NIAMINI
Hapo zamani za kale alikuwepo kijana mmoja fukara sana, aliishi maisha ya tabu baada ya kutafuta kazi na kuchoka 😥😥
Kipindi hiki alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja ambaye ni rubani, kusema ukweli walipendana sana tangu utotoni ✈️✈️
Siku moja kijana alihitaji kuwasiliana na mpenzi wake, alituma SMS lakini hazikujibiwa, hofu na mashaka yalikuja juu yake, akajiuliza mpenzi wake ana tatizo gani maana katika mahusiano mawasiliano ni kitu cha muhimu sana ☎️☎️
Baada ya binti kutoka kazini na kabla hajarudi kwao, alipita kwanza kwa mpenzi wake kumwambia kila kitu;
"Samahani sana Baruti wangu, najua umechukia lakini sijafanya makusudi kutojibu SMS zako, ukweli ni kwamba sina salio ndio maana nimekuja kukuona, siwezi kukupoteza maishani mwangu, nakupenda kuliko kitu chochote, wewe ndio ua na pumzi ya maisha yangu"
Kusema ukweli yalikuwa ni maneno ya dhati toka moyoni mwa huyu binti, kijana akatoa elfu moja akampa mpenzi wake akanunue vocha, binti alipokea kwa mikono miwili na kushukuru, akuamini katika maisha yake hatakuja kupata mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kama yule, ila ukweli ni kwamba huyu binti ana kazi nzuri, mshahara wake kwa mwezi ni milioni 10 lakini amepokea elfu moja toka kwa mpenzi wake, kijana hakumpa kisa tu mpenzi wake alikuwa na kazi nzuri hapana, ni moyo wake uliridhia, haya ndio mapenzi bhana....!!
Sasa siku moja kijana aliugua sana, hakuwa na pesa ya kwenda hospitali, binti baada ya kusikia hivi alijisikia vibaya sana, akatoka kazini kwa ajili ya kwenda kumuona mpenzi wake, aligharamia kila kitu kwa mshahara wake na kuhakikisha mtu wake anapona, akamuachia na laki 5 imsaidie kwa mambo mengine pale hospitali 🏨🏨
Siku zikapita, kijana akapona, binti akiwa kazini alipoteza simu yake yenye gharama kubwa sana aliumia moyoni, kijana wake ambaye kwa sasa ni boss katika kampuni moja akachukua simu yake kubwa akampa mpenzi wake kisha yeye akaenda kununua kitochi...!
Kusema ukweli mahusiano yao yalikuwa ni ya ushirikiano mkubwa 🤝🤝
Baada ya siku kupita sasa, huyu binti akanunua gari la milioni 20🚙 mpenzi wake akimnunulia gari la milioni 35 🚗
Baada ya mwaka kupita waliingia katika ndoa rasmi baada ya kukamilisha dhamira yao, waliishi kwa upendo na furaha 🥰🥰
𝗖𝗛𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗙𝗨𝗡𝗭𝗔
𝗝𝗲 𝘂𝗺𝗲𝗷𝗶𝗳𝘂𝗻𝘇𝗮 𝗻𝗶𝗻𝗶 𝘁𝗼𝗸𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗱𝗶𝘁𝗵𝗶 𝗵𝗶𝗶, 𝗷𝗲 𝘂𝗻𝗮𝘁𝗮𝗺𝗮𝗻𝗶 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝗵𝗶𝗶?
𝗞𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗲𝘁𝘂, 𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗮 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝘆𝗮 𝗮𝗶𝗻𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝗻𝗶 𝘃𝗶𝗴𝘂𝗺𝘂 𝘀𝗮𝗻𝗮, 𝘂𝗻𝗮𝘄𝗲𝘇𝗮 𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝘀𝗵𝗶𝗱𝗮 𝗹𝗮𝗸𝗶𝗻𝗶 𝗶𝗽𝗼 𝘀𝗶𝗸𝘂 𝗺𝗼𝗷𝗮 𝘂𝘁𝗮𝗳𝗮𝗿𝗶𝗷𝗶𝘄𝗮
𝗧𝘂𝗻𝗮𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝗻𝗶 𝗶𝗺𝗮𝗿𝗮, 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝘀𝗮𝗶𝗱𝗶𝗮𝗻𝗮 𝗻𝘆𝗮𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘇𝗮 𝘀𝗵𝗶𝗱𝗮 𝗻𝗮 𝗿𝗮𝗵𝗮, 𝗸𝘂𝗽𝗲𝗻𝗱𝗮𝗻𝗮, 𝗸𝘂𝘃𝘂𝗺𝗶𝗹𝗶𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗶𝘀𝗵𝗶 𝗽𝗮𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗵𝗮𝗹𝗶
𝗠𝗽𝗲𝗻𝗱𝘄𝗮 𝘂𝘀𝗶𝗸𝗮𝘁𝗲 𝘁𝗮𝗺𝗮𝗮, 𝗺𝗮𝗽𝗲𝗻𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗸𝘄𝗲𝗹𝗶 𝗯𝗮𝗱𝗼 𝘆𝗮𝗽𝗼, 𝗺𝘂𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗮𝗸𝘂𝗽𝗮𝘁𝗶𝗲 𝗺𝘁𝘂 𝘀𝗮𝗵𝗶𝗵𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘆𝗮𝗸𝗼 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗲 𝘂𝗻𝗮𝘁𝗮𝗺𝗮𝗻𝗶 𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮𝗲
𝗪𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗪𝗔𝗞𝗢 𝗨𝗧𝗔𝗙𝗜𝗞𝗔 🏃🏃
𝗜𝗺𝗲𝘁𝘂𝗻𝗴𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝗱𝗶𝗸𝘄𝗮 𝗻𝗮;
𝗝𝘂𝘀𝘁𝗶𝗻 𝗕𝗮𝗿𝘂𝘁𝗶,
𝗠𝘁𝘂𝗻𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝘄𝗮𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗶 𝘄𝗮 𝗿𝗶𝘄𝗮𝘆𝗮, 𝘁𝗮𝗺𝘁𝗵𝗶𝗹𝗶𝗮, 𝗵𝗮𝗱𝗶𝘁𝗵𝗶 𝗳𝘂𝗽𝗶 𝗳𝘂𝗽𝗶 𝗻.𝗸
+255752 474 397
Tags
HadithiFupi