TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

SOYENZI (BINTI MFALME 2)

SOYENZI
SEHEMU YA PILI
Namba ya WhatsApp- 0683944333
__________________________________________
Mzee pelo aliona live bila chenga mtoto wake wa kike chungu akiwa amelaliwa na mtoto wake wa kiume Tino bila kuwa na nguo.

Aliwashtua kwa sauti "nyieee"

Chungu na tino kule ndani walishtuka sana.

Mzee pelo aliingia ndani akaenda chumbani walipo hao watoto wake.

Alianza kuhema sana kwa jinsi presha ilivyompanda.

Alisema "wa..wanangu kwanini mmefanya hivi?"

Chungu alijibu kwa jazba "baba nimefanya ili nisiolewe sitaki kuolewa..."

Mzee pelo alijishika moyo kwanza akakaa chini, alisema kwa huzuni "mwanangu nimealika watu huko nnje waje kuona harusi ya mwanangu lakini  mmeamua kunidhalilisha?" Mzee alishindwa kujizua machozi yakamtoka.

Tino alipiga magoti kuomba msamaha "Nisamehe baba dada ndio kanilazimisha, samahani baba"

Mzee pelo alitamani hata kuwapiga wanawe kwa hasira ila hakuwa hata na hizo nguvu, presha ilimkamata.

Kwa bahati mbaya kwa nnje  kuna mtu alikuwa anapita njia akasikia hayo mazungumzo yote.

Alipotoka hapo alienda kutangaza kijiji kizima kuwa Watoto wa mzee pelo wamefanya laana.

Habari zilimfikia bwana harusi aliyetaka kumuoa chungu siku hiyo hiyo akagairi hiyo ndoa.

Habari hizo zilimuongezea presha mzee pelo akawa hoi hoi kitandani. Hakutaka kula wala kunywa chochote.

Siku hiyo mzee pelo alizidiwa sana akawaita wanae, alianza na chungu  akamwambia
 " kwa kuwa umefanya kusudi ili asiolewe basi nakulaani  asije kuolewa tena kwenye maisha yako.."

Kisha alimgeukia na tino nae akamwambia ila wakati huo hali ilikuwa imezidi kuwa mbaya. "Ti..tino..kwa..kuwa..ume..fanya..kusudi..na..na..we..we." kabla hajamalizia Mzee pelo alikufa hapo hapo. 

Simanzi ilitawala kwa chungu na tino.

Baada ya kumaliza msiba wa baba yao Tino na Chungu waliishi hapo kijijini kwa kukebehewa kila walipopita, watu waliwatenga kwa kuwaona wana laana na pia wamesababisha kifo cha baba yao.

Chungu na Tino waliamua kuhamia kwenye himaya nyingine kuishi ili kuondokana midomo ya watu.

Waliamia kwenye Himaya ya CHATA Katika kijiji cha kalayu.

Walifanya kazi za vilimo baadae Tino alipata kazi ya kuwa askari kwa mtawala wa kijiji. wakaweza kujenga nyumba yao ya udongo yenye vyumba viwili.

Kwa kuwa walipewa laana waliamini kwenye maisha yao hawatoweza tena kupata wenza hivyo Chungu na tino waliamua kuendeleza uhusiano wao wa mapenzi,  nnje kwenye macho ya watu walijiita kaka na dada ila ilipofika usiku walilala kitanda kimoja.

Maisha yao yalikuwa hivyo lakini yalikuja kubadilika baada ya Tino kutokea kumpenda  mwanamke mwingine  wa hapo kijijini.

Tino alimtongoza huyo mwanamke nae akakubali kuolewa na Tino.

Hapo Tino aliona kama bahati kukubaliwa na mwanamke kumuoa kwamaana walipewa laana.

Tino alimfuata dada yake chungu akamwambia "Dada naomba tubadilishe maisha yetu tufanye tambiko la kuvunja kile tulichokuwa tunakifanya, sasa nataka kuoa ili nitengeneze familia nahisi baba yetu huko aliko ametusamehe ndio maana nimepata mchumba naamini na wewe utapata utengeneze familia yako.."

Chungu hakutaka kuelewa kwa 
 Maana alikuwa ameshanogewa na penzi la ndugu yake Tino.

 Baada ya kuona Tino kachachamaa kutaka kuoa ilimbidi akubali kushingo upande tu.

Baada ya siku kupita Tino alioa mke wake akamleta pale nyumbani kwao.

Chungu hakuwa akimpenda wifi yake alikuwa anamuonea wivu sana hasa ikifika usiku alikuwa anapata wakati mgumu sana kila akisikia jinsi kitanda kinavyolia lia kutokea chumbani kwa kaka na wifi yake...

Hisia zilipomzidia chungu alimuomba ndugu yake Tino awe anampa unyumba kisiri siri walau hata mara moja kwa mwezi lakini Tino alikata kata kata kwa kusema hawezi tena kurudia kufanya ile michezo na dada yake.

Chungu  Alivumilia huku kujipa Imani kuwa na yeye atapata mwanaume mwingine...

Siku zilipita, miezi ilipita na miaka nayo ikakatika. chungu hakupata mwanaume hata wa kumdanganya tu.  Ujana uliondoka utu uzima ukabisha hodi  kutokea kuitwa chungu hadi bi chungu bado yupo vile vile.

Tokea hapo chungu alimchukia kaka yake  na familia yake nzima...
..............................

Yote hayo bi chungu aliyakumbuka huku analia sana. Alisema "Siwezi kukusamehe kaka mie laana imenishika lakini wewe mwezangu unafamilia yako..."

Bi chungu alilia sana.. giza lilipozidi kuingia nae aliingia ndani kulala akafunga mlango.

Bi chungu alikuwa analala kitanda kimoja na soyenzi, alipofika kitandani alimuangalia Soyenzi kwa jicho la chuki sana alitamani hata amfunike na mto amuue huyo mtoto wa kaka yake ila nafsi yake ilimwambia "Tulia bi chungu muda utafika na utaisambaratisha familia ya Tino...

Asubuhi kulipopambazuka Soyenzi alikuwa anaelekea msituni kutafuta kuni, njiani alikutana na msafara wa mtawala wa kijiji hicho Mzee Gumbo akiwa na askari wake.

Soyenzi alipiga magoti chini kama ishara ya heshima kwa kiongozi huyo wa kijiji.

Mzee gumbo alipomfikia Soyenzi aliamuru askari wake watangulie mbele kisha yeye akabaki usawa wa soyenzi.
Alimwambia "Binti mrembo wa mzee Tino inuka usiumize magoti yako hapo chini.."

Soyenzi alimtazama mzee gumbo kisha akamsalimia kwa kiluga "Shikalaaa" maana yake ni shikamoo.

Mzee gumbo alimwambia "Ni mara ngapi nilishakukataza usiniamkie Soyenzi? mie mbona sio mkubwa kiivo jamani hata miaka 60 sijafika.."

Soyenzi alisema kwa upole

"Mtawala gumbo kwa ridhaa yako naomba niondoke..."

"Sawa inuka uwende..nitaongea na baba yako Mzee Tino ngoja niwahi kwa mfalme kuna kikao leo.."

Soyenzi aliinuka akaendelea na safari yake.

Gumbo alibaki anamtazama tu binti alivyokuwa anaondoka.

Soyenzi alikuwa ni binti mzuri mwenye nyama zake nadhani mnanielewa nikisema nyama.
Hakuwa mweupe wala hakuwa mweusi saizi ya kati tu, alijaaliwa urefu alioridhi kutoka kwa baba yake.

 Gumbo aliendelea na safari yake huku moyoni akijisemea "Soyenzi lazima uolewe na mie mtawala ili unizalie watoto wazuri kama wewe... "

********************* 
KWA MFALME.

Ilikuwa mida ya usiku kwa mfalme kenzo baada ya watu wote kuenda kulala Atu alinyata akaenda chumbani kwa Muba kama kawaida yake.

Alipofika walifanya yao usiku kucha alfajiri Atu aliwahi kutoka...

Kesho yake mida ya mchana Malkia Awena alikuwa chumbani kwake anapanga mataji yake. nyuma yake alikuwa amesimama msimamizi wake ambae ni Atu.

Atu alimuuliza "Malkia wangu karibia ugawe taji lako la thamani kwa malkia ajae.."

Awena alijibu "Ndio kiukweli natamani sana mwanangu Muba aowe haraka ili nimpate mkamwana wa kumpa hili taji..."

Atu alitabasamu kusikia hivyo. Akauliza "Malkia wangu Muba si ataoa hapa hapa kwetu?"

"Sijui kiukweli ila popote atakapotaka miye sina neno kubwa iwe ni kwenye hii Imaya yetu ya Chata"

Kuna askari alibisha hodi Atu akaenda kufungua mlango, askari kuna  ujumbe alikuwa kauleta alimpa atu akamwambia amkabidhi malkia Awena.

Atu alipeleka ule ujumbe kwa malkia awena.

Awena hapo hapo aliusoma kisha aliachia tabasamu.

Atu alimuuliza "Malkia wangu mbona umefurahi nini kilichokufurahiaha malkia wangu.."

Awena alimjibu "Muda ukifika utajua maana nahisi unakuhusu pia ni habari njema, baki hapa naenda kuongea faragha na mume wangu mfalme kenzo.."

Atu alijibu sawa.

Malkia awena aliondoka na ule ujumbe akaenda kwa mumewe.

Atu alivyobaki hapo peke yake alianza kuyaangaalia yale mataji ya malkia. Akaanza kujipima moja moja huku akijiangalia kwenye kioo.
Alisema "Hili limenipendeza sana, nasubiri siku ya kunikabidhi Taji nikiwa kama mke wa mwana mfalme Muba...oooh!"

Atu alijihisi raha sana...

Malkia Awena alipofika kwa mumewe alimwambia.

"Mume wangu mfalme kenzo nimepokea ujumbe kutoka kwa malkia mwezangu  wa himaya ya Gongola. Amesema amempenda sana mwanangu Muna anataka aolewe na kijana wake, pia kama kuna binti mwingine mrembo basi nimpe aolewe na mpwa wake, kigezo kikubwa  wawe wanamwari tu..."

Mfalme alifurahishwa na habari hizo akasema "Inamaana Binti yangu Muna ataenda kuwa malkia kwenye himaya ya huko?"

"Ndio mume wangu wanataka kuoa Binti wa himaya yetu ili kudumisha amani na ushirika..."

"Vizuri sasa je huyo binti wa pili tutampa nani wakati sie tuna mtoto wa kike mmoja tu"

"Namfikiria Atu wacha nae akaolewe na mpwa wa mfalme wa himaya ya Gongola  ili Muna asiwe peke yake huko.."

Mfalme alijibu 

"Sawa ila vipi kuhusu iyo sifa waliyoitaja, wewe ndio mama unaamini mwanao muna anahiyo sifa?"

"Kabisa kwa nilivyomlea mwanangu lazima atakuwa bado ni mwari, sina shaka hata na Atu pia kwa maana huwa nashinda nae siku zote hadi usiku sio rahisi kuwa ameshaharubu usichana wake, wanajua mila na desturi zetu"

"Sawa...ila kama unavyojua mila na desturi zetu ni lazima kwanza aanze kaka mtu Muba kuoa ndio afuate Muna..."

"Sawa mume wangu...leo utakuwa na kikao na viongozi wa vijiji wa himaya yako wacha nikuache ujiandae.."

Malkia awena aliondoka zake...
******************

Soyenzi alienda kukata kuni msituni wakati anakata aliuona m'buyu kwa mbaali ambao ndio huwa wanauabudu.

Soyenzi aliongea kwa sauti huku anatazama ule m'buyu
"Eeeh! Mizimu ninatamani kuja kuwa malkia wa himaya yetu hii ya Chata mizimu nisikieni na mimi kitukuu chenu"

alipomaliza kuomba vile soyenzi alienda mtoni kuogelea. Wakati anaoga alisikia sauti ya mtu akilia kutokea mbali kidogo na alipo.

 aliisikiliza vizuri ile sauti akagundua kuwa ni sauti ya mtu mzima.

 Alitoka kwenye maji akavaa nguo zake kisha akaanza kufuatilia ile sauti ilipotokea huku akiwa kakoki mshale wake vizuri wa kujihami kama kukitokea kitu kibaya.

Soyenzi alisogea hadi ilipotokea ile sauti alimkuta bibi kikongwe akiwa analia huku anaomba msaada.

Soyenzi alishangaa kumuona huyo bibi kwa maana sura yake ilikuwa ngeni kwenye macho yake. Aliangaza huku na huko kama ataona mtu mwingine hapo lakini hakukua na mtu mwingine.
Yule bibi alipomuona Soyenzi alimnyooshe mkono akamwambia "Naomba nisaidie mjukuu wangu niinue hapa nimenasa  hapa siwezi kuinuka"

Soyenzi aliogopa sana kwa maana yule bibi alionekana kuwa ni kiumbe wa ajabu maana macho yake yalikuwa na rangi nyekundu sana na isitoshe ni mgeni machoni mwake, Soyenzi alihisi yule atakuwa jini maana humo misituni kuna historia ya kuwa na viumbe vya ajabu sana.

Soyenzi alimuacha huyo bibi kizee hapo akakimbia...

Wakati Soyenzi anakimbia yule bibi aliita "Nisaidie mjukuu wangu usinikimbieeee"

 Soyenzi alisimama.

Alianza kukumbuka ile hadithi aliyosimuliwa na mama yake jana usiku kuhusu yule nyoka wa ajabu,  akakumbuka na kile mama yake alichomwambiwa baada ya hadithi (usidharau kitu  chochote kinachokuja mbele yako, kizingatie kabla hujafanya maamuzi)

Soyenzi ndipo alipata ujasiri akaamua kurudi tena kwa yule bibi huku akijisemea "isije kuwa ni bahati kutoka kwa mizimu yetu"

 alipomfika yule bibi alimuuliza "We ninani?"

Yule bibi alimjibu " mimi ni kiumbe kama wewe naomba nirudishe nyumbani nimepotea nikaangua hapa ..."

Soyenzi alishangaa sana kusikia hiyo kuangukia hapa akajiuliza "alikuwa anapaa au anaruka hadi akaanguka?"

Alimuuliza
"Nyumbani! Kwako unaishi wapi?"

"Nitakuelekeza niinue unisindikize..."

Yule bibi alimnyooshea mkono Soyenzi, soyenzi aliupeleka mkono wake kumgusa yule bibi huku akiwa anatetemeka sana.

Soyenzi alijikaza akagusa mkono wa  yule bibi akamsaidia kuinuka.

Yule bibi alimwambia Soyenzi "mjukuu wangu nipeleke   ng'ambo.."

Soyenzi alimshika mkono yule bibi vizuri akaenda nae alipotaka huku binti anaogopa sana.. walivuka mto baada ya kuvuka Soyenzi alimwambia nishakuvusha ng'ambo naomba mimi nirudi bibi"

 Yule bibi alimwambia "Hapana nipeleke nyumbani..."

Soyenzii aliogopa sana alihisi akimkatalia anaweza hata kumdhuru maana haelewi kama ni mtu mzuri au mbaya.
 Ikabidi ampeleke huko alikotaka.

Walitembea sana hadi jua lilianza kuzama bado wanatembea tu.

Yule bibi alimwambia Soyenzi "Usijali mjukuu wangu utarudi kwenu salama"

Soyenzi hakuongea kitu njia nzima alikuwa amejawa na uoga.

Walitembea sana walivuka vijiji na vijiji bila ya kufika.

Soyenzi alianza hadi kulia kwa maana alipo ni mbali sana na kwao na hata hajui yupo wapi.

Walitembea hadi kwenye pango moja yule bibi alimwambia soyenzi waingie humo ndani ya pango. 
Tayari giza lilikuwa limeshaingia muda huo.

Yule bibi alimwambia Soyenzi
 "Giza limeingia utalala hapa kesho asubuhi itarudi kwenu, miye nimefika kwangu.."

Soyenzi alikuwa analia huku  akisema miye..na..najua tu .. unataka kunila nyama.."

Yule bibi kizee alicheka akamjibu "mjukuu wangu sio kila binadamu ni wa kuliwa nyama na watu wabaya wengine ni wa kupongezwa tu kwa mioyo yao ya dhahabu, nilikusikia ulivyokuwa unaomba siku moja uje kuwa malkia, mjukuu wangu hakuna kitu kinachokuja kirahisi lazima ukifuate ndio nimekuleta sasa unatakiwa kunishukuru.."

Soyenzi hakumuelewa yule bibi hata kidogo.

Yule bibi alimwambia
 "haya kula hayo matufaa na ulale hapo kwenye sufi, kesho asubuhi utarudi kwenu, nakusihi usije ukaondoka huu usiku"

Yule bibi alianza kuondoka.
 Soyenzi alimfuata akampigia magoti huku analia.

"Bibi tafadhali usiniache peke yangu kwenye hili pango naogopa sana ona ni  giza..."

Yule bibi alimwambia "Hili ndio jaribu lako ukiliweza basi yatajibiwa maombi Yako yote uliyokuwa unaomba, asante kwa kuniinua nilipoanguka  ipo siku na mimi nitakusaidia ukianguka...kwa heri"

Yule bibi aliondoka.

Soyenzi  alibaki analia  kwenye pango huku anatetemeka, kuna kapepo kalimpuliza usoni mwake akalalaa hapo hapo.

Asubuhi Soyenzi aliamka alifurahi kukuta kumeshakucha,  haraka kaanza kupanda ili kutoka nnje ya pango. Maana lilikuwa ni pango la kudumbukia chini.

Alivyotoka kwenye pango  alikuta kuna mwanaume yupo hapo juu anafanya mazoezi. 
Mwaaume huyo hakuwa mwingine alikuwa ni mwana mfalme Muba.

Muba alikuwa anafanya mazoezi huku kifua chake kipo wazi.

Soyenzi alimtazama huyo kwanaume hasa kifuani akajisemea kimoyo moyo "Ewalaaaaa"

Muba alipogeuka alimkuta mtoto wa kike anamtazama, macho yao yakagongana wakawa wameganda wamatizamana kwa dakika nzima.
Kisha Soyenzi alipita kando yake akawa anaondoka.
 Muba alimtazama kwa muda  yule binti alivyokuwa mrembo akajiuliza "Huyu binti ni wawapi mbona sura yake ni ngeni?"

Muba alimuita soyenzi "We binti hebu simama uniambie wewe ni nani na kwanini umetokea kwenye hili pango?"

Soyenzi alisimama akamjibu "Samahani kuna bibi nilimleta humu kwakuwa ilikuw ni usiku ilinilazimu kulala humo, sasa hivi ndio narudi kwetu..."

Muba alimsogelea Soyenzi akamuuliza "Bibi gani umemleta hili ni pango ambalo wanaume wa kijiji hiki huwa wanafanyiwa tohara humo.."

Soyenzi alishtuka kusikia hivyo akajisemea moyoni mwake "ina maana yule bibi kwake sio hapa? Kwanini sasa kanileta sehemu ya kufanyia tohara?.."

Alimjibu muba

 "Samahani mimi ni mgeni hapa nilimsaidia tu bibi kizee kumleta...sijui kama hapa ni jandoni"

Muba alicheka sana kisha akamsogelea Soyenzi bila uwoga alimkamata kiunoni akamsogeza karibu yake.

Soyenzi alibaki anatoa macho kwa maana ndio mara  yake ya kwanza kaguswa hivyo na mwanaume, pia alishangaa kuona jinsi huyo mwanaume alivyojiamini hadi kamgusa vile bila ridhaa yake.

Muba alicheka huku kamshika binti kiunoni kisha alimwambia

 "Niliona ulivyokuwa unanitazama hebu sema tuu kama ulikuja hapa kunitafuta mimi maana wanawake wa hichi kijijii wote wanajua kuwa asubuhi huwa nafanyaga mazoezi hapa.."
Muba alipoongea hivyo alianza kusogeza mdomo wake kwenye lips za Soyenzi bila hata ya uoga 

Soyenzi alimsukuma muba akampiga na kibao.
"We kaka mimi sio kama hao wanawake wanaokuwinda na kujirahisisha kwa wanaume ovyo, nimekwambia nilimleta bibi kizee wewe unasema eti nilikuja kukuvizia wewe kwa kuwa wewe ni nani? Hivi unapata wapi ujasiri wa kunishika mwili wangu bila ruhusa?"

Muba alimtazama Soyenzi kwa hasira akasema
 "Umeweza je kunipiga? Ni wazi wewe ni mgeni wa hiki kijiji ndio maana umedhubutu kunipiga sasa nikuambie tu Naitwa Muba mwana mfalme Kenzo lazima ulipie kwa kunipiga kibao mtoto wa mfalme wako"

Soyenzi alishtuka kusikia hivyo hapo sasa ndio alijua kuwa hapo alipo kumbe ndio kwenye kijiji anachoishi mtawala wa himaya yao ya CHATA mfalme kenzo na huyo aliyempiga ni mwana mfalme.

Soyenzi alipiga magoti chini hapo hapo akaanza kuomba msamaha huku analia
 "Samahani mwana mfalme sikujua kama hapa nilipo ndipo kwenye kijiji anachoishi Mfalme wetu nisingekuvunjia adabu kiasi hiki Mwana mfalme."

Muba alipiga filimbi askari wake wakaja aliwaambia "mkamateni huyu mpelekeni nyumbani kifungoni..."

Askari walimshika Binti wakaondoka nae.
 Njia nzima Soyenzi alilia huku anaomba msamaha kwa mwana mfalme....

Nyumbani kwa mfalme Kenzo.
 Kulikuwa na kikao cha mfalme na viongozi wa vijiji ambapo kila kiongozi alipeleka changamoto zilizopo kwenye kijiji chake kwa mfalme.

Vijiji vingine vilikuwa na ubaha wa chakula, kingine maji, kingine mavazi vitanda na mifugo nk.

 mfalme kenzo aliwasikiliza viongozi wa kijiji  akawaahidi kuzitatua changamoto zao zote kufikia wiki ijayo.

kikao kikafungwa asubuhi kwa maana kilianza tokea jana yake.

Viongozi wa vijiji walibusu mkono wa mfalme kama ishara ya kumpa heshima kisha walianza kutoka nnje mmoja mmoja.
 Mfalme na mke wake nao walitoka nnje kusindikiza wageni.

Mtawala Gumbo nae alikuwa ni miingoni mwa viongozi wa vijiji waliohudhuria kikao hicho.

https://pl18822542.highrevenuenetwork.com/e5/66/b9/e566b918719ab7fa060cf1804c59cf70.js
wakati wanaondoka hapo walimuona Muba akiwa anakuja na askari ambao wamemkamata Soyenzi.

Mtawala Gumbo alishangaa sana kumuona Soyenzi hapo.

Soyenzi alivyomuona Mtawala Gumbo alisema huku analia  "mtawala wangu naomba nisaidie turudi wote kijiji kwetu..."

Mtawala gumbo alimuuliza Muba "Samahani mwana mfalme umemtoa wapi huyu binti?"

Muba alijibu "Kwani unamjua?"

"Ndio ni mtu wa kijijini kwangu kalayu.."

"Anha! Huyu binti nimemkuta kwenye pango la jandoni, haijatosha kanipiga kibao anastahili adhabu na lazima aseme kaja huku kijijini kwa Mfalme kufanya nini bila ruhusa"

 mfalme Kenzo  aliuliza

" kuna nini hapa?"

Muba alimjibu baba yake

 "Baba nimemkuta huyu binti mgeni jandoni nilipomuuliza kanipiga kibao, niwazi huyu katokea nnje ya hii himaya  yetu au katumwa na maadui, siamini kama katokea kijiji cha kalayu "

Mfalme kenzo aliamuru binti atupwe kifungoni ili akahojiwe vizuri.

Mtawala Gumbo alifikiria akapata wazo la kusema uongo ili amuokoe Soyenzi.

"Hapana Mfalme msimfungie kifungoni  huyo binti ni wa himaya yetu hio ya CHATA ametokea kijiji kwangu kalayu.. Kiukweli huyo binti  tulikuja nae jana tulivyokuja kwenye kikao cha viongozi, sasa nilijua kikao kitawahi kuisha hivyo nilimuacha atembee tembee huko nnje, kwa bahati mbaya kikao kimechelewa hadi tumelala hapa, naona yeye ndio aliamua kuenda kulala kwenye pango kwa maana hakuwa na mwenyeji huko nnje, niliogopa kuja nae hapa nyumbani kwa mfalme kwa maana hakua na mualiko wa kuingia hapa kwenye kasri.. Naombeni mumsahe hakujua kama kule alipoenda ni jandoni.."

Malkia Awena alisema "Ooh! Maskini Binti wa watu kalala pangoni peke yake vipi kama angepatwa na kitu kibaya, ulipaswa kuja nae hapa..."

Mfalme kenzo aliamuru askari wamuachilie Soyenzi aondoke na mtawala Gumbo.

Muba alichukia kuona baba yake karuhusu binti aachiwe bila kujali kama amempiga.

Muba alimsogelea Soyenzi akamwambia "kile kibao ulichonipiga lazime ukilipie..."

Kisha aliingia zake ndani.

Soyenzi alipiga magoti akamshukuru sana Mfalme kenzo kwa kumsamehe alisema

 "Nilikuwa nasikia kwa watu wakisema kuwa Mfalme Kenzo ni mtu mzuri na mwenye huruma leo ndio nimeamini, najivunia kufika hapa na kuwaona mfalme na malkia kwa macho yangu ni bahati kwangu, Malkia Awena Neema ya mizimu yetu iwe na wewe na kizazi chako asanteni na kwaherini..."

Binti alienda kupanda kwenye usafiri wa mtawala gumbo ambao ulikuwa ni mkokoteni uliendeshwa na ng'ombe wawili.

Mtawala gumbo na askari wake nao walimuaga mfalme kenzo na malkia Awena kwa heshima kisha walipanda kwenye usafiri na safari ya kurudi kijijini kwao kalayu ilianza...

Itaendelea 
Full shilingi 1000

Njoo WhatsApp katika namba hii hapa 0683944333

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post