TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

DAAAH! 1-4

1 - 4.
DAAAH ! 1

MTUNZI HURU

WHATSAPP 0743433005
Laula Ni binti ambae anasoma chuo Cha Biashara  mwaka wa pili, anatoka kwenye  familia yenye maisha ya kawaida pia  Ni binti anaejituma Sana alijitafutia pesa zake  kwa kutengeneza urembo wa wanawake kwa kutumia shanga. Biashara yake hio ilimpatia pesa za kukidhi nahitaji yake . Laula alipanga chumba  na marafiki zake wawili Ave na Rose , pia hapo chuoni alikuwa na mpenzi wanaependana Sana anaitwa Rahim. 

Rahimu alikuwa anaishi na Kaka yake pamoja na shemeji yake ( mke wa Kaka yake) na maisha yake yatakuwa mazuri Sana kutokana na fitna  za shemeji yake  hakutaka  Rahim apewe nahitaji anayostahiki kutoka kwa Kaka yake akidai aneenda kuwafilisi ,Kuna wakati alikosa hata nauli na kwenda chuo kwa miguu pia alipokuwa chuo kula yake ilikuwa ya shida, Mara nyingi  Laula  alikuwa akimsaidia na kujitolea Sana kwa mpenzi wake.
Kitendo Cha Laula kumuhudumia Rahim na kumpatia pesa kilikuwa kina wakera Sana marafiki zake  Rose na Ave. Siku moja Rahim alienda nyumbani kwa Laula na kumuomba amuazime pesa kidogo kwaajili  ya kununulia dawa kwani alienda kupima  lakini kapungukiwa pesa ya dawa. Laula hakuona tatizo aliingia ndani akachukua pesa na kumpatia kiasi Cha  shiling 20000
" Nashukuru Sana mpenzi wangu, Yani unanisevu Sana kwenye shida zangu.
" Usijali mpenzi wangu kwani hata Mimi sipendi kuona unapata shida.
" Kuna wakati najisikia vibaya , Mimi ndio natakiwa kukuhudumia lakini kwangu imekuwa kinyume.
" Usijali mpenzi ipo siku kila kitu kutakuwa sawa haya ni mapito ya muda mfupi kikubwa unatakiwa kuwa mvumilivu na kuweka juhudi kwenye masomo. Mara Ave alipita Kati Kati yao na kuwatenganisha alipofika mbele aligeuka kumuangalia Rahim Kisha akatingisha kichwa kana kwamba anamsikitikia. Rahim na Laula hawakuongea kitu kwasababu walijua wakiongea kinachofuata Ni Rahimu  kudhalilishwa. Ave alienda anakoenda na baada ya dakika chache alirudi na kupitia katikati yao huku akisema
" Huu Sasa Ni ubinti , wanaume wanaojitambua wanatafuta kazi kwaajili ya kuhudumia wanawake zao Ila wengine wapo milangoni  kuomba pesa kwa wanawake wao . Rahim alijisikia vibaya akamuangalia  Laula usoni .
" Mpenzi achana nae tuondoke hapa. Laula aliushika mkono wa Rahim wakaondoka.
" Nisamehe kwa kile alichokisema rafiki yangu. Rahim alishusha pumzi kisha akasema 
"Siku zote ukweli huwa unauma Ila alichoongea kina ukweli.
" Lakini hatusikilizi wanachosema kipaombele chetu Ni kupendana  siku zote.  Rahim alimuangalia Laula Kisha wote wakatabasamu 
" Asante Sana mpenzi wangu kwa kujielewa Hali yangu, nakupenda Sana.  
" Mimi Ni zaidi ya Sana. Walitembea huku wakiongea mpaka wakafika kituo Cha daladala. Waliagana Rahim alipanda daladala na Laula  alirudi nyumbani.  Alipoingia ndani Rose na Ave walimpokea kwa maneno.
" Laula unatutia aibu , hivi utamuhonga yule mwanaume mpaka lini? Kwani yeye hawezi kujitafutia. Alisema Ave
" Kwani Nani kawaambia kuwa alifuata pesa ? Ave na Rose walicheka  kucheki Cha umbea
" kwani hatujui kila akija anashida ya pesa, na utapofuka hayo macho kwa kufuma shanga alafu pesa unampa yule boya wako. 
" Yani nakushangaa Sana Laula , mbona wewe Ni mrembo na unaweza kuwa na mwanaume  mwenye pesa zake , wewe unatakiwa kuhudumiwa na sio kuhudumia acha ushamba.
" Wapenzi nimewasikia mlichokisema Ila naomba mniache na mpenzi wangu  mbona Mimi siwaingilii kwenye mapenzi yenu na madanga yenu.
" Khaaa , ngoja tukuache huenda sio akili yako umerogwa wewe.

Siku zilizidi kwenda na penzi la Laula na Rahim lilizidi kushamiri ,waliziba masikio hawakusikiliza watu wanasema Nini. Hatimae walifanya mtihani wao wa mwisho wakamaliza chuo.  Laula na rafiki zake waliamua kutafuta nyumba kubwa iliyokuwa na vyumba vitatu , sitting room , jiko na choo. Kila mmoja alikuwa na chumba chake Cha kulala lakini sehemu nyingine walitumia pamoja. Kila mmoja alitafuta shughuli za kufanya kwaajili ya kulipa Kodi  na Mambo mengine huku waliendekea kutafuta kazi.

Siku moja Rahim alimpigia simu  akamwambia .
" Mpenzi uko wapi?
" Nipo nyumbani.
" Tunaweza tukaonaba Ile sehemu tunayokutana ?
" Sawa.
" Naomba iwe Sasa hivi Kuna Jambo nataka tuongee Ni muhimu Sana.
" Sawa , natoka hapa mida hii hii.  Baada ya kukata simu Laula alichukua pochi yake akatoka na kwenda kwenye bustani moja ambayo wanaoenda kwenda kukaa na kuongea Mambo yao. Laula alikaa karibia saa moja akimsubiri Rahim, kila alipompigia simu na kumuuliza kafika wapi alimwambia yupo karibu kufika. Mwisho Laula alikata tamaa akataja kuondoka, muda huo huo Rahim alifika akiwa kachoka .
" Vipi mbona umeniweka hivi?
" Nisamehe mpenzi ...
" Na mbona umechoka hivyo.
" Mbona nipo sawa. Laula alimuangalia akatambua kwanini Rahim kachekewa na amefika pale akiwa kachoka .
" Umekuja kwa miguu? Tuachane na hayo. Rahim alijaribu kuficha lakini Laula alimuona huruma .
" Subiri nakuja. Laula alinyanyuka na kwenda kununua chupa kubwa ya maji na juice mbili. Aliporudi alikaa akatoa chupa ya maji na kuifungua Kisha akampatia 
"Shika kunywa. Rahim alipokea na kuyanywa Yale maji moja kwa moja mpaka yalipobakia kidogo akaweka kopo chini Kisha akasema 
" Nashukuru Sana.
" Huna haja ya kumshukuru , niambie ulitaka kuniambia Nini?
" Nimepata kazi lakini Ni nje ya mkoa ..... Laula kusikia hivyo alifurahi Sana 
" Asante Mungu amesikia kilio chetu, nilikuwa nikikuombea usiku na mchana. Hongera Sana mpenzi wangu .
"Asante. Rahim aliitikia  lakini ghafla alionekana kuwa na huzuni.
" Vipi Tena mbona hivyo?
" Laula naona hata aibu kuongea Ila nitafanyaje .....
" Umeanza lini kumuona aibu mpenzi wako na usiponiambia Mimi utamwambia Nani?
" Sina pesa ya nauli  , nimeongea na Kaka lakini hajali kabisa . 
" Usijali mpenzi , inahitajika kiasi gani?
" Laki moja inatosha pia nakuahidi nitairudisha.
" Kama utairudisha Basi rudusha zote ambazo umetumia. Rahim alitabasamu Kisha akasema 
" Sawa Tena nitairudisha zaidi. Laula alitabasamu pia .
"Twende ATM nikatoe. Waliondoka na kwenda kutoa pesa Kisha akampatia laki mbili.
" Hiyo nyingine utakuwa nayo Kama akiba maana hujui unakoenda. Rahim alimshukuru Sana Laula  kwani amekuwa mkombozi wake kila anapokuwa na shida na Laula alimsaidia kwa moyo mmoja licha ya rafiki zake kumkejeri  na kumsema vibaya.
Rahim alisafiri  mpaka mbeya  alipokelewa na mwenyeji wake na kupekekwa kwenye apartment alivyokuwa kaandaliwa na kampuni.  
" Bwana Rahim hii ndio sehemu itakavyokuwa unaishi.
" Nashukuru Sana .
" Kwakuwa umechoka kesho utapumzika, kesho kutwa asubuhi  dereva atakuja kukuchukia  kwaajili ya kuripoti kazini.
"Sawa.
" Ngoja nikuache upumzike. Yule mwenyeji wake aliyempokea aliondoka,  Rahim alizunguka kuikagua Ile nyumba uku akiwa na furaha 
" Sasa shida zimeisha nitamchukua Laula wangu nije kuishi nae hapa.
 
Baada ya hapo Rahim  alienda kuoga,wakati anatoka bafuni simu yake ilianza kuita alipoangalia aliona  Ni Laula alitabasamu na kunipokea 
" Niambie mpenzi 
" Safi , mbona kimnya huniambii Kama imefika au bado upo safarini?
" Nimefika muda sio mrefu ,hata hivyo  nilikuwa nawaza kukupigia.
" Sawa,imefika salama?
" Ndio , nimefika salama Ni uchovu tu wa safari.
" Pole 
" Asante.
" Ngoja nikuache upumzike tutaongea kesho. Baada ya kuagana walikata simu Laula alinyoosha mikono juu kushukuru Mungu kwa kumfikisha salama mpenzi wake pia hakuacha kuendelea kuomba Dua za mafanikio kwa Rahim. 
Ave alimsikia alivyokuwa akiomba akisubiri mpaka alipomaliza maombi  alafu akamwambia
" Ukiwa unamuombea mafanikio usisahau kumuomba Mungu akutunzie asije kugeuzia gia angani.
"Una maana gani kusema hivyo?
" Kwani hujui kuwa masikini akipata.....

DAAAH 2

MTUNZI HURU

WHATSAPP 0743433005

LAULA  hakuona haja ya  kujibishana na ave aliingia chumbani kwake  akaenda kulala .

Siku zilienda Rahim alianza kazi , akajituma kwa bidii ili kutimiza malengo aliyopanga.   kwanza ilikuwa kunisaidia familia yake iliyokuwa na uwezo mdogo pili kufunga ndoa na mwanamke anaempende na kumthamini aliyemvumilia kwenye shida zake . kila wakati alikuwa akiongea na laula, waliahidiana vitu vingi kwaajili ya maisha yao ya badae pia kila mwisho wa mwezi Rahim alipopokea mshahara alitoa kiasi Cha pesa na kumtupia Laula, hakuweza kusahau fadhila alizomuonyesha  na Laula alizidisha maombi ili azidi kufanikiwa . Kwa muda wa miezi michache aliyofanya kazi   maisha ya Rahim yalibadilika mno, alikuwa mtu mwingine kabisa na sio yule aliyedhalauliwa kwa kukosa hata elfu moja ya nauli.

Ulipita mwaka mmoja Rahim na Laula bila kuonana  zaidi ya kuwasiliana kwenye simu . Siku moja Laula alipiga Sana simu ya Rahim lakini haikupokelewa , alijaribu Mara nyingine Hali ilikuwa ni Ile Ile . Siku hiyo Laula alishinda hana Raha. Wenzake walipomuuliza tatizo  hakuweza kuwaambia kinachomsumbua alijua lazima wangeongea maneno ya kumuuliza .
" Laula Kama unaumwa si useme kuliko kutukalia kimnya.
" Siumwi jamani Mimi nipo sawa kuweni na amani.
" Hiyo amani inatoka wapi wakati mwenzetu umejikunyata Kama kifaranga kilichonyeshewa na mvua. Alisema Ave
" Au bwana shemeji kakuvuruga? Rose aliuliza huku akimvutia kwake na kutaka kumkumbatia
" Jamani niacheni mkiwa mnaongea  hivyo naona Kama vile mnazidi kunichanganya.
" Hahaha imeisha hiyo nimeshaijua hiyo utakuwa inamuhusu Rahim, niambie shoga yangu Rahim lakufanya nini?
" Hapokei simu zangu, na sio kawaida kufanya hivyo.
" Kwahiyo wivu unakusumbua, unahisi atakuwa na mwanamke? Alisema Rose. Ave akadakia
" Itakuwa kwani wanaume Wana maana.
" Sio rahisi kunisaliti , anaweza kuwa kapata tatizo. 
Rose na Ave waliangaliana Kisha wakacheka , Rose akamwambia
"Ngoja nikukumbushe kitu mwali wangu, kwenye hii dunia hakuna Cha peke yako alafu usisahau kuwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka. Maneno ya Rose kama yalimuingia Laula.
" Sasa mnanishauri nifanye Nini?
" Funga safari mfuate ukaangalie mazingira anayoishi.

Laula aliubeba huo ushauri na kupanga kuufanyia kazi. Kesho yake asubuhi Rahim alimpigia simu Laula.
" Samahani mpenzi Jana nilikuwa bize Sana na kazi nikashindwa hata kushika simu.
" Hata ulipotoka kazini ulishindwa kunitafuta?
" Nilirudi nikiwa nimemchoka Sana  hivyo nilifika na kulala tu.
" Oooh pole mpenzi.
" Asante.
" Rahim nataka kuja kukutembelea. Alisema Laula na Rahim alinyamaza kimnya kwa muda .
" Mbona kimnya hunijibu?
" Ahaaaa sawa Hilo halina shida kabisa Tena nitafurahi Sana ukija maana nimekumiss Sana, umepanga kuja lini?
" Hata kesho naweza kuja.
" Kwa kesho hapana , nipe muda wa kufanya maandalizi ya kukupokea pia nipunguze kazi ili ukija nipate muda mzuri wa kuwa na wewe mpenzi.
" Sawa Ila isichukue muda mrefu.
" Haitachukua muda mrefu sababu hata Mimi nimekumiss Sana kichuna wangu. Baada ya kumaliza kuongea alikata simu na kushusha pumzi na kujilaza kitandani, Mara mlango wa chumbani ulifunguliwa akaingia dada mmoja aliyekuwa kajifunga upande wa kanga kifuani kwake , yule dada alienda mpaka alipolala  Rahim na kujilaza juu yake na Rahim alitabasamu na kunyanyua kichwa chake akagusanisha lips zake na za yule dada na kumbusu. Yule dada akamuuliza 
" Umeshaoga?
" Bado ,nitawezaje kuoga peke yangu bila wewe?
" Lakini nimeshaoga nilipoamka na chai ipo tayari.
" Turudi tukaoge wote alafu tutaenda kunywa chai . Walinyanguka pale kitandani wakaenda bafuni kuoga.

 walipomaliza kuoga walienda kunywa chai, walionekana kuwa na furaha na mwenye mapenzi ya Hali ya juu.
Rahim alionekana kutekwa na penzi la Faith na kuanza kumsahau  Laula  mwanamke aliyetoka nae mbali.

Laula kila alipomwambia swala la kwenda kumtembelea Rahim alikuwa hakosi sababu. Hili lilizidi kumnyima furaha Laula.

  Baada ya miezi  miwili Laula aliamua kufanya maamuzi alienda kukata tiketi na kwenda mbeya bila kumwambia  Rahim. Alipokuwa kwenye Basi alikaa Siti moja na dada mmoja ambae alikuwa mcheshi Sana , huyo dada hakuwa mwingine alikuwa ni Faith.
" Wewe ni mwenyeji wa mbeya? Faith alimuuliza  na Laula akamjibu
" Hapana , sijawahi kufika hii ndio Mara yangu ya kwanza kwenda huko, wewe Ni mwenyeji wa wapi?
" Mimi mwenyeji wa mbeya  nimetoka kuchukua mizigo yangu kwaajili ya biashara .
" Oooh kumbe wewe nimfanya biashara?
" Ndio Nina  duka la nguo na vipodozi.
" Hongera Sana.
" Asante. Waliendekea kuongea na 
Kila walipopita Faith alikuwa alimwambia Laula sehemu waliyofika hiyo ilimsaidia kujua Yuko wapi. Majira ya saa kumi na mbili jioni walifika stendi ya Mbeya . 
" Hapa ndio stendi ya Mbeya mjini, karibu Sana  Mbeya.
" Asante. 
Walishuka kwenye Basi  Laula akaenda kukaa sehemu na kumpigia simu Rahim, wakati huo Rahim alikuwa anaenda stendi kumpokea Faith. Rahim alipokea simu 
"Niambie mke wangu .
" Safi hubby, Sasa Mimi  nipo hapa stendi unaweza kunielekeza kwako ili nije?  Rahim alishituka na kuuliza 
" Unasemaje?
" Nipo stendi ya hapa Mbeya , nielekeze unaishi ni wapi au njoo unichukue .
" Laula hebu acha kunifanyia hivyo Basi.
" Sikutanii ....
" Aaaah Sasa unakujaje bila kunipa taarifa?
"Nimeamua kukufanyia surprise.
 Rahim alipatwa na kigugumizi hakujua aongee Nini ili kumkwepa Laula , wakati anaongea na Laula , Faith alikuwa kasimama pembeni alipiga simu ya Rahim wakati huo ilikuwa inatumika anaongea na Laula.
" Laula sijui hata nikwambie Nini ili unielewe mpenzi.
" Kwani Kuna tatizo gani?
" Nipo nje ya mji, sijui Sasa tunafanyaje.
" Kwani unarudi lini?
" Nitakaa huku kwa siku mbili.
" Oooh, lakini hakijaharibika kitu mpenzi nitakaa hotelini mpaka utakaporudi Nia yangu Ni kukuona mpenzi wangu.
" Sawa mpenzi nashukuru Sana kwa kunielewa, Basi ukifika hotelini  utanijulisha.
" Sawa. Baada ya kukata simu  Rahim alimpigia Faith.
" Uko wapi mpenzi?
" Nipo stendi nakusubiri, unajua nimechoka na safari.
" Najua mpenzi lakini Mambo yameingiliana  nimepigiwa simu na boss anataka twende Mbalizi  Kuna watu anataka kwenda kufanya nao biashara.
" Aaaah Sasa ndio nini Mimi nimekaa hapa muda wote huo nakusubiri alafu  kumbe hauji.
" Nisamehe mpenzi sikujua Kama hiki lingetokea Ila nakuahidi  kesho  tutakuwa pamoja.  Faith alikata simu  na kufikiria  kwenda kutafuta usafiri wa kumfikisha  nyumbani kwao Mara akamuona Laula akiwa kakaa  pembeni yake.
" Laula kumbe upo hapa? mwenyeji wako hajafika kuja kukupokea?
" Ndio ,  kaniambia yupo nje ya mji....
" Oooh pole, Sasa itakuwaje?
" Nitaenda hotelini.
" Sikiliza Laula Mimi na wewe tumeshakuwa marafiki Sasa sioni haja ya wewe kwenda kupoteza pesa kwaajili ya kulipa hotel wakati Mimi rafiki yako nipo na Nina sehemu ya kukupa hifadhi.
" Unamaanisha unataka twende wote nyumbani kwako?
" Ndio.
" Laula alisita kwanza  maana hakumjua vizuri Faith walikitana tu kwenye gari.
" Usiwe na wasiwasi , siwezi kukufanyia kitu kibaya.
 Laula alikubali  kuondoka na Faith wakaenda kupanda taxi na kuelekea maeneo Airport huko ndipo anayoishi  Faith pamoja na wadogo zake
DAAAH 3

MTUNZI HURU

WHATSAPP 0743433005

Walifika kwenye nyumba anayoishi Faith walipokelewa na mabinti wawili  waliokuwa kubeba mizigo yao na kuingiza ndani.
" Laula karibu Sana  jisikie upo nyumbani kuwa na amani.
" Asante. Walifika sebleni wakakaa .
" Nyie wasichana hebu njooni.  Faith aliwaita wale mabinti waliowapokea.
" Laula , Hawa Ni wadogo zangu, huyu ni Sara  mdogo wangu anaenifuata na huyu Ni Tumaini  Ni dada wangu wa kazi. 
" Nashukuru kuwafahamu.
" Mabinti huyu ni rafiki yangu anaitwa Laula.
" Karibu dada Laula jisikie upo nyumbani.
" Asante Sana.
" Sasa nendeni mkatuandalie chakula njaa zinatuuma Sana . Faith aliwaambia wakina Sara . Sara na  Tumaini walienda jikoni , Faith akamwambia  Laula.
" Twende nikakuonyeshe chumba Cha kupumzika  alafu ukaoge ili kupunguza uchovu.

Walinyanguka na kwenda upande wa vyumba wakaingia kwenye chumba Cha wageni kilichokuwa kimetandikwa vizuri na kila kitu lilikuwa kwenye mpangilio mzuri. Utapumzika hapa  na hapa Ni chooni.
" Nashukuru Sana dear.
" Ok, ngoja na Mimi niende nikaoge. Faith alitoka na kuelekea chumbani kwake . 

Wote walioga baada ya kumaliza walitoka sebleni kwaajili ya kupata chakula. Laula hakuchangamka Sana kwaajili ya ugeni .
" Laula mbona hauli, unamuwaza shemeji? Faith alimwambia Laula akatabasamu
"Hapana .
" Najua unafikiria kuwa muda huu mngekuwa pamoja  mkifurahi lakini usijali yupo kwenye utafitaji siku sio nyingi mtaonana.
" Sawa bwana , Ila chakula kitamu bwana nimekipenda mnoo. Faith aliwaangalia Sara na Tumaini Kisha akauliza 
" Wasichana mmesifiwa, kwani Nani kapika?
" Tumepika wote. Alijibu Sara.
" Nina mashaka na wewe uliejibu haraka sidhani Kama umepika.
" Kwani unanionaje dada, Mimi ndio mpishi.
" Hamna kitu Kama hicho wewe Cha uvivu uingie jikoni kabisa utupikie. Waliendelea kula huku wanataniana. Baada ya hapo kila mmoja alienda chumbani kwake kulala. Faith alikuwa chumbani kwake kajilaza huku anachat na Rahim pia Laula alikuwa chumbani kwake nae alikuwa anachat na Rahim.
Rahim aliwajibu wote wawili bila kujua kuwa wanawake hao wapo pamoja.

Kulipokucha waliamka na kupata pamoja kifungua kinywa pamoja.
" Laula shoga yangu nilitamani leo twende wote dukani kwangu lakini Mambo yameingiliana , sitakwenda dukani naenda kuonana na shemeji yako.  Laula alitabasamu alafu akasema 
" Usijali kipenzi wewe nenda tu.
" Asante kwa kunielewa Ila kabla haujaondoka nataka ninikutanishe nae.
" Sawa usijali.  Faith aliondoka  huku nyuma Rahim alimpigia simu Laula   ili kumjulia hali.
" Vipi mpenzi umeamka salama?
" Ndio nipo salama hofu yangu kubwa Ni kwako.
" Nipo salama pia, nilikuwa nataka kukupa habari njema ....
" Habari gani?
" Kesho narudi hivyo Basi nitakuja kukuchukia ulipo. Maana Sina muda mrefu wa kuwepo hapa natakiwa kusafiri tena kikazi safari hii nitakwenda Tabora.
" Sawa , hata nikiwa nawe  kwa siku mbili itakuwa Ni furaha kwangu.
" Hata Mimi hivyo hivyo , nimekumiss Sana mpenzi.  Baada ya kumaliza maongezi yao walitakiana siku njema. Siku hiyo Rahim alitumua muda wake  kufurahia mapenzi na Faith. 

Faith alirudi nyumbani akiwa nafuraha  walikaa na Laula na kuanza kummwagia sifa mpenzi wake na Laula alimpongeza kwa kuwa na mwanaume anaemjali na kumuonyesha mapenzi ya dhati. Pia Laula alimpa habari za kirudi kwa mpenzi wake hivyo kesho anaweza kuondoka.
" Jamani huyo Shem angekaakaa kidogo , unajua nimeshakuzowea mwenzio. Faith alimwambia Laula
" Mmm wewe unafurahia kukutana  mpenzi wako acha na Mimi nikamuone mpenzi wangu unajua Ni mwaka Sasa sijamtia machoni zaidi ya kusikia sauti yake kwenye simu.
" Sawa Ila natamani kesho ifike haraka nimuone maana Nina shauku ya kumjua.
" Usijali kikubwa tuombe uzima.
Kesho yake kulipokucha waliliamka mapema na kupata kifungua kinywa  Kisha wakakaa kumsubiri Rahim.
" Hivi ulisema shemeji yangu anaitwa Nani vile? Faith aliuliza
" Rahim. Faith hakuweza kushituka maana hakuwa anajua mpenzi wake  jina lingine  anaitwa Rahim alimtambua kwa jina la Nassibu  jina ambalo alitumua kazini pia kwenye cheti chake Cha kuzaliwa Hilo la Rahim Ni jina lake la pili ambalo wanamuita watu wake wa karibu hasa nyumbani kwao na mtaani Kwao
" Ok Sasa  ngoja tumsubiri, alafu nikuombe kitu mpenzi , Jaribu kuongea na shem uweze kuhamia huku nimeipenda Sana kampani yako. Laula aliachia tabasamu Kisha akasema 
" Nitaongea nae maana hata Mimi sipendi kukaa mbali nae. Faith alifurahi  Sana kusikia hivyo.

Laula aliendelea kuwasiliana na Rahim huku alimuelekeza sehemu na mtaa alipo. Laula alikuwa akimpa maelezo kupitia wenyeji wake.  
Rahim alitoka na gari yake  alianza safari ya kwenda kumchukua . Wakati wakiwa wanamsubiri Rahim kwa hamu simu ya Faith ikaita.  Alipokea na kuongea alionekana kuongea maswala ya biashara  anazofanya, baada ya kumaliza kuongea akamwambia Laula.
" Kipenzi siwezi Tena kuendelea kumsubiri Shem , nimepigiwa simu mzigo wangu umefika inabidi niende nikaufuatilie.
" Sawa kipenzi kwakuwa bado nipo nitapanga siku tukutane uweze kufahamiana na Rahim.
" Itakuwa vizuri hata Mimi nitafanya mipango ninikutanishe na Nassibu.
" Sawa.
Waliagana Faith akachukua pochi na kuondoka.

Baada ya nusu saa Rahim alifika nje ya nyumba ya Faith akampigia simu  Laula na kumwambia atoke ili waweze kuondoka. Kwakuwa Faith hakuwepo Laula hakuona haja ya Rahim kuingia ndani aliamua kutoka na begi lake huku akiwa anasindikizwa na  Tumaini. Rahm alipomuona Laula aliachia tabasamu , Laula alimfuata na kumkumbatia.
" Siamini Kama nimekuona Tena mpenzi. Alisema Rahim
" Nimefurahi Sana kukuona....
" Ok tutaenda kuongea nyumbani. 
Rahim alichukua begi la Laula na kulipabdisha kwenye gari Kisha wakaagana na Tumaini na wao wakaondoka.

Hatimae walifika nyumbani kwa  Rahim, Laula alifurahishwa na mapokezi aliyopokelewa na mpenzi wake pia alifurahishwa na maisha alivyokuwa akiishi Rahim.
" Nimefurahi Sana kuona umetimiza malengo yako. Raula alimwambia  Rahim
" Asante , haya yote Ni majibu ya Dua zako nzuri siku zote ulikuwa ukiniombea mema na mafanikio. Alafu  bado malengo yangu hayajafanikiwa. Laula alimuangalia alafu akamuuliza 
" Unataka Nini tena?
" Bado kupata pambo la nyumba yangu, la kunifanyia niwe mwanaume nilie kamilika. Laula alitambua alichomaanisha  alitabasamu.

Wiki ya mwanzo Rahim alimuonyesha Laula mapenzi Moto Moto, aliwajibu Kurudi kutoka kazini pia kila alipokuwa anatoka kazini akinunua zawadi kwaajili yake. Laula alikuwa anafurahi Sana na kumsifia kuwa Ni mwanaume Bora kwake pia alipoongea na Ave na Rose aliwaeleza Rahim Ni mtu wa aina gani pia Ni mwanaume sahihi Sana kwake .

Baada ya siku kusogea Rahim alianza kuchelewa kurudi nyumbani na alikuwa akifika nyumbani 
hakuwa na furaha alikuwa anasema anachoka Sana kwasababu ya kazi nyingi za kutwa nzima.
Siku zote hizo Rahim alikuwa alikutana na Faith hotelini. Alikuwa akimdanganya Faith kuwa ndugu zake wamekuja kumtembelea  hivyo hawezi kumpeleka nyumbani kwake  kabla hajampeleka nyumbani kwao kumtambulisha.

Siku moja  Rahim alirudi nyumbani majira ya saa Saba usiku na kumkuta Laula amekaa sebleni huku akiwa kashikilia simu yake.
" Rahim umetoka wapi saa hizi?
Laula aliuliza , Rahim hakumjibu aliingia chumbani akakaa kitandani akaanza kuvua viatu
" Rahim nakuuliza nijibu?
" Kwani wakati natoka asubuhi nilikuaga naenda wapi?
" Uliniambia unaenda kazini, lakini mpaka muda huu ulikuwa kazini?  Rahim alimuangalia Laula kwa jicho baya alafu akamwambia 
" Sitaki kupelekwa pelekwa Mimi Ni mtu mzima na Sasa nafanya kila ninachotaka kwa pesa yangu kwahiyo naomba usinipande kichwani. Aliongea Rahim kwa hasira
" Kwahiyo Kama unapesa ndio unikosee ....
" Kama unaina nakukosea njia nyeupe unaweza kwenda kuendelea na maisha yako,  tusisumbuane bwana. Laula alibaki mdomo wazi hakuamini Kama Rahim anaongea maneno Kama yale.
DAAAH 4

MTUNZI HURU

WHATSAPP 0743433005

" RAHIM ni maneno gani unayoniambia? Laula aliuliza huku akiwa analia
Rahim hakumjali alifungua vifungo vya shati na kulivua Kisha akaingia bafuni kuoga, Laula alikaa kitandani akiwa anatafakari maneno aliyoambiwa na Rahim.
Rahim alitoka bafuni akavaa nguo zake za kulalia kisha akapanga kitandani na kujifunika duvet hadi kichwani huku akiwa kageukia pembeni, Laula alishindwa kupata usingizi  alimuangalia huku akiendelea kulia wakati mwenzie akiwa anakiroma

 Kulipokucha  Laula aliamka mapema akaandaa kifungua kinywa kwaajili ya Rahim. Rahim alipomaliza kujiandaa akawa anataka kuondoka
" Nimekuandalia chai. Laula alimwambia
" Sihitaji. 
" Rahim inamaana umenikasirikia?
" Hivi unajua  nikikasirika ninavyokuwa?
" Sasa mbona unanifanyia hivyo?
" Wewe ndio sababu, hata hivyo Sina muda wa kuuongelea hayo Mambo kwanza  nachekewa kazini.  Rahim alifungua mlango akaondoka akamuacha Laula akimuangalia kwa huzuni
" Huyu mtu mbona kabadilika hivi, inamaana maswali niliyomuuliza Jana ndio sababu ya kunikasirikia?
Laula alijiuliza maswali mengi bila kupata majibu yaliyokamilika

 Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo matendo ya Rahim yalizidi kumvuruga  Laula  na kuzidi kumnyima furaha na amani. Lakini alinipa matunaini na kusema yatapita na kila kitu kitakuwa Sawa kwa sababu wametoka mbali na wamevumiliana kwa mengi hivyo Mambo madogo Kama yale hayawezi kuteteresha penzi Lao. Siku moja ilikuwa siku ya ijumaa jioni Rahim alirudi kutoka kazini akapituliza moja kwa moja mpaka bafuni , wakati anaoga simu yake ilikuwa inaita  Laula alisogea na kuangalia Nani aliekuwa anapiga  akakutana na jina lililo save  my darling . Laula alijua huyo ndio kidudu mtu aliyeingilia penzi lao alipotaka kupokea Rahim alitoka bafuni na kumkuta akiwa kashika simu yake. Alimfuata haraka akamnyang'anya Ile simu
" Rahim huyo uliem save my darling Ni Nani?
" Mbona Kama unanifuatilia Sana, Laula Mimi nimtu mzima naelewa ninachokifanya. Alafu kwa ushauri tu Kama unataka kuepukana na maudhi madogo madogo Kama haya unatakiwa kuacha kunifuatilia . Laula hakuwa na lakusema  alimuangalia tu. Rahim alivaa nguo zake haraka akaondoka bila kuaga. Laula alikaa chini na kuanza kulia huku akisema 
" Kwahiyo miaka yote nilikuwa mpumbavu kwa kumthamini na kumvumilia? Kumbe hakuwa na mapenzi ya kweli kwangu. Laula alilia Sana na kukutia mno kwa kupoteza nguvu zake pamoja na muda wake kwa mwanaume asiekuwa na shukrani.
Rahim hakurudi nyumbani kwa muda wa siku mbili, weekend yote alitumua kufurahia pamoja na Faith. Siku ya jumapili  usiku Rahim alirudi na Wala hakuwa na story na Laula , alipanda kitandani .
" Rahim tunaweza kuongea? Laula alimuuliza
" Nimemchoka Sana nataka kupumzika. Alijibu Rahim alafu akamgeukia upande wa pili na kujifunika vizuri. Laula hakuweza kupata usingizi , baada ya kufikiria Sana alipata wazo la kuchukua namba ya huyo mwanamke wa Rahim. Alichukua simu ya Rahim  akachukua zile namba na kuhamishia kwenye simu yake badae alikunja kushitukakuona zile namba zipo kwenye simu yake Tena Ni namba za rafiki aliyempokea  kwenye huo mji. Faith.
Laula hakuamini alienda kuangalia Whatsapp kwenye profile picha aliyoweka  na kufananisha na yake akakuta zipo sawa.
" Mbona Kama Ni miuziza hii unawezekanaje  faith anipokee alafu awe mpenzi wa Rahim?
Usiku ule ilipita Laula akiwa amewaza Mambo mengi Sana pia alikuwa amepanga Nini Cha kufanya.
Kulipokucha  Rahim aliondoka akaelekea kazini. Laula alipata nafasi ya kuongea na Faith akamuomba Kama itawezekana jioni aende akamtembelee alipo. Bila hiyana  Faith alikubali  na Laula akamuelekeza sehemu alipo lakini hakumwambia Ni nyumba gani. Haikuwa ngumu kwa faith kwasababu Ni maeneo aliyozowea kwenda .

Jioni baada ya kumaliza kazi zake faith alifungua duka na kwenda Kule alikoekekezwa na  Laula . Alimkuta Laula amesimama kwenye genge moja akimsubiri, Laula hakuonyesha tofauti yoyote alimchangamkia na kufurahia uwepo wake .
" Karibu Sana kipenzi.
" Asante.
" Ok Sasa ngoja twende nyumbani. Laula alimpokea pochi Faith wakaongozana huku waliendelea kuongea mpaka walipofika getini kwa Rahim  ndipo Faith akashituka.
" Wewe hebu subiri kwanza, hapa ndipo ulipofikia?
" Ndio karibu. Faith aliingia lakini alionekana kuwa na wasiwasi Sana.
" Usijali bwana karibu ndani. Waliingia ndani Laula akaandaa vinywaji wakaanza kunywa. Laula alichukua simu yake na kumuonyesha Faith picha ya Rahim.
" Huyu ndio mwanaume niliemfuata huku, nikimaanisha ndio mpenzi wangu.
" Mbona huyu Ni mpenzi wangu Nassibu?
" Anaitwa Rahim.
" Laula acha kunichanganya huyu Ni mpenzi wangu Mimi anaitwa Nassibu.
" Faith sijakuita hapa ili tuue turumbane, nimekuita hapa ili kuliweka wazi hili ijulikane Nani anapendwa na Nani hapendwi.
" Shoga Mimi ninachojua kuwa napendwa maana Nina mipango mingi Sana na huyu mwanaume...
" Sawa ngoja aje tujue moja. Laula aliongea kistaarabu lakini faith alikuwa kapaniki japo Laula alijitahidi Sana kumtuliza.
Rahim aliporudi kutoka kazini alishituka Sana kumuona Faith  akiwa nyumbani kwake .
 Laula na Faith wakigeuka kumuangalia, Rahim alisimama mlangoni na kuwaangalia.
" Nassibu njoo uweke Mambo sawa, tunahitaji maekezo yako hapa. Aliongea Faith.
" Kwani Kuna tatizo gani?
" Njoo uniambie huyu Ni Nani? Faith alisema  na Rahim alisogea na kukaa kwenye Kochi. Laula alimuangalia na kumwambia 
" Rahim hatimae kila kitu kipo hadharani  tunataka kujua Kati yangu Mimi na Faith Ni Nani unaempenda? Laula aliuliza. Rahim alitulia kwa muda alafu akasema 
" Laula naomba niwe muwazi kwenye hili, Ni kweli tuketoka mbali lakini moyo wangu upo kwa faith hisia zangu zipo kwake. Faith alitabasamu baada ya kusikia hivyo Laula aliachia tabasamu uchungu  lililoambatana na machozi.

Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post