kijana,

"Ni hili?" Kijana akajibu "hapana?"

Malaika akaingia mtoni akatoa shoka la Almasi kisha akamuuliza tena yule kijana,
"Ni hili?" Kijana akajibu "hapana

Malaika akaingia mtoni na kutoa shoka la kawaida na kumuuliza tena yule kijana,

" Ni hili? Kijana akajibu "ndio.

Yule Malaika akafurahi kwa uaminifu aliouonyesha kijana akaamua kumpa Yale mashoka yote matatu kisha wakaagana.

Wiki moja baadae yule kijana akapita tena pale darajani akiwa ameongozana na mkewe. Kwa bahati mbaya mkewe akateleza na kutumbukia mtoni. Yule kijana akapiga mayowe ya kuomba msaada Mara yule malaika akamtokea tena akamsimulia kilichomkuta. 

Malaika akamuonea huruma akaingia mtoni na kumtoa mwanamke mrembo mrefu mwenye nywele mpaka mgongoni na hips pana kisha akamuuliza yule kijana,

" Ni huyu? Kijana akajibu "ndio.

Malaika akakasirika baada ya kuhisi kijana amekosa uaminifu kwa mkewe. Kijana akalitambua hilo ikabidi ajieleze,

" Samahani sana ndugu yangu najua umechukia lakin Mimi nimejibu ndio nimeogopa isiwe kama siku ile nilijibu hapana Mara mbili Mara ya tatu nikajibu ndio halafu ukanipa mashoka matatu...sasa ningejibu hapana kwa huyu uliyemtoa sasa hivi ungemtoa wa pili ningejibu hapana..watatu ndio ungemtoa mke wangu...sasa nimeogopa ungenipa wake watatu mimi kipato changu kidogo sana nisingeweza kuwamudu."

Yule malaika akatabasamu akamwambia,

"Kijana una busara sana".

Malaika akaingia mtoni akamtoa mke wa yule kijana kisha akamkabidhi mkewe na kumwambia,

" Kauze Yale mashoka ya dhahabu na Almasi mtapata pesa mtaishi kama King na queen.

Yule malaika akatoweka. Kijana akamkumbatia mkewe. Busara na uaminifu vikawafanya waishi KIFALME.

𝗦𝗮𝘆𝗶𝗱.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post