TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

13 HOURS IN BENGAZI

Setting yake ni mwaka 2012, baada kupinduliwa na kung'olewa madarakani Muammar Gaddafi hivyo mji wa Benghazi nchini Libya ukawa ni mojawapo ya maeneo hatari zaidi duniani 

Nchi zote zenye ubalozi mjini benghaz wakaamua kufunga ofisi zao kasoro ubalozi wa Marekani tu, na maili moja kutokea ubalozi wao kuna kituo cha siri cha CIA ambacho kinalindwa na wanajeshi maalumu wa siri.

 Balozi wa Marekani Chris Stevens anaingia Benghazi february 17 mchana ili kudumisha uhusiano wa kidiplomasia wakati huo kukiwa na machafuko makali ya kisiasa 

 Maghrib ya siku hio hio aliowasili bwana Stevens kundi la wanamgambo wa Ansar al-Sharia  wanaamua kuvamia ubalozi wa marekani.  

Walinzi wachache wanashindwa kuzuia uvamizi huo na balozi anajificha kwenye safe room na mtaalamu wa IT, wahuni kuona jamaa kajifichia uko ndani wanaamua kulichoma moto jengo hilo wakitumaini kumuua balozi na waliosalia umo ndani.

kambi ya timu ya CIA inapata taarifa inataka kwenda ubalozini kusaidia, lakini Chief wa CIA anakataa kwa kuhofia kwamba kuondoka kwa timu hiyo kungefichua uwepo wao hapo

 Mwisho jamaa wanaamua kwenda kibabe, wanafanikiwa kuingia kwenye jengo wakimtafuta balozi ila hawakupata hata mwili wake, baada ya mapigano makali walifanikiwa kurudi kambini, wajamaa wanawafata huko huko, ni usiku wa deni, usiku mrefu katika maisha yao

wanaomba msaada jioni alafu msaada unaingia alfajiri 😂, ni masaa 13 ya moto ndani ya mji wa Benghazi, kama unapenda movie ngumu za kivita itafute hii hutojutia kuangalia, nimeiweka kwenye group la telegram kaipakue bure,link ya group ipo
 sehem ya comment 👇

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

2 Comments

Previous Post Next Post