*ROYAL TOUR❤*
*1-6*
*By SIMULIKA NASI*
*_____________________________________*
*SEHEMU YA KWANZA*
Royal tour, Royal Tour , hizi ndio zilikuwa habari zilizokuwa on trend chuoni kwetuu , kila mahali ilikua ikiongelewa hii tour
Sio last year wala sie hapa first year , kila mtu alisema lazima niende lazma niendeee
Hata mimi nilisema lazma niendee yaan afe kipa afe bekiii lazima niendeee 😅😅
Chuo bwana kiliandaa Tour , wakaipa Jina Royal Tour unajua kwanini 🤗🤗
Yaan pale chuoni kwetu bwana watoto wa ma don walikuwa kibaooo kwahiyo hii ilitakiwa kuwa tour ya kifalme ,tuende ki boss tuvimbee huko full kujiachiaaa wakasema tunaenda kwenye mbuga flan hivi huko kila mtu akaoneshe 😅😅
Yaan sie bwana , Kile chuo mi sijui nilienda bahati mbaya mwaya mimi baba angu hana hata pesa ki vileeee😊😊mana nyumbani kwetu kugombana na kaka zangu kisa njaa inauma hicho kitu cha kawaida sanaaaa afu sie tumelelewa na baba etu tu kitambo sana mama aliikimbiaga njaa 😔😔😔 akasema kabisa baba atampa shida ya vidonda vya tumbo akatuacha mpaka sisi et alienda hapo hana watoto sie tusimpe mzigo wa kipuuzi akaondoka bila hata mtoto mimi ndie nilikuwa wa mwisho baada ya kaka zangu wawili
Afu wakati mama anaondoka nilikuwa mdogo kwahiyo mapenzi ya mama hata siyajui
Mi najua tu mapenzi ya baba angu na kaka zangu yaan wananipenda hao mi yai laooo ukijichanganya hapaa unavunjwa mguu, ukiwa mwanaume kaka angu mkubwa alinambia ,Salma nikimjua msela wako walai namkata kikojoleo chakee😅😅🤣🤣🤣🤣🤣
Nikamwambia kaka mie hata sina tabia mbayaa ujuee😅 akasema we kazana tu , sema tu mie nilikuwa mcharuko mcharuko ila sikuwahi kujua hata hao wanaume
Kaka zangu wao waliacha shule kitamboo wakazama mtaani kutafuta maishaaa nguvu zao zote waliweka kunilea mimi na kuhakikisha nasoma vizuri na baba walimwambia apumzike wao watapambana
Nimesoma kwa bidii sikutaka hata siku moja kuwaangusha kaka zangu, shule ya msingi nilikimbiza hatari ,nimeingia sec nilikuwa nawabeba mpaka wanaume , nikaenda Five na Six nilisoma kwa kufadhiliwa na wazungu flani hivii , na hao ndio waliamua kunilipia chuo baada ya kuona nipo Serious na masomo
Sasa kile chuo nilichoenda kilikuwa chuo cha watoto wa ma fogi(matajiri), nilijukuta mimi na baadhi sana tupo pale kwa msaada wa wazungu , ila bwana kaka zangu kawakuwa wanyongee niliambiwa chochote nachotaka niseme kuliko kuingia kwenye mahusiano na mafataki siku hizi wanawaita et ma sponsor 😅😅😅ila vidada vimaraya bwana , vimeona vijitetee Kuwaita mafataki et sponsors 😂😂😂 sio shida zangu miee wala sikuwa na muda na sponsor kwanza kaka lisema tabia za wadada wa chuo ni chafuu kwahiyo mie nijitulize nikasema usijali My broh nyie ni zaidi ya wazazi wangu ani😘😘😘
Much love kwenu na Respect kama yotee🥰🥰🥰Mpaka leo nipo chuo heshima kwenuu na sifanyi mchezo kwenye masomo nakimbiza kweli, nguo zangu zote yaani nguo za mitoko huwa napewa pesa na kaka zangu nisiwe mnyonge chuooo , kula bata uhuru nimepewa ila huwa siutumii hata vibaya bwanaaa😘🤗🤗🤗
Basi ndio kuna tred ya watu kwenda tour tena ilipambwa na kupigiwa debeee hatar kila mtu akawa na kiu ya kwenda huko kila mtu anahamu ya kwenda huko ni hatari
"Salma ushatoa helaa??" Shoga angu aliniuliza kuhusu kutoa pesa ya tour hapo imepita kama siku nne tangu tangazo litoke
"Nishaongea na ma broh hiyi issue ndogo sanaa" nilimjibu nikiwa na uhakika siwezi feli japo mpunga ulikuwa mrefuu mmmh ila nikaona kina kaka nishalifikisha hilo fasta tu mambo yanakaa sawa
"Yaan natamani iwe hata kesho shoga anguu Uuuh can't imagine itakavyokuwa hivyo aaaweeeeeh"
"Hahaha we mpuuzi kweli ushatoa"
"Ohoo kitamboo mbaba wangu anakazi gani dudu nampa kila siku"
"Hahaha..."
Tulikua tunaongea wakati huo tunatoka zetu kwenda home
Huyu shoga angu huyu nae yupo hapa kwa ufadhili yaan kati ya watu wachache tulio fadhiliwa yeye pia ni mmoja wao, lakini yeye amelelewa na kukua kwenye kituo cha watoto yatima kwahiyo hanaga ndugu
Ana masponser mpaka keroo yaani ..
Tuliachana mi nikasepa zangu home, nilimkuta kaka angu yule mdogo yaan wapili kuzaliwa
Alipo niona tu akaniuliza we ulikuwa unataka lini ile pesa ,Nikasema mambo ndo hayaa weuweee 🥰🥰🥰
Nikamwambia kaka J3 ndio safari mwisho wa kulipa pesa ni ijumaa akasem poa hii hapa basi nikahesabu mpunga (pesa) imenitimia na ya akiba ipo akaniuliza una nguo ,nikasema nguo ninazo za kutambia asante kaka angu akasema usijali nilimkiss nampenda kaka angu yaani mi nawapenda wote na wote wananipenda mno..
Sasa hiyo siku bro amenipa pesa ilikuwa jumatano ambayo alihamis ndio nikalipe na ijumaa ni mwisho wa kulipia , nilikuwa na raha zote nikachukua beg yangu nilipanga nguo vizuri , mitoko yangu ya uhakika mamaaa🥰😊🥰😊
Siku yenyewe ndo nikalipe pesa ya Tour nyie ng'ombe wa maskini hazani akizaa anazaa dumee , mi wangu alizaa kabisa tena jikee ila ndo lilikufa siku yake ya kwanza tu duniani mweeh😥😥
Siku enyewe naamka najianda kwenda Chuo baba si akaanguka kwenye mpapai alipanda kuangua papai jamani baba yangu huyu umri wake wenyewe umeenda et anapanda juu sijui alikuwa anawaza nini afu asubuhi asubuhi tu jamniðŸ˜ðŸ˜
Akaanguka chini wakati huo wote tulikuwa hatujatoka , tukasikia puu kutoka baba yupo chini anavuja damu puani
Jamani tulichanganyikiwa alikuwa hawezi kusimama ,ilibidi haraka tumpeleke hospital
Alikuwa amevunjika mguu na mkono na kiuno kimeshtuka mweeh , gharama zikawa kubwa za kumtibu nyiee nitafanyaje sasa ilibidi kaka anambie nitoe ile hela ye akaforce leo mpaka jioni ataniletea kesho nikalipe daah...
*SEHEMU YA PILI*
ilibdi tu nitoe huku uhakika wa kupata tena pesa ndo hakuna kabisaa , siku hiyo sikuingia class mana tulikuwa na heka heka za kumuuguza baba
Ijumaa asubuhi kaka aliniita akanisihi sana yaan kaka angu alikuwa anaongea huku anahangaika kutafuta neno la kuniambia ili tu nisimfikirie sijui vibaya au nisiwe mnyonge yaan basi tu 😥😥
Ila kikubwa bwana mishe zake zimefel et yaani mimi sintaenda tour kaka alinipa maneno kibao ya kunitoa wasi wasi , sikuonesha mfadhaiko mana hata hivyo baba alikuwa bado yupo hospital afu ali yake ni mbaya bado daah basi bwana ng'ombe wa maskini hazai .....
Nilienda chuo hiyo siku nimenyongea sana kwanza hali ya baba afu na Tour siendi na nilivyokuwa nimeipania Awee roho iliniuma mnoo ,
Na hiyo ndo ilikuwa siku ya mwisho kutoa hela ,hapo zijulikane mbivu na mbichi
Yaan baada tu ya kufika chuo aaah nikasema baba angu ni muhimu haya mambo yapo tu bwanaa mbona kina kaka wananipa kila kituu, kwahiyo nilidharau nikajipa mood, sikutaka kujiweka kinyoooge hata sikutaka ..
"Kwahiyo Salma we kweli huendi??" Shoga angu eliza alikuwa kama bado haamini kila muda aliniuliza hili swali mi nacheka tu
"Kwahiyo hutaki au huamini eeeh" nilimuuliza namie huku nacheka , hapo tulikuwa nje kwenye kibweta pale pale chuo
Tulikuwa tumenunua zetu chips hapo na juis tunakula na vistory vya hapa na palee
"Aaah umezingua bwana , sa mie nitapata wapi kampani jamanii aah"
"Wee sasa nikatazie baba angu asilipiwe matibabu kisa tu niende mie kwenye ujinga aah wee !! Wakati mwingine nitaenda"
"Wakati mwingine wapi?? Linii?? Hii ndio ilikuwa tamuu , salma bwana umezingua!!"
"Sa nimezingua nini elizaaa??"
"Nakwambia kila siku tafuta danga mjini kunataka mipango au we unajiona mtoto enhee "
"Akaa!! Mi bado mtoto mwenzangu sitaki habari zenu hizo ,bikra yangu natunza kwa mume wanguuu!!"
Tulicheka wotee baada ya kusema nitatunzaa bikra yangu
Eliza alicheka sana akanambia
"Acha ushamba wewe ,Bikra mambo ya kizamani kweli sijui upoje wewee, yaan kwanza siku hizi bi harusi ukiwa bikra huna issue dada we wa wapiiiii???"
"Weeee niache bwana "
"Mkubali yule baba Salma hivi unajua anakupenda ki ukweli , sema sasa hivi mi nimpigie simu analipa chap kabla muda haujaisha"
"Weee eliza yule babuuu???"
"Ana ubabu gani naweweee , mpe uone kama ni babu"
"Akhaaa anifiee, si ki babu kile eliza jamani mmh hapana mwenzangu "
"Hahaha yaan wewe unapishana na Gari ya mshahara "
"Acha tu inipite dada na liendeeee , kama kile kizee"
"We bwana sio mzee "
kuna huyo mbabu mi namuona babu japo eliza amekuwa akipinga mara kinao anasema et ni mbaba sio babu , yaan huyu ameanza kunitaka mie muda mrefu sana ni mfanyakazi kwenye shirika la bina za afya ni Manager, huyu mzee anapesa yaan sio hela pesa za kuchezea na mie nimemjua kupitia Eliza nae amenijua pia kupitia eliza ,
Amekuwa akinitaka muda sanaa, akhaa mi bado bint ndio kwanzaa naitafuta miaka 20 mwaya yaan sijafikisha 20 kamili ila nakaribia bado miezi kadhaa mbele nifike huko , afu niende kutembea na mbaba ambae sina hakika kama hajamzidi baba yangu hata miaka miwili aisee, sema tu mzee hana hela anaonekana amechoka mwili .
Nikamwambia eliza twende bwana karibu kipindi kinaanza huko, hapo kula tulikuwa tumemaliza kabisa , tumekaa kupiga umbea
"Kwahiyo nimpigie??" Eliza aliniuliza wakati naweka weka vitu vyangu tuondoke
"Bwana eliza sitaki mie , yaan ki shida kidogo hivi niende nikajiuze siku nikipata kubwa si nitauza figo kabisa , hapana bwana"
"Alisema unajiuza nani bwana"
"Bwana si......" nilisita kuendelea baada ya kuona kuna mtu pembeni , yaan pale tulipo kuwa tumekaa sie kulikuwa na mti mkubwa ndio tumeegamia tunapiga umbea wetu
Hakiamungu sikujua kama nyuma ya ule mti kuna mtu amekaa , niliona aibu kweli kwel , baada ya kukumbuka maongezi yangu na eliza hee yalinishuka afu mkaka
"We eliza amesikia??" Nilimuuliza eliza kwa sauti ya chini wakati tunaondoka pale
"Ni najuaje sijui yupo hapo tangu sa ngapi!! Atajua mwenyewe bwana si tulikuwa tunaongea yetu kwani tumemsema"
Eliza bwana ni yule mtu asie jali ila mie nilikuwa naona aibu jamani niliona aibu mnoo
Nilitamani kurudisha masaa nyuma ili nisiongee
Nilikumbuka nilivyokuwa najitapa et mi bikraa uwiii ndo natamani kabisa nifute ilo file ...
"Na hivi simpendagi basi tu!!" Eliza alikandamizia yaan hampendi huyo kaka ,nikabaki najichekesha
Huyu mkaka ni mkaka maarufu sana hapa chuo yupo mwaka wa pili , ana bebwa na vitu vingi sanaaa
Moja baba yake ni Fogi mbayaa, pesa kwao ipo sio poa , mbili ni handsome ni handsome yaan SUPER HANDSOME Afu ni mkaka ambae ana jisikia yaan anajisikia sanaaaa , Ndio.sababu wengi hawampendi haswa wanaume wenzie
Hata wale wadada wanao jielewa huwa hawamkubali kwenye midomo lakini moyoni nina uhakika kabisaaa wanatamani hata aseme Hiii!! Kwaoo
Halafu ndie mkaka mmoja tu ambae anamiliki gari gariii kuliko hata wakufunzi ,hakuna tu anaefikia Gari yake na sio mojaa ..
Ila mi sipo kwenye kumchukia wala kumpenda namuona tu kawaida yaan..
Basi ilibidi nikaushe tu ila nilikuwa natembea huku nageuka kumtazama , nikagundua amevaa phone maskioni , afu yupo bize na Pc yake ,Ooohpss nilishusha pumzi hajasikia kumbee daah nikapata na nguvu za kutembea .
*SEHEMU YA TATU*
Baada ya vipindi mi nikaondoka zangu kwenda home , wakati natoka getini nilikuwa bize natafuta simu yangu kwenye pochi , wakati nahangaika kuitafuta hata sitazami mbele , na simu nayo siioni nikajikuta nachanganyikiwa labda nimeipoteza hapo nahangaisha akili nimeacha wapi simuu??
Hatimae niliipata simu yangu yaan pochi zingine bwana nusu niumwe uchizi jamani kumbe ilikuwa imejibana huko pembeni kabisaa
Nilipo ichukua tu nainua macho hamadi hapa na hapa , niligongana na mkaka simu yangu ikaanguka chini jamani ki simu chenyewe ndo hichi tu
Nilijukuta nasema uwiii simu yangu miee ,mikono nikaweka kichwani baada ya kuona juu kuna mpasuko wa kioo
Sasa ndo nikamtazama vizuri nilie gongana nae mana alikuwa nae bado kasimama hapo mbele yangu
Moyo ulifanya paah nikamuona yule yule kaka ambae mara ya mwisho nilimuacha kule
We niliokota simu yangu fasta fasta , wakati nainuka akanambia Sorry aisee , mmh hata sikujibu wala kumtazama mi mbele ,
Kama hatua mbili , kuna wadada flani hivi nilipishana nao
Nikasikia wanasema
"Hey karimu vipiii??"
Niligeuka tu nikawatazama sijui hata aliwajibu nini ila niliona wamesimama wanaongea ongea
Moyo wangu unadunda nimekuwa sijiamini tu kwa huyu mkaka aah bwana atajua mwenyewe kwanza hakusikia , wakati najiwazia zangu
. Eliza akaniita alikuwa anakuja kwa nyuma yangu
"Ndo unaenda??"
"Eeh!!"
"Twende kwanza hapo kwa joy ,tunywe juice bwana nasikia kiu"
"Mi sina hela bwana , huyo dada anabei kweli mi hayo maisha ya kunywa juice ki glass 18000 aakhaa bado"
"TWENDE weee nakulipia"
Eliza akanivuta mkono hapo , tukabadili uelekeo
Kuna sehemu moja hivi pembeni ya chuo ,kuna dada anauza juice anajiida Joy ma juice , anauzaga ki shua kweli anabei kweli mi ndo hata sizishaukiagi na nilivyo bahili aah weee ..
Tukaenda hapo Eliza akawa ameagiza juice glass mbili moja yangu na yake , akanambia tuchukue na chips , mmh nikamwambia we Eliza bwana hamnaa hapo wana bei kweli , si bora twende tukaagize kwenye vibanda vya njee , Eliza akacheka kweli akanambia embu acha roho ya kimaskini bwanaaa ,
Akanambia nenda kaagize hapo sahani mbili fasta tule tusepe"
Nikainuka tena si ndio boss , nikatembea zangu mpaka pale kwenye chips kwa yule muuza
Nikamwambia
"Kaka naomba chips hapo"
"Zipi unataka kavu au yai??" Aliniuliza yule muuzaji huku anachota viazi kwenye kabati lake
"Nipe ka...."
"Kaka embu nipe chips yai apo fast "
Kabla hata sijamaliza nilishangaa tu yule kaka yaan karimu sasa anaongea nyuma yangu kabisa yaan hapa na hapa uwii nilibaki kimyaa akaagiza ye akaondoka nikawa namkata jicho la chini chini anaenda kukaa wapi moyo una dunda duu duu duu ..
Yaan mimi huyu kaka nina mjua ile sio ile sanaaaa hapana , nilikuwa naskia sana sitory zake kabla ya kumuona anajulikana mno chuo chote kwa Ustar wake wengi wanasema ana nyodo kweli .
Kumuona ona kwakwel sikumbuki tangu nimeanza kusikia habari zake , niliwahi kumuona kama mara mbili hivi tena ile kwa mbaliii
Sasa leo tangu ,nimuone pale nyuma ya mtu nikaongea ule ujinga wangu mungu nashangaa namuona yaan imekuwa kila wakati nakutana nae kila sec et nakutana nae
.eeh makubwa na kila nikimuona moyo unakimbizana kweli yaan nakumbuka tu ile situation ule muda naropoka ,akili ingine inaniambia hata hajasikia lakini mmh nahisi kasikia kuna muda nasema hata akisikia kwani ina muhusu nini??
Ila kuna muda nahisi aibuuu kweli ..
Basi nikaagiza zangu chips nikarudi kukaa mezani macho yangu yapo kwa chini chini namtazama huyo kaka, alikuwa amekaa meza moja na wadada flan hivi wale niliwaona wanamuita pale wapo watatu ni vidada vya kishua kweli navyo baba zao sio wa pole polee
Eliza akanambia "yaan huyu kaka badala akae na wanaume wenzie kutwa kuongozana na wanawake " alikuwa anaongea huku anatazama upande alio kuwa amekaa karimu na wale wadada
"Naniii??" Nikajidai kama sijamuelewa
"Si huyo baba malingo utafikiri yeye ndo anawalipa walimu mshahara "
Nilimuangalia huyo baba malingo mi hata sikuona sababu ya kumchukia kaka wa watu ila nilitazama simu yangu imekufa kwa ajili yake ,
Simu enyewe hii kaka alitunza hela karibu mwaka mzima wakaninunulia aah
Tukala hapo mi nikamwambia eliza naenda zangu om ili niwahi hospital kumuona baba akasema kwahiyo Salma kweli hauendi Tour
"Mi siendi Lizzy kweli"
"Yaan bado hata siamini unajua nitakuwa bored eeh, ungekubali tungemchuna yule mzee daaah ingekuwa magoli hatari"
"Umeanza mambo yako tenaaa"
"Ayaa nimeacha , uwahi basi j3 ili uniage shost"
'Sawa"
Nilimuitikia tu lakini hata hiyo j3 sikuwa na mpango wa kuja class , mana nilihisi kabisa nitanyongonyea Kwahiyo sikutaka kujitia huzuni .
Nikifika nyumbani, nikajiandaa kwenda hospital sikumkuta mtu , kaka alinipigia akaniuliza upo wapi nikamwambia nisharudi ndo nataka kutoka akanambia ngoja kidogo nakuijia twende wote nikasema sawa haina shida ..
Nilisubiri kidogo kaka akawa amefika , kaka yangu huyu mdogo yaan tunafatana nae yeye ni boda boda akanichukua tukaenda mpaka kwa baba kumuona , alikuwa hata bado hajapata afadhari akaniuliza vipi mnaenda kule ulikuwa unasema, yaan kwenye Ile Tour nikamwambia ndio baba nitaenda nilimuongopea tu
Muda wa kuona wagonjwa ukaisha tukaondoka kurudi nyumbani na kaka mkubwa alikuwa tayari amekuja kwahiyo tulirudi wote ,.
Kaka akawa ananiambia salma hata usijali mdogo wangu , utaenda sehemu tu nyingi na utafurahi ili tufanye ilikuwa bahati mbayaa
Nikaona tu vile wana wasi wasi kuhusu mie nikajichekesha nikawaambia bro mi niko freshi bwana kwanza hata nishasahau ujue .
*SEHEMU YA NNE*
Basi W/end ilipita nipo zangu home tu., baba alitoka hospital akarudi kuja kuugulia nyumbani, kidogo hali yake ilianza kuwa nzuri tu sema ndo ana pio pio mpaka basii ..
J3 niliwaambia akana kaka mi siendi chuo nitakuwa tu nyumbani hakuna alenigombeza hata ..
Sasa ile siku ya J3 mi sina hata habari nilisha sahau habari za TOUR mida kama ya sa tatu hivi eliza akanipigia simu, niliitazama tu nikasema mi hata sipokei najua tu anataka kuniuliza mbona sijaenda huko
Alipiga sana sikupokea akanitext , we muongo kweli ulinambia hujalipa kumbe umelipa !!
Mmh 🤔🤔nikaguna kwanza yaan nimelipa vipi kiaje sijaelewa text yake
Nikataka kumjibu lakini nikasema hapana anaweza jua kuwa sikupokea simu yake maksudi ngoja nikaushe kidogo
Niliacha simu nikaenda zangu kuosha vyombo baada ya kumaliza ndo nikarudi kushika simu nikakuta msg zake kibao
(We mwehu kwani uko wapi?? Au umepata campani ingine shoga, )
Ikabidi nimpigie simu
"We eliza sielewi msg zako ujue "
"Upo wapi??"
"Nipo home"
"Kwanini sasa na umelipiaaa,??"
"We mi nimelipia wapiii, sijalipia bwana"
"Mbona jinalako limetoka hapa kwenye mkondo wetu watu wanaoenda tour nawe umoo"
Nilishangaa nikamwambia itakuwa wamekosea mi sijalipa pesa yeyote bwana na kina salma wapo wengi
"Hapa naona kabisa salma omari, Embu ngoja nikupigie picha afu nakutumia sa hivi WhatsApp uone"
"Haya sawa"
Nilikata ile simu nikawasha data , bwana kweli watu wanaoenda et jina lakingu lipo ,kivipi sasa ? Kiaje mana mi sijatoa pesa,yeyote ile imekuwaje niwepo??
Nikawaza huyu eliza itakuwa ameliomba lile zee hela afu akaenda kunitolea mana mi sina mtu mwingine zaidi yake
Nilimpigia simu fasta tena nikiwa na hasira
"Eliza umemuomba hela yule mzee wako eeh??"
"Unaongea nini sikuelewi??"
"We ndio umenilipia hiyo pesa sio"
"Hahaha we mwehu kweli , kwa maisha gani niliyonayo mie au pesa gani , afu usinambie unataka kusema nimeongea na yule baba anaekutak we komaaa mi siwezi lazimisha hivyo wakati faida ni yako!!"
Majibu ya eliza yalikuwa kama ananisuta mpaka nikaishiwa pozi kabisa , sasa imekuwaje mie jina langu liandikwe kwenye orodha ya watu wanaoenda Tour?? Mana mi sio maarufu sio mtu yule wa makuzi hata , nipo nipo tu hapo sa imekuwaje ???
Nilishusha pumzi nikamwambia Eliza bwana mi siji huko hilo jina wamekosea tu !!
Eliza akanambia njoo bwana hivyo hivyo huenda ndio bahati enyewe kwani wametumwa wakosee embu njoo , nikasmea bwana mi siendi nisije kudhalilika bure huko
.haya nimefika tu naingia kwenye gari inajulikana majina yalichanganywa akaa!!
Nimeridhika kutokwenda wala siumiii ..
Eliza alinibembeleza kweli msimamo wangu ulikuwa ule ule , siendiii full stop .
Nilikata simu ya eliza ndo nikaona kuna sms juu nikaifungua ilikua namba ngeni
("Hello) nikaitazama nikajibu
(Hi) sec hiyo hiyo ikajibiwa yaani ni kama mtu alikuwa ameandika kabisa au alikuwa amshika simu mkononi anasubiri text yangu
(Upo wapi)
Nikamuuliza (we nani)
Akanijibu (mi rafiki yako bwana ,vipi huendi tour naona jina lako afu we sikuoni)
Mungu wangu huyu tena nani ,niliipiga ile namba badala ya kujibu ile text lakini haikupokelewa nikapiga tena haikupokelewa , nikacheka nikaandika text
(Baba angu kama umedanganyana na Eliza huko we nenda tu kachukue hela yako mi sitaki sitaki sitaki mniache )
Nilijua tu hii inaweza kuwa michezo ya eliza hii baada ya kuandika hiyo text , sikujibiwa tena kitu ambacho nikaamini kabisa litakuwa lile baba limepewa namba yangu na eliza kunishawishi mfyuu nilisonya nikatupa simu yangu kutandani nikatoka kuendelea na kazi zangu..
Zikapita kama dakika kumi , kaka alikuja (mkubwa) akanambia we Salma embu njoo nikaenda ndani akasema nimepokea simu kutoka chuo kwenu , nikashtuka nikamuuliza inasemaje??
"Amejitambulisha kuwa ni uongozi wa chuo , akanambia kuna wanafunzi wamepata Kufadhiriwa kwenda tour kwahiyo mmelipiwa gharama zote huko Na jina lako lipo ndio taarifa nilizo pata"
Moyo ukafanya ku duuuu!!! Nikasema kaka kweli akanambia ndo mana nimekuja hapa mbio kukuambia uwahi mana we wanasema simu yako hupokei
"Tuone hiyo namba kaka"
Kaka akatoa akanipa kuangalia hiyo namba mungu wangu ndo ile imenitext mie muda si mrefu kule na nilipiga haikupokelewa
Mmh nikasema hapa sichezewi kweli, sec tano tu nimeshika bado najiuliza nifurahi au nifanye nini
Simu ikaita namba ni ile ile , kaka akaipokea afu akaweka sauti kubwa mpaka mie nisikie
"Habari za muda??"
Alisalimia kwenye simu hee niliijua ile sauti.kweli ni msimamizi wa ile TOUR ndie yeye kabisaaaa
Nilitamani kuruka angani sio kwa ile furaha ilinivaa gaflaa😂😂 kidogo nimkumbatie kaka wee
"Vipi salma anakuja?? Tunaondoka hapa sa 6 na nusu sa tano wote wanatakiwa kuwa hapaa"
Haloooo😂😂😂sitaki ku imagine ile furaha nilikuwa nayo ule mudaaaaa, kaka akasema anakuja simu ikakatwa akaniuliza si unaenda , weee nani asema hapanaaaa nilijibu fast ndio kaka, akanambia haya jiandae Razack anakuijia nishamtumia sms
Razack, yule kaaka angu tunae fatana nae ,nilikimbia chumbani nikachukua simu fasta nikamtext eliza shoga nakujaaa , akanipigia muda huo huo ,
Nikamwambia shoga kumbe nimepata ofa ya kufadhiriwa akanambia una bahati haya njoo nakusubiri nikakata simu nikapanga nguo fasta fasta mitoko yangu ile naiamini ile mama achaa🤗🤗🤗
Vipodozi kama vyotee, kaka akanambia chukua hii hela matumizi madogo madogo , yaan kaka alijuajee, mungu awatunze siku zote kaka zangu😘😘 nawapenda mnooo
Alikuja kaka Razack yule boda boda akanambia eeeh naona unafuraha kweli ,mi nacheka cheka tu ,nikamuaga baba yangu hapo safari ya wiki zima mbugani we hutakii😜😜
Kaka ananiambia '"Salma utusamehe kwa hili tumeshindwa kukutimizia " nikamwambia " kaka mi niko sawa jamani akanambia jitunze huko sawa kuna mambo.mengi ya kijinga najua we nenda ka tulize tu akili sio ufanye upuuzi sawa"
"Sawa kaka" nikasepa zangu , kwenda chuo
*SEHEMU YA TANO*
Tulifika na kaka mpaka nje ya geti akanambia maneno maneno pale ya kuniaga kwakua tuliwahi kufika na muda ulikuwa bado wa kuondoka kaka anambia twende kwa hiyo msimamizi wenu kwanza, basi mi niliona aibu nikakumbuka ile text ile ya kumchamba mi najua ujinga wa eliza uwiii😂😂😂
Nilikuwa natembea kama nataka kujikwaa hivi kaka ananiuliza we unashida gani mi mh mh kumbe moyoni naona hayaaaaa hatari😫😫😫
Kaka mbele mi nyuma , tulipo karibia Kwenye ofisi akanambia embu pita we mbele mi sipajuai hata , ndo nikatangulia
Sasa nimefika nikajikaza kuingia mule ofisi uso nikasema nauinamisha wala simtazami kwanza ye kwanini hakupokea simu yangu embu amiache kwanza , nikapita nafika mlangoni nataka kugonga nao unafunguliwa hapo hapo , nikajikuta natizamana na huyu kaka karimu , yaan tulitazamana hivi macho kwa macho yupo mbele yangu
Moyo nao Paaa!!!❤ nilihisi kutetemeka ,
Yaan mimi tangu niaze kumuona huyu kaka mara kwa mara ,walai nahisi moyo wangu unatamani niendelee tena na tena kumuona , et watu wanajishauwa ooh mi simpendi kweli analinga sijui anajisikia , Wengine anajikuta kama vile yeye ndio analipa wakufunzi mshahara simpendi kwelii,
Aisee sio kweli , kama ikitokea wakaambiwa wadada embu mkimbie kwenda kwa karimu atakae wahi kumfikia ndie atakuwa wake wa maisha naapa kwa mungu hakuna girl ambae angekaa et mi siendi simpendi , nakwambia Tulikuwa tunavunja miguu mladi uwahi kufika kwa huyu kaka .
Kwanza ni Mtanashati wa maana , kuanzia mavazi yake , alivyonyoa,simu yake viatu mwendo wake he's so perfect walai😘🥰🥰🥰 hiyo sura sasa kwa mara ya kwanza leo mi ndo nimehisi kusema mwenyewe moyoni huyu kaka nampendaa🤗🤗🤗🤗
"Ooh sorry" weuweee😋😋 alinambia huku anapisha njia mi niingie ofisini hiyo sauti yake naisikia kwa mara ya pili , hii leo nikaisikia kwa utofauti mana ilichomaaaa ka moyo kangu ❤❤
Vile ananukia sasa uwiii🙌🙌🙌
Afu unakuta kuna mtu anakwambia et mi simpendi huyu kaka ana nyodo😂😂😂 Sasa mzuri hivi asilinge auuu??
Kwanza anasauti ya kistaarabu tofauti na story za watu huko kitaa cha chuo embu wamuache bwana🤦♀️🤦♀️🤦♀️
Mi hata sikujibu nikaingia kaka nae akafata nyuma , ye karimu akaondoka zake
"Ahaaa salma hujambo??" Baada ya kuingia sasa lecture ambae ndie alikuwa kama msimamizi mkuu wa ile safari akanambia huku anacheka cheka mi moyoni nasema anacheka kwa ile sms niliyo mtumia mana mi sina mazoea nae hata hivyo
Basi kaka alitambulisha hapo, akauliza kuhusu hiyo ofa , Akaeleweshwa vizuri nami nikaelewa akasema kuna watu kumi ndio wamepata ofa hiyo , basi mi nikashukuru sanaaa , mana hii safari nina hamu nayo mnoo yaan mnooo😇😇😇😇
Tulitoka ofisini mi nikamsindikiza kaka mpaka kwenye packing akachukua piki piki yake wakati anataka kutoka Eliza akawa amefika hapo akamwambia kaka yaan Zack bora umemleta huyu mtu kwakweli
Eliza anapenda sana kumuita kaka yangu Zack badala ya Razack
Kaka akacheka cheka tu wakasalimiana akaondoka zake
"Yaan kaka yako angekuwa na hela huyu angenioa nampendanga kweli" eliza aliniambia wakati tunatembea kwenda karibu kusubiri muda wa kuondoka
"Mmmmh hata hakuwezi mwenzangu tena muache hivyo hivyo"
"Kwani mi nimesema namuweza ni handsome hela hana sa mi nitakula Uzuri wake??"
"Hahah we mwehu embu achana na kaka yangu"
Tulisogea mpaka karibu na mazingira ya safar yaan hapo sio wadada wala wakaka watu wamewaka hatari , watu amejimaliza balaaa
Basi zilikuwa mbili, tulikaa kidogo tu tukawa tumeitwa sehemu moja tukapewa maelekezo kuwa safari imekaribia kuanza kwahiyo kila mtu ajiweke sawa
Kimoyo kilianza tu tuu tuu !! Hapo na hamu na hiyo safari aloo achaaa , mana imekuwa kama bahati tu kuwa hapa sa hii ningekuwa nipo nyumbani hukoo sijui hata ingekuwaje jamani daah!!
Basi tupo pale ,ndo tunaanza kuingia kwenye gari , Nikasikia kuna wadada walikuwa nyuma yetu wanasema mmh mbona karimu anakuja panda Basi nayeye makubwa , niliangaza huku na kule kuangalia kama nitakuona karimu , nikamuona kweli anakuja upande huu wetu ,nilijikuta miguu inakanyagana
Gafla tu pale story zilibadilika kila mtu anasema huyu vipi leo haendi na Gari yake si wanaendaga na gari zao afu wapo wote leo mmh
Eliza akanambia "yaan huyu karimu na huyo mwenzake wamekutwa na nini leo wanakuja kugombania basi huku"
Niliwatizama kama sijajali hivi walikuwa wawili na mkaka mwingine tu hata simjui zaidi tu.ya kusikia jina lake
"Kaamua jamani"
"Basi wadada humo kwenye gari atakalo panda karimu eeeh kama nawaona basi ndo anazidi kunyodokaaa mfyuu"
Mi mwenyewe ni mmoja wa hao wadada mana nilipunguza mwendo kabisaaa, nataka kujua anaingia gari gani nami niingie humo humoo,
Najua ye hata hanijui lakini basi nimuone tu mi mwenyewe amenivuruga kanivurundaa akili yangu woii😋😋😋
Sasa ye alikuwa na huyo mkaka mwingine wamesimama mwisho kabisa hata hawaingii kwenye gari , eliza akanivuta tuwahi siti bwana jaman nililaani angejua basi tu
Tukaingia kwenye gari kumbe kila mtu ana siti yake kabisa kuingia tu mwalimu alituma karatasi kama tikeck tukauliza ya nini akasema kaa kwenye siti ya namba hiyo okay
Tukawa tumekaa mi na eliza siti moja, dakika ngapi akaingia karimu nae akawa amekaa siti ya nyuma yangu, Jamani ni kama vile nilikuwa naisikia pumzi yake mana alikaa upande wangu wote tulikuwa Dirishani
Eliza yupo bize ananipigisha story za kila Rangii mimi akili yangu nimeiacha nyuma ya siti yangu😀😀😀😀🙌 ila basi tu
*SEHEMU YA SITA*
Nasikia ki harufu cha yule kaka mweeh alo , eliza anaongea kama kasetiwa basi mie hata siongei mana karimu anaonekana sio muongeaji sanaaa, kwahiyo sikutaka kuwa muongeaji
Jamani hivi mnajua hata moment ninayo ipitia mie kwanza?? hata sielewi ila nahisi tu huyu mkaka kama ataniona basi anione nikiwa perfect 😂😂😂utafikiri hata amenambia ananiangalia mie ndo najimaliza kabisa ..
Basi bwana safari yetu humo ilikuwa na raha kama zote , unajua ile wanafunzi mnapo kuwa kwenye safari kama hii kuna kila aina ya mambo mladi tu msipooze
Kuna muda nyimbo zilikuwa zinapigwa humo watu wanajimaliza kucheza hatari, kuna couple humo zinajilamba mate mbele yetu aah haswa hawa mwaka wa tatu sijui wanajikuta kina nani tu yaan 🤔🤔🤔 mi yangu macho tu
Eliza ananiambia yaani hawa wapuuzi mie siwezi date na kimwanafunzi hata siku moja huo upuuzi siwezi fanya
Yaan kinategemea pesa kiombe kila nikikiomba aah weee!!!
Basi namwambia kwa sauti ya chini kweliii 😂😂 ili wa nyuma yangu asisikie namwambia we nae umeanza embu tuliaaa , eliza anatulia sasa khaa anajua kuongea huyu mwanamke mmh🙌🙌
Tulifika bwana safari yetu kulikuwa na vibe sio la nchi hii💃💃💃💃 mpaka mwili ulikuwa unanisisimkaaaa , nikatamani hata kulia jamani mana na Assume kama nisingekuwepo mie hapa sijui ingekuwajeeee ningeona Stutas za Eliza uwiii ningeliaaa🤣🤣🤣🤣
Ilikuwa kila mtu anajifotoa kwenye nafasi yake , Utaratibu ulifanywa wote wa kujisajiri kama watalii hapo na viongozi wetu
Baada ya muda tukaambiwa hatuta chukua Hotel ila Tunaweka kambi kwenye poli ambapo kule ni salama hakuna viumbe wakali , wakatusibitishia kabisa kuwa ni salama
Basi tukaenda mpaka huko, yakawekwa ma hema bwana weuwee yaan palinogaa tulifika ilikuwa inaingia usiku mana jua lilikuwa limejificha kabisa,
Ililetwa nyama ya poli hata sijui ya mnyama gani , moto ukawashwa zikaanza kuchomwa huku kuna mziki jamani sio siri nilikuwa natamani kuruka ruka tu kwa furaha mana kausiku kalinoga kaleee hatari ni kama tour ilianza usiku huo
Tukaambiwa kuna mto ulikuwa pembeni kidogo ya pale tumeweka kambi, tulitangaziwa kuwa sehemu ya kuoga kwa anaetaka ni pale , wakaelekeza upande wa wanawake na upande wa wanaume ili tusioneane ..
Aisee nilikula nyama mie hiyo siku hatari, mda wa kulala tulitangaziwa wote,kuwa kuingia kwenye Tenti lako unalala ..
Kwenye Tenti letu tuliwekwa wanne mie ,eliza na kuna wadada wawili hivi nao ma shost,
Sasa mule kila mtu nakwambia anaongea na mpenzi wake mpaka ikawa kero afu kama wanashindana hiviii, usingizi hata hauji nipo tu nageukia huku nageukia kule
Simu yangu ikawa inaita kaka ndo alikuwa anapiga , nikaona humu ndani hata hatuwezi kuelewana mana kama kero na hivi nalala na eliza hapo kwenye tandiko moja anavyo jibebisha aah nikainuka zangu kutoka nje ili niongee kwa kujiachia
Nikasogea pembeni kidogo ya Tenti letu, kulikuwa na mioto imewasha mafungu mafungu ,palikuwa pametulia sanaaa , zilisikika sauti za ndenge na vyura na vile vidudu huwa vinawaka waka taa flan hivi nyuma ya mkalio yao wakipaa ndo vilikuwa vimetanda kila sehemu
Mi nikajivuta zangu pembeni kidogo tu na tunapo lala mule ,sikutaka kwenda mbali nilikuwa bado nina ogopa ni porini pale mwenzangu mmh we kuwezaa japo wametuambia hakuna wanyama wakali wanafika eneo hilo ila wee simba huwa anasikia harufu ya binadamu hata awe wapi na anaifata nakumbuka shoga angu mmoja hivi aliwahi kutuhadithia shule ya msingi kipindi hicho ,basi hadithi yake ilikuwa inajirudia kichwani muda huu
Kaka akawa ananiuliza vipi huko mmefika salama nikasema ndio nilikupigia hukupokea akanambia alikuwa bize ndio mana nikasema sawa hata kaka mkubwa nae hakupokea akasema wote tulikuwa bize , nikauliza vipi hali ya baba akanambia anaendelea vizuri sasa hivi nikasema jambo la kheri
Basi kaka akawa ananiambia kuna vibe huko au ndio kumepooza?? Nikamwambia yaan kaka acha tu nimependa kuwa hapa sijui siku zingine akawa ananipa pale maneno ya wosia nisifanye ujinga
Tuliongea na kaka mpaka nikajisahau kuwa nipo nje pale kulikuwa na baridi ndio ikanishtua mana sikuwa hata na nguo nzito juu , kaka akaniaga nikamwambia msalimie baba akasema ameshalala nitamwambia kesho ,poa poa
Nikawa nimekata zangu simu, nikabaki tu najifikiria , moyoni nilikuwa namuombea baba mungu ampe afya huku nikijifurahia kuhusu kaka zangu ,
Nilitulia kwa sec , mara tu hadith ya shoga angu si ikaanza kujirudia kichwani , mwili ulisisimkaa akili ikanambiaa we unajiamini nini kukaa hapo usiku huu huku polini kuna majini, wee nilishtukaaa😂😂😂😂😂 Moyo ukaanza kwenda mbio nikajikuta kweli mwili wote una sisimka ,nikainuka fasta huku naogopaaa , Ile nageuka tu niliona kimvuli pembeni ya Tent la jirani yetu kama mtu amechuchumaa flani hivi mungu wangu akili ikasema Jini si ndo hiliii
Nilijikuta nimepiga keleleee kaliii sasa kile kiwewe nilienda chini mana nilijikwaaa wakati nataka kukimbia ,
"We salma niniii!!!???" Alitoka Eliza mbio akifatana na wale wadada wengine wawili ,mi bado nipo chini mwili hauna nguvu natetemekaa aisee
"Eeeh mungu wangu nimeshtukaa eeeh " nilikuwa nainuka huku najifuta futa , pale kweli alikuwa amekaa mtu mana baada ya mimi kupiga kelele na kuanguka ndo akainuka sema alikuwa kwenye ki giza kidogo
Wakawa watu watu baadhi wametoka, na mwalimu nae alikuja kila mtu ananitazama mie
"Sa umeogopa nini??" Mwalimu akaniuliza
"Kwanza usiku mnatoka nje kufanya nini et we karimu"
Yaan aliekuwa amekaa pale nje akanitisha kumbe ni karimu khaa , hata hakujibu karimu alitupita wote akaingia kwenye ndani
"Kwani kuna nini??" Akaniuliza mie mwalimu nikawa nimejielezea kuwa nilitoka kuongea na simu huku nje ,nikatoa maelezo yangu yote , akanambia nisiwe natoka nje usiku huku ni ugenini pia sio salama sana hatuwezi kupaamini sana
Nikakubali , tukaingia na Eliza ndani, na kila mtu akashika njia yake
"Ila karimu analinga jamani huyu kaka hivi anajikuta nani kwani??" Alikuwa anaongea mdada mmoja kati ya wale wawili ambao tuna lala nao , afu wao walikuwa ni second year mi hata sikuwa nawajua
"Mfyuuuu simpendi aisee huyo kaka basi tu"
Mwenzie akamjibu huku anachukua simu yake ,mi niliwatizama tu hata sikuchangia mada mana pale natamani hata nisinge piga zile kelele
"Mwenzio Eda hapo ndo humwambii kitu aisee anampenda huyo kaka, lakini na Ustaa wake wotee alishashindwa kumpata!!"
"Aaah we Zubeda wewe unafikiri karimu hajamla Edaa mmh aah wapi nyama inavyo jiachia vile hata hanisi angetia vidole ili yaishe "
"Hahahaha Huenda nae karimu sio Rizk we mkaka mzuri vile, Kila siku ana skendo za wanawake kumgombania afu ukiuliza hakuna hata mmoja alielala nae wala kumtongoza hapa chuo "
Walikuwa wanapiga story zako hapo ,mi nawasikiliza tu ila nikapata kitu kipya tena , huyo Eda ni mdada mashauzi nae hata uje leo chuo lazima umjue ni mdada Classic afu wapo kundi watatu ndo mashost
Niliwahi kuwaona na karimu wakiongea kama mara mbili hivi
ITAENDELEA..
Soma muendelezo kwa sh 1000
Njoo Whatsapp 0743433005
Tags
simulizi