*1------4*
HADITHI: MKONO WA JINNI
Na Mwaisa Story.
Whatsapp:0743433005
SEHEMU YA 1
MWANZO : Ilikuwa ni majira ya saa saba mchana, siku ya juma mosi, kilomita mbili toka kati kati ya mji maarufu sana Kisiwani Pemba, Chake Chake, ni wakati ambao zilikuwa zime tawala habari za uchaguzi mkuu, wa raisi wabunge na wawakirishi, wa mwaka 2005, kipindi ambacho kwa kawaida zilijaza hofu kwa wananchi wa kisiwa hiki, kutokana matukio ya chaguzi zilizopita, asa wa mwaka elfu mbili, sasa basi, kwenye nyumba moja ya kulala wageni, iliyopoa kwa utulivu wake, (tofauti tulivyozowea tanzania bara) inayofahami ka kwa jina la Madungu Guest house, iliyopo maeneo ya Madungu, pembezoni mwa barabara kuu iendayo kusini pemba, itokayo Chake Cheke, kwenda mkoa wakusini Pemba, kupitia Mtambile mpaka Mjini wa Mkoani (Ndiyo jina la mjihuo) barabara ambayo ilonekana kupambwa kwa bendera za vyamba mbali mbali vya siasa, madugu guest ikiwa jilani kabisa na makao makuu ya jeshi la polisi, la mkoa wa Chake Chake.
Naam tukuwa hapo Madungu Guest house, aliingia kijana mmoja mwenye hasiri ya uchotara wa mswahili na mwarabu, japo hasirimia kubwa alikuwa ni mwarabu, alie valia kitanashati, japo kwa wakazi wa Tanzania bara, wangesema alivalia simple, ila kwa huku ungesema amevaa kiungwana, maana ukiachia kofia yake ya duara, (baraghashia) nyeupe nyenye kudaliziwa kwa nyuzi za hariri, pia alivalia shati lake blue, lenye draft nyeupe na nyekundu, pasipo kuchomekea, na suruali yake nyeusi, huku chini akivalia viatu vya wazi, sijuwi kama ndio maandiko sahihi, kwamba ni sendoz, lakini ndivyo tunavyo itaga.
Kijana yule mwenye mwonekano wa hali nzuri ya kimaisha, huku kidevu chake kikitawaliwa na ndevu nyeusi za kung’aa, ambazo zilionyesha urabu wake, alielekea moja kwa moja mpaka mapokezi, na kuongea na kijana mmoja wakiume alie kuwepo pale mapokezi, ambae mala moja alimpatia funguo na kumtajia chumba na kumi na moja, kwamba ndio chumba alicho takiwa kijana yule mwarabu akaingie, na huku wakiwa kama walisha wai kuonana kabla ya hapo, yani ilionekana kuwa yule kijana alisha tangulia mwanzo, kuja kufanya mipango ya chumba kwenye ile nyumba ya kulala wageni, “sasa nikuambie kitu, we nenda kamchukue mlango wa nyuma” alisema yule kijana mwarabu, hapo kama walio elewana toka mwanzo, yule kijana akaenda kule kwenye mlango wa nyuma.
Naam ile anaukaribia tu mlango, akasikia arufu nzuri ya manukato, hapo yule kijana mhudumu wa vyumba mwenye hasiri ya watu toka bara, ambao huku kisiwani upewe jina la mnyamwezi, akajikuta akisisimkwa na mwili wake, maana alijuwa fika kuwa harusi ile inatoka kwa mschana alie simama nje ya yumba ile, na alie jiandaa kwa kuja kupewa dudu, labda kuna kitu nikudokeze, ni kwamba mschana wa kiarabu au anaefwatamaduni hiyo uwa anamaandalizi makubwa sana pale anapoenda kwenye tendo la ndoa, wanasema ni moja ya ibada, na anatakiwa kumfanya mwanaume avutike na kuamasika katika wakati ana mpatia dudu, huvyo ujifukiza marashi ambali mbali, na kujinyunyuzia utuli wa kila aina,ufikia wakati baadhi ya wanaume ujikuta anasimamaisha mnazi ata pale anapo kutana na mschana huyu ndani ya dala dala, au kupishana nae njiani.
Ndiyo ilivyo kuwa kwa kijana huyu mhudumu wa hii guest house, mala tu alipofunguwa mlango ule mdogo wenye gate la chuma, na kumkuta mschana mmoja, mwenye umbo na kimo vya kupendeza, maana, kwa haraka haraka ungesema ni mschana toka bara, sababu miili mingi ya waschana wenyeji wa visiwa hivi, livyopo mashariki mwa Afrika, walikuwa ni wenye maimbo ya kiingreza, yani wembamba, kama waarabu, tofauti na huyu ambae usawa wa macho yake alionekana kuwa ni mweupe kabisa, tena kama mwarabu, lakini umbo lake ni zaidi ya mtu wa mschana wa bara mwenyewe, maana alikuwa mschana mrefu kiasi, mwenye kifua cha wastani, wembamba wake asa maeneo ya tumboni, ungesema kuwa ni mvivu wa kula, japo alikuwa ame valia nguo ndefu nyeusi, yani baibui lenye halili za rangi ya dhahabu, kwenye pindozake, na kifuani, lakini usage shindwa kuona jinsi alivyo jaliwa makalio na mapaja yani hips, mapana yenye kuvutia kila mwanaume mwenye macho yenye kimbele mbele kama ya Mwaisa, huku akifunika nywele zake kwa ushungi mweusi, pia aliziba uso wake kwa kitambaa flani cheusi, wapiganaji wa kijapan, wenye hasiri ya Ninja, kwa wale wa uarabuni wanaita nicab, harufu nzuri ya manukato ilitawala eneo alile, “asalam aleykum” ilikuwa ni sauti nyororo, na nzuri, iliyo jaa aibu kilo mia, toka kwa mschana huyu, mzuri, ambae alionekana mwenye mwasi wasi mwingi, kana kwamba ile ndio ilikuwa mala yake yakwanza kuingia sehemu kama ile, ambayo kikawaida mtu akiingia anajuwa kinachofwata ni kitu gani, yakwamba ni kupeana dudu tu! na sijambo jingine, ukichukulia pengine ni mwenyeji wa maeneo aya aya, na siyo msafiri, “aleykum salaam shemeji, karibu ndani” alisema kijana mhudumu, kijana mhdumu wa guest, ambae alivutiwa na mwonekano wa mschana huyu, ata alipo jaribu kumtazama usoni mwanamke huyu, hakika ilikuwa nivigumu sana, maana mschana huyu, alikwepesha macho kwa aibu na kutazama chini, na yule mschana akaingia ndani, akimfwata nyuma kijana yule mwenye hasiri ya kutoka tanzania bara,
Naam talishi wa nyumba ya wageni bwana Hassan Mohamed, ambae ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, Pemba alikuja kutafuta maisha, alimchukuwa yule mschana na kumpeleka kwenye chumba namba kumi na mmoja, ambako aligonga mlango ukafunguliwa na yule kijana chotara, ambae jina lake alijulikana kama Adbulkadir Amer, (unaweza ita Ame) na yule mschana akaingia haraka ndani, ungesema aliona mtu ambae anaweza kuwafumania, “hooo! punguza wasi wasi basi, si hivi umesha ingia na ajakujuwa mtu” alisema Abdulkadiri, kwa lafudhi ya kipemba, huku akimshika mkono mpenzi wake huyo, kama vile anamzuwia, akikimbie sana, kisha akamwingiza ndani ya chumba kile namba kumi na moja, huku bwana Hassan, mnyamwezi wa tabora pale Itigi, anataka kuondoka zake, ili kuwapisha wapenzi awa wafanye ya kwako, “sasa Hans hee! ebu niagizishie sahani mbili za chips, mishikaki mi nne, juice ya ukwaju, na bakuri moja la urojo” alisema Abdulkadir, huku anampatia noti ya shilingi elfu kumi bwana Hassan, au Hans kama walivyo kuwa wanamwita, “chenji ni yakwako” alisisitiza Abdul, kisha akaingia ndani na kufunga mlango kwa ndani, hapo Hassan kuweza kuondoka mala moja, alisimama kidogo pale mkangoni, nikama kuna jambo alikuwa analisubiri, huku akitikisa kichwa kwa masikitiko ya wivu, “dah! dogo anafaidi huyu, ebu, ona ule mzigo, umejazia wowo kama amesusiwa, alafu sijuwi amelitoa wapi lile demu, utazani ametoka bara” aliwaza Hassan akiwa ameganda kwenye mlango wa chumba kile namba kumi na moja, ambao ulikuwa umesha fungwa, “ngoja kwanza nioge basi, mbona unaharaka weye” ilisikika ile sauti tamu ya kike, yenye rafudhi ya kipemba, “siuvue basi ukaoge sasa unaenda oga na nguo zako” alisema Abdurkadir, kwa saut ya kubembeleza, “naenda vulia msalani, naona aya mie” alisema tena yule mwanamke, sauti yake ikiambatana na kicheko ambacho kilionyesha wazi kuwa amejawa na aibu, ungeweza kusema kuwa mschana huyu ndio alikuwa anaingia kwa mala ya kwanza na mwanaume katika madhingira kamahaya, “aya bwana mshindi mwenye nenda kaoge” alisikika Abdur, kijana mwenye jina kubwa sana hapa mjini, Cheke chake, kutokana na biashara yake ya manukato na mapambo ya wanawake, kama vile mikufu na hear ring (heleni) pia viatu na nguo za ndani, “na lile dirisha lifungwe bwana wasije kuchungulia” alisikika tena yule mwanamke ambae mimi nawewe atuja mfahamu ni nani, kutokana na kufunika sura yake, “usijari nitafunga we nenda kaoge tu” alisema Abdulkadir Ame.
Hapo Hassan akuona sababu ya kuendelea kukaa maali pale, akatoka zake na kuelekea alikotumwa, ambako ni kamwendo kidogo, ni umbali wa mita miatano, tok nyumba ya kulala wageni, akuwa na wasi wasi yakuwa, endapo atakuja mteja mwingine kule ofisini kwake, na kumkosa, maana Nyumba ile ya wageni yenye vyumba kumi na saba, aikuwa na wateja wengi, kama zilivyo nyumba nyingi za kulala wageni za Tanzania bara, maana huku Pemba, kuna wakati bwana Hassan ukaa ata week, ajaona mteja ata mmoja, labda kipindi cha siku kuu, au msimu wa watalii na kipindi cha uchaguzi, maana watu wengi wa kisiasa uja na kuchukuwa vyumba pale Madungu guest house, na ndio maana bwana Hassan utamani kama kila mwaka kungekuwa na uchaguzi, pasipo kujali vurugu na usumbufu unaotokeaga.
Nusu saa baadae tayari Hassan alikuwa ameshapata Chips, urojo juice ya ukwaju, na vitu vyote alivyo agiziwa bwana Abdulkadir, na sasa alikuwa njiani anarudi kule ofisini kwake, huku muda wote akiwaza jinsi Abdul atakavyo kuwa anafaidi kitumbua cha yule mwanamke, japo akumwona kwa sura, lakini umbo la yule mwanamke lilitosha kabisa kuonyesha kuwa alikuwa ni mzuri na mtamu kiasi gani, nikama alichizika kijana huyu, ambae licha ya kuwepo huku Pemba kwa miaka saba, lakini ukweli waschana wazuri wakipemba, ambao idadi yao kubwa wenye hasiri ya kichotara wa kiarabu, aliishia kuwaona kwa macho tu!, na kuwaita shemeji, maana akukuwa kazi ndogo kumpata mwanamke wa kipemba, na ukamshawishi akupe kitumbua bila kutangaza ndoa, na sifa kubwa lazima uwe mtu wa dini na ushiriki ibada pamoja na swala tano, hapo bwana Hassan ambae unaweza kusema kuwa, ni jina lake pekee ndilo linalo mtambulisha kuwa ni muislam, akaanza kubahatisha kwa waschana toka bara, ambao wengi wao ni wakutoka Tanga, wanaokuja kufanya kazi kwenye bar maalufu ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa moja pekee, inayo milikiwa na Jeshi la ulinzi, inafahamika kama staring Mess, hapo ndipo bwana Hassan alipokuwa anapunguzia mzigo wake, sasa Hassan alikuwa anatembea barabarani, huku anatathmini kila mwanamke anae pishana nae, kama ange mwona wa kumzidi yule alieingia hotelini na Kijana Abdulkadir, “haaa! huyu awezi kutia mguu pale, ile mashine bwana” aliwaza Hassan, akiwa anapishana na waschana mbali mbali, na kuwa tazama makalio, huku ana mfuko ulio jaa mazaga zaga mkononi mwake.
Lakini wakati Abdul anatembea huku anawaza juu ya yule mschana, na kuwatazama wengine sehemu za makalio, mala akamwona mschana mwingine kama yule yule, alie mwacha na mteja wake kule nyumba ya kulala wageni, akija mbele yake, mwenye kimo na umbo kama lile, tena amevaa vile vile, na kujiziba nicab usoni, aikuwa ajabu kwa watu wa huku, maana ni moja ya stara kwa wanawake, Hassan alimtazama vizuri yule mwanamke, ambae alionekana akitembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa mwenye wasi wasi mwingi, akielekea mjini Chake Chake, yani kule alikokuwa anatokea Hassan, ata alipopisha nae na kupiga hatua kadhaa, akageuka na kutazama makilo ya mwanamke huyu, nikweli na yeye alikuwamefungasha, “sikuhizi wapemba nao wamo” alijisemea Hassan, huku anatazama mbele anakoelekea, “na baada ya kutembea mita kama kumi mbele, akageuka tena nyuma kwa lengo la kumtazama tena yule mschana, akiitaji kutazama tena makalio ya mschana yule mwenye kufanana na demu wa mteja wake, alie mwacha kule guest house, chumba namba kumi na moja.
Lakini ile anageuka na kumtazama yule mwanamke nae ndio wakati alikuwa anageuka, na kama vile alikuwa anamtazama yeye, na macho yao yalipo kutana, yule mschana akatazama mbele haraka, huku anaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka sana, Hassan alitabasamu kwa ujinga wake, wa kutazama makalio ya waschana, unajuwa aikuwa hajabu sana kwa mwanamke wa kisiwa hiki kuvaa kamavile, sababu ni moja ya utaratibu, walio ulithi toka kwa wakoloni wao, ambao ni waharabu, pia ata dini yao inawashauri kuifadhi miiliyao, “duh! sijuwi demu amekolea, mbona aligeuka kuni tazama?” aliwaza Hassan kisha kageuka tena, na kumtazama yule mschana.
Naam Hapo Hassan akashikwa na mshangao mkubwa sana, maana akumwona tena yule mschana, inamaana alisha toweka…………
SEHEMU YA 2
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA : na macho yao yalipo kutana, yule mschana akatazama mbele haraka, huku anaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka sana, Hassan alitabasamu kwa ujinga wake, wa kutazama makalio ya waschana, unajuwa aikuwa hajabu sana kwa mwanamke wa kisiwa hiki kuvaa kamavile, sababu ni moja ya utaratibu, walio ulithi toka kwa wakoloni wao, ambao ni waharabu, pia ata dini yao inawashauri kuifadhi miiliyao, “duh! sijuwi demu amekolea, mbona aligeuka kuni tazama?” aliwaza Hassan kisha kageuka tena, na kumtazama yule mschana.Naam Hapo Hassan akashikwa na mshangao mkubwa sana, maana akumwona tena yule mschana, inamaana alisha toweka…………endelea…………
Hassan akageuka kabisa na kutazama, pengine alihisi ametazama kwa haraka ndio maana ajamwona yule mschana, lakini aliona watu wengine tu! ila mwanamke anae fanana na yule mschana, akuonekana kabisa, “mh! au jinni nini?” aliwaza Hassan na kupuuza mawazo yake ya kutazama makalio ya waschana, nakuelekea ofisini kwake.***
Naam Hassan alipofika pale ofisini kwake, moja kwamoja akaufwata mlango wa chumba namba kumi namoja, akatega sikio kusikiliza kinachoendelea ndani, ya chumba hicho, lakini akusikia chochote, siyo mlio wa kitanda wala miguno ya kimapenzi, akajuwa kuwa walipo ndani wameamua kujipumzisha baada ya kupeana dudu mzunguko wa kwanza, hapo akamua kugonga mlango kidogo, lakini akupewa jibu lolote toka ndani zaidi ya harufu ya manukato, Hassan akagonga tena mlango, akirudia mala kadhaa, huku akiongeza nguvu ya ugingaji, bila kupata majibu lolote, ndipo Hassan akahisi kuwa kijana Abdul atakuwa juu ya kitumbua, lakini nje ya kitanda, hivyo akaona awape nafasi ya kufaidi, na wakisha maliza, lazima Abdul ata mfwata mapokezi kuchukuwa mzigo wake.***
Lakini kwa mujibu wa bwana Hassan, yalipita masaa matatu bila kuona Abdulkadiri, akija kuchukuwa mzigo wake, ndipo bwana Hassan Mohamed, alipo amua kwenda kugonga tena mlango wa chumba namba kumi na moja, ambapo akukuwa na jibu wala dalili ya jibu toka ndani ya chumba hicho, Hassani katika maelezo yake akasema kuwa, alipoona hivyo akajuwa kuwa pengine wateja wake wapo katika kupeana dudu, ukweli ni kwamba, bwana Hassan licha ya kuwa ni tarishi wa muda mrefu pale hotelini, lakini alikuwa na kautaratibu flani wakati mwingine, ka kupiga chabo, akaona hiyo ndiyo njia itakayofaa kuangalia kile wanachokifanya wateja wake, kwa muda mrefu namna hii, kwanza kufanya hivyo kwanza akaanza kwa kutega sikio mlangoni kwa mala ya pili, na kusikiliza ndani, ikawa kama mwanzo, akusikia chochote, hakukuwa na dalili ya uwepo wawatu ndani, “mh! inamaana alishaondoka kimya kimya, au?” alijiuliza Hassan, kabla ajapata wazo la kuzunguka nyuma ya nyumba hii ya kulala wageni, ili akachungulie dilishani, kuhakikisha kama wateja wake bado wapo ndani.
Sekunde chache baadae tayari bwana Hassan alikuwa amesha zunguka jengo la hotel hii iliyopo Madungu, pembeni ya mji Chake Chake, kitu cha kwanza Hassan aliona kuna jiwekubwa sana chini ya dirisha lile, ambalo lilikuwa wazi, akushangaa sana, maana akukumbuka kama mala ya mwisho alipo kuwa ana chungulia wateja wake kiasi cha siku nne zilizopita, kama alilitoa au akulitoa, hivyo akasimama juu ya jiwe pale kwenye dirisha la chumba namba kumi na mmoja, ambalo dirisha na panzia lake lilikuwa wazi, hivyo ikawa kazi nyepesi kwa Hassan, kuweza kuchungulia ndani ya chumba hicho, pasipo kujiuliza kwanini dirisha lilikuwa wazi kiasi hicho, wakati aliwasikia wawili awa wakikumbushana kulifunga kabla ya kuanza kupeana dudu.
Naam ile Hassan alipochungulia ndani ya chumba kile, alishtuka na kujikuta akianguka kwa uwoga kubwa ulio mpata, “mamaaaaa!!” alipiga kelele Hassan, huku ana inuka na kujaribu kukimbia, lakini akaijibwaga chini kwa miguu yake kukosa nguvu, maana alishtushwa na kuogopeshwa, na hali aliyo iona mle ndani, ukweli ni kwamba japo Hassan aliweza kuona mwili wa mtu mweusi kama mkaa, ukiwa umelala ksakafuni, mwili wa mtu ambae, ulikuwa na dalili nyingi sana za kuwa ni Abdulkadiri, nikutokana na zile ndevu, na nguo alizo vaa, lakini kwa sasa alikuwa amebadirika na kuwa mweusi, kama alie banikwa kwenye moto mkali, usinge weza kuamini kuwa ndie yule kijana Abdulkadir ambae ni chotara wakiarabu kabisa.
Hassan aliinuka haraka pale chini na kuanza kutimua mbio kuelekea barabarani, huku anapiga kelele kama mtu aliechanganyikiwa, “Jini!! jamani jiniiii!” hivyo ndivyo alivyo sema, bwana Hassan, akiamini kuwaw Abdulkadir alikuwa ameuwawa kwa nyinywa damu na jinni, japo toka amefika hapa pemba akuwai kuona wala kutokewa na jinni, tena aliamini kuwa jinni mwenyewe ni yule mwanamke, ambao amesha wai kusikia habari zao mala nyingi sana, hapa kisiwani, ukizingatia, akuonyesha dalili ya kuwepo mlendani.***
Hassan alipofika barabarani alisimama kwa sekunde kadhaa, huku akipiga kelele, za “jinni jinni” huku watu wakimshangaa, maana alikuwa anaendelea kupiga kelele, kama Mtu anae weweseka, “jinni !! jamani Jini” kwa wasio mfahamu kilicho tokea, wakajuwa kuwa Hassan ni chizi freshi, lakini ukweli lilikuwa ni tukio la kushangaza kwa Hassan, alie amini kuwa Abdulkadir, ame uliwa na jinni.
Baada ya dakika chache za kuweweseka, ndipo Hassan akapata wazo la kwenda kituo cha cha polisi, na kituo cha polisi ambacho kilikuwa karibu yake, ni kile cha polisi mkoa wa Chake Chake, yani Madungu Polisi, ambacho kilikuwa mita chache toka pale hotelini, ambako alitoa taalifa ya kifo cha kijana yule, ambae siyo mgeni machoni ma masikioni kwa wakazi wa Chake Chake, maana Adbdulkadir, alikuwa ni mfanya biashara na mwagizaji wa vifaa vya wakina mama, toka nchi za falme za kiarab.
Naam polisi walifika eneo la tukio, na kukuta mwili wa kijana Abdul Kadir, na kuanza uchunguzi wa kina, ambapo kwa msaada wa madoctor, waligundua kuwa kijana Abdulkadir, amekufa baada ya kukaukiwa na damu, japo kulikuwa na utata mkubwa sana madoctor kushangazwa na ukaukajiule wadamu, kwa mtu ambae ameingia mwenyewe pale hotelin, na kuja kukaukiwa damu na kufa mala moja, hapo kila mmoja alifananisha kifo hicho, na vifo vingine kadhaa vilivyo wai kutokea miaka ya nyuma, vifo vya aina hiyo hiyo, ilivyo usishwa na jinni wa kike anausika na vifo hivyo.***
“Lakini kuna mtu mmoja pekee, anae fahamika kwa jina la Jonh Joseph, akulizika na maamuzi ua au imani ya wanachi na jeshi la polisi hapa kisiwani pemba, kuwa kuna jinni anafanya mauwaji hayo, hivyo amekuja ofisini kwetu, na kuomba tufanye uchunguzi wakina, ili kubaini ukweli juu ya mauwaji hayo, na wewe ndie ulie chaguliwa kwenda kisiwani pemba kufanya uchunguzi huo” alisema bwana, Winfred Mbogo, mkurugenzi wa kampuni binafsi, ya upelelezi na uchunguzi, ya MSC (Mbogo Spy COM), alipokuwa anamaliza, kunisomea simulizi nzinto ya kusisimua na kutisha, nikiwa nimekaa mbele yake, ndani ya ofisi yake, tukutenganishwa na meza kubwa yenye vikolombwezo vya kila aina vilivyo ashilia kuwa hii ni ofisi, iliyopo mbezi mwisho jijini dar es salaam, “lakini mkurugenzi inawezekana vipi, mimi nikaenda kumchunguza jinni?” licha ya kwamba hii iilikuwa ndiyo kazi yangu ya kwanza, toka nirudi nchini toka masomoni, na nilikuwa natamani kupata kazi, japo moja nionyeshe uwezo wangu, lakini kwa jukumu ilo, nilikuwa mbishi kidogo, ni kutokana na sababu ambazo nitakueleza mbele, japo ubishi huo aukuweza kuzaa matunda, maana amri ilikuwa ni moja tu kwenda kisiwani pemba, kuchunguza kifo cha Abdulkadir, lakini kichwani mwangu nikipanga kuwa nitenda kuzuga, ili muda upite kisha nirudi na kusema kuwa sijafanikiwa.****
Wapo waliopenda kuniita mvuvi wa nchi kavu, asa wale nilio kuwa nasomanao, shule ya msingi, secondary ata chuo cha chao kuikuu, cha dar es salaam, nilikokuwa nasomamemea usalama wa nchi na mausiano ya kimtaifa, nilipewa jina ilo, kutokana na jinsi nilivyo weza kuingia kwenye mausiano na baadhi ya waschana ambao walionekana kuwa ni wakipekee, labda kutokana na hali zao za kimaisha kuwa za juu sana, au tabia zao za upole na kuto kuitaji mwanaume wa kupeana dudu, pasipo malengo yoyote ya baadae, japo inasifa ya kuitwa mpenda mademu, au mzinzi kama wakina John Bonge wa nizibe mdomo, au Edgar Haule wa kwenye mama mwenye nyumba, mimi naitwa Eric Frank, lakini uwa napenda kujiita mkono wa jini, yani nisie shindwa kitu, jina nilililojipati mwenyewe, nikiwa kwenye moja kati ya vyuo vya kipelelezi nilivyo wai kupitia, ikiwa nisehemu ya kujinadi na kujisifu, japo sikuwai kupata kazi ya kuchunguza yenye mwonekano kama huu.
Yap, nimeona nikusimulie mkasa huu ambao ulitokea miaka kumi na nne iliyopita, yani toka mwaka huu wa 2019, kipindi hicho nikiwa na miaka 25 tu! nina mwaka wa tatu toka nime jiunga na kampuni binafsi ya upelelezi wa siri, hapa nchini, yenye makao yake Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, huku rafiki zangu wengi wakijuwa kuwa, nafanya kazi kwenye kampuni ya kuchapisha vitabu, ya MSP COM, nikiwa kama fundi na mtaalamu wa kutengeneza compter, yani hardwere na softwere, nikweli nilikuwa na uwezo mzuri katika vifaa na programe za computer, sababu katika mafunzo ya upelelezi na mapigano ya kujiami kwa mikono, na silaha za jadi na zile za moto, niliyo ya chukuwa, kwa miaka mitatu toka mwaka 2002 mapaka mwaka 2005, katika nchi za Japan Cuba China na Israel, pia nilikuwa najifunza sana kuhusu internet tecnolog.
Japo ni muda mrefu umepita, toka nipewe na kulifanya jukumu ili, lakini sidhani kama itakuwa vibaya nikikusimulia mkasa huu, ambao ukiachilia kuwa ndio jukumu langu la kwanza kulifanya, baada ya kutoka mfunzoni, pia ni moja ya mikasa, kati ya mikasa ambayo ilinisisimua sana, na kunipa wakati mgumu.**
Ilikuwa ni tarehe kumi na moja ya mwezi wa tano ya mwaka 2005, ni kabla ya miezi mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu, wa raisi wa serikali ya muungano na raisi wa zanzibar, wabunge, wa wakilishi na madiwani, Mida ya saa kumi na mbili za asubuhi ndio mida ambayo Meli kubwa ya MV mapinduzi, ilipotia nanga kwenye bandari ya mkoani, kusini Pemba, tukiwa tuna itimisha safari iliyo ni chukuwa taklibani masaa kumi na saba, toka bandari ya dar es salaam, ukweli muda wote wa safari nilikuwa sina amani moyoni mwangu, japo mimi kimwonekano ni mpole, na ilo nalifahamu toka nikiwa mdogo, lakini safari hii upole wangu ulizidi mala dufu, kutokana na kuhofia hii safari, na kitu kilicho nifanya nikose amani juu ya hii safari, ni mambo matatu, moja nilikuwa nikutokana na kipindi ninachoenda, ambacho ni cha uchaguzi, maana nalikuwa naifahamu vizuri mikasa ya uchaguzi, jinsi inavyo kuwa, asa nikiangalia uchaguzi, wa nyuma yake, wa mwaka elfu mbili, ambao ulikuwa na habari nyingi za vurugu, na mwaka huu wa 2005, ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi, nambaya zaidi ni kwamba kulienea uvumi wa kuwa, kuna watu wa kutoka tanzania bara, wameingia kule visiwani kuongeza nguvu ya chama flani cha kisiasa katika upigaji wa kura, hivyo basi kila mtu mwenye hasiri ya kutoka bara, kwajina la utani chogo, alishukiwa kuwa, ni mmoja wa wanachama waliokuja kuvuruga uchaguzi,
Pili nilikuwa nilihofia sana kuhusu habari za majini (jinni), ukweli nilishawai kusikia habari nyingi sana za mitaani, kuwa Pemba kuna majini mengi sana, nakwamba unaweza kumwona mtu na ukaongea nae vizuri kabisa, kumbe ni jinni, na kwamba wakati mwingine majinni hao, wanaweza kukuchukia, na kukudhuru bila sababu yoyote, au wanaweza kukupenda, na kukung’ang’ania uwe mpenzi wake, huku wakikupatia mashariliti, magumu sana katika mapenzi yenu, na endapo utashindwa au kukataa kutimiza mahariti yao, basi cha moto utakiona, na ukichukulia mimi kama mimi, siyo kwamba najisifu, ila ukweli kutokana na jinsi nilivyo na mwonekano wangu, umesha wasumbua sana waschana wengi sana, toka nikiwa shule, asa kipindi tukiwa kwenye michezo ya shule za sekondari UMISHUNTA, nikiwa mchezaji wa Baskert ball, waschana wengi sana walipenda kuwa na mimi, na kunitumia vijizawadi kama vile post card na mialiko ya matembezi ya pamoja, hivyo nilipata wasi wasi awa majini lazima wange nipenda tu, lakini hiyo siyo kesi sana, kesi hipo hivi.
Niliwai kusikia, kuwa kuna majini yakiume, ambayo ubaka binadamu wakiume, yani hapo ndipo nilipo iona dunia kuwa ndogo, na kulahani kazi hii ya upelelezi,ambayo mwanzo niliiona kuwa inanifaa kutokana na kipato kikubwa, na sasa ndio najuwa maana ya ule mshahara wa million moja na laki nane, kwa mimi mfanyakazi wa miaka mitatu, wakati mfanyakazi wakawaida alikuwa analipwa kiasi cha shilingi, elfu tisini na nane, mpaka laki moja na elfu tano, ikiwa ni kima cha kati cha mishara, pia niliwaikusikia kuwa, unaweza kukuta kifuu au kitu chochote uka kipiga teke, nacho kika kuuliza kwanini unanipiga, na ata ukikimbia unge kikuta mbele, bado kinge kuuliza, au kupatwa na matatizo makuibwa ukweli nilizidi kukosa amani.
Tatu, Kazi yenyewe, ambayo nilikuwa naenda kuifanya, ilikuwa unausishwa na imani za kishirikina na majini, ili kuwa kazi yangu ya kwanza , zaidi ya hapo upelelezi nilikuwa na ufahamu ule wa kwenye vitabu pekee, yani chuoni, hakika iliniogopesha sana, maana niliamini kuwa, kama ni kweli watu hao wameuliwa na jinni, basi ilo jinni tayari limesha juwa kuwa, kuna mtu anaingia pemba kwaajili ya kuchunguza mauwaji liliyo yafanya, na kibaya zaidi akuna mwalifu ambae anamwacha salama, mpelelezi anae mfwatilia, hiyo ndiyo moja ya kitu nilicho jifunza.***
Niliendelea kuwaza ata niliposhuka toka kwenye meli ya mv Mapinduzi, kwenye bandari ya mkoani, pemba ya kusini, ambapo niliweza kuona madhari ya pemba jinsi ilivyo, kilicho ni shangaza na kuni vutia, ni uvaaji wa wakazi wa kazi wa kisiwa hiki, ambao ni kama utamaduni, kwa wanawake walivalia magauni marefu, ya kupendeza huku idadi kubwa wakiwa ni waschana ambao wenye hasiri ya kichotara wa kiharabu, sema awakuwa na maumbo makubwa kama walivyo kuwa wanawake wa Tanzania bara, yani hips na makalio makubwa, vijana wa sasa wanaita msambwanda, ila sura zao zilikuwa ni nzuri na zakuvutia, ila sikuwa na uhakika juu ya maumbo yao, sababu walivalia magauni marefu na kuficha nywele zao kwa mitandio, huku wengi wao wakiwa wamevalia mababuibui meusi, Kwa upande wa wanaume wengi walikuwa wamevalia kawaida, suluali mashati ya bila kuchomekea, na viatu vya wazi, yani sendos.
Nilikatiza kwenye geti la kutokea pale bandarini, na kufika eneo la stendi ya magari yaendayo sehemu mbali mbali, ikiwa pamoja na Chake Chake, Mtambilie Konde Wete yani Pemba ya kaskazini, nikaungana na wasafiri wenzangu kuingia kwenye magari aya, ambayo huku tunaita dala dala, ambayo ukiachia mabasi madogo, kama vile Toyota coster na Toyota hiace, pia kulikuwa na gari aina ya suzuk Center, ambazo zili tengenezwa bord yake kwa mbao, nalo kutumika kama gari la abiria, zamani tulikuwa tunaita chai maharage.
Nilifanikiwa kupata nafasi kwenye Toyota hiace, na safari ya kwenda Chake Chake ikaanza, ukweli sikuwa na raha ata kidogo, nilijikuta na ichukia Pemba bila ata sababu, ata nilipokuwa naitazama barabara nyembamba, yenye kona nyingi sana, kali na za ghafla, huku nikishuhudia karafuu zikiwa zimeanikwa pembeni ya barabara, ghafla nika jikuta nikiichukia ile arufu ya karafuu, huku ule wimbo wa marashi ya pemba, ukinijia kichwani, na kujikuta na wenyewe nauchukia vibaya sana, nikiona kama unanisanifu……
SEHEMU YA 3
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI : Nilifanikiwa kupata nafasi kwenye Toyota hiace, na safari ya kwenda Chake Chake ikaanza, ukweli sikuwa na raha ata kidogo, nilijikuta na ichukia Pemba bila ata sababu, ata nilipokuwa naitazama barabara nyembamba, yenye kona nyingi sana, kali na za ghafla, huku nikishuhudia karafuu zikiwa zimeanikwa pembeni ya barabara, ghafla nika jikuta nikiichukia ile arufu ya karafuu, huku ule wimbo wa marashi ya pemba, ukinijia kichwani, na kujikuta na wenyewe nauchukia vibaya sana, nikiona kama unanisanifu…… endelea…………..
Saa sita mchana tayari nilikuwa nimesha fika sehemu ambayo nilipangiwa kufikia, ni pembezoni kidogo mwa mji wa chake chake, mashariki mwa Pemba, sheia (kata) ya Vitongoji, tukiwa tume katiza mji wa Chake chake, ambapo tulikuta watu wengi na uchangamfu wa hali yajuu, japo ilikuwa ni barabarani, pia tuka katiza, macho manne ambako tuliacha barabara ya wete, na kuifwata ile ya Vitongoji, na kupita Wawi, kuelekea Vitongoji.
Kwanza nilienda moja kwa moja kwenye shule ya sekondali ya Feidel Castor, ni moja ya shule kubwa sana za Sekondali, nchini Tanzania, shule ambayo viongozi wengi wakubwa, na watu mashuhuri hapa nchini, asa kisiwani pemba, walisoma kwenye shule hii, ambayo nilipangiwa kuja kuwa kama mwalimu wa computer, ikiwa kama kificho cha kazi yangu, (cover) “hooo asalam alaeykum mwalimu Eric” alinisalimia mwalimu mkuu wa shule hii, mala baada ya kuingia ofisini kwake, kwa lengo la kureport, nilisha julishwa kuhusu salamu za huku kisiwa cha pemba, yakwamba salamu yoyote kwa wenyeji ni salamu aley kum” aleykum salam mwalimu” niliitikia salamu ile ambayo iwe mtu mzima au mtoto ungepaswa kumsalimia hivyo, “karibu sana mwalimu, naona umewai kabla ya vifaa avija fika” aliema mwalimu huyu, ambae alinipa maelezo mafupi, na utaratibu wa pale shuleni, na kisiwa kwa ujumla wake, ikiwa ni miiko na maadiri kwa ujumla, huku akisisitiza sana kuhusu ukaribu na wanafunzi wa kike, pamoja na waschana wa huko mtaani, maana ilo swala lilikuwa ni baya kuliko, swala jingine kisiwani hapa, “kwani uebahatika kuwa na mke?” aliuniliza mwalimu mkuu, na hapo nilicheka cheka kidogo, maana achilia kuwa na mke, ukweli sikuwa na ata mwamke mmoja wa kumwita mchumba, “bado sija bahatika mwalimu, lakini nazani nikirudi nitaowa” nilisema kwa sauti ya kujiamini, maana kiukweli nilijiona bado mdogo kuwa na mke, nikamwona mwalimu mkuu anatoa macho kwa mshangao, unangoja nini kijana, ebu ona, unataaluma nzuri, ya ufundi wa computer na network, ambayo inakupatia kipato kikubwa, wakati wenzako wanaishi kwa kazi ngumu zenye ujira mdogo, lakini wametimiza ibada ya ndoa” alisema yule mwalimu ambae kiukweli ni mzee wamakamo, alie valia baraghashia kichwani mwake, huku chini, akiwa amevalia shati refu ambalo akuchomekea, kwenye suruali yake, na miguuni alivalia viatu vya wazi, yani sendo, “unajuwa mwalimu, muda mwingi nilikuwa masomoni, hivyo sasa nime rudi naamini nitafanya hivyo” nilijibu tu kwalengo la kumtuliza mwalimu yule, ili maongezi yaishe na mimi niondoke zake kwenda sehemu niliyopangiwa kufikia, japo nikapumzike kwa uchovu wa safari, “nivyema, ila nahakika utaondoka na mke huku huku pemba” alisema yule mwalimu mkuu, huku nikimwona anaachia kicheko cha furaha, hapo nika jitabasamulia, kidogo, maana nilikumbuka wale waschana niliokuwa naowaona kule njiani, japo ni wazuri wa ura na rangi, lakini maumbo yao ayakunivutia, “kwanini mwalimu, inamaana huku kuna waschana wazuri kuliko sehemu nyingine?” niliuliza kwa sauti yenye udadisi, maana sikutaka kumfanya yule mwalimu anione mwenye dharau, “kwani uzuri was mwanamke ni nini, maana huku ndiko kwenye wake wenye maadili na hekima, mwanawake wacha mungu, ata kwa uzuri ni wazuri aswaaaa” alisema mwalimu mkuu, kwa sauti ya kusifu, na kunadi, “na kisiani hapa wavulana wenye maumbo kama yako ni wachache sana, hakika utawavutia wengi sana, hivyo inakubidi ywe makini sana, sababu, huku pemba, akuna mtu anaependa binti yake achezewe, na matokeo yake uwa mabaya sana” aliniambia tena mwalimu mkuu akinisisitiza.
Baada ya hapo mwalimu mkuu akanikaeleza kuwa, kutokana na usalama kuwa mdogo, asa kwa watu kutoka nje ya pemba, ambao mala nyingi kwa miaka hii ya uchaguzi, uonekana wanakuja kufanya hujuma kwenye uchaguzi, wameniombea nikae kwenye kambi moja ya Jeshi la ulinzi, ambalo lipo jilani kabisa na shule hii ya sekondali, kambi hiyo ili linaitwa Ali Khamis Camp, (sikuwai kupata historia ya huyo bwana Ali Khamis alikuwa nani, ila ninacho kumbuka niliambiwa kuwa, eneo lilipo kambi ilo, liliwai kuwa kambi la mtu huyo alie itwa Ali Khamis).
Nakumbuka wakati natoka pale shule, shule ya mchanganyiko wa wanafunzi wakike na wakiume, niliweza kuona wanafunzi wa kike, waliojitanda vilemba vyeupe vichwani mwao, wakichungulia madirishani, huku wengi wao wakiwa ni waschana wenye sura nzuri kweli kweli, ukweli niliona wazi kuwa kuna ugumu sana kuishinda mitihani ya huku pemba, lakini kwa kuzingatia nilicho elezwa na mwalimu mkuu, nikaachana nao na kuendelea na safari yangu, japo iliitaji moyo mgumu sana kupotea.
Nikaenda pale jeshini, ambapo palipakana na shule ile, nikapokelewa na askari mwenye kuvalia sale za jeshi la ulinzi, na bega la kulia, alivalia kitambaa cheupe, chenye maandishi makubwa begani kwake, MP, ikiwa ni kifupi cha neno Military Polisi, yani polisi wa jeshi, ambae alinipeleka moja kwamoja kwa afisa wa utawala, wa kikosi kile, ambae alionyesha tayari anataarifa za ujio wangu, kwa jinsi alivyo nipokea, “hooo bwana Eric, karibu pemba pelemba” alinikaribisha yule afisa wa utawara wa kambi lile, kwa sauti iliyo jaa uchangamfu na ucheshi, ambae alikuwa na nyota mbili pande zote za mabega yake, tena alionekana ni kijana ambae kama alinizidi umri, basi mwaka mmoja au miwili au ata naweza kuwa nime mzidi umri, ambae cheo chake kinaitwa lutein, “asante sana kamanda, kweli hii ni pemba pelemba” aliitikia kwa sauti ya ucheshi na uchangamfu kama yule lutein wa jeshi, ambae alikuwa ni mcheshi sana.
Naam baada ya kusalimiana, na afisa wa utawala, ambae kwa majina anaitwa Simon Malambo, tuliongea mawili matatu, kisha akampigia simu askari mmoja kuwa aje mala moja pale ofisini kwake, dakika chache baadae, tukiwa tunaendelea kuongea ili na lile, kwa kiasi kikubwa tulikuwa tuna zungumzia juu ya mambo ya computer, ikiwa kama taaluma yangu, mala akaja askari mmoja mwenye cheo cha koplo, ambae alipiga saluti, “chumba kipo tayari?” aliuliza yule afisa utawala, mala baada ya kuitikia ile salamu ya kijeshi, “kipo tayari toka jana afande” alisema yule askari mwenye cheo cha koplo, akimweleza yule afisa utawala wa kambi lile la Ally Khamis, hapo yule afisa akamweleza yule askari mwenye V mbili mabegani, kuwa anipeleke, kwenye nyumba waliyo iita ya kijani, “mpeleke Green House, hakikisha unapeleka taarifa kule mess ili awe anapewe chai na chakula cha mchana” alisema yule afisa, na kabla sija jiuliza kuhusu chakula cha jioni, yule afisa akanipa jibu, “bwana Eric, kuhusu chakula cha jioni, utakuwa unakula staring Mess, nazani utakuwa unaitaji kwenda ku refresh hakiri, mida ya jioni” alisema yule afisa, na mimi nika itikia japo sikujuwa anamanisha nini anaposema kurefresh, ila jioni ya siku ile, nilielewa alicho kuwa anamaanisha.
Ilikuwa hivi, baada ya kupelekwa kwenye jengo moja dogo lenye bati za kijani, iliyopo ndani ya kambi lile lile, tena upande ule ule karibu na shule ya Fidel Castor, jengo ilo likitazamana na barabara kubwa ya lami, inayoenda vitongoji, mpaka makaani, pwani ya mashariki ya pemba, nikaonyeshwa chumba ambacho kiliandaliwa kwaajili yangu, nikweli kilikuwa chumba kidogo lakini kizuri, chumba kilicho kuwa na kila kitu, mpaka bafu na choo ndani, ukweli kilikamilika, ukiachilia kitanda kimoja kidogo cha chuma, pia meza ndogo, ya mbao, na kochi moja dogo, la kisasa, aina ya sofa jipya kabisa, hapo nika pata wazo la kuongeza baadhi ya vitu ambayo vilipungua mle ndani, ikiwa pamoja na ki TV kidogo na deck yake, sababau niliona kuepusha kuingia kwenye vishawishi na mabaraha ya mtaani, bola wakati mwingine niwe na jifungia ndani ya chumba hiki natazama filamu, “samahani bro, eti huku nako wanauza vifaha Used, kama unguja?” nilimwuliza yule askari koplo, sababu nilisha wai kusikia habari za vitu hivyo vyenye bei lahisi, “tena huku unaweza kupata kitu kizuri, utazani akija tumika” alisifia yule jamaa, hivyo nikapanga jioni ya siku ile, niende Chake, nikafanye uchunguzi wa mambo mawili, kwanza sehemu ya kufanyia mazoezi ya baskert, sababu sikutaka kusahau mazoezi, pili kuchunguza bei ya vifaa hivyo, ambavyo vita nisaidia kwa kipindi ambacho nitakuwa huku Pemba, sababu sikufikilia kukamilisha uchunguzi, sasa jinni mimi nitalichunguzaje, ukweli nilipanga kukaa miezi kadhaa, kisha nipelekea report ya uongo, alafu nigeuze zangu, kurudi Dar es salaam, “ila bro, kama unaenda Chake, inabidi uwai, kabla awajafunga maduka” alisisitiza yule afande koplo, na mimi nikachukulia kuwa ni msisitizo wa kawada tu! sababu niliona muda bado mwingi sana.***
Ukweli nyumba hii ya kijani ilikuwa imekaa sehemu nzuri sana, ilikuwa inatazamana na makazi ya askari na familia zao, ikitenga nishwa na barabara, ambayo ilikuwa ni ya lami, iliyo kuwa inatoka mjini, kwenda makaani, ambako ni baharini, ikipita Vitongoji mjini, mbuyuni mpaka huko baharini, mbako kulikuwa kuna fahamika kama makahani, baada ya kupanga vifaa vyangu vizuri, ikiwepo na Lap top yangu, ambayo uwa siiachi popotenapokwenda, kutokana na kuwa ndio kifaha pekee cha kutunzia kumbu kumbu, nilicho kuwa nacho, nikaweka vizuri vifaha vyangu vya kazi, ikiwepo pisto (bastora) yangu ndogo sana aina ya A. G. P -5.2mm, hii niliipata Russia inaitwa Automatic Gun Pistor, yenye mzingo wa mm 5.2, nikaifadhi na risasi zake box mbili, camera ndogo, ikiwa ni digtal, kisu kidogo, kikiwa ni Automatic spring knife, ambavyo nilivihifadhi vizuri, kabla sija fwatwa na kuambiwa kuwa natakiwa kwenda kula, ndani ya mesi, hapo nikajuwa kuwa wanajeshi sikuzote ufanya mambo yao kwa ratiba iliyo nyooka, muda wa kula ni muda kula, na muda wakazi ni muda wakati, nikaelekea huko messi ambapo nilikuwa nakula pamoja na maafisa wa jeshi, ambao walikuwa wengi kidogo, hapo licha kuanza kuzoweana nao, na kunifanya nipunguze uoga na upweke, pia niliweza kuanza kusikia habari za hiyo sehemu inayoitwa staring Mess, ambako niligundua kuwa kulikuwa na bwalo kubwa la jeshi, huko mjini, karibu na macho manne, yani wawi, ambapo wakati mwingine uwa kama bar, kwaajili ya askari wenyewe, na raia ambao wanaitaji kuja kupata vinywaji, asa vilevi, ambavyo kwa kipindi hicho, vilikuwa vina patikana hapo pekee, pia hapo hapo kulikuwa na hotel kubwa, kwaajili ya wale maafisa, ata mimi nilitakiwa nikale pale, story zile zilinivutia sana, maana nilisikia kuwa nisehemu iliyo changamka na kufanana na sehemu za starehe kama za tanzania bara, hapo nikapanga kuwa, baadae nikitoka mjini chake chake, nitapitia sehemu hiyo, ili nikapate na chakula cha jioni, kama nilivyo elekezwa.
Wakati tuna kula nika mwona afisa utawala nae akija mle ndani, akanieleza kuwa kama ningependa kwenda kutembea uwanja wa ndege, kuna gari lilikuwa lina mpeleka kiongozi flani, hivyo naweza kupata lifti, na mimi nikasema japo sito enda huko uwanja wa ndege, ila nitapanda mpaka mjini, nikatazame sehemu ya mazoezi, na maduka ya vifaa used, bahati nzuri na yeye afisa utawala akanieleza kuwa, “uwanja wa baskert ball, hupo upande wa hospital ukifika pale kwa nyuma utaona uwanja, jioni kunakuwa na vijana wengi wanafanya mazoezi” alisema yule afisa na kunieleza kuwa ata pale kambini kwao pia, uwa wanafanya mazoezi siku za juma nne na ijumaa asubuhi, nikaahidi kushiliki siku hizo, huku akinieleza kuwa kuna watu uwa wanafanya mazoezi ya mpira wa volley ball, kila siku jioni, kama ninge penda kwenda kushiriki ukweli niwkamba mchezo huo japo nilikuwa naucheza wakati mingine lakini sikuupa kipaumbele kama ulivyo mchezo, wa mpra wa kikapu.**
Naam, saa kumi na robo, ndio muda ambao, nilishuka toka kwenye gari la jeshi, pale chake chake, nikalitazama gari lile ambalo liliendelea na safari yake upande wa madungu, kuelekea uwanja wa ndege, likitokomea zake, mimi nikiwa nime valia tishert na jinsi na raba, nilisimama barabarani, na kutazama kwa mshangao, kushoto na kulia pasipo kuelewa nini kimetokea, hapa mjini, maana akukuwa na dalili ya uwepo wa watu yoyoye mida ile ya saa kumi, hapa mjini Chake chake, kwakifupi usinge weza kuamini kuwa hapa ndio chake chake mjini, ambapo masaa kadhaa yaliyopita, nilipita maali hapa, nakukuta watu ni wengi kweli kweli, lakini sasa palikuwa kimyaa kabisa, ata magari machache yaliyo kuwa yana katiza kutokea macho manne, au upande wa madungu, aya kuwa yakisimama pale Chake chake mjini, lakini kwa mbali sana upande wakuelekea upande wa madungu, nikaoliona duka moja tu, likiwa wazi, kilicho nionyesha kuwa lipo wazi, ni bidhaa na mtu mmoja alie simama nje.
Hapo japo nilikuwa na wasi wasi, lakini nikaanza kutembea taratibu, kueleka ndani ya mitaa, ambayo kosa kuwa majengo ambayo yapo vizuri, tungesema ni magofu, maana akukuwa na watu kabisa, nikatembea taratibu, kufwata barabara inayo ingia ndani ya mitaa, nikizania kuwa, pengine huko ndiko kwenye mji mkubwa na watu wengi zaidi, akukuwa na mtu wa kumwuliza, mji ulikuwa mweupe na kimya kabisa.
Lakini basi, baada ya kuingia ndani kidogo, na licha ya kufwata barabara kubwa za mitaa, sikuona dalili ya mtuu yoyote, bola ata kule barabarani, nilikuwa naona magari, hapo nika pigwa na butwaa, unajuwa msomaji uwezi kupata picha kamili, yani sawa na kwamba, unafika sehemu kama kaliakoo mida hii ya saa kumi jioni, unajikuta upo peke yako, “au wanakimbia majini” ndivyo nilivyo jiuliza, huku natembea taratibu kusonga mbele, Maduka na ofisi zote zilikuwa zimefungwa, zaidi kilicho nionyesha kuwa aya ni maduka, nimajina ya maduka yale, kwenye viambaza, au juu ya nguzo za milango yake
Naam katika zunguka zunguka yangu, niliibukia sehemu moja ambayo, ilionyesha kuwa ni sokoni, tena soko kubwa, ata hivyo, nilikuta sehemu ile imeimesha fungwa, na bidhaa zime funikwa kwa vipande vya magunia, au ma tulubai makubwa, kwenye vibanda vyake, ukweli nilishangaa sana, kiasi cha kusimama kabisa, na kukodolea macho soko lile la chake chake, hapo nikapata wazo la kuitafuta hospital, ili nikaone kama kutakuwa na watu wanafanya mazoezi, kama livyo ambiwa, lakini ile nageuka kutazama mbele nilikokuwa na elekea, usawa wa macho mita hamsini mbele, “mama yangu jinni” nilijikuta nashtuka na kujisemea kwa sauti ya kunong’ona, ni baada ya kumwona mschana mmoja mmoja mwenye urefu wa wastani, ambao ungelingana kidogo na mimi, akiwa amevalia babuibui jeusi lenye kudalidhiwa kwa nyuzi langi ya blue na dhahabu,sikujuwa ametokea wapi, na lipomtazama vizuri, nilibahatika kuona viatu vyake vya mikanda, vyenye rangi ya dhahabu, na visigino virefu, vilivyoonekana kidogo kwenye miguu yake, huku sehemu kybwa ya viatu ikifunikwa na baibui lake jeusi, lililo shonwa kwa mtindo wa kipekee na wakisasa, likiukamata mwili wake vizuri na kuonyesha vyema uumbaji, maana ukiachia hips zake pana na makalio makubwa tofauti na waschana wengi niliopata kuwaona toka alipo ingia ndani ya kisiwa hiki, mschana huyu mzuri ambae alionyesha wazi kuwa ni chotara wa kiarabu alikuwa na sura nzuri kweli kweli, japo alikuwa amefunika nywele zake kwa ushungi, alio ubana kwa pini flani nazo rangi ya dhahabu, lakini niliweza kuhisi kuwa alikuwa na nywele ndefu zilizo lala kwenye mgongo wake, mschana huyu mrembo alikuwa anatembea taratibu kuja upande niliokuwepo, na ukweli ni kwamba akukuwa na njia ya kuchepuka, wala kukatiza, upende wakushoto kwangu kulukuwa na safu ya amaduka, na kulia kwangu, kulikuwa na soko, dada huyu, alitembea kwa mwendo wa madaha huku akinikazia macho, japo usowake ulionyesha tabasamu.
kwa kifupi tulikuwa wawili tu, ndani ya eneo la soko kuu la chake chake, na mbaya zaidi mwanamke huyu niliweza kumfanisha na mwanamke ambae nilisoma sifa zake kwenye maelezo ya mwanamke alie ingia na bwana Abdulkadir, kwenye nyumba ya wageni, na kisha kukutwa ame kauka na kubadirika rangi.
Hapo siku jiuliza mala mbili, nikageuka mala moja na kutazama nilikotoka kisha nikaanza kutembea kwa haraka kurudi nilikotoka, moyoni nikajilahumu kwa kuto kubeba bastora yangu, pengine ningeweza kulitisha lile jinni, (kama nilivyo amini, kuwa yule ni jini) niliendelea kwa mwendo wa kawaida ili lile jinni, lisishtukekuwa nalikimbia lenyewe, huku kila baada ya hatua kadhaa nikitazama nyuma kumtazama yule mwanamke, kama ana nikaribia au bado yupo mbari, ambae nilimwona kama aliongeza mwendo pia, sababu alikuwa anazidi kunisogelea, kila nilipo geuka kumtazama, hapo nikapata wazo la haraka, kwamba nikipata njia yoyote inayochepuka, nibadiri njia, ilinione kama mwanamke huyu atakuwa ananifwata mimi, au alikuwa na safari zake, ili kama ana nifwata mimi ikiwezekana nichukue uhamuzi mwingine wa kujiokoa, na akukuwa na njia nyingine ambayo skuwa na uhakika kama itaniokoa, nayo ni kutimua mbio mpaka barabarani, niliamini kuwa kule barabarani, huyu jinni asinge weza kuni dhuru, zaidi linge yeyuka na kupotea zake.
Niliendelea kutembea sasa nikiwa nimeongeza mwendo, na lipopiga hatua kama kumi mbele, niliweza kuona barabara moja upande wa kulia, nika ifwata hiyo barabara nyembamba kidogo, ambayo niliamini kuwa inaenda kutokea barabara kuu, tena usawa wa lile duka, maana ni upande huo huo, nilitembea mita thelasini mbele, kwenye ile barabara nyembamba, huku nikipita chochoro nyingine nyingi tu ambazo siku zifahamu, zinaelekea wapi, vinginevyo ningeifwata moja wapo, pengine inge kuwa msaada kwangu, lakini hatua tano mbele, nilipo tazamana nyuma, nika mwona yule mwanake nae akikata kona kufwata upande ule ule, nilio kuwepo mimi, “hii pemba pelemba” nilijisemea kwa hofu, ukweli nilihisi miguu inakosa nguvu, lakini nikajuwa nikilegea tu! nita kwisha kweli, nikaongeza mwendo, haraka kuwai mwisho wa barabara hii ambako kulikuwa na kona flani upande wa kushoto, ikionyesha barabara ilielekea barabara kuu, itokayo mkoani.
Lakini nilipo ifikia ile barabara, nika geuka nyuma kutazama, yule mwanamke ninae mkimbia amefikia wapi, hapo nika duwaa kwa mshangao, maana sikumwona yule mwanamke, wawla dalili ya uwepo wa mwanamke huyo, wala dalili ya kiumbe chochote eneo lile, nika tazama kule nilikokuwa na elekea, na huku nazidi tembea kwa speed nikiofia isije kuwa lile jinni likaja kuibuka mbele yangu, sababu ata upande ule nilio zania kuwa naelekea barabara kuu, sikuweza kuona mbele kuna nini, kutokana na majengo marefu ambayo yalijengwa na wa arabu, kabla ya mapinduzi, pamoja na kona fupi fupi, ambazo zilinikinga nisione mwisho wa ile barabara nyembamba, lakini baada ya kutembea kama mita sabini mbele, nika weza kuona barabara, kuu ikiwa mbele yangu, kama mita ishilini au therasini, toka nilipo kuwepo, hapo nikapunguza mwendo na kutabasamu kidogo, huku nikishusha pumzi nzito ya kusema afadhari, maana nilikuwa na uhakika kuwa ile barabara hipo mbele yangu, na kilicho nipa uhakika ni lile duka lililokuwa wazi, mana nililiona mbele yangu, Sasa nilikuwa natembea taratibu kwa kujiamini, huku nikiwa na lisogelea lile duka.
Naam nikiwa nime bakiza mita kama kumi au ishilini, kulifikia lile duka lililokuwa barabarani, ghafla nikamwona yule dada, akiibiuka toka kwenye chochoro moja ya upande wa kushoto ukweli nilitamani kukimbia au kupiga kelele, lakini nikamwona akigeuka na kutazama upande nao tokea mimi, huku sura yake ikiwa katika hali flani ya tabasamu……….
SEHEMU YA 4
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU : Naam nikiwa nime bakiza mita kama kumi au ishilini, kulifikia lile duka lililokuwa barabarani, ghafla nikamwona yule dada, akiibiuka toka kwenye chochoro moja ya upande wa kushoto ukweli nilitamani kukimbia au kupiga kelele, lakini nikamwona akigeuka na kutazama upande nao tokea mimi, huku sura yake ikiwa katika hali flani ya tabasamu………. endelea…….
Kisha akatazama mbele, huku anatembea taratibu, kuelekea upande wa barabara kuu, hapo mimi nikapunguza mwendo, na kuendelea kumtazama yule dada ambae mwendo wake ungesema yupo kwenye jukwaa la walimbwende, huku nikiweza kuona jinsi alivyo jaliwa katika umbo lake, asa upande wa mgongoni.
Naam ilimwona yule mschana mzuri sana, ambae ataka ni jinni, lakini unaweza kujikuta una ingia mkenge, anachepuka nakuingia kwenye lile duka, ambalo wakati napita nikatambua kuwa ni duka la vifaa vya watoto, kutokana na vitu vilivyo kuwepo pale nje, na ndani, ambako pia niweza kumwona yule dada akiongea na muuzaji wa kiume, nilitamani nimweleze yule jamaa kuwa anaongea na jinni, lakini nikaofia pengine na yeye anaweza kuwa ni jinni, maana licha ya kuwa duka kubwa sana, kama super market, lakini akukuwa na mteja yoyote zaidi ya wao wawili, na akuwa na sababu ya kulifungua mida ile, sababu mji mzima aukuwa na watu, sasa anamuuzia nani.
Nikaamua ni jikaushe na kuendelea na safari yangu, lakini macho yangu yenye kieleele yakajikuta yametazama tena kule dukani, hapo nilikutana na macho mazuri ya duara ya huyu dada, ambae sikujuwa alikuwa anaongea nini wakati ule, maana niliweza kuona tabasamu pana sana usoni kwake, japo alikuwa amegeuka kunitazama, nikatazama mbele haraka, na kuongeza mwendo haraka kuingia barabarani, kisha nikaanza kuifwata barabara ya kuelekea macho manne, kule ambako nilikotokea wakati nakuja, nabahati ilikuwa upande wangu, maana sikutembea sana, nilienda kama mita mia ambili hivi, nikasikia ngurumo ya gari, nyuma yangu, kuchek nyuma lilikuwa ni lile gari la jeshi, ambalo lilikuwa limeenda airport, nika shukuru sana kwa kuonekana kwa gari ilo, maana nilikuwa na hofu kubwa ya kutokewa tena na yule jinni mrembo, “vipi umeona hen?, mida hii chake akuna mtu” aliniuliza dereva wa gari lile la jeshi, aina ya land rover defender, huku tunaanza kuondo, kuelekea upande wa kaskazin, yani wete, “mh! mji natamani nirudi dar es salaam ata leo” ilo lilikuwa ndilo jibu langu, ambalo yule dereva alilichukulia juu juu, sababu niliwai kusikia kuwa kila alie kujapemba kikazi lazima aliwai kutamka neno ilo “utazowea tu, ukianza kwenda mess, pale pana changamka sana, asa siku za week end” sikumjibu yule jamaa, zaidi nilizatama upande wa kushoto wa barabara, ambako kulikuwa na njia panda, barabara kubwa kabisa ya lami ilikuwa inaelekea upande huo wenye majengo pia, ambako licha ya safu ya maduka na ofisi zilizo fungwa pia kulikuwa na na jengo kubwa la kanisa, na kingine, kwenye barabara hiyo, kwa mala nyingine niliweza kumwona kijana mmoja wakiume, akija upande wa barabara akiwa juu ya piki piki flani ambazo, kwa watu wa pemba wanaziita Vesper, alikuwa analitazama kwa umakini sana lile gari letu, kwa umakini mkubwa, “ila bro unaonekana kuwa umeichukia sana pemba, maana umekosa amani ghafla” alisema yule dereva wa defender, ambae ni askari wa jeshi la ulinzi, na mimi nikiwa naendelea kumtazama yule kijana ambae ni mtu mweusi asie na mchanganyiko wowote, yani yupo kama sisi wengine, “hapana nazani ni kwaajili ya ugeni tu! kama ulivyosema” nilijibu kwa sauti flani ya kujaribu kujichangamsha, huku natazama mbele, tulipokuwa tunaenda, tukiwa tumeshapita ile njia panda, ambayo baadae niliifamu kuwa inaelekea Wesha, lakini ukweli nikwamba, bado nilikuwa na hofu kubwa sana, juu ya yule mwanamke ambae alikuwa anani fwatilia, ambae mimi niliamini kuwa ni jinni, nasema niliamini sababu sikuwa nimethibitisha kama ni jinni au binadamu wa kawaida.***
Nilipitia pale mess kama nilivyo ambiwa kuwa, ndiyo sehemu ambayo nita pata chakula cha jioni, ukweli mpaka inafika mbili na robo za usiku, namaliza kula, sikuona dalili ya kuchangamka kwa maali hapa, japo palikuwa na mandhari flani ya kupendeza, na watu wachache waliokuwa wanakunywa bia, huku wengine, wakiwa wamekaa na wanawake, ambao mavazi yao kukweli, usinge amini kama hupo pemba, mavazi ambayo toka nime ingia hapa pemba leo asubuhi, siku yaona maali hapa, na wavaaji wa mavazi hayo, walionekana wazi kuwa ni wenyeji wa kisiwa hiki, japo baadhi yao walikuwa siyo machotara, japo wapo waliovalia magauni ya kawaida na miushungi vichwani mwao, lakini pia, wengine walivaa kama ni gauni, basi awakufunika nywele, na zaidi ya hapo basi walivalia tishet na jinsi, nilijiuliza wametokaje kwao, na nguo zile, sikupata jibu, ila hapo baadae tutajuwa wanatokaje, lakini zaidi ya hapo sikuona kitu ambacho kitanifanya nijisikie vizuri kukaa huku pemba, ukizingatia nilisha ona dalili ya kufwatiliwa na jinni.***
Licha ya kwamba story zilikuwa nyingi sana mle ndani, wale maafisa wa jeshi, akiwepo na yule afisa utawala, hapo nika juwa kuwa askari uwa wanafanana hakiri zao, maana wote, walikuwa wakisimulia matuko mbali mbali ya wanawake wao, ambao wengi wao walikuwa wanatokea Tanga, walisimuliana jinsi walinavyo starehe na kupeana vitumbua na waschana hao, lakini mimi siku zifwatilia sana, bado nilikuwa nimepoa, nawaza kilicho nitokea bado sikujuwa kama yule ni mtu au jinni, hivyo sikuitaji kukaa sana, pale messi, nilipomaliza kula nikamweleza yule afisa utawara yani Luteni Simon Malambo, kuwa sito kaa sana pale messi, ambapo maafisa wengi, yani wale wenye nyota walikuwa wana lala pale pale, nae akaangiza gari moja linirudishe kambini, yani kule ahl khamis camp, yani vitongoji.
Naam wakati tuma jiandaa kuingia kwenye gari, yani mimi na yule dereva wagari la jeshi, ambae ni askari mwenye umri kama wangu, ambae akuwa na harama yoyote mabegani mwake, ila walimwita private, kama cheo chake, mala likaingia range Lover moja rangi ya silver, linang’aa kwa upya wake, ambalo likuja na kusimama pembeni yetu, yani pembeni ya gari letu, la jeshi la ulinzi, lile land Rover defender, ilichukuwa kama dakika mbili hivi, mpaka mlango wa gari kufunguliwa, na ilifunguka yote miwili ya mbele, yani wadereva na wa abiria, ukweli mimi ni mmoja wawatu ambao walitamani kuwaona watu waliokuwa wanashuka toka kwenye lile gari la kifahari.
Naam hapo nilimwona mwana dada mmoja mzuri sana, japo akuwa chotara, lakini uzuri wake ulionekana wazi kabisa, mschana ambae alikuwa amevalia gauni la kawaida na mtandio kaulaza mabegani, akiachia nywelezake nyeusi na ndefu zionekane kwa uwazi kabisa, na wakati na shangaa yule mwanamke, nika kumbuka kuwa ajaja peke yake, nika tazama upande wa mlango wa dereva, hapo nika shtuka kidogo, maana nilikutana macho kwa macho, na kijana yule ambae nilimwona masaa machache yaliyopita anatokea barabara ya kanisani, yani ile yawesha, ni yule alikuwa anaendesha pipiki aina ya Vesper, na kilicho nishangaza na kunishtua, ni kwamba kijana huyu, ambae akuwa na chembe ya uchotara, mchana alikuwa na Vesper, na sasa ana range rover, tena ya kifahari ambayo ingenunuliwa kwa fedha nyingi sana, hakika niliona hajabu sana, lakini sikupenda kuliweka lile kichwani, sababu uwe sipendi kuumiza kichwa kwa mambo ya mtu mwingine, ila kwamwonekano huyu, kijana ambae kiumri anaonekana kunizidi kidogo sana, kama siyo yeye basi nyumbani kwao wanauwezo mkubwa kifedha, japo uvaaji wake ulikuwa ni wakawaida tu, hiyo ni kwa jinsi mimi nilivyo ona, “salam aleykum” alisalimia yule jamaa, alie kuwa anamtazama yule dereva niliekuwa nae, huku ana geuza usowake kuni tazama, hapo nikamwona akishtuka kidogo, “aleykum salaam, niaje Usi” aliitikia yule dereva mwanajeshi, akionyesha kumfahamu yule jamaa, ambae na mimi nililifahamu jina lake kuwani Usi, “poa dogo, naona leo mapema unasepa zako” alisema yule jamaa yani Ussi kwa rafudhi ya kipemba, “hapana bwana, nampeleka huyu mshkaji alafu na geuka sasa hivi” alisema yule dereva ambae mpaka dakika hiyo sikuwa na mfahamu jina, “ok! kumbe naye ni kamanda” alisema Usi, huku ananitazama, akionyesha kuwa nikama alinikumbuka, kama mimi nilivyo mkumbuka, “hapana huyu ni mwalimu wa computer pale fidel castor” alisema yule dereva, huku nikisoma jambo jingine kwa huyu jamaa, anaeitwa Usi, kiukweli tokea alipoingia hapa alikuwa ananitazama kwa macho flani hivi, ambayo nilishindwa kuya elewa ni macho ya nini, sababu ni mala yangu ya kwanza kukutana nae na nilikuwa na uhakika kuwa anifahamu, “ok! karibu pemba kaka” alisema yule jamaa, huku ana funga mlango wa gari lake, kisha akaingia kwenye gari na kumshika mkono yule mwanamke wake, alafu wakaelekea mlangoni, tayari kuingia ndani ya ukumbi, ule wa messi, huku na sisi tukianza safari ya kueleka kambini, kule vitongoji.***
Ukweli nilizidi kushanganyikiwa kwa jinsi mambo yalivyo kuwa yanaenda, asa juu ya yule mwanamke, ambae ukiachilia uzuri wake, ila lile tukio la kunifwatilia alafu akatoweka na kuibukia mbele yangu, liliniogopesha sana, ukichukulia ni siku yangu ya kwanza tu ndani ya pemba, usiku kucha niliwaza juu ya jambo ilo, likininyima raha, na aman, niliona naelekea kupoteza maisha, hakika nilitamani siku ya pili nidondoke zangu kurudi D res salaam, lakini ninge waeleza nini kule makao makuu, ukizingatia waliniamini na kunifanyia maandalizi makubwa na kunipatia fedha nyingi sana, kwaaji ya safari hii.
Siku yapili asubuhi, niliamka mapema na kueleka shuleni ambako nilikutana na mwalimu mkuu, ambae alinielekeza kwenye ofisi ya walimu wenzangu, yani staff ofisi, ambako nilikutana na walimu wengu sana wakike kwa wakiume, ambao kiukweli uvaaji wao, ulikuwa tofauti na mimi, ambae nilikuwa nimevalia tishirt na jinsi, na chini nilivalia raba, ndiyo vazi ambalo nalipenda sana, “salamu aleykum” nilisalimia mala baada ya kuongia ofisini, walimu wenzangu wakaitikia kwa pamoja, na hapo mwalimu mmoja wakike akanionyesha sehemu ya kukaa, yani meza na kiti, na mimi nika weka vitabu na makablasha juu yameza ile ambayo ilikuwa karibu na meza ya mwalimu mmoja wa kike, ambae licha ya kuwa na kiuchotara kwa mbali, lakini kiukweli alikuwa ni mzuri asawaaaa, na kwakuzingatia aliyo niambia mwalimu mkuu, nikajifanya kumpotezea, “naitwa mwalimu Aisha, karibu sana pemba” aliniambia yule mwalimu wakike, kwa sauti yake nyororo yenye rafudhi ya kipemba, huku ananipa mkono, kama salam, na mimi nika mpa mkono, “asante sana, mimi naitwa mwalim…” kabla sija malizia, akamalizia yeye, “mwalimu Eric, tulipata habari zako toka jana, lakini ukaondoka bila kuja kutusalimia” alisema Aisha, huku mimi nikisilizia jotola kiganja chake cha mkono, ambao akudumu sana kwenye mkono wangu, tukaachana, “nikweli maana niliwai kupumzika, siunajuwa usafiri wa huku kwenu, nilikesha kwenye meli usiku kucha” nilisema huku najitaidi kumtazama usoni mschana huyu, ambae kiumri nikama nilimzidi kwa miaka kati ya miwili au mitatu, “kwanini ukupanda express, na ukapanda meli kubwa?” aliuliza Aisha na kuni ng’amua ku kuna meli za express, “sikujuwa kama kuna meli za hivyo, zinatumia muda gani kutoka dar es salaam?” niliuliza kwa mshangao, ikionyesha wazi kuwa sikuwa najuwa.
Tuliongea mengi na Aisha, ambae akuwa na kipindi asubuhi ile, alinieleza kuhusu, ratiba boti ya express, ambayo ilikuwa inakuja pemba jumanne ijumaa na jumapili, wakti mwingine jumamoss, kwa gharama ya tsh elfu thelasini na tano, na utimia masaa matano mpaka sita, “dah! kumbe nilibugi, au sababu nilikata tiketi jumatatu” nilisema kwa sauti ya kujilahumu, maana licha ya kukata tiketi jumatatu, nilisafiri jumanne, siku ambayo kulikuwa na bot ya express.
Tuliendelea kuongea, na kuzoweana kwa muda mfupi, ata mida ya chai, yani saa nne, ilinilazimu kuacha kwenda kule kambini, baadae yake tulienda pamoja na aisha kwenye mgahawa ambao, walimu wenzangu walikuwa wanaenda kununua chai kwa asubuhi na chakura cha mchana, ukweli siku kifurahia kwa sikuile ya kwanza, maana akukuwa na kitafunwa kingine zaidi ya mikate midogo iliyo uzwa shilingi mia mia, ikifahamika kwa jina la bofolo, nililazimika kunywa chai ile, na mimi ndie nilie lipia, huku nikiendelea kuongea na Aisha, ambae muda mwingi alikuwa ananitazama kwa macho ya udadisi, “Eric hivi umesha owa weye” aliniuliza Aisha, huku anacheka cheka, wakati tuna rudi ofisini, “bado sijaowa vipi wewe umesha olewa” nilimwuliza Aisha, ambae pia alitabasamu kabla ya kunijibu, “niliwai kuolewa, lakini niliachika mume wangu akutaka nikasome” alisema Aisha, hapo nika tulia kidogo kutafakari aina ya mwanaume wa Aisha, “basi kama ujaowa utapata mke huku pemba, kuna waschana wazuri tu” alisema Aisha, ikiwa ni mtu wapili ananieleza jambo ilo, “mh! pemba siwezi kuowa, nita juwaje kama huyu ni mtu na huyu ni jinni?” nilisema kwa namna flani ya kushtuka, kiasi cha kumshangaza ata Aisha, ambae aliangua kicheko, kiasi cha wanafunzi wa kidato cha tatu, kuchungulia dirishani, “nani kakuambia pemba kuna majini kiasi hicho?” aliuliza Aisha, huku akiendelea kucheka, hapo nikatulia kidogo na kuongeza umakini katika maongezi yale, maana nilisha ona kuwa sitakiwi kukulupuka ila naitaji kupata habari flani, toka kwa Aisha, asa ziusuzo majini, “unataka kuniambia kuwa pemba akuna majini?” nilimwuliza Aisha, ambae alikuwa anamalizia kucheka.
Hapo tuka simama kabisa, nje ya ofisi yetu, “izo ni habari tu, mi mwenyewe toka nimezaliwa mpaka sasa nafikia miaka 22, sija mwona jinsi wala binamu yake jinni” alisema Aisha, ambae niliona ni mtu anaejaribu kunitoa wasi wasi, maana jana nilimwona mtu ambae niliamini kuwa ni jinni kabisa, “hapana Aisha inamaa ujawai ata kusikia kuhusu majini?” nilimwuliza tena Aisha, ambae alitazama saa yake ya mkononi kisha akajibu, “kutokana na vitabu vya dini, majini yapo na yaliumbwa kabla ya binadamu wa kwanza, majini wapo sehemu zote duniani, na wao ni kama sisi, wapo wakorofi na wapo wapole, awawezi kumfwata mtu bila sababu za msingi, japo kwa elimu nyingine ni kwamba wapo majini wabaya ambao utumiwa na watu kwenda kutenda uovu” alinieleza Aisha, ambae mala kwa mala alikuwa anatazama Saa yake, “kwahiyo unataka kuniambia kuwa jinni kama jinni, awezi kukuona njiani na kuanza kukufwata?” milimwuliza Aisha, nikiitaji uhakika wa kile nilicho kiona jana, kule chake chake mjini, “inawezekana Jini akakufwata, ni kutokana na sababu, pengine unajanaba, alafu umeita sehemu ambayo kuna hao majini” alinijbu Aisha, “kwahiyo jinni awezi kukupenda tu na kuamua kukufwata uwe mpenzi wake” nilimwuliza Aisha, ambae alianza kwa kutabasamu, “nasikia kuwa inatokeaga mala chache, jinni kutokea kumpenda binadamu, lakini sijawai kusikia kwa ukaribu swala ilo, nacho fahamu mimi binadamu mwenyewe kumpenda jinni, pasipo kujuwa, na jinni kumkubari kwa lengo la kumwadhibu, lakini pia kuna habari za jinni la kike, ambalo mwenzi mmoja uliopita limetoka kuuwa mtu kule madungu, guest house habari za jinni hilo nilianza kulisikia toka tunasoma shule ya msingi pale Msingini Primary, lilisha wai kuuwa wavulana wanne, ilo ndilo ambalo naweza kusema kuwa ndilo jinni ambalo la kwanza kusikia habari zake, lakini siyo kuliona kwamacho” ilo lilikuwa jibu la Aisha ambae aliniaga kuwa anatakiwa kuingia darasani, maana muda wa kipindi chake umesha fika, japo majibu yake ya mwanzo yalianza kunitoa wasi wasi, lakini ili la mwisho lilinirudisha kwenye wasi wasi, na uoga mkubwa, usiniulize naogopaje wakati ni bastora, jinni uwa afi kwa risasi.***
Saa nane na nusu, ndio muda ambao, kengere ya wanafunzi kutoka darasani ilisikika, ndio muda ambao mwalimu Aisha alitoka darasani, niliagana nae na kuahidiana kuwa tuta kutana kesho, siku ya alhamisi, mwalimu Aisha alipanda kwenye basi la shule, ambalo kikawaida upandwa na walimu na wafanyakazi wa shule tu, na siyo wanafunzi, ambao niliwaona wakipita mbele ya ile nyumba ninayoishi, yani nyumba ya kijani, na mimi nikiwa nimekaa kwenye ngazi nje ya nyumba ile, kabla sija ingia ndani, kwa lengo la kutafakari yale niliyoelekezwa na Aisha, ambae aliaidi kuwa week end ata nipeleka mjini kwenye maduka ya watu anao wafahamu ambao wataniuzia vitu kwa bei ya chini kidogo, .
Niliweza kuwaona wanafunzi wakiendelea kupita barabarani, barabara iliyopo mita kama ishilini tu toka kwenye nyumba ile ya kijani, huku wanafunzi wakike wakionekana kunitazama sana, kiasi cha kunifanya niingie ndani, kukwepa macho ya waschana wae ambao kiukweli macho yao ayakuwa ya awaida, yalijaa hali flani ya kuitaji, na mimi niwatazame.**
Jioni ya siku ile nilipelekwa kule mess kupata chakura cha jioni dereva wa siku ile akuwa yule wajana, leo alikuwa na cheo cha koplo, yani alikuwa na alama mbili za V, niifahamu kuhusu vyeo vya kijeshi nilipokuwa na nasoma CUBA, na siku ile niliamua kukaa kidogo ili nitazame jinsi inavyo kuwa eneo lile, ambalo inasemekana kuwa ndiyo sehemu pekee, ambayo mtu yoyote ata wale wenye kipato kidogo, wanaweza kwenda kustarehe.
Nikiwa nime tulia kwenye meza moja peke yangu, na kunywa bia taratibu, huku watu wakiwa wachache, japo walionekana mmoja mmoja wakiingia pale ukumbini, ambapo ata music ulikuwa unasikika kwa sauti ya chini, mpaka baadae kidogo ndipo niliweza kuona mambo mengi sana usiku ule, ni mala tu baada ya sala ya Insha, yani kuanzia mida ya saa mbili na nusu, ndio muda ambayo watu walianza kumiminika pale Staring mess.
Mpaka saa tatu, tayari ukumbi ulikuwa umeshajaa, wanawake na wanaume, askari kwa raia, wote walikuwa wanaendelea na burudani zao, za kunywa pombe na kucheza music, ata mimi nilishanza kuhangamka, na kuondokewa na unyonge ambao toka nije pemba, ulikuwa umenishika, nikama nilisahau kuwa nipo pemba kwa sasa.
Hakika aikuwa pemba ile niliyo iona jana, leo asubuhi mpaka mchana, hakika watu walikuwa wameshangamka kweli kweli, hakika ilinifariji, japo sikutaka kulewa sana, kutoka na kwamba kesho yake niliitajika kwenda pale shuleni, hivyo isingekuwa vyema niende nikiwa na hang over, nilweza kuwaona baadi ya watu wakipita na kutazama pale nilipokaa, kama vile wanajiuliza huyu ni nani, nika gunduwa kuwa wakazi wengi wa kisiwa hiki wengi wanafahamiana, hivyo ata akiingia mgeni lazima ata onekana wazi kuwa ni mgeni.
Naam katika kung’azang’aza macho nikamwona Ussi, yule jamaa wajana, akiwa ametulia kwenye meza moja, ambayo ilikuwa mita chache kutoka kwenye ile meza niliyokuwepo mimi, yani tulitenga nishwa na meza moja tu! katikati, akiwa na mschana mwingine, ambae siyo yule wajana, wakiwa wamechafua meza kwa vinywaji, huku kasha zima la sigara likiwa lime lala mezani, kwakifupi nikajikuta nayapenda maisha ya jamaa huyu, ambae alionekana kutokea kwenye maisha ya kitajiri sana, “niambie brother naona umekuja kuchek, jinsi wapemba wanavyo jiachia” niligutushwa na sauti ya mtu toka toka upande wangu wa kushoto, nika geuka na kumtazama………..
Itaendelea.........
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo WHATSAPP 0743433005
Tags
simulizi