🤓1-------5
Story………………..MCHUMBA WA PLAY BOY (01)
Powered by…………….CHAMA HURU MEDIA
________________________________
Umri………………..18+
Leonard Briggs, hilo ndilo jina lake. Msanii maarufu sana mwenye mamilioni ya mashabiki, yeye ni mwimbaji, rapper na pia dansa, ni mwimbaji maarufu zaidi katika tasnia ya burudani.
Ana mvuto wa kila aina mbele ya warembo, mwonekano wake uliwavutia wadada wengi, yeye ni p*sy f*ker mbele ya wanawake. Leonard Briggs ana wasichana wasiohesabika, ni kijana mdogo,ni kijana tajiri na ni kijana mwenye nyota.
Ni kijana asiyependa Ndoa, mara zote husema hawezi kuoa kamwe na anaichukia sana ndoa huku akiwa na siri kubwa nyuma yake.
Utata unaibuka baada ya Leonard Briggs kumchumbia binti mrembo kwa kulazimishwa na Bibi yake!,
Je?, Leonard Briggs atakubali kumuoa binti aliyemchumbia!?
Yote haya yanapatikana katika mkasa huu.
ANZA NAYO......
Ndani ya jiji la NEW YORK kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKF, Ikiwa ni Desemba ya tarehe 30 mida ya saa 7:30 AM,
Uwanja wa ndege ulijaa mamia ya watu huku baadhi ya watu wakiwa na kamera, picha kubwa ya Leonard Briggs, na wengine wakiwa na ubao ambao jina la Leonard limeandikwa kwa herufi kubwa, baadhi yao pia walikuwa na barua na zawadi.
Leonard Briggs alikuwa nje ya New York kwa mwezi mmoja kwa ajili ya biashara muhimu kulingana na usimamizi wake, taarifa zilitolewa ndege yake itawasili baada ya dakika thelathini zijazo, mashabiki zake walisubiri kwa subira kuwasili kwake, hivyo ndivyo anavyopendwa Leonard Briggs. wengine walifika mapema huku wengine wakiendelea kukimbia ili kuhakikisha hawachelewi.
"Louis mbona unaendesha kama konokono!?" Jeremy alifoka, akitazama nje ya gari.
"Oh tulia jamani, uongozi wa Leonard umesema atafika saa nane na bado tuna dakika kumi zaidi" Louis alifoka huku akipaki gari yake pembeni.
Jeremy alimpuuza na kunyakua kamera yake.
"Bado wewe sio mwandishi, utafanya nini ukishakuwa mmoja wao?" Louis alimdhihaki ikiwa Jeremy ni mwandishi kama yeye.
“Naipenda sana kazi yangu kuliko maisha yangu” Jeremy alisema na kushuka kwenye gari.
Louis naye alishuka na kuanza kuingia ndani, Jeremy alianza kupiga picha karibu kila hatua waliyokuwa wakipiga
Jeremy ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Diamond, chuo kikuu maarufu zaidi huko New York kwa sababu watu mashuhuri wengi husoma chuo hicho, akiwemo Leonard Briggs mwenyewe.
Jeremy anasomea taaluma ya Mass Communication na louis ni rafiki yake wa karibu.
Walipita katikati ya umati wa watu walioanza kuwafokea lakini Jeremy hakujali, ilibidi asimame mbele ili apate taarifa vizuri, yeye ndiye anayesimamia blogu ya shule na karibu kila siku anapata habari mpya.
Dakika chache mbele kelele za watu zilisikika na hatimaye Leonard alitokea
" Ahhhhhhh!!!!!"
"Yupo hapa!!!!!!"
baadhi ya mashabiki walianza kukimbia wakimkimbilia Leonard lakini walinzi waliwazuia.
"Leonard!!!!"
"Tunakupenda!!!!"
"Karibu nyumbani!!!!!"
"Wewe ni mzuri sana!!!"
"Leonard !!!"
"Alibadilisha mtindo wake wa nywele tena, He's so hot!!"
Ni sauti za mashabiki wa Leonard zilizosikika.
Jeremy alikuwa anashughulika kuchukua video na picha nyingi kwa wakati mmoja, Louis pia alikuwa na shughuli nyingi.
Wakati huo Leonard aliendelea kupunga mkono akitabasamu huku mashabiki wakiendelea kulipigia kelele jina lake, alifanikiwa kupokea zawadi kutoka kwa mashabiki na barua huku walinzi wake nao wakichukua baadhi ya zawadi, mashabiki zake waliendelea kumfata huku wakipiga kelele mpaka alipofika kwenye gari.
Mlinzi alimfungulia lakini Leonard aliwageukia mashabiki zake.
"I love you all, see you all tonight" alisema na kuwapiga busu.
Baadhi ya wasichana walizimia hapohapo huku wengine wakiendelea kupiga kelele, hatimaye aliingia kwenye gari na dereva wake aliondoka gari akifuatiwa na magari mengine.
Jeremy na Louis waliingia kwenye gari na Jeremy alianza kuchapisha video na picha kwenye blogu ya shule
LEONARD BRIGGS AMERUDI NA KUWAFANYA WASICHANA WADONDOE TENA
Jeremy baada ya kumaliza kuchapisha aliituma.
"Seriously umeshatuma tayari? upo haraka sana?" Louis aliuliza kwa mshtuko baada ya kupata taarifa kwenye simu yake.
“Ndio maana naitwa Jeremy fast finger” Jeremy aliongea kwa majivuno na Louis alicheka huku akiwasha gari.
"Tumekaribia kufungua chuo Jeremy!?" Louis aliongea akiwa na huzuni.
"Bora ata tufungue maana nimekumbuka kusoma" Jeremy alimjibu.
"Najua unapenda kusoma lakini mimi sipendi"
"Ndio maana unakuwa wa mwisho darasani ila nashangaa wewe kuwa rafiki yangu"
Louis alibaki akitabasamu kwa maneno aliyozungumza Jeremy.
*****************************
Kwenye nyumba ya Julius, Mariana bado alikuwa amelala fofofo, kengele ilionekana sakafuni kutokana na yeye kuirusha ilipoanza kumpigia kelele, kichwa chake kilikuwa juu ya mto, ghafla mlango ulifunguliwa na Octavia aliingia ndani kama mtu anayefukuzwa.
"Mari J!!!!!!!!!!!!" Octavia alipiga kelele na Mariana alikurupuka kutoka kitandani kwa hofu kutokana na kushituliwa kutoka usingizini.
"Msaada!!!" Mariana alipiga kelele huku akikimbia kuelekea mlangoni bira kuangalia mtu aliyemshitua.
Alifika mlangoni na kutaka kufungua mlango lakini alipogeuza shingo yake alimwona Octavia.
"Oc....Octavia?" Aliita na Octavia alianza kucheka
"Unapenda kulala sana Mariana!" Octavia aliongea huku akiendelea kumcheka.
"Leo utanitambua kwa kuniharibia usingizi wangu!" Mariana aliongea huku akimsogelea na kuanza kumkimbiza Octavia, wote walianza kukimbizana huku na huku ndani ya chumba hicho.
Mariana baada ya kuona hawezi kumkamata Octavia alichukua begi dogo na kutoka ndani ya chumba hicho.
"Inamaana amechukia!?" Octavia aliongea na kumfata Mariana alipoelekea, alimshuhudia akikimbilia bafuni na kuufunga mlango kabla Octavia hajamfikia.
"Mari J?" Octavia aliita huku akigonga mlango lakini hakujibiwa
"Mari...."
“Sijambo Octavia” Mariana alimjibu bira kutoka bafuni lakini Octavia alihangaika kumbembeleza atoke na baada ya mda Mariana alipotoka.
"Uko salama!?" Octavia aliuliza.
“Ndio nipo salama!” Mariana alitabasamu na kulitoa begi kwenye mkononi yake.
"Kuna ni nini ndani ya begi hilo!?" Octavia aliuliza.
"Hamna kitu cha maana, nilikumbuka ghafla kuwa nilitumia lotion ya uso ambayo nilipaswa kujisafisha" Mariana alijibu.
“Oh..sawa” Octavia alitabasamu
"Kwanini uko hapa?" Mariana alimuuliza
"Leonard amerudi!!" Octavia alipiga kelele na kuanza kucheza ila Mariana aliyatoa macho yake na kuingia chumbani na kwenda kukaa kitandani.
"Kwa hiyo umeniharibia usingizi wangu kwa sababu ya huyo Leonard? ngoja nikuue tu?" Aliongea na kutaka kumkaba mwenzake.
"Acha usinikabe Mari J ila hii ni habari nzuri sana, Tunatakiwa kujiandae kwa usiku wa leo" Octavia aliongea na kukaa kitandani alipokuwa amekaa Mariana.
"Nini kinatokea usiku wa leo?" Mariana aliuliza.
"Tamasha la Leonard bila shaka, nataka twende wote" Octavia alizungumza.
"Sina hamu, nataka kulala" Mariana baada ya kuongea alilala kitandani na Octavia alianza kumtikisa.
"Twende basi Bestie, tafadhali naomba twende pamoja"
"Sawa!!" Mariana alipiga kelele baada ya Mariana kukubali.
"Asante Mariana!! Nitakusaidia kwa mavazi...." Octavia alinyenyuka na kukimbilia chumbani kwake.
Mariana alimtazama huku akifoka kwani hakupenda kwenye tamasha la Leonard lakini simu yake iliita iliyomfanya atoe tabasamu baada ya kuiona, ni Royce, mpenzi wake.
"Hey Babe" Mariana alitabasamu
"Usiku nimeota ndoto nzuri inayotuhusu sisi wawili mrembo!" Royce alizungumza na Mariana aliona haya!
"Seriously?" Royce alicheka
"Ndio"
Octavia aliingia chumbani na kumkuta Mariana akizungumza na simu.
"Upo tayari kuwa na mimi jioni ya leo kupata chakula pamoja?" Royce aliuliza.
"Leo jioni Royce?" Mariana aliuliza kwa furaha lakini Octavia alitikisa kichwa na kumpokonya simu.
"Hey Royce, sahau kwenda na mpenzi wako usiku wa leo, utakuwa naye kesho ila sio leo!" Octavia aliongea huku simu ikiwa kwenye masikio yake.
"Octavia!!" Mariana alifoka na kumpokonya simu ila Octavia alibaki akicheka
"I'm sorry babe, Octavia kaniomba nimsindikize jioni ya leo!"
"Mtakuwa nyie wawili tu!?" Royce aliuliza.
"Ndio, anataka niende naye kwenye tamasha la Leonard" Mariana aliongea
"Basi tunaweza kuahirisha na tutakuwa pamoja siku ya kesho" Royce aliongea na Mariana akatabasamu.
"Asante babe, nakupenda" aliibusu simu yake.
“I love you more, i will call you later” Royce alizungumza na kukata simu.
Mariana alimgeukia Octavia akiwa amekunja uso.
"Kumbe unampenda kiasi hicho Leonard? ila sijapenda ulichomfanyia Royce na tambua kuwa mimi sio shabiki yake huyo Leonard!" Mariana alizungumza kwa hasira.
"Nitusi unavyotaka ila tunaenda kwenye tamasha pamoja" Octavia alimjibu.
"Kwanza nina njaa hapa nilipo!" Mariana alizungumza.
"Utakula mda sio mrefu ila umeona video ya mwisho ya dansa? anajaribu kucheza kwa bidii" Octavia aliongea huku akitazama simu yake.
"Nani? Tessa?" Mariana aliuliza, akimsogelea Octavia aliyekuwa akitazama video ya Tessa akicheza
"Anajaribu lakini kujifunza" Mariana aliongea baada ya kuiona video ya Tessa.
"Anataka kuwa mchezaji mzuri kama wewe" Octavia aliongea na Mariana alicheka
Mariana ni dansa, sawa na Tessa. Wote wawili ni wacheza densa maarufu katika Chuo Kikuu cha Diamond na kila Ijumaa kunakuwa na maonyesho mazuri katika ukumbi wa chuo, wote wawili ni wacheza densa wazuri lakini Mariana ndiye anayependwa zaidi na pia ni dansa bora kuliko Tessa
Kitu kingine, wao ni maadui ambao kamwe hawatawahi kuonekana pamoja isipokuwa ni mabishano au mapigano.
Mariana na Tessa wanachukiana sana
"Ni kweli maana kila mtu anataka kuwa hodari" Mariana aliongea huku akitabasamu na kuanza kucheza.
"Yes baby!! Wape!!, Shake your body!, tikisa baby, tikisa!!!" Octavia aliongea akipiga kelele za ukichaa huku Mariana akicheza kwa kutikisa kiuno chake!......ITAENDELEA.
________________________________
Story………………..MCHUMBA WA PLAY BOY (02)
Powered by…………….CHAMA HURU MEDIA
________________________________
Umri………………..18+
ILIPOISHIA....
"Ni kweli maana kila mtu anataka kuwa hodari" Mariana aliongea huku akitabasamu na kuanza kucheza.
"Yes baby!! Wape!!, Shake your body!, tikisa baby, tikisa!!!" Octavia aliongea akipiga kelele za ukichaa huku Mariana akicheza kwa kutikisa kiuno chake!..
ENDELEA........
leonard alishuka kwenye gari akiwa na meneja wake Collins na mara moja alisogelewa na waandishi wa habari lakini walinzi wake walijitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha hakuna hata mmoja wao anayemgusa.
"Karibu tena nyumbani Leonard, una kipi cha kuwaambia mashabiki zako waliokusubiri kwa hamu!?"
"Neno tu tafadhali"
"Je, tutegemee burudani ya aina gani kwenye tamasha la leo usiku?"
Leonard hakuongea neno lolote zaidi ya kuendelea kuingia ndani ya kampuni, alikuwa amevaa miwani na alikuwa anatafuna bigijiii mdomoni mwake.
Hatimae aliingia na waandishi waliacha kumfuata.
"Kando ya tamasha, nina nini kwa leo?" Alimuuliza Collins bila kugeuza uso wake.
"Mahojiano lakini tayari nimeshazungumza nao hivyo yataahirishwa hadi kesho... ratiba iliyombele yako ni tamasha tu" Collins alimjibu na Leonard aliitikia kwa kichwa.
“Hey Buddy” Sauti ya kawaida iliita mara baada ya Leonard kuingia, aligeuka na kumuona Sarah, msanii kama yeye, wako chini ya kampuni moja na pia ni marafiki wa karibu pamoja na wengine wawili, Ricardo na Fatma ambao ni wanamitindo maarufu.
“Ni mda hatujaonana!” Leonard aliongea akitabasamu huku Sarah akimkumbatia
"Karibu tena"
"Asante, nimekuwa nikijaribu kuwatafuta Ricardo na Fatma bira mafanikio yoyote yale" Leonard alizungumza.
"Oh!, nadhani wako busy" Sarah alimjibu.
"Nipo hapa kuonana na mkurugenzi, tuonane baadae" Aliongea na kumkonyeza Sarah kabla ya kuondoka.
Alipokaribia kuingia kwenye ofisi ya mkurugenzi alikutana na Angelo aliyekuwa akitoka. Angelo ni mpinzani wa Leonard katika tasnia ya muziki.
Ingawa Leonard haoni kama mpinzani, ilikuwa ngumu kwa Angelo kuacha kumdhihaki baada ya kumuona maana na yeye pia ni maarufu kama ilivyo kwa Leonard lakini Leonard ni maarufu zaidi.
“Karibu kwa mara nyingine, tumekukumbuka sana” Angelo aliongea kwa kejeli na kuachia tabasamu la uwongo ambalo lilitoweka mara moja likatoka nje.
Leonard alimpuuza kabisa na kuingia ofisini pasipo kumjibu.
"Leonard!!!" Mkurugenzi aliita kwa furaha na kumkaribisha Leonard aliyeingia ndani ya ofisi.
*****************************
Ikiwa ni mida ya SAA tatu usiku Ukumbi ulikuwa tayari umeshajaa mashabiki, walikuwa na hamu ya kumshuhudia Leonard akiwa jukwaani kwa mara nyingine, ni tamasha lake la kwanza tangu miezi kadhaa ipite pasipo kutumbuiza.
Ukumbi ulikuwa na mwonekano wa kipekee, Octavia na Mariana walikuwa tayari wameshawasili.
"Leo kuna watu wengi sana, ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria tamasha lake," Mariana aliongea.
"Bila shaka, ni moja ya uwanja mkubwa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki elfu themanini, tiketi ziliuzwa ndani ya wiki moja tu, nilikuwa miongoni mwao wa kwanza kuupata," Octavia aliongea kwa kujigamba.
"Nilijua tu lazima usijisifu hivyo sishangai!" Mariana alimdhihaki na mara mayowe makubwa yalisikika ukumbini, ulikuwa ni mda wa Leonard kupanda jukwaani
"Ahhhhhh!!!!!!!!"
"Leonard!!!!!"
"Wewe ni mzuri sana!!!"
"Tunakupenda!!!!"
"Nakupenda Leonard!!!" Octavia aliongea kwa sauti ya juu huku Mariana akiwa pembeni yake na Mariana ilibidi azibe masikio yake.
Macho yake pia yalikuwa kwa Leonard ambaye hakuacha kutabasamu, alikuwa kavalia shati jekundu la mbunifu lililolegea, aliacha vifungo vinne vya kwanza wazi vikionesha kifua chake chenye mvuto, nywele zake zilikuwa zimepambwa kwa uzuri sana, alitumia lenzi ya macho inayoonekana vizuri. "Habari zenu mashabiki zangu!!!" aliongea na yowe la mashabiki lilisikika.
"Ni vizuri sana, asante kwa kurejea nyumbani"
"Nawapenda wote!" Leonard aliongea kwa mara nyingine huku akiitoa lenzi aliyokuwa amevaa kwenye macho yake.
"Moyo wangu jamani!!!"
"Yeye atakuwa mtu wa mwisho wangu"
“Moyo wangu masikini” Octavia alizungumza huku akigusa kwenye kifua chake, Mariana alikuwa kimya akimtazama Octavia.
Tamasha lilianza, Leonard aliimba, alirap, alicheza, karibu kila kitu alikifanya kwa ukamilifu.
Kila alipokuwa akiimba mashabiki karibu wote walikuwa wakiimba pamoja naye, ni Mariana pekee aliyeonekana asiyeujua nyimbo za Leonard.
"Ikiwa tu kuna neno lingine"
"Neno lingine bora kuliko UPENDO"
"Wewe ni mtoto wangu wa ulimwengu"
"Nikiwa na wewe, wengine sio muhimu"
Ni baadhi ya maneno yaliyokuwa kwenye nyimbo za Leonard, hadi tamasha linaisha, ilikuwa ni saa 6 usiku.
Mariana na Octavia walianza kutoka nje ya ukumbi baada tamasha kuisha.
"Koo langu linauma" Octavia aliendelea kusafisha koo lake huku wakiitafuta njia ya kutoka nje ya ukumbi.
"Unapaswa kuwa mtu wa mwisho kulalamika Octavia, mashabiki wa kweli hawapaswi kulalamika, ulikuwa ukipiga kelele mwanzo mwisho" Mariana alimjibu baada ya kumsikia akilalamika.
"Unanidhihaki?"
"Ndiyo ukome ulikuwa unajifanya unajua kuimba!" aliongea huku akitabasamu
“I hate you” Octavia aliongea kwa utani akiyatoa macho yake.
Ghafla, kelele zilisikika na kuwafanya wageuka nyuma.
"Ni Leonard!!" Octavia aliongea na kuondoka akimuacha Mariana huku akikimbia alipo Leonard.
Mashabiki wengine pia walianza kukimbia kuelekea upande ule, walianza kumgonga Mariana aliyekuwa amesimama, Mariana alianguka mpaka chini na ilibaki kidogo tu wamkanyage Mariana.
Mariana alishindwa kusimama na ghafla alisikia sauti na karibu kila mtu alinyamaza.
Ilikuwa ni sauti ya Leonard aliyekuwa akisogea upande wake na karibu kila mtu alianza kusogea pembeni.
Macho yalimtoka baada ya kumuona Leonard akija upande wake, alisahau kabisa kuwa yuko chini.
"Uko sawa miss?" Leonard alimuuliza na yeye aliitikia kwa upole.
"Mkono wangu unauma" aliongea huku akiachia tabasamu.
Leonard alimshika mkono mariana na kumvuta juu.
"Nina wivu!"
"Natamani ningekuwa mimi!!"
"Naomba mtu anisukume na mimi"
"Ahhh wewe!"
Maneno ya shabiki wa kike wa Leonard aliyekuwa karibu yao.
“Kuwa makini” Leonard aliongea kwa upole na kutabasamu kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka.
Leonard aliondoka akiwa na walinzi wake na Mariana alibaki akiwa bado ameachama mdomo wake, Octavia alimsogelea.
"Funga mdomo wako Mari J, mwisho inzi waingie mdomoni" Octavia alimnong'oneza na Mariana alicheka
Upande wa Leonard alikuwa tayari ameshafika kwenye gari.
"Umeunda habari kwa kila mtu, video iko kila mahali" Collins aliongea akiwa kakaa kando ya Leonard kwenye gari.
"Unajua mimi sijali kuhusu habari......" Leonard alisita kuendelea kuzungumza na alishangaa!.
"Hii sio njia ya kwenda nyumbani kwa Bibi...."
"Ndio, kaniambia nikupeleke!" Collins alimjibu.
"Unapaswa angalau kunifahamisha, unajua jinsi Bibi alivyo, nikifika nyumbani lazima atazungumza habari za mimi kuoa, siko tayari kwa hilo" Leonard aliongea huku akifoka........ITAENDELEA.
________________________________
Story………………..MCHUMBA WA PLAY BOY (03)
Powered by…………….CHAMA HURU MEDIA
________________________________
Umri………………..18+
ILIPOISHIA.....
Leonard alisita kuendelea kuzungumza na alishangaa!.
"Hii sio njia ya kwenda nyumbani kwa Bibi...."
"Ndio, kaniambia nikupeleke!" Collins alimjibu.
"Unapaswa angalau kunifahamisha, unajua jinsi Bibi alivyo, nikifika nyumbani lazima atazungumza habari za mimi kuoa, siko tayari kwa hilo" Leonard aliongea huku akifoka........
ENDELEA.........
Walipofika Leonard aliingia mpaka ndani.
"Mjukuu wangu huyo" mara moja Bi Briggs alisimama na kumkumbatia Leonard
"Nimefurahi kukuona Bibi! ila ulitakiwa kuwa umelala sasa ivi!?" Leonard alitabasamu, akimkumbatia kwa nguvu.
"Sijali kuhusu hilo ila umezidi kuwa mzuri mwanangu" Bi Briggs aliongea na kumpapasa nywele kabla ya kumwachia
"Nimetoka kwenye tamasha nimechoka" Leonard aliongea na kuketi.
"Najua......umeshapata rafiki wa kike!?" Bi Briggs alimuuliza huku akitabasamu, Leonard alihema
"Bado Bibi...."
"Kwahiyo uliishi karibu miezi mitatu nchini Italia bira kupata mwanamke? au unataka kufa ukiwa peke yako?" Bi Briggs alimuuliza.
"Bibi tafadhali, nimeshakwambia mara nyingi kuwa sipo tayari kuoa!"
"Utakuwa tayari lini?! Nataka niwaone wajukuu zangu kabla sijafa!! Una miaka ishirini na mbili!!" Bi Briggs aliongea.
"Nimefurahi kuwa unakumbuka umri wangu Bibi, ila bado ninamda wa kutosha" Leonard aliongea
"Una wazimu?!"
"Kwa sasa mwanamke hayupo kwenye mipango yangu, tunaweza kuzungumza juu ya jambo lingine bibi?" Leonard aliongea
Ghafla, Bibi Briggs aliangua kilio, na kumshitua Leonard.
"Bibi!?" Aliita
"Kwanini unanifanyia hivi!?Je, ni dhambi kutaka wajukuu??, wewe ni tajiri tayari, kwa hiyo tatizo ni nini??" Bi Briggs aliongea akilalamika tena alianza kulia na Leonard alimsogelea
"Bibi tafadhali, acha kulia...."
"Sitaki, nitaendelea kulia kila siku hadi upate mchumba, unajua maana yake?? wajukuu ndio sababu ya machozi yangu" Aliongea huku akizidi kulia zaidi.
"Bibi......basi nitaanza kutafuta msichana aliyesahihi" aliongea ili kumtuliza Bibi yake aache kulia, Bibi Briggs alifuta machozi yake.
"Huna haja ya kutafuta!, nimeshamtafuta mtu kwa ajili yako tayari" Aliongea na Leonard alipingwa na butwaa.
"Bibi!!"
"Niamini mjukuu wangu, ni binti wa rafiki yangu na ni mrembo sana. Ingawa bado hatujazungumza naye, lakini hakuna kijana wakumkataa huyo binti!" alitabasamu mbele ya mjukuu wake aliyekuwa akimkazia macho.
"Kwahiyo...unataka nimchumbie?" Alimuuliza kwa sauti ya upole.
"Sio kumchumbia tu ila utamuoa kabisa"
"Bibi!!"
"Nafanya hivi kwa sababu mimi ni Bibi yako!!! unategemea nikae kimya kisa huna nia ya kuoa kwa sasa!?!!! lazima umuoe huyo binti!!!" Bi briggs aliongea kwa msisitizo.
"Nitamuoaje mtu ambae sijakubali hata kumchumbia" Leonard aliongea kwa hasira.
"Najua, ndio maana nimekushirikisha, nyie wawili mtaonana na lazima atakuwa mchumba kwako"
"Bibi....."
"Tafadhali nifanyie hivi mjukuu wangu, umesema unanipenda, kama kweli unanipenda basi naomba ufanye kwa ajili yangu...tafadhali" Aliongea kwa sauti ya upole ambayo alijua mjukuu wake utakuwa ngumu kukataa.
Leonard alipumua na kumjibu.
"Basi sawa nimekubali!"
Sawa" aliongea na kuweka tabasamu mbele ya Bibi yake.
"Nitamjulisha rafiki yangu na nitakuambia sehemu ya nyie wawili kukutana sawa?"
Leonard alisimama pasipo kumjibu na kuongea.
"Tutaongea kesho Bibi, usiku mwema".
Leonard aliondoka akimuacha Bibi yake akimtazama.
"Mjukuu wangu mkaidi sana" Bi Briggs aliongea na kumpigia rafiki yake kwa ajili ya kumjulisha aliyeitwa Clara.
Siku iliyofata nyumbani kwa Mariana, alionekana kijana nje ya nyumba hiyo akigonga mlango, na Mariana alienda kuufungua mlango.
"Nimeagizwa niletea vitu hivi kwenye nyumba hii!"
“Asante” Mariana alimjibu huku akitabasamu, alichukua kifurushi cha zawadi kutoka kwa kijana na kuingia nacho ndani.
Alikifungua na kushuhudia nguo nzuri kwa ajili ya chakula chake cha jioni na Royce jioni hiyo, alianza kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake ila alisikia sauti ya shangazi yake aitwae Clara.
"Njoo hapa Mariana"
Mariana aligeuka mara moja na kurudi chini
"Ndiyo shangazi?"
"Nini hicho mkononi mwako?" Clara alimuuliza huku akinywa mvinyo.
"Ni zawadi ya gauni la chakula cha jioni" Mariana alimjibu huku akitabasamu.
“Good time” Clara aliongea na Mariana alikunja uso.
"Unazungumza nini?" Mariana ilibidi amuulize.
“Keti Mariana nikwambie vizuri”
Mariana alikaa chini kama alivyoambiwa na shangazi yake.
“Mda sio mrefu utaingia kwenye uchumba” Clara alitamka na Mariana alishtuka
"Nini!?"
"Niliwahi kuwekeana ahadi na rafiki yangu kuwa utaolewa na mjukuu wake..."
"Shangazi! unawezaje kuniambia ghafla kuwa nitachumbiwa!?” Mariana alimuuliza.
"Ni mjukuu wa rafiki yangu...."
"Siwezi kuchumbiwa na mjukuu wa rafiki yako! Nina mpenzi na ninampenda sana!" Mariana aliongea kwa kufoka na kusimama.
"Nini unachoongea Mariana!?"
"Ndio hivyo shangazi, nina mpenzi? hivyo sipo tayari kwa hilo......"
"Hii inahusu biashara Mariana, ni matajiri sana...."
"Kwa hiyo unaniuza kwa sababu ya pesa!?" Mariana aliongea kwa hasira.
"Una kichaa Mariana?!! Unathubutu vipi kunifokea?!! unafikiri wewe ni nani?!! kwanza unapaswa kunishukuru!! Nimekuwa nikikutunza tangu wazazi wako walipokufa kifo ambacho hakuna anayekijua!! Nakulisha, nakuvisha, nakusomesha!!!! Unafikiri huwa natoa wapi pesa?, unathubutuje kwenda kinyume na matakwa yangu!!” Clara aliongea kwa sauti ya juu iliyomfanya Mariana akae kimya.
"Jitayarishe, utaenda kuonana nae usiku wa leo," Clara aliongea.
Mapigo ya moyo ya Mariana yaliongezeka ghafla, alikimbia juu huku akijitahidi kupumua, alipofika mlangoni alifungua mlango kwa nguvu.
Mkono wake ukiwa umeshika kifua chake kwa nguvu huku akifungua begi ambalo anaweka vidonge vyake, alichukua vidonge viwili na kuvimeza kwa maji.
Alianza kupumua kwa nguvu hadi mapigo ya moyo yakarudi sawa, Ana ugonjwa wa moyo uitwao Arrhythmia ambao ni mapigo ya moyo yasiyofaa, wakati mwingine mapigo ya moyo huwa kawaida, wakati mwingine huwa polepole na wakati mwingine huwa haraka kama sasa.
Alishika kifua chake na kuketi kitandani kwa upole kuanza kuangua kilio.
Aliligundua tatizo hilo toka miaka miwili iliyopita na tangu wakati huo, amekuwa akitumia dawa hizo bila mtu yeyote kujua, hata shangazi yake hajui kuhusu hilo. na karibu kila sehemu hutembea na dawa na huhakikisha hakuna mtu atakayejua kuhusu tatizo alilonalo.
Clara aliingia chumbani na Mariana alifuta machozi yake baada ya kumuona shangazi yake.
"Kipi kilichokuleta huku chumbani!?"
"Hamna cha maana shangazi!"
"Basi jioni ya leo utaondoka na mimi kwenda kukukutanisha na mchumba wako!"
"Basi sawa!"
Mariana alimjibu na Clara aliondoka na kumuacha keke yake ndani ya chumba.
*****************************
Kwenye nyumba ya Ricardo mlango ulifunguliwa na Leonard aliingia.
"Hatimae uko hapa!!!" Ricardo alisimama na kwenda kumkumbatia.
"Tamasha lilikuwaje? sikupata mda wa kuja!" Ricardo alimuuliza.
"Iilienda vizuri" Leonard alimjibu huku akimimina kinywaji kwenye glasi.
"Sipo sawa kwa sasa Ricardo!?"
"Kuna tatizo gani star wetu!?"
Ricardo alimuuliza na Leonard aliketi kwenye kiti.
"Bibi amenitafutia mchumba wa kuoa!" Leonard aliongea.
"Nini?!!!"
"Ndiyo hivyo, naingia kwenye uchumba na msichana nisiyemfahamu" Leonard aliongea.
"Hongera kwa hilo Leonard!"
"Sijapenda alichonifanyia Bibi!" Leonard aliongea kwa kufoka.
"Bora utulie na mwanamke mmoja ili uache kutembea hovyo na wanawake!"
Leonard alimtazama Ricardo na mda huohuo simu ya Leonard ilianza kuita
Ni Bibi yake aliyekuwa akimpigia, aliamua kuipokea mbele ya Ricardo.
"Jiandae jioni ya leo utaonana na mchumba wako!"
"Ni nini Bibi!?" Leonard aliuliza kwa mshangao.
"Usivunje ahadi yangu mjukuu wangu" Bi Briggs alikata simu na Leonard alimtazama Ricardo.
“Unakutana na huyo msichana usiku wa leo!?” Ricardo alimuuliza.
"Ndio, nitafanya hivi kwa sababu yake tu ila sipo tayari kuwa kwenye mahusiano nae" Leonard aliongea huku akinywa kinywaji chake...........ITAENDELEA.
________________________________
Story………………..MCHUMBA WA PLAY BOY (04)
Powered by…………….CHAMA HURU MEDIA
________________________________
Umri………………..18+
ILIPOISHIA.....
Bibi yake aliyekuwa akimpigia, aliamua kuipokea mbele ya Ricardo.
"Jiandae jioni ya leo utaonana na mchumba wako!"
"Ni nini Bibi!?" Leonard aliuliza kwa mshangao.
"Usivunje ahadi yangu mjukuu wangu" Bi Briggs alikata simu na Leonard alimtazama Ricardo.
“Unakutana na huyo msichana usiku wa leo!?” Ricardo alimuuliza.
"Ndio, nitafanya hivi kwa sababu yake tu ila sipo tayari kuwa kwenye mahusiano nae" Leonard aliongea huku akinywa kinywaji chake.......
ENDELEA......
Masaa yalisogea na mida ya jioni ilifika. Nyumbani kwao Mariana.
"Royce samahani kwa kuvunja ahadi kipenzi changu, kuna mahali naenda na shangazi!” Mariana alimsihi Royce kwenye simu.
"Ni sawa tu Mariana kama imeshindikana basi tutaonana siku nyingine" Royce alimjibu.
"Nakuahidi kesho nitakuja kulala nyumbani kwako". Mariana alimuahidi.
"Haina haja ya kuja, kesho nitakuja mwenyewe kukuchukua" Royce aliongea na Mariana alicheka na kutabasamu.
"Naisubiri kwa hamu siku ya kesho baby, tutaonana kesho, Nakupenda!" Mariana aliongea na kukata simu.
Baada ya kuongea na mpenzi wake alienda kwenye kioo ili kujiangalia, tayari alikuwa ameshavaa tena akiwa kwenye mvuto wa kipekee.
"Natamani asinipende, sitaki kuchumbiwa naye" alijisemea moyoni.
"Mariana!!!" sauti ya Clara ilisikika masikioni mwa Mariana.
"Nakuja shangazi!"
Alichukua simu na begi lake kabla ya kutoka nje ya chumba chake, alishuka na kukutana na Clara akiwa tayari anamsubiri kwenye gari.
"Umependeza sana leo" Clara aliongea huku akimtazama
"Asante" Mariana alimjibu na kwenda kupanda kwenye gari lake, dereva aliondoa gari nje ya jumba lile.
Baada ya muda, walisimama mbele ya jumba la kifahari, walitoka nje ya gari na mwanamke mwenye umri wa miaka hamsini na zaidi alitoka mara moja
"Clara!" Aliita kwa furaha.
“Jules” Clara naye aliita na kwenda kumkumbatia
Baada ya kukumbatiana, Bi Briggs alimgeukia Mariana
"Amependeza sana?" Aliongea huku akimtazama Mariana.
“Mariana njoo karibu” Clara aliongea huku akitabasamu na Mariana alisogea karibu yao.
“Habari Bibi” Alisalimia
"Nzuri, wewe ni mrembo sana. Nina hakika mjukuu wangu atakupenda, njoo hapa unikumbatie" Bi Briggs alifungua mikono yake na Mariana alimkumbatia.
Waliingia wote ndani na Mariana alianza kuingiwa na woga
"Mjukuu wako yupo!?" Clara alimuuliza
"Hapana hayupo, lakini atakuwa hapa sio mda" Bi Briggs alimjibu, hofu ilipungua kwa Mariana kidogo.
Walitulia wote sebuleni na kijakazi alianza kuwahudumia vinywaji, akili ya Mariana haikuwa pale, alikuwa akiwaza! mwanaume atakuwaje anayetaka kumuoa?, je kama ni mbaya atakubalije kuolewa naye!?
Ghafla walisikia mlango ukifunguliwa.
"Yupo hapa" Bi Briggs aliongea, na kumshitua Mariana.
'Nini?!!!!!! Leonardo??!!!' Mariana alipiga kelele kichwani mwake huku akimkazia macho Leonard.
"Mjukuu wangu ulikuwa wapi jamani!?"
"Nina dakika ishirini tu Bibi, tunaweza kuongea haraka tafadhali" Leonard aliongea bila kumuangalia binti anayehitaji kumchumbia ambae ni Mariana.
"Aya mjukuu wangu ila huyu ndiye binti niliyekuambia" Bi Briggs aliongea huku akitabasamu akimwonyesha Mariana.
Leonard hakutaka kumwangalia Mariana zaidi ya kuangalia saa yake.
"Mbona haniangalii!? au mimi sio type yake?? ina maana hakumbuki kama jana tulionana!?" Mariana aliwaza.
Ilikuwa ngumu kwa Leonard kumkumbuka kutokana na yeye kuwa na mabilioni ya mashabiki.
"Mimi ni Clara, shangazi yake" Clara ilibidi aongee huku akitabasamu na Mariana nusura asimame ili ampige kofi.
"Basi, tutawaacha wawili ili mfahamiane" Bi Briggs aliongea na kumvuta Clara na kuondoka naye.
Ukimya ulitawala kati ya Leonard na Mariana, Mariana alikuwa akitamani sana asipatwe na ugonjwa wake wa moyo kwani vidonge vyake alivisahau nyumbani siku hiyo.
Baada ya muda, aliamua kuvunja ukimya ili kuzuia moyo wake usienda mbio.
"Hi...mimi naitwa Mariana Julius, nina hakika hunijui lakini pia nasoma Chuo Kikuu cha Diamonds......"
"Anakulipa kiasi gani?" Leonard alimuuliza swali lililomshangaza Mariana
"Nanii!???" Mariana aliuliza huku macho yakimtoka.
“Nina uhakika Bibi yangu na shangazi yako wana makubaliano, nataka kujua kiasi ulichoahidiwa ili kuolewa na mimi niweze kukulipa, ila naomba uigize kana kwamba umekubali nikuchumbie lakini sitaki uwe unazungumza na mimi, sitajali kuhusu wewe" Leonard aliongea na Mariana hakuamini kama mwanaume mwenyewe hana mpango naye.
Walimaliza kuongea na Mariana aliondoka akiwa na shangazi yake.
"Nimeshaikamilisha kazi yako, kwa sasa sihitaji kurudi nyumbani" Mariana alizungumza.
"Unataka kwenda kwa mpenzi wako!?" Clara alimuuliza.
"Sijui ila sijisikii kurudi nyumbani sasa ivi!"
"Oky, kuwa makini!" Clara alimjibu na kuingia ndani ya gari.
Mariana alichukua usafiri uliompeleka moja kwa moja kwenye nyumba ya mpenzi wake Royce.
Alifika kwenye mlango wa kuingilia ila mlango ulikuwa umefungwa.
"Hayupo nyumbani!?" aliongea na kujaribu kuingiza lock code za mlango, mlango ulifunguka na Mariana aliingia ndani.
Alifunga mlango na kuingia chumbani kwa Royce, alisogea na kulala kitandani kutokana na uchovu aliokuwa nao na kuchukua simu yake na kupiga namba ya Royce.
Simu ilipokelewa na Mariana aliweza kusikia muziki mkubwa kwenye simu yake, ni wazi mwenzake alikuwa akiburudika mda huo.
“Hey babe” sauti ya Royce ilisikika.
"Nipo kwako, uko wapi?" Mariana alimuliza
"Nilidhani hutokuja kipenzi..."
"Nilimaliza mapema kilichonipeleka ila usiwe na haraka endelea kufurahia na marafiki zako tu mimi nipo siku nzima" Mariana aliongea na kukata simu.
Alisimama na kuvua nguo zake na kuingia bafuni, dakika chache baadae alitoka akiwa amelowa. alijifuta maji yaliyokuwa kwenye mwili wake na kwenda kuvaa shati la Royce mpenzi wake.
Mariana alienda kwenye friji na kuchukua chupa ya juisi ya nanasi, alichukua katoni ya popcorn na kuanza kula.
“Tamu” Aliongea huku akitafuna akienda sebuleni.
Alikaa kwenye kochi na kuwasha Tv.
"Angelo!!!!!!!!" alipiga kelele huku uso wake ukiwa kwenye Tv.
Ni video ya wimbo unayoitwa ALL FOR LOVE ulioimbwa na Angelo.
Upendo wake kwa Angelo ni mkubwa, amekuwa akimpenda Angelo na kuzipenda nyimbo zake kuliko Leonard, aliangalia wimbo huo anaoupenda mpaka pale ulipoishi na wimbo mwingine ulifatia.
"Talking of the devil" Aliongea huku akiyatoa macho yake baada ya kuona wimbo wa Leonard umekuja kwenye Tv baada ya wimbo wa Angelo kuisha.
Alidhihaki na kwenda kubadilisha mara moja huku akiendelea kumeza popcorn, hakutaka kuendelea kumuona Leonard kwenye Tv, ghafula mlango ulifunguliwa na kumfanya ageuka.
"Royce" aliita na kudondosha popcorn zilizokuwa kwenye mkononi wake, akimkimbilia Royce kwenda kumkumbatia.
"Nimekukumbuka sana Malikia" Royce aliongea
“Mimi pia” Mariana alijibu huku akimkumbatia kwa nguvu zaidi
"Nilidhani hutakuja sasa ivi..."
"Nilikuwa nyumbani kwa Finn uliponipigia simu" Royce aliongea, Moja ya rafiki wa Royce ni Finn.
"Nilihudhunika sana uliponiambia hutakuja!"
"Samahani ila nipo hapa kwa ajili yako baby" Mariana aliongea.
Royce alimbeba kwa staili ya maharusi huku wakielekea chumbani.
"Utakaa hapa kwangu walau wiki moja"
"Royce!! Shangazi ataniua" Mariana aliongea huku akicheka.
"Umepandlga kuondoka lini?" Royce alimuuliza
“Usijali, nipo hapa mpaka Jumatatu” Mariana alimjibu na Royce alitabasamu.
"Unawaza nini na hilo tabasamu lako la kihuni?"
"Nawaza utamu nitakaoupata mpaka jumatatu" Royce alimjibu huku akimkonyeza.......ITAENDELEA.
________________________________
Story………………..MCHUMBA WA PLAY BOY (05)
Powered by…………….CHAMA HURU MEDIA
________________________________
Umri………………..18+
ILIPOISHIA......
Royce alimbeba kwa staili ya maharusi huku wakielekea chumbani.
"Utakaa hapa kwangu walau wiki moja"
"Royce!! Shangazi ataniua" Mariana aliongea huku akicheka.
"Umepandlga kuondoka lini?" Royce alimuuliza
“Usijali, nipo hapa mpaka Jumatatu” Mariana alimjibu na Royce alitabasamu.
"Unawaza nini na hilo tabasamu lako la kihuni?"
"Nawaza utamu nitakaoupata mpaka jumatatu" Royce alimjibu huku akimkonyeza.........
ENDELEA.......
Nyumbani kwa Jessica, mlinzi alimfungulia mlango Leonard na alishuka kutoka kwenye gari, aliwageukia walinzi na kuongea.
"Msinifuate" Walinzi waliinama wakikubaliana na amri yake.
Walimtazama akiingia ndani nyumba hiyo ya kifahari.
Jessica ni mwimbaji kama yeye akiwa pia ni mwanamitindo, alikuwa na sherehe nyumbani kwake na alialika watu mashuhuri tu!, muziki ulisikika kwa sauti kubwa mpaka upande wa nje wa nyumba hiyo.
Leonard aliingia ndani ya nyumba hiyo na wanawake walianza kumkazia macho kama ilivyokawaida.
"Hii nyumba ina joto sana!" aliongea huku akitembea, hakuacha kumtazama karibu kila mtu alipokuwa akitembea na kwa bahati nzuri alimuona Ricardo akiwa bize kuongea na msichana mmoja.
Leonard aliketi kando yake kwa utulivu na msichana aliyekuwa amekaa karibu na Ricardo alimpiga busu Leonard.
"Heeee! na wewe tena unampenda huyu!? basi ondoka hapa sitaki kukuona tena!" Ricardo alifoka kwa hasira na kumfukuza msichana.
"Sikutegemea kama atakukiss" Ricardo aliongea.
"Mambo ya kawaida haya" Leonard alimjibu huku akichukua glasi ya kinywaji kutoka kwa mhudumu na kumeza fundo moja.
"Sikutegemea kukuona hapa!"
"Imebidi nije sehemu hii!" Leonard aliongea na kuchungulia, aliona watu mbalimbali mashuhuri wakiburudika.
Wasichana karibu wote walikuwa uchi huku wengine wakiwa kwenye bwawa wakicheza muziki, wavulana walifurahia zaidi huku wakizidi kushuhudia makalio ya warembo mbalimbali.
Fatma na Sarah pia walikuwa kwenye bwawa, Sarah hakuwa na mpango wa kuwepo kwenye sherehe hiyo ila ilimlazimu kuwepo baada ya kulazimishwa na Ricardo pamoja na Fatma.
Fatma alikuwa akiburudika sana huku macho ya Sarah yakiwa tayari kwa Leonard, alijaribu kumkonyeza ila Leonard hakuwa na habari nae.
Leonard simu yake iliita hivyo alisimama na kwenda kuipokea simu. Wakati huo huo, Jessica alikuwa akija upande wake.
Angelo pia aliyekuwa maeneo hayo alimshuhudia Jessica, alimeza mvinyo wake akiwapuuza wasichana waliokuwa pembeni yake huku akijiandaa kumfata Jessica, lakini ghafla alichukia baada ya kumuona Leonard.
"Mwanaharamu huyo anataka kuongea nini na Jessica!?" Aliongea kwa hasira.
"My dea....."
“Poteeni hapa” Angelo aliwafokea wasichana aliokuwa nao.
"Mmmh!"
"Nimesema ondokeni hapa!" Angelo aliongea kwa mara nyingine na wasichana hao waliokuwa wamevaa nusu utupu waliondoka.
Aliona bora aondoke na katika kutembea kwake aligongana na Ricardo
"Tembea vizuri wewe jamaa" Ricardo aliongea kwani zilikuwa hazipandi kabisa yeye na Angelo.
Angelo alimkazia macho na kuondoka zake na Ricardo alimwangalia kwa hasira.
Akiwa bado anamtazama Angelo walifika wasichana wawili.
"Baby, siwezi kusubiri tena!" Msichana aliyekuwa kando yake aliongea na kuanza kumbusu, Msichana wa pili naye alianza kumshikashika
"Msiwe na haraka, d**k yangu inawatosha wote wawili" aliongea huku akiwakumbatia kwa kushika viuno vyao.
Leonard alikuwa ameshamaliza kuongea kupitia simu yake, aligeuka ili aondoke ila alimshuhudia Jessica akiwa amesimama mbele yake. Alitabasamu baada ya kumuona.
“Bora tumekutana Leonard” Jessica aliongea na kuanza kumsogelea huku akitembea kwa madaha.
Alipomfikia alizungushia mikono yake kwenye shingo ya Leonard na kuusogeza mdomo wake karibu zaidi na mdomo wa Leonard na kuanza kumbusu kwa matamanio.
"Twende chumbani kwangu Leonard" Aliongea kwa kunong'ona na Leonard alitabasamu huku akimshika mkono na kuongozana nae.
Walifika chumbani na kuanza kubusiana kwa njaa, Leonard alirarua sidiria ya Jessica na kuminya M***t yake, Jessica alitoa miguno ya kimahaba.
Leonard aliutazama mwili wa Jessica na kuongea.
"Geuza @ss yako"
Jessica alitabasamu na kugeuza @ss yake.
Leonard alivua nguo zake na kujiandaa kwa ajili ya msukumo wa kwanza
"F**k me Leo!"
"Aah!!!"
"Ndio!!!!!"
"Ohh!! Haraka!!!"
"Just f**k me forever Leo!!!"
"F**k!!!"
Miguno ya Jessica ilijaa chumbani.
Upande wa Fatma na Sarah.
"Ricardo na Leonard hawaonekani tena bira shaka wameenda kuburudika na wanawake huko" Fatma alimwambia Sarah walipokuwa wakitoka kwenye bwawa, Sarah hakumjibu kitu zaidi ya kujifunika taulo.
"Naondoka, tutaonana baadae"
"Ana shida gani huyu!?" Fatma alijiuliza baada ya kuona mwenzake hana raha.
*****************************
Ikiwa ni siku ya Jumatatu ndani ya chuo kikuu cha Diamonds.
"Unajisikiaje kurudi shuleni??"
Jeremy alionekana akiwahoji baadhi ya wanafunzi muhimu shuleni na kila mtu alimjibu kwa ufasaha.
Jeremy alipomuona Tessa akija aliachia tabasamu kabla ya kwenda kwake, aliacha kuwahoji wengine na kumfata Tessa aliyemkazia macho pasipo kuonesha tabasamu lolote lile.
"Inatakiwa utabasamu maana tupo live na dunia inashuhudia mahojiano haya!" Jeremy alimnong'oneza sikioni Tessa aliyeamua kutabasamu mbele ya kamera.
"It's a joke, fake life" Jeremy aliongea na kuondoka zake na Tessa alikunja sura yake na tabasamu lilipotea.
Jeremy alimuona Mariana akishuka kwenye gari na ndiyo maana hakutaka kuendelea kumhoji Tessa.
Mariana aliongozana na Octavia.
Tessa alikunja ngumi kwa hasira baada ya kumuona Mariana na mabinti wawili walisogea alipokuwa amesimama Tessa.
"Namchukia huyo jamaa, ananikera" Daisy, mmoja wa marafiki wa Tessa aliongea akimaanisha Jeremy.
"Namchukia kuliko wewe" Bella naye alitania.
"Ee Mungu wangu!!! Ni Mariana"
"Malkia wa urembo!!"
" Dah kiukweli ni mzuri sana!"
Tessa alimtazama Mariana kwa chuki baada ya kuwasikia marafiki zake wakimsifia.
"Naona mmeamua kuja kunipigia kelele hapa!?"
"Hapana Tessa ni huyu Daisy!" Bella alizungumza lakini Tessa aliondoka.
"Umemkasirisha tayari!" Daisy alizungumza na kumfata Tessa alipoelekea, Bella naye aliamua kuwafata.
Upande wa Jeremy alianza kumhoji Mariana.
"Hujambo Mariana, karibu sana chuoni kwa mara nyingine!"
"Asante Jeremy, nakupenda” Mariana aliongea huku akitabasamu.
"Ee moyo wangu mimi!"
Jeremy aliongea huku akigusa kifua chake na Mariana alicheka.
"Waambie watu jinsi tunavyopendana!?" Jeremy alimhoji kwa kuweka utani.
"No word" Mariana alimjibu.
Ghafla, sauti za watu zilisikika, Wanafunzi walianza kukimbia kuelekea yalipo magari mawili ya kifahari.
Walinzi walikuwa wa kwanza kushuka kwenye magari hayo na kufungua milango ya magari.
Ricardo na Leonard walitoka nje kwa wakati na wasichana walianza kupiga kelele.
"Leonard!!!!!!!!!"
"Ricardo!!!"
"Ah!!! Leonard, kuwa wangu tafadhali!!"
"Wewe ni maisha yangu naapa Leonard"
Leonard na Ricardo hawakujali maneno ya mashabiki zako, walinzi waliwalinda huku wanafunzi wakiendelea kuwakimbiza hadi walipoelekea kwenye jumba lao la mihadhara la kibinafsi.
Mariana akiwa na Octavia.
"Siamini kama tumefungua chuo!?" Octavia aliongea kwa kulalamika kando ya Mariana huku wakitoka kwenye darasa lao.
"Hutaki kusoma kwani!?" Mariana alimuuliza huku akicheka.
Waliendelea kutembea na walipishana na Nico, mwanafunzi bora kwenye darasa lao, yeye ni kijana maarufu na anapendwa na wasichana katika chuo hicho.
"Nico!" Wasichana watatu walimfuata huku wakimuita.
"Simpendi huyu huwa anajiona sana darasani ila nashangaa kuona wasichana wenzetu wakimshobokea, kwanza hawezi kumzidi umaarufu Leonard wangu!" Octavia alimdhihaki Nico na kukumbatia simu yake iliyokuwa na picha ya Leonard.
"Acha kuongea hayo jamani Octavia mbona Nico ni kijana mtaratibu tu!" Mariana aliongea.
Waliendelea na safari yao na kufika kwenye mgahawa na mara simu ya Mariana iliita.
"Shangazi ananipigia simu!"
"Mpokee umsikilize!"
Mariana aliipokea simu.
“Njoo huku nyumbani mara moja” Clara aliongea.
"Aya shangazi!"
Simu ilikatwa na Clara.
Mariana alimeza fundo la mate na kuuma mdomo wake kwa hasira.
"Nini tatizo?" Octavia alimuuliza
"Unapaswa kula peke yako, nahitaji kwenda nyumbani. Nitakupigia" Mariana aliongea na kutoka nje ya mgahawa.
Kwanza alikimbilia darasani alipoacha begi lake na kuishia kugongana na Nico mlangoni.
"Oh sorry" Mariana aliongea na Nico alimtazama kwa sekunde moja kabla ya kuondoka.
Mariana hakujali, aliingia darasani na kushika begi lake na kutoka nje ya darasa kwa kasi. Aliipigia namba ya Royce ili amsaidie kumpeleka kwao lakini hakuipokea simu.
"Ngoja nikapande teksi" Alinong'ona na kusongea sehemu za teksi.
Akiwa anatembea, gari la Leonard lilionekana. Alitamani kuomba lifiti ila alipokumbuka kuwa hawana mazoea alibaki akilitazama.
"Amelewa umaarufu sana huyu mtu ata kujali watu wengine hajali kwani kashindwa kujiongeza kunipa lifiti?" Aliongea huku akiendelea kutembea......ITAENDELEA.
Pata mwendelezo kwa sh 1000
Namba ya malipo na WhatsApp ni Airtel Tz 0781858056 jina la usajili Anjela
Tags
simulizi